22 Ni Vizuri Sana Kwamba Mwenyezi Mungu Amekuja
1
Ni bahati kweli kukutana na Mungu mwenye mwili.
Kristo wa siku za mwisho anaonekana na kufanya kazi.
Anaonyesha ukweli na kuleta hukumu.
Ili kumwokoa mwanadamu, Yeye anafanya kazi binafsi.
Yeye ni wa kawaida, Ana huzuni na furaha.
Yeye ni wa utendaji, Anacheka na kunena.
Maana ya kupata mwili Kwake ni kubwa sana,
Mungu wa kweli anaweza kuonekana.
Tuna furaha kumwona Mwenyezi Mungu.
Tunapata furaha kupitia kuabudu.
Kumsifu Yeye kunatuacha wepesi na huru.
Maisha yetu siyo bure, kwa maana tunamjua Yeye.
2
Katika siku za mwisho Mungu anaonekana katika mwili.
Yeye Mwenyewe anawakamilisha wale wanaompenda.
Matamko Yake huwaongoza watu Wake,
yakimpa mwanadamu ukweli na uhai.
Ikiwa maneno ya Mungu yanafichua au kumsihi mwanadamu,
ni ili kumwokoa na kumtakasa.
Kwa kupitia hukumu ya maneno Yake,
tunamwona Mungu ni mwenye haki na mtakatifu.
Mungu huteseka kwa ajili ya mwanadamu na anaelewa udhaifu wake.
Maneno Yake humkimu na kumpa nuru mwanadamu.
Anampa mwanadamu imani na Anamletea mwanga,
hufidia kile akosacho mwanadamu na kuongoza njia yake.
3
Mungu hupitia mateso ya mwanadamu
na husimama na mwanadamu anapoadibiwa.
Anayafikiria maisha ya mwanadamu wakati wote.
Mungu pekee ndiye aliye karibu sana naye.
Kwa kimya Anastahimili kukataliwa.
Katika dhiki Yeye yuko pamoja na mwanadamu.
Anaanzisha njia kuelekea mbele.
Sura ya Mwenyezi Mungu inanitia moyo.
Tangu nyakati za kale, kumwona Mungu kumekuwa kugumu sana.
Thamini wakati mzuri tulio nao na Mungu.
Sasa ni nafasi ya kuona uzuri wa Mungu.
Hebu tuje kumjua Mwenyezi Mungu.
Ni vizuri sana kwamba Mwenyezi Mungu amekuja.