446 Kuwa na Uhusiano wa Kawaida na Mungu ili Ukamilishwe

1 Ni wakati tu uhusiano wako na Mungu unapokuwa wa kawaida ndipo unaweza kukamilishwa na Yeye; ni wakati huo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, ufundishaji nidhamu, na usafishaji wa Mungu vifanikisha athari zake zilizokusudiwa ndani yako. Hiyo ni kusema, ikiwa wanadamu wanaweza kumweka Mungu mioyoni mwao na wasifuatilie faida ya kibinafsi au kufikiria matarajio yao wenyewe (kwa njia ya mwili), lakini badala yake wabebe mzigo wa kuingia katika uzima, wajitahidi kabisa kuufuatilia ukweli, na kuitii kazi ya Mungu—ikiwa unaweza kufanya hivi, basi malengo unayoyafuatilia yatakuwa sawa, na uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

2 Kuufanya uhusiano wa mtu na Mungu uwe muwafaka kunaweza kuitwa hatua ya kwanza ya kuingia katika safari ya kiroho ya mtu. Ingawa hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Mungu na imeamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na mwanadamu, kama unaweza kukamilishwa na Mungu au kupatwa na Yeye kunategemea ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Kunaweza kuwa na sehemu fulani ndani yako ambazo ni dhaifu au zisizotii—lakini mradi maoni yako na nia zako ni sawa, na mradi uhusiano wako na Mungu uko sawa na wa kawaida, basi unastahili kukamilishwa na Mungu.

3 Ikiwa huna uhusiano muwafaka na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili au familia yako, basi bila kujali jinsi unavyotia bidii, itakuwa bure. Ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii kitu kingine chochote, lakini tu ikiwa maoni yako katika imani yako katika Mungu yako sawa: unamwamini nani, unaamini kwa ajili ya nani, na kwa nini unaamini. Ikiwa unaweza kuona mambo haya waziwazi na kutenda wakati maoni yako yakiwa na mwelekeo mzuri, basi utaendelea katika maisha yako, na pia utahakikishiwa kuingia kwenye njia muwafaka.

Umetoholewa kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 445 Mfanano wa Wale Wanaotumiwa na Mungu

Inayofuata: 447 Hali ya Kawaida ni Nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp