827 Washindi Ni Wale Wanaotoa Ushahidi Mkubwa kwa Mungu
1 Imani katika Mungu inahitaji utiifu Kwake na uzoefu wa kazi Yake. Mungu Amefanya kazi nyingi sana—inaweza semekana kuwa kwa watu yote ni kukamilishwa, yote ni usafishaji, na hata zaidi, yote ni kuadibu. Hakujakuwa na hatua hata moja ya kazi ya Mungu ambayo imelingana na dhana za binadamu; kile watu wamefurahia ni maneno makali ya Mungu. Mungu Atakapokuja, watu wanapaswa kufurahia enzi Yake na hasira Yake, lakini haijalishi maneno Yake yalivyo makali, Anakuja kuokoa na kukamilisha binadamu.
2 Kama viumbe, watu wanapaswa watekeleze wajibu ambao wanafaa kufanya, na kusimama shahidi kwa Mungu katikati ya usafishaji. Katika kila jaribio wanapaswa washikilie ushahidi ambao wanapaswa washuhudie, na kushuhudia ushuhuda mkubwa kwa Mungu. Huyu ni mshindi. Haijalishi Mungu Anavyokuboresha, unabaki kuwa na imani kubwa na kutopoteza imani katika Mungu. Ufanye kile mwanadamu anafaa kufanya. Hiki ndicho Mungu Anahitaji kwa mwanadamu, na moyo wa binadamu unapaswa kuweza kurudi Kwake kikamilifu na kumwelekea katika kila wakati. Huyu ni mshindi.
3 Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi.
4 Kuwa na msimamo ni muhimu sana katika kukamilishwa kwa watu na Mungu. Kama huna shaka na hatua yoyote ya kazi ya Mungu, unatimiza wajibu ya mwanadamu, unashikilia kwa uaminifu kile Mungu Amekufanya ukiweke katika matendo, hiyo ni, unakumbuka mawaidha ya Mungu, na haijalishi Anachokifanya sasa husahau mawaidha Yake, huna shaka kuhusu kazi Yake, unadumisha msimamo wako, kushikilia ushahidi wako, na una ushindi katika kila hatua ya njia, mwishowe utakamilishwa kuwa mshindi na Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili