980 Umepungukia Kaisi Kipi Matakwa ya Mungu?
1 Haijalishi kile mnachosadiki, mambo Ninayoyasema na kufanya hayanuii kukufanya ninyi kuhisi kama mnamwagiliwa maji baridi. Badala yake, yananuia kuboresha uelewa wenu wa nia za Mungu, na kuboresha ung’amuzi wenu kuhusu kile ambacho Mungu anafikiria, kile ambacho Mungu anataka kukamilisha ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anapenda, nini kinachukiza Mungu, nini Mungu anadharau, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anataka kumpata, na ni mtu wa aina gani ambaye Mungu anatupilia mbali. Yananuia kupatia akili zenu uwazi, kuwasaidia kujua wazi ni kiwango kipi vitendo na fikira za kila mmoja wenu yamepotea kutoka kwa kiwango kinachohitajika na Mungu.
2 Kwa sababu Ninajua mmesadiki kwa muda mrefu, na mmesikiliza mahubiri mengi, lakini kwa hakika haya ndiyo mambo yanayokosekana zaidi. Mmerekodi kila ukweli katika daftari zenu, mmerekodi pia kile ambacho nyie wenyewe mnasadiki kibinafsi kuwa muhimu katika akili zenu na ingawa mnapanga kutumia haya kumridhisha Mungu wakati wa kutenda kwenu, kuyatumia mnapojipata mkihitaji msaada, kuyatumia kupitia nyakati ngumu zilizo mbele yenu, au mnaacha ukweli huu uandamane na ninyi mnapoishi maisha yenu tu.
3 Iwapo mnatenda tu, namna mnavyotenda hasa si muhimu. Nini, basi, ndicho kitu cha muhimu sana? Ni kwamba wakati unatenda, moyo wako hujua kwa uhakika wote kama kila kitu unachofanya, kila kitendo, ndicho kile anachotaka Mungu au la; kama kila kitu unachofanya ni sahihi au la, kila kitu unachofikiria ni sahihi au la, na matokeo na shabaha katika moyo wako yanatosheleza nia za Mungu au la, kama yanatilia maanani mahitaji ya Mungu au la, na kama Mungu anayaidhinisha au la. Haya ni mambo muhimu.
Umetoholewa kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha” katika Neno Laonekana katika Mwili