991 Unapaswa Kuyachukuliaje Maneno na Vitendo Vyako Mwenyewe
1 Je, unaamini maneno Yangu? Je, unaamini kulipiza kisasi? Je, unaamini kuwa Nitawaadhibu wale waovu wote wanaonidanganya na kunisaliti? Je, unatarajia siku hiyo ije haraka au ije baadaye? Je, wewe ni mtu ambaye anaogopa adhabu, ama mtu ambaye angenipinga ingawa lazima avumilie adhabu? Siku hiyo itakapowadia, unaweza kukisia ikiwa utaishi katikati ya shangwe na kicheko, au ikiwa utalia na kusaga meno yako?
2 Je, unatarajia kukumbana na mwisho wa aina gani? Je, umewahi kufikiria kwa uzito ikiwa unaniamini asilimia mia moja au una tashwishi nami asilimia mia moja? Je, umewahi kufikiria kwa uangalifu matendo na mwenendo wako vitakuletea matokeo ya aina gani? Je, unatumaini kwa kweli kuwa maneno Yangu yote yatatimizwa, ama unaogopa kuwa maneno Yangu yatatimizwa kama matokeo?
3 Ikiwa unatumaini kuwa Nitaondoka hivi karibuni ili Niyatimize maneno Yangu, je, unapaswa kuyachukuliaje maneno na matendo yako mwenyewe? Ikiwa hutumainii kuondoka Kwangu na hutumaini maneno Yangu yote yatimizwe mara moja, kwa nini uniamini hata kidogo? Kwa kweli unajua mbona unanifuata? Ikiwa sababu yako ni kupanua upeo wako tu, hakuna haja ya kujisumbua kufanya hivyo. Ikiwa ni ili ubarikiwe na kuepukana na msiba unaokuja, mbona hujali kuhusu tabia yako mwenyewe? Mbona hujiulizi ikiwa unaweza kuyakidhi mahitaji Yangu? Mbona pia hujiulizi ikiwa unastahili kupokea baraka zitakazokuja?
Umetoholewa kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili