423 Hakuna Huduma ya Kweli Bila Ombi la Kweli
1 Maombi si aina ya tambiko; ni ushirika wa kweli kati ya watu na Mungu, na huwa na umuhimu wa kina. Tunaweza kuona nini kutoka kwa maombi ya watu? Tunaweza kuona kuwa wao wanamtumikia Mungu moja kwa moja. Ukitazama maombi kama tambiko, basi bila shaka hutamtumikia Mungu vyema. Ikiwa maombi yako hayafanywi kwa ari au kwa dhati, basi inaweza kusemwa kwamba kutoka kwa mtazamo wa Mungu, wewe kama mtu hupo; hali ikiwa hivyo, utakuwaje na Roho Mtakatifu akifanya kazi kwako? Kuanzia sasa na kuendelea, bila maombi, hutaweza kufanya kazi. Ni sala ndiyo huleta kazi, na sala ndiyo huleta huduma. Ikiwa wewe ni mtu ambaye huongoza na mtu anayemtumikia Mungu, ilhali hujawahi kujitoa kwa sala wala hujawahi kuwa makini katika maombi yako, basi njia ambayo unatumia kuhudumu itaishia kukusababisha uanguke.
2 Ikiwa unaweza kuja mbele ya Mungu mara kwa mara, na unaweza kumwomba mara nyingi, inathibitisha kwamba wewe unamchukulia Mungu kama Mungu. Ikiwa mara nyingi unajifanyia mambo na ikiwa mara kwa mara unapuuza kuomba, kufanya hiki na kile bila Yeye kufahamu, basi humtumikii Mungu; bali, unatekeleza tu biashara yako mwenyewe. Hivyo, je, hutahukumiwa? Kutoka nje, haitaonekana kana kwamba umefanya chochote cha kuvuruga, wala haitaonekana kwamba umemkufuru Mungu, lakini utakuwa unatenda tu mambo yako mwenyewe. Kwa kufanya hivyo, je, hukatizi? Hata kama, kwa juu, inaonekana kana kwamba hukatizi, kiasili unampinga Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Umuhimu na Mazoezi ya Sala” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo