1028 Maisha Mapumzikoni

1 Maisha ya pumziko ni yale bila vita, bila uchafu, bila udhalimu unaoendelea. Hii ni kusema kwamba hayana unyanyasaji wa Shetani, upotovu wa Shetani, na pia uvamizi wa nguvu yoyote inayompinga Mungu. Kila kitu kinafuata aina yake na kuabudu Bwana wa uumbaji. Mbingu na dunia ni shwari kabisa. Haya ni maisha matulivu ya binadamu. Mungu aingiapo rahani, hakuna udhalimu wowote utakaoendelea duniani, na hakutakuwa na uvamizi wowote wa nguvu za uhasama. Binadamu pia wataingia ulimwengu mpya; hawatakuwa tena binadamu waliopotoshwa na Shetani, lakini badala yake binadamu ambao wameokolewa baada ya kupotoshwa na Shetani.

2 Siku ya pumziko ya binadamu pia ni siku ya pumziko ya Mungu. Mungu alipoteza pumziko Lake kwa sababu wanadamu hawakuweza kuingia rahani; haikuwa kwamba Hakuweza awali kupumzika. Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo.

3 Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi ndani ya mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1027 Wanadamu Waingiapo Mapumzikoni

Inayofuata: 1029 Mto wa Maji ya Uzima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp