116 Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu

1

Zamani nilifuatilia utajiri na umaarufu.

Niliacha viwango vyote vya kutenda,

Nilidanganya ili nipate riziki.

Sikujali chochote kuhusu dhamiri

au maadili,

chochote kuhusu uadilifu au heshima.

havikuwa vya maana kwangu.

2

Niliishi tu kuridhisha tamaa

na uroho wangu vilivyozidi kukua.

Kwa moyo usio na amani,

nilitembea katika matope ya dhambi,

bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.

Utajiri wa maisha na raha za muda mfupi

hazingeweza kuficha utupu na maumivu ndani ya moyo wangu.

Mbona ni vigumu sana

kuwa na uadilifu maishani?

Mbona wanadamu ni wenye hila sana, wabaya sana?

Hii ni dunia ya aina gani?

Nani anayeweza kuniokoa?

Nilisikia sauti ya Mungu

na kurudi mbele ya Mungu.

Ni ukweli unaoonyeshwa na Mungu ndio huutakasa upotovu wangu.

Maneno ya Mungu ya hukumu

na kuadibu yatembea nami maishani mwangu.

Kukubali uchunguzi wa Mungu katika mambo yote

huufanya moyo wangu uwe mtulivu na wenye amani.

Hakuna udanganyifu, hakuna uongo,

ninaishi katika nuru.

Kwa moyo ulio wazi, mimi ni mtu mwaminifu,

na ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu mwishowe.

3

Nafaidika kutokana na kusoma maneno Yake,

kusoma maneno ya Mungu kila siku.

Naelewa ukweli mwingi sana,

kuwa na sheria za tabia ya binadamu.

Nikipitia majaribio na usafishaji, nimeuona uso wa Mungu,

na kupata maisha mapya ndani ya maneno ya Mungu.

Sasa naweza kuwa mtu mwaminifu.

Nilisikia sauti ya Mungu

na kurudi mbele ya Mungu.

Ni ukweli unaoonyeshwa na Mungu ndio huutakasa upotovu wangu.

Maneno ya Mungu ya hukumu

na kuadibu yatembea nami maishani mwangu.

Kukubali uchunguzi wa Mungu katika mambo yote

huufanya moyo wangu uwe mtulivu na wenye amani.

Hakuna udanganyifu, hakuna uongo,

ninaishi katika nuru.

Kwa moyo ulio wazi, mimi ni mtu mwaminifu,

na ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu mwishowe.

Mimi nina shukrani milele

kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!

Nina shukrani milele kwa Mwenyezi Mungu!

Iliyotangulia: 115 Ukweli wa Maneno ya Mungu ni wa Thamani Sana

Inayofuata: 117 Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp