561 Jinsi ya Kuchunguza Asili Yako

1 Ili kujua asili yako, lazima utimize vitu vichache. Kwanza, lazima uwe na uelewa dhahiri wa kile upendacho. Hili halihusu vitu unavyopenda kula au kuvaa; bali, linamaanisha aina ya vitu unavyofurahia, vitu unavyohusudu, vitu unavyoabudu, vitu unavyotafuta, na vitu unavyozingatia moyoni mwako. Katika asili za watu, kuna sifa zenye usawa kuhusu vitu ambavyo wao hupenda. Yaani, wanapenda watu, matukio na vitu ambavyo watu wengine wanahusudu kwa sababu ya mwonekano wa nje, wanapenda watu, matukio na vitu vinavyoonekana vizuri na vya anasa, na wanapenda watu, matukio na vitu ambavyo huwafanya watu wengine kuwaabudu kwa sababu ya sura zao za nje. Hivi vitu ambavyo watu hupenda ni vizuri, vya kung'aa, vya kupendeza, na vya fahari. Watu wote huabudu vitu hivi. Inaweza kuonekana kwamba watu hawana ukweli wowote, wala hawana mfano wa wanadamu wa kweli. Hakuna kiwango hata kidogo cha umuhimu katika kuabudu vitu hivi, ilhali watu bado huvipenda.

2 Kila unachopenda, kile unachozingatia, kile unachoabudu, kile unachohusudu, na kile unachofikiria ndani ya moyo wako kila siku vyote ni viwakilishi vya asili yako. Inatosha kuthibitisha kwamba asili yako inapenda udhalimu, na katika hali mbaya, asili yako ni mbovu na isiyotibika. Unapaswa kuichambua asili yako kwa njia hii; yaani, chunguza kile unachopenda na kile unachoacha katika maisha yako. Ni kwa kuchangua tu asili za watu tu ndio unaweza kujua kweli dutu na upotovu wa mwanadamu na kufahamu watu wanamilikiwa na nini hasa, kile watu wanakosa kweli, kile wanapaswa kujizatiti nacho, na jinsi wanapaswa kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Kuchangua kweli asili ya mtu si rahisi, na haiwezi kufanywa bila kupitia maneno ya Mungu au kuwa na uzoefu wa kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 560 Jinsi ya Kuelewa Asili ya Binadamu

Inayofuata: 562 Kujua Mawazo na Mitazamo Yenu Wenyewe ni Muhimu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp