Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

799 Ayubu Alitumia Maisha Yake Yote Kutafuta Kumjua Mungu

1 Ayubu alimiliki na kufuata mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawaje alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawaje alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuna binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawaje miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu ukosefu wa kina hiki cha maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

2 Katika macho yake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Alikuwa hajamwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa kina duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu hakikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala hakikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote.

3 Maisha yake yalikuwa utambuzi wa ukuu na mipangilio ya Mungu, ambaye amefichwa miongoni mwa mambo yote, katika maisha yake ya kila siku. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti na maneno ya moyoni, ambayo Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote, alionyesha kupitia kwa kutawala Kwake kwa sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule uelewa na maarifa sawa ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Sababu ya Ayubu Kupata Sifa ya Mungu

Inayofuata:Thamani ya Maisha ya Ayubu

Maudhui Yanayohusiana