602 Njia ya Imani ya Mafanikio Katika Mungu

1 Hatima ya Paulo na hatima ya Petro ilipimwa kulingana na iwapo wangeweza kutekeleza wajibu wao kama viumbe wa Mungu, na wala si kulingana na ukubwa wa michango yao; hatima zao ziliamuliwa kulingana na kile ambacho walitafuta tangu mwanzo, wala si kulingana na kiasi cha kazi waliyofanya, au makadirio ya watu wengine kuwahusu. Kwa hivyo, kutafuta kutekeleza kikamilifu wajibu wa mtu kama kiumbe wa Mungu ndiyo njia ya mafanikio; kutafuta njia ya upendo wa kweli kwa Mungu ndiyo njia sahihi kabisa; kutafuta mabadiliko katika tabia ya zamani ya mtu, na kutafuta upendo safi kwa Mungu, ndiyo njia ya mafanikio.

2 Njia kama hii ya mafanikio ndiyo njia ya kurejeshwa kwa wajibu wa awali na vile vile pia kuonekana kwanza kwa kiumbe wa Mungu. Hiyo ndiyo njia ya kurejeshwa, na pia ni lengo la kazi yote ya Mungu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kama harakati ya mwanadamu inatiwa doa na madai badhirifu ya kibinafsi na tamaa isiyo ya akili, basi athari ambayo inatimizwa haitakuwa mabadiliko katika tabia ya mwanadamu. Hii ni kinyume na kazi ya kurejeshwa. Bila shaka siyo kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu, na hivyo hii inathibitisha kuwa harakati ya aina hii haikubaliki na Mungu. Harakati ambayo haijakubalika na Mungu ina umuhimu gani?

Umetoholewa kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 601 Njia za Petro na Paulo

Inayofuata: 603 Unaitembea Njia ya Paulo Wakati Hufuatilii Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp