565 Mtu Anaweza Kujichukia tu Anapojijua kwa Kweli

1 Kwa nini watu wengi hufuata tamaa zao za kimwili? Kwa sababu wanajiona kuwa wazuri kabisa, wakihisi kuwa vitendo vyao ni viadilifu na vya haki, kwamba hawana makosa, na hata kwamba wako sahihi kabisa, kwa hiyo wao wana uwezo wa kutenda kwa dhana kuwa haki iko upande wao. Wakati mtu anapotambua asili yake ya kweli ilivyo—jinsi ilivyo mbaya, jinsi inavyostahili kudharauliwa, na jinsi ilivyo ya kusikitisha—basi yeye si mwenye majivuno sana, hajigambi ovyo ovyo sana, hajifurahii kama hapo awali. Mtu kama huyo huhisi, “Lazima niwe mwenye ari na mpole, na nitende baadhi ya maneno ya Mungu. Kama sivyo, basi siwezi kufikia kiwango cha kuwa mwanadamu, na nitaona aibu kuishi mbele ya Mungu.” Kwa hakika mtu hujiona kuwa hafifu, kama kweli asiye na maana. Wakati huu, inakuwa rahisi kwake kutekeleza ukweli, naye ataonekana kwa kiwango fulani kuwa kama mwanadamu anavyopaswa kuwa. Ni pale tu ambapo watu kwa hakika hujichukia kabisa ndipo wanaweza kunyima mwili. Kama hawajichukii, hawataweza kunyima mwili.

2 Mtu kujichukia kweli kunajumuisha mambo machache: Kwanza, kujua asili yake mwenyewe; na pili, kujiona kama yeye ni mwenye shida na wa kudharaulika, kujiona kuwa mdogo kupindukia na asiye na maana, na kuona nafsi yake kuwa yenye kudharaulika na chafu. Mtu anapoona kikamilifu kile alicho kwa hakika, na matokeo haya yakafikiwa, basi yeye kweli hupata ufahamu juu yake mwenyewe, na inaweza kusemwa kwamba amekuja kujijua mwenyewe kikamilifu. Ni hapo tu ndipo anaweza kwa hakika kujichukia mwenyewe, kufikia hata kujilaani mwenyewe, na ahisi kwa kweli kwamba amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hafanani tena na mwanadamu. Kisha, siku moja, wakati tishio la kifo linapoonekana, mtu kama huyu atafikiri, “Hii ni adhabu ya haki ya Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye haki; Kwa hakika mimi lazima nife!” Wakati huu, yeye hatalalamika, wala kumlaumu Mungu, akihisi tu kwamba yeye ni wa kudharaulika, mchafu sana na mpotovu, kwamba anapaswa kuangamizwa na Mungu na roho kama yake haifai kuishi duniani. Wakati huu, mtu huyu hatampinga Mungu, sembuse kumsaliti Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 564 Kujitafakari kwa Njia Hii ni Muhimu

Inayofuata: 566 Mungu Huwabariki Wale Walio Waaminifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp