971 Binadamu Hukua Chini ya Ulinzi wa Mungu

1 Wakati wowote Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kazi, wala haweki kando ama kupuuza wale ambao amechagua. Badala yake, bila kuvuta macho hata kidogo, kwa siri, kwa ukimya, Mungu anafanya yote yanayohitajika. Anakuchagulia familia, pia Anachagua tarehe ambayo utazaliwa. Mungu anaangalia unapozaliwa katika dunia hii ukilia, Anatazama kuzaliwa kwako, Anatazama unapotamka maneno yako ya kwanza, Anatazama unapoanguka na kutembea hatua zako za kwanza, ukijifunza kutembea. Katika mchakato wa kukua, unaweza kukutana na mambo mengi ambayo hupendi, kukutana na magonjwa na kuvunjika moyo. Lakini unapotembea njia hii, maisha yako na bahati zako ziko chini ya ulinzi wa Mungu kabisa. Unaishi chini ya macho ya Mungu, unakua, unapevuka.

2 Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Kimsingi kila mtu amekutana na hali nyingi hatari na kupitia majaribu mengi. Hii ni kwa sababu Shetani yupo kando yako, macho yake yakikutazama kila wakati. Anapenda janga linapokupata, wakati maafa yanakupata, wakati hakuna chochote kinaenda sawa kwako, na anapendelea unaponaswa na wavu wa Shetani. Kuhusu Mungu, anakulinda kila wakati, kukuweka mbali na bahati moja mbaya baada ya nyingine na kutokana na janga moja baada ya jingine. Hii ndiyo maana Nasema kwamba kila kitu ambacho mwanadamu anacho—amani na furaha, baraka na usalama wa kibinafsi—yote hakika yanadhibitiwa na Mungu, na Anaongoza na kuamua hatima ya kila mtu.

3 Anaongoza kila mtu kwa mkono, Anakuchunga kwa kila muda na Hajawahi kuondoka upande wako. Watu wanapokua katika mazingira haya na kukua na usuli wa aina hii, tunaweza kusema kwamba watu kwa kweli wanakua katika kiganja cha mkono wa Mungu? Mambo haya yanaleta baraka, amani na furaha kwa mwanadamu. Yanamleta mwanadamu kwa amani na kwa furaha katika macho ya Mungu na ndani ya familia Yake; kisha wanaishi mbele ya Mungu na kukubali wokovu wa Mungu na fikira na mawazo ya kawaida. Mungu ni mwaminifu na kila kitu Anachofanya ni halisi. Ni Yeye pekee ambaye watu wanaweza kutegemea na Mungu ambaye watu wanaweza kuaminia maisha yao na yote wanayo Kwake.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 970 Ni Muhimu Sana Kuelewa Asili Takatifu ya Mungu

Inayofuata: 972 Mungu Huongoza Maisha ya Mwanadamu Daima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp