Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Je, “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Je, una ufahamu wowote wa juujuu kuhusu jambo hilo? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu. Ni kupitia tu kwa mawasiliano ya Mungu ya kipengele hiki cha ukweli ndipo nimehisi kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote na uhai wa vitu vyote unapewa na Mungu, kwamba Mungu anatengeneza sheria hizi, na kwamba Anavilea vitu vyote. Kutokana na uumbaji Wake wa vitu vyote ninaona upendo wa Mungu.) Wakati uliopita, kimsingi tuliwasiliana kuhusu uumbaji wa Mungu wa vitu vyote na jinsi Aliunda sheria na kanuni kwa ajili ya vitu hivyo. Chini ya sheria hizi na chini ya kanuni hizi, vitu vyote huishi na kufa na mwanadamu na kuishi pamoja kwa amani na mwanadamu chini ya utawala wa Mungu na machoni pa Mungu. Kwanza tulizungumza kuhusu Mungu kuumba vitu vyote na kutumia mbinu Zake kuamua sheria zao za ukuaji na vilevile njia na mpangilio wa ukuaji wao. Pia aliamua njia njia ambazo vitu vyote huendelea kuishi katika ardhi hii, ili viweze kuendelea kukua na kuzaana na kutegemeana kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa mbinu na sheria hizi, vitu vyote vinaweza kuwepo na kukua katika nchi hii kwa ufanisi na kwa amani. Ni kwa kuwa tu na mazingira kama haya ndipo wanadamu wanaweza kuwa na makao na mazingira ya kuishi yaliyo thabiti, na chini ya uongozi wa Mungu, waendelee kukua na kusonga mbele, kukua na kusonga mbele.

Wakati uliopita, tulijadili kuhusu wazo la msingi la Mungu kuruzuku vitu vyote: Mungu kwanza huvipa vitu vyote kwa njia hii ili vitu vyote viwepo na kuishi kwa ajili ya wanadamu. Yaani, mazingira kama haya yapo kwa ajili ya sheria zilizotungwa na Mungu. Ni tu kwa Mungu kudumisha na kusimamia sheria kama hizi ndio wanadamu wana mazingira ya kuishi waliyonayo sasa. Tulichozungumzia wakati uliopita ni hatua kubwa kutoka kwa ufahamu wa Mungu tuliozungumzia awali. Kwa nini hatua kama hiyo ipo? Kwa sababu tulipozungumzia hapo awali kuhusu kuanza kumjua Mungu, tulikuwa tunajadili katika eneo la Mungu kuwaokoa na kuwasimamia wanadamu—yaani, uokoaji na usimamizi wa watu waliochaguliwa na Mungu—kuhusu kumjua Mungu, matendo ya Mungu, tabia Yake, kile Anacho na Alicho, makusudi Yake, na vile Anampa mwanadamu ukweli na uhai. Lakini mada tuliyozungumza kuihusu wakati uliopita haikujikita tu katika mipaka ya Biblia na katika eneo la Mungu kuwaokoa watu Wake waliochaguliwa. Badala yake, ilitoka nje ya eneo hili, nje ya Biblia, na nje ya mipaka ya hatua tatu za kazi ambayo Mungu anafanya kwa watu Wake waliochaguliwa na kujadili Mungu Mwenyewe. Hivyo basi ukisikia sehemu hii ya mawasiliano Yangu, lazima usiwekee mipaka ufahamu wako wa Mungu kwa Biblia na hatua tatu za kazi ya Mungu. Badala yake, unahitaji kuuweka wazi mtazamo wako; unahitaji uone matendo ya Mungu na kile Anacho na alicho miongoni mwa vitu vyote, na vile Mungu anatawala na kusimamia vitu vyote. Kupitia kwa mbinu hii na juu ya msingi huu, unaweza kuona vile Mungu anapeana vitu vyote. Hii inawawezesha wanadamu kuelewa kwamba Mungu ni chanzo halisi cha uhai kwa vitu vyote na kwamba huu ni utambulisho halisi wa Mungu Mwenyewe. Hiyo ni kusema, utambulisho wa Mungu, hadhi na mamlaka na kila kitu Chake havilengwi tu kwa wale wanaomfuata Yeye wakati huu—havilengwi tu kwa kundi hili la watu—bali kwa vitu vyote. Basi eneo la vitu vyote ni pana sana. Ninatumia “vitu vyote” kueleza eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote kwa sababu Ninataka kuwaambia kwamba vitu vinavyotawaliwa na Mungu si vile mnavyoweza tu kuona kwa macho yenu, bali vinahusisha ulimwengu yakinifu ambao watu wote wanaweza kuuona, na vilevile ulimwengu mwingine usioweza kuonekana kwa macho ya binadamu nje ya ulimwengu yakinifu, na zaidi unahusisha anga na sayari nje ya mahali ambapo wanadamu wapo sasa. Hilo ni eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote ni pana zaidi. Kwenu ninyi, mnachopaswa kuelewa, mnachopaswa kuona, na kutoka kwa vitu mnavyopaswa kupata maarifa—hivi ndivyo kila mmoja wenu anahitaji na ni lazima aelewe, aone, na awe na hakika navyo. Ingawa eneo la hivi “vitu vyote” ni pana, Sitawaambia kuhusu eneo msiloweza kuona kabisa au msiloweza kukutana nalo. Nitawaambia tu kuhusu eneo ambalo binadamu wanaweza kukutana nalo, wanaweza kuelewa, na wanaweza kufahamu, ili kila mmoja aweze kuhisi maana halisi ya kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Hivyo, chochote Ninachowasilisha kwenu hakitakuwa maneno matupu.

Wakati uliopita, tulitumia mbinu ya kuhadithia ili kutoa maelezo rahisi ya jumla ya mada hii “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote,” ili muwe na ufahamu wa msingi wa jinsi Mungu huvipa vitu vyote. Ni nini kusudi la kuwafundisha kidogokidogo wazo hili la msingi? Ni kuwafanya mjue kwamba, nje ya Biblia na hatua tatu za kazi Yake, Mungu pia anafanya hata kazi nyingi zaidi ambayo wanadamu hawawezi kuiona au kukutana nayo. Kazi kama hiyo inatendwa binafsi na Mungu. Kama Mungu angekuwa anaongoza tu watu Wake waliochaguliwa kwenda mbele, bila hii kazi iliyo nje ya kazi Yake ya usimamizi, basi ingekuwa vigumu sana kwa binadamu hawa, ikiwemo pamoja na ninyi nyote, kuendelea kusonga mbele, na binadamu hawa na ulimwengu huu haungeweza kuendelea kukua. Huo ndio umuhimu wa kirai hiki “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote” Ninachowasilisha kwenu siku hii.

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu

Tumejadili mada nyingi na maudhui yanayohusiana na kirai hiki “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote,” lakini mnajua ndani ya mioyo yenu ni vitu vipi Mungu anatoa kwa wanadamu mbali na kuwapa ninyi neno Lake na kutenda kazi Yake ya kuadibu na hukumu kwenu? Watu wengine huenda wakasema, “Mungu hunipa neema na baraka; Yeye hunifundisha nidhamu na kunifariji na Hunipa utunzaji na ulinzi kwa kila njia iwezekanayo.” Wengine watasema, “Mungu hunipa chakula cha kila siku na kinywaji,” ilhali wengine hata watasema, “Mungu hunipa kila kitu.” Kuhusu vitu hivi ambavyo watu wanaweza kukutana navyo katika maisha yao ya kila siku, nyote mnaweza kuwa na majibu yanayohusiana na matukio mnayopitia katika maisha yenu ya kimwili. Mungu humpa kila mtu mmoja vitu vingi, ingawa tunachojadili leo hakijawekewa mipaka katika eneo la mahitaji ya watu ya kila siku, lakini kinanuiwa kupanua mtazamo wa kila mmoja wenu na kuwawezesha kuona vitu kutoka mbali zaidi. Kwa sababu Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, Anadumisha vipi uhai wa vitu vyote? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho Mungu huleta kwa vitu vyote ili kudumisha kuwepo kwa vitu hivyo na kudumisha sheria za kuwepo kwa vitu hivyo? Hilo ndilo wazo kuu la kile tunachojadili leo. Je, mnaelewa Nilichosema? Mada hii huenda ikawa msiyoifahamu sana, lakini Sitazungumza kuhusu mafundisho ya dini yoyote ambayo ni ya kina sana. Nitajitahidi kuwafanya nyote muelewe baada ya kusikiliza. Hamhitaji kuhisi mzigo wowote—mnachotakiwa kufanya tu ni kusikiliza kwa makini. Kwa hali yoyote, bado Ninahitaji kuisisitiza zaidi kidogo: Ninazungumza juu ya mada gani? Niambieni. (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Basi ni vipi ambavyo Mungu huvipa vitu vyote? Ni nini ambacho Yeye huvipa vitu vyote ili isemwe kwamba “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? Je, mna dhana ama mawazo yoyote kuhusu hili? Inaonekana kwamba mada hii Ninayozungumzia kimsingi haileti kinachotumainiwa ndani ya mioyo yenu na ndani ya akili zenu. Lakini Natumai mtaweza kuunganisha mada hii pamoja na vitu Ninavyoenda kuzungumzia kwa matendo ya Mungu, na sio kuviunganisha kwa ufahamu wowote au kuvihusisha na desturi zozote za binadamu au uchunguzi. Ninazungumza tu kuhusu Mungu na kuhusu Mungu Mwenyewe. Hilo ni pendekezo Langu kwenu. Unaelewa, sivyo?

Mungu ametoa vitu vingi kwa wanadamu. Nitaanza kwa kuzungumza kuhusu kile ambacho watu wanaweza kuona, yaani, wanachoweza kuhisi. Hivi ni vitu ambavyo watu wanaweza kuvielewa na wanaweza kukubali. Hivyo basi kwanza tuanze na ulimwengu yakinifu kujadili kile ambacho Mungu amewapa wanadamu.

1. Hewa

Kwanza, Mungu aliumba hewa ili mwanadamu aweze kupumua. Hewa ni chembechembe ambayo kwayo wanadamu wanaweza kuwasiliana nila siku na ni kitu ambacho kwacho wanadamu hutegemea mara kwa mara, hata wanapolala. Hewa ambayo Mungu aliumba ina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu: ni kijenzi muhimu cha kila pumzi yao na cha uhai wenyewe. Kiini hiki, kinachoweza tu kuhisiwa lakini hakionekani, kilikuwa zawadi ya Mungu ya kwanza kwa vitu vyote. Baada ya kuumba hewa, je, Mungu aliacha kufanya kazi? Baada ya kuumba hewa, je, Mungu alizingatia uzito wa hewa? Je, Mungu alizingatia yaliyomo kwenye hewa? Mungu alikuwa anafikiria nini alipoumba hewa? Kwa nini Mungu aliumba hewa, na fikira Yake ilikuwa gani? Wanadamu wanahitaji hewa, na wanahitaji kupumua. Kwanza kabisa, uzito wa hewa unapaswa kuwa unaofaa mapafu ya binadamu. Kuna yeyote anayejua uzito wa hewa? Hili si jambo ambalo watu wanahitaji kujua; hakuna haja ya kujua hili. Hatuhitaji idadi kamili kuhusiana na uzito wa hewa, na kuwa na wazo la jumla ni vizuri. Mungu aliumba hewa yenye uzito ambao ungefaa zaidi mapafu ya mwanadamu kupumua. Yaani, wanadamu wanafurahia na haiwezi kudhuru mwili wanapoivuta. Hili ndilo wazo kuhusu uzito wa hewa. Basi tutaongea kuhusu yaliyomo kwenye hewa. Kwanza, yaliyomo ndani ya hewa si sumu kwa wanadamu na hivyo hayatadhuru pafu na mwili. Mungu alihitaji kuzingatia haya yote. Mungu alihitaji kuzingatia kwamba hewa ambayo wanadamu wanapumua inapaswa kuingia na kutoka taratibu, na kwamba, baada ya kuvuta hewa, kadiri na kiasi cha hewa vinapaswa kuhakikisha damu pamoja na hewa chafu ndani ya mapafu na mwili vingejenga na kuvunjavunja kemikali mwilini vizuri, na pia kwamba hewa hiyo haipaswi kuwa na vijenzi vyovyote vya sumu. Kuhusu viwango hivi viwili, Sitaki kuwalisha mafungu ya maarifa, lakini badala yake nataka tu mjue kwamba Mungu alikuwa na mchakato maalum wa mawazo akilini mwake Alipoumba kila kitu—bora zaidi. Aidha, kuhusu kiasi cha vumbi katika hewa, kiasi cha vumbi, mchanga na uchafu duniani, na vilevile vumbi inayoelekea chini kutoka angani, Mungu alikuwa na mpango wa vitu hivi pia, njia za kuviondoa ama kuvisababisha vivunjike. Huku kukiwa na vumbi kiasi, Mungu aliiumba ili vumbi isidhuru mwili na upumuaji wa mwanadamu, na kwamba vipande vya vumbi viwe na ukubwa usiokuwa na madhara kwa mwili. Je, uumbaji wa Mungu wa hewa haukuwa wa ajabu? Je, ulikuwa rahisi kama kupuliza pumzi ya hewa kutoka kinywani Mwake? (La.) Hata katika uumbaji wake wa vitu rahisi sana, maajabu ya Mungu, akili Zake, mawazo Yake, na hekima Yake vyote ni dhahiri. Je, Mungu si mwenye vitendo? (Ndiyo, yeye Ndiye.) Maana ya hii ni kwamba, hata katika kuumba vitu rahisi, Mungu alikuwa akifikiria kuhusu mwanadamu. Kwanza kabisa, hewa ambayo wanadamu hupumua ni safi, yaliyomo yanafaa kwa upumuaji wa mwanadamu, si sumu na hayasababishi madhara kwa wanadamu, na uzito huo umekadiriwa kwa upumuaji wa wanadamu. Hewa hii ambayo wanadamu huvuta pumzi na kutoa ni muhimu kwa mwili wao, umbo lao. Ili wanadamu waweze kupumua kwa uhuru, bila kizuizi au wasiwasi. Waweze kupumua kwa kawaida. Hewa ni kile ambacho Mungu aliumba mwanzo na ambacho ni cha lazima kwa upumuaji wa wanadamu.

2. Halijoto

Kitu cha pili ni halijoto. Kila mtu anajua halijoto ni nini. Halijoto ni kitu ambacho mazingira yanayofaa kuishi kwa wanadamu ni lazima yawe nacho. Ikiwa halijoto iko juu sana, tuseme ikiwa halijoto iko juu zaidi ya nyuzi Selisiasi 40, basi haingekuwa inachosha sana kwa wanadamu? Je, haingekuwa inachosha kwao kuishi? Je, na halijoto ikiwa chini sana, na kufikia nyuzi hasi Selisiasi 40? Wanadamu hawataweza pia kuistahimili. Kwa hiyo, Mungu alikuwa mwangalifu sana katika kuviweka vipimo hivi vya halijoto. Vipimo vya halijoto ambavyo mwili wa mwanadamu unaweza kufanya mabadiliko kimsingi ni nyuzi hasi Selisiasi 30 hadi nyuzi Selisiasi 40. Hiki ndicho kipimo cha halijoto cha msingi kutoka kaskazini mpaka kusini. Katika maeneo ya baridi, halijoto inaweza kuteremka mpaka nyuzi hasi 50 hadi 60 Selisiasi. Eneo kama hilo si mahali ambapo Mungu anamruhusu mwanadamu kuishi. Mbona kuna maeneo ya baridi hivyo? Katika hayo kuna hekima na makusudi ya Mungu. Hakuruhusu kusonga karibu na sehemu hizo. Mungu hulinda sehemu zilizo na joto sana na baridi sana, kumaanisha Hayuko tayari kumruhusu mwanadamu kuishi huko. Si kwa wanadamu. Kwa nini akaruhusu sehemu kama hizo kuwepo duniani? Ikiwa Mungu hangemruhusu mwanadamu kuishi au kuwepo huko, basi kwa nini akaziumba? Hekima ya Mungu imo humo. Yaani, halijoto ya msingi ya mazingira ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu pia imerekebishwa na Mungu vya kutosha. Kuna sheria hapa pia. Mungu aliumba vitu vingine kusaidia kudumisha halijoto kama hiyo, kudhibiti halijoto hiyo. Ni vitu gani vinatumiwa kudumisha halijoto hii? Kwanza kabisa, jua linaweza kuwaletea watu uvuguvugu, lakini watu wataweza kustahimili iwapo ni vuguvugu sana? Je, kuna yeyote anaweza thubutu kukaribia jua? Je, kuna kifaa chochote duniani kinachoweza kusonga karibu na jua? (La.) Mbona? Ni joto sana. Kitayeyuka kikaribiapo jua. Kwa hiyo, Mungu ametengeneza kipimo maalum cha umbali wa jua kutoka kwa wanadamu: Amefanya kazi maalumu. Mungu ana kiwango cha umbali huu. Vilevile kuna Ncha ya kusini na Ncha ya Kaskazini za dunia. Kote huko kuna mito ya barafu. Wanadamu wanaweza kuishi juu ya mito ya barafu? Inafaa kuishi kwa wanadamu? La, hivyo watu hawataenda huko. Kwa vile watu hawaendi katika Ncha za Kusini na Kaskazini, mito ya barafu itahifadhiwa, na itaweza kufanya wajibu wake, ambao ni kudhibiti halijoto. Unaelewa? Ikiwa hakuna Ncha za Kusini na Kaskazini na jua linawaka juu ya dunia kila wakati, basi watu wote juu ya dunia watakufa kutokana na joto. Je, Mungu hutumia tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto inayofaa kuishi kwa wanadamu? La, pia kuna kila aina za viumbe vyenye uhai, kama vile nyasi juu ya mbuga za malisho, aina mbalimbali za miti na kila aina ya mimea iliyo ndani ya misitu vinafyonza joto la jua na kwa kufanya hivyo, vinabatilisha nishati ya joto ya jua kwa njia inayorekebisha halijoto ya mazingira ambamo wanadamu wanaishi. Pia kuna vyanzo vya maji, kama vile mito na maziwa. Sehemu ya juu ya mito na maziwa si kitu kinachoweza kuamuliwa na yeyote. Hakuna yeyote anayeweza kudhibiti kiasi cha maji yaliyo juu ya dunia, wapi maji hayo yanatiririka, mwelekeo wa kutiririka huko, wingi wa maji hayo, au spidi ya mtiririko huo. Mungu pekee ndiye ajuaye. Vyanzo hivi mbalimbali vya maji, yakiwemo maji ya chini ya ardhi na mito na maziwa yaliyo juu ya ardhi ambayo watu wanaweza kuona, yanaweza pia kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Zaidi ya hayo, kuna kila aina ya uumbaji wa kijiografia, kama vile milima, tambarare, korongo kuu na ardhi ya majimaji wa uumbaji huu mbalimbali wa kijiografia na sehemu zao za juu na ukubwa vyote vina umuhimu katika kudhibiti halijoto. Kwa mfano, ikiwa mlima una mzinga wa kilomita mia moja, kilomita hizi 100 zitakuwa na athari ya kilomita 100. Lakini kuhusu safu za milima na korongo kuu ngapi kama hizo ambazo Mungu ameumba juu ya dunia, hili ni jambo ambalo Mungu amelifikiria kabisa. Kwa maneno mengine, nyuma ya kuwepo kwa kila kitu kilichoumbwa na Mungu kuna hadithi, na pia kina hekima na mipango ya Mungu. Tuseme, kwa mfano, misitu na kila aina mbalimbali za mimea—safu na ukubwa wa eneo ambamo vinapatikana na kukua haudhibitiwi na mwanadamu yeyote na hakuna anayetawala vitu hivi. Kiasi cha maji ambayo vinafyonza, kiasi cha nishati ya joto ambayo vinafyonza kutoka kwa jua pia haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote. Vitu hivi vyote viko katika eneo la kile kilichopangwa na Mungu alipoumba vitu vyote.

Ni kwa sababu tu ya upangaji wa makini, fikira, na utaratibu wa Mungu katika vipengele vyote ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Kwa hiyo, kila kitu ambacho mwanadamu anakiona kwa macho yake, kama vile jua, Ncha za Kusini na Kaskazini ambazo watu mara nyingi husikia kuzihusu, vilevile viumbe mbalimbali vilivyo hai juu na chini ya ardhi na ndani ya maji, na sehemu za juu zenye misitu na aina zingine za mimea, na vyanzo vya maji, mikusanyiko mbalimbali ya maji, kuna kiasi gani cha maji chumvi na maji baridi, kuongezea mazingira mbalimbali ya kijiografia—Mungu hutumia vitu hivi kudumisha halijoto ya kawaida kwa kuishi kwa mwanadamu. Hii ni thabiti. Ni kwa sababu tu Mungu ana fikira kama hizi ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Haiwezi kuwa baridi zaidi wala joto zaidi: sehemu zenye joto zaidi na ambapo halijoto inazidi kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea bila shaka hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili yako. Sehemu zenye baridi zaidi na ambapo halijoto ni ya chini zaidi; sehemu ambazo, punde tu wanadamu wanapowasili, zitawafanya wagande sana baada ya dakika chache mpaka wasiweze kuzungumza, ubongo wao utaganda, wasiweze kufikiri, na hatimaye watakosa hewa—sehemu kama hizo pia hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Haijalishi ni aina gani ya uchunguzi wanadamu wanataka kufanya, au kama wanataka kuvumbua au wanataka kutengua mipaka hiyo—haijalishi watu wanafikiria nini, hawataweza kamwe kuzidi mipaka ya kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea. Hawataweza kuondoa mipaka hiyo ambayo Mungu alimuumbia mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu aliwaumba wanadamu, na Mungu anajua bora zaidi ni halijoto gani mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea. Lakini wanadamu wenyewe hawajui. Mbona nasema wanadamu hawajui? Ni mambo gani ya upumbavu ambayo wanadamu wamefanya? Je, hakujakuwa na watu wachache ambao kila mara wanataka kushindana na Ncha za Kaskazini na Kusini? Watu kama hao daima wametaka kwenda kwenye sehemu hizo kumiliki ardhi hiyo, ili waweze kujisitawisha huko. Hiki kingekuwa kitendo cha upumbavu. Hata iwapo umechunguza kikamilifu pembe za dunia, halafu nini? Hata iwapo unaweza kuzoea joto na una uwezo wa kuishi hapo, ingeweza kumfaa mwanadamu kwa njia yoyote iwapo “ungeboresha” hali ya sasa ya maisha katika Ncha za Kusini na Kaskazini? Wanadamu hawana mazingira ambayo kwayo wanaweza kuendelea kuishi ndani, lakini wanadamu hawabaki hapo kwa ukimya na utiifu, ila badala yake wanasisitiza kuenda maeneo ambapo hawawezi kuishi. Kwa nini ni hivyo? Wamechoshwa na kuishi katika halijoto hii ya kufaa. Wamefurahia baraka nyingi sana. Mbali na hayo, haya mazingira ya kuishi ya kawaida yameharibiwa kiasi sana na wanadamu, hivyo wanaweza basi kwenda kwa Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini ili wafanye madhara mengi zaidi au kujihusisha katika “kusudi,” fulani ili waweze kuwa “watangulizi” wa aina fulani. Si huu ni upumbavu? Hivyo ni kusema, chini ya uongozi wa babu yao Shetani, wanadamu hawa wanaendelea kufanya kitu kimoja cha upuuzi baada ya kingine, wakiharibu bila hadhari na kwa utukutu makao mazuri ambayo Mungu aliwaumbia wanadamu. Hili ndilo Shetani alifanya. Zaidi ya hayo, kwa kuona kwamba kuendelea kuishi kwa wanadamu duniani kuko katika hatari kidogo, watu wengi sana wanataka kutafuta njia za kwenda kuishi juu ya mwezi, kutafuta njia ya kuondoka kwa kuona ikiwa wanaweza kuishi huko. Hatimaye, inakosekana kwenye mwezi. Je, wanadamu wanaweza kuendelea kuishi bila oksijeni? Kwa vile mwezi hauna oksijeni, si mahali ambapo mwanadamu anaweza kuishi huko, ilhali mwanadamu anaendelea kutaka kwenda huko. Hii ni nini? Ni kujiangamiza, sivyo? Ni mahali pasipo na hewa, na halijoto haifai kwa kuendelea kuishi kwa mwanadamu, hivyo hapajatayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu.

Mada yetu sasa hivi, halijoto ni kitu ambacho watu hukutana nacho katika maisha yao ya kila siku. Halijoto ni kitu ambacho miili yote ya wanadamu inaweza kuhisi, lakini hakuna anayefikiria vile halijoto hii iliumbwa, au ni nani anasimamia na kudhibiti halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu. Hiki ndicho tunaanza kujua sasa. Je, kuna hekima ya Mungu katika hili? Je, kuna kitendo cha Mungu katika hili? (Ndiyo.) Ukifikiria kwamba Mungu aliumba mazingira yenye halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu, je, hii ni njia moja ambayo Mungu huvipa vitu vyote? Ni kweli.

3. Sauti

Kitu cha tatu ni nini? Pia ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Pia inaweza kusemwa kwamba viumbe vyote vyenye uhai haviwezi kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Hivyo hiki ni kitu gani? Ni sauti. Mungu aliumba kila kitu, na kila kitu kinaishi mikononi mwa Mungu. Machoni pa Mungu, vitu vyote vinasonga na vinaishi. Yaani kuwepo kwa kila mojawapo ya vitu vilivyoumbwa na Mungu kuna thamani na maana. Yaani, vyote vina umuhimu katika kuwepo kwao. Kila kitu kina uhai machoni pa Mungu; kwa kuwa vyote viko hai, vitatoa sauti. Kwa mfano, dunia daima inazunguka, jua daima linazunguka, na mwezi daima unazunguka pia. Sauti daima zinatolewa katika uzalishaji na kuendelea na miendo ya vitu vyote. Vitu juu ya dunia daima vinazaa, kukua na kusonga. Kwa mfano, misingi ya milima inasonga na kubadilisha nafasi, na vitu vyote vyenye uhai katika kina cha bahari vinasonga na kuogelea na kwenda hapa na pale. Hii inamaanisha kwamba vitu hivi vyenye uhai, vitu vyote anavyoviona Mungu, vyote viko mara kwa mara, kwa mwendo wa kawaida, kulingana na mifumo iliyoanzishwa. Kwa hivyo, ni nini kinaletwa na uzalishaji wa siri na maendeleo na miendo ya vitu hivyo? Sauti za nguvu. Mbali na dunia, kila aina ya sayari daima ziko katika mwendo, na viumbe vyenye uhai na viumbe hai juu ya sayari hizo pia daima vinazaa, vinakua na viko katika mwendo. Yaani, vitu vyote vilivyo na uhai na visivyo na uhai daima vinasonga mbele machoni pa Mungu, na pia vinatoa sauti wakati huo huo. Mungu pia ameshughulikia sauti hizi. Mnapaswa kujua sababu ya mbona sauti hizi zinashughulikiwa, sivyo? Unaposonga karibu na ndege, sauti ya kunguruma ya ndege itakufanyia nini? Masikio yako yatazibwa muda unavyozidi kusonga. Je, mioyo yenu itaweza kuistahimili? Wengine wenye mioyo hafifu hawataweza kuistahimili. Bila shaka, hata wale wenye mioyo yenye nguvu hawataweza kuistahimili ikiendelea kwa muda mrefu. Hiyo ni kusema, athari ya sauti kwa mwili wa mwanadamu, kama ni kwa masikio au moyo, ni yenye maana kabisa kwa kila mtu, na sauti ambazo ni za juu sana zitaleta madhara kwa watu. Kwa hiyo, Mungu alipoumba vitu vyote na baada ya hivyo kuanza kufanya kazi kwa kawaida, Mungu pia aliweka sauti hizi—sauti za vitu vyote vilivyo katika mwendo—kupitia kwa utendeaji wa kufaa. Hii pia ni mojawapo ya fikira muhimu alizokuwa nazo Mungu alipoumbia wanadamu mazingira.

Kwanza kabisa, kimo cha angahewa kutoka kwa uso wa dunia kitaathiri sauti. Pia, ukubwa wa utupu ndani ya mchanga, pia utaendesha na kuathiri sauti. Kisha kuna mahali mito miwili inapoungana pa mazingira mbalimbali ya kijiografia, ambapo pia pataathiri sauti. Hiyo ni kusema, Mungu hutumia mbinu fulani kuondoa sauti zingine, ili wanadamu waweze kuendelea kuishi katika mazingira ambayo masikio na mioyo yao vinaweza kustahimili. La sivyo sauti zitaleta kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu; zitaleta matatizo makubwa kwa maisha yao. Hili litakuwa tatizo kubwa kwao. Hiyo ni kusema, Mungu alikuwa mwenye kujali sana katika uumbaji Wake wa nchi, angahewa, na aina mbalimbali za mazingira ya kijiografia. Hekima ya Mungu iko ndani ya haya yote. Ufahamu wa wanadamu kuhusu haya hauhitaji kuwa kinaganaga sana. Kila wanachohitaji kujua ni kwamba kitendo cha Mungu kimo humo. Sasa Niambieni, hii kazi ambayo Mungu alifanya ilikuwa muhimu? Yaani, uendeshaji wa taratibu sana wa sauti ili kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu na maisha yao ya kawaida. (Ndiyo.) Ikiwa kazi hii ilikuwa muhimu, basi kutokana na mtazamo huu, je, inaweza kusemwa kwamba Mungu alitumia mbinu kama hii kupeana vitu vyote? Mungu aliwapa wanadamu na kuumba mazingira haya tulivu, ili kwamba mwili wa mwanadamu uweze kuishi kwa kawaida kabisa katika mazingira haya bila vizuizi vyovyote, na ili kwamba mwanadamu ataweza kuwepo na kuishi kwa kawaida. Je, hii si njia mojawapo ambayo kwayo Mungu huwapa wanadamu? Je, jambo hili alilofanya Mungu lilikuwa muhimu sana? (Ndiyo.) Lilikuwa muhimu sana. Je, ni vipi ambavyo mnashukuru hili? Hata kama hamwezi kuhisi kwamba hiki kilikuwa kitendo cha Mungu, wala hamjui vile Mungu alikifanya wakati huo, je, bado mnaweza kuhisi umuhimu wa Mungu kufanya hilo? Je, mnaweza kuhisi hekima ya Mungu au umakini na wazo Aliyoweka katika jambo hili? (Ndiyo.) Kuweza tu kuhisi hili ni sawa. Yatosha. Kuna vitu vingi ambavyo Mungu amefanya miongoni mwa vitu vyote ambavyo watu hawawezi kuhisi na kuona. Lengo la Mimi kukitaja hapa ni kuwapa tu habari kiasi kuhusu matendo ya Mungu ili muweze kuanza kumjua Mungu. Vidokezo hivi vinaweza kuwafanya mjue na kumwelewa Mungu vizuri zaidi.

4. Nuru

Kitu cha nne kinahusiana na macho ya watu—nacho ni, nuru. Hiki pia ni muhimu sana. Unapoona nuru inayong’aa, na mwangaza wa nuru hiyo ukafikia kiasi fulani, macho yako yatapofushwa. Hata hivyo, macho ya wanadamu ni macho ya mwili. Hayawezi kustahimili kuwashwa. Je, kuna yeyote anayethubutu kulitazama jua moja kwa moja? Watu wengine wamejaribu. Unaweza kutazama ukiwa umevaa miwani ya jua, sivyo? Hilo linahitaji usaidizi wa vifaa. Bila vifaa, macho makavu ya mwanadamu hayathubutu kutazama jua moja kwa moja. Hata hivyo, Mungu aliumba jua ili awape wanadamu nuru, na pia aliendesha nuru hii. Mungu hakuliacha tu jua na kulipuuza baada ya kuliumba. “Nani anajali iwapo macho ya mwanadamu yanaweza kulistahimili!” Mungu hafanyi vitu hivyo. Yeye hufanya vitu kwa uangalifu sana na huzingatia vipengele vyote. Mungu aliwapa wanadamu macho ili waweze kuona, lakini Mungu ametayarisha pia umbali wa mwangaza ambao wanaweza kutazama chini yake. Haitawezekana iwapo hakuna nuru ya kutosha. Iwapo kuna giza sana mpaka watu hawawezi kuona mkono wao ulio mbele yao, kisha macho yao yatapoteza kazi yake na hayatakuwa na faida yoyote. Sehemu iliyo na mwangaza mwingi itakuwa haivumiliki kwa macho ya mwanadamu na pia hawataweza kuona chochote. Hivyo katika mazingira wanayoishi ndani wanadamu, Mungu amewapa kiasi cha nuru kinachofaa macho ya wanadamu. Nuru hii haitaumiza wala kudhuru macho ya watu. Zaidi ya hayo, haitayafanya macho ya watu yapoteze matumizi yake. Hii ndiyo sababu ambayo Mungu aliongeza mawingu yanayozunguka jua na dunia, na uzito wa hewa unaweza pia kuchuja kwa kawaida nuru inayoweza kuumiza macho ya watu au ngozi. Haya yanahusiana. Kuongezea, rangi ya dunia iliyoumbwa na Mungu huakisi pia nuru ya jua na kuondoa ile sehemu ya mwangaza katika nuru inayofanya macho ya wanadamu kutokuwa na raha. Kwa njia hiyo, watu hawahitaji kila mara kuvaa miwani myeusi sana ya jua ili waweze kutembea huko nje na kufanya shughuli za maisha yao. Katika hali za kawaida, macho ya wanadamu yanaweza kuona vitu vilivyo katika eneo la kuona kwao na hayataingiliwa kati na nuru. Yaani, nuru hii haiwezi kuwa ya kuchoma sana wala ya kufifiliza, ikiwa ya kufifiliza sana, macho ya watu yatadhuriwa na hawataweza kuyatumia kwa muda mrefu sana kabla ya macho yao kuacha kutumika; ikiwa ina mwangaza sana, macho ya watu hayataweza kuistahimili. Nuru ii hii ambayo watu wanayo inapaswa iwe ya manufaa kwa macho ya wanadamu kuona, na madhara yanayoletwa kwa macho ya wanadamu na nuru yamepunguzwa na Mungu kupitia kwa mbinu mbalimbali. Haijalishi ikiwa nuru huleta faida au kikwazo kwa macho ya wanadamu, inatosha kuyawezesha macho ya watu kuendelea kuishi mpaka mwisho wa maisha yao. Je, Mungu hajalifikiria hilo kikamilifu sana? Lakini wakati Shetani, ibilisi, anafanya mambo, hafikirii mambo haya. Nuru hiyo ama ina mwangaza sana au inafifiliza sana Hivi ndivyo Shetani hufanya vitu.

Mungu alifanya vitu hivi katika vipengele vyote vya mwili wa mwanadamu—kuona, kusikia, kuonja, kupumua, hisia … kuongeza hadi upeo uwezo wa kubadilisha wa kuendelea kuishi kwa wanadamu ili waweze kuishi kwa kawaida na kuendelea kuishi. Yaani ni kusema, mazingira ya kuishi kama hayo yaliyopo yaliyoumbwa na Mungu ni mazingira ya kuishi yanayofaa zaidi na yenye faida kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wengine wanaweza kufikiri kwamba hii haitoshi na kwamba yote ni ya kawaida sana. Sauti, nuru, na hewa ni vitu ambavyo watu hufikiria kwamba walizaliwa navyo, vitu wanavyoweza kufurahia tangu wakati wa kuzaliwa. Lakini kile alichofanya Mungu kinachosababisha kufurahia kwao kwa vitu hivi ni kitu wanachohitaji kujua na kuelewa. Haijalishi ikiwa unahisi kuna haja ya kuelewa au kujua vitu hivi, kwa ufupi, Mungu alipoumba vitu hivi, alikuwa ametumia fikira, Alikuwa na mpango, Alikuwa na mawazo fulani. Hakuwaweka wanadamu katika mazingira ya kuishi kama haya kwa kawaida, kwa bahati, au bila kufikiria. Huenda mkadhani kwamba Nimezungumza kwa kwa fahari kuhusu vitu hivi vyote vidogo, lakini kwa mtazamo Wangu, kila kitu ambacho Mungu aliwapa wanadamu ni muhimu kwa kuendelea kuishi kwa binadamu. Kuna tendo la Mungu katika hili.

5. Bubujiko la Hewa

Kitu cha tano ni kipi? Kitu hiki kinahusiana sana na kila siku ya mwanadamu, na uhusiano huu thabiti. Ni kitu ambacho mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi bila katika ulimwengu huu yakinifu. Kitu hiki ni bubujiko la hewa. “Bubujiko la hewa” ni neno ambalo watu wote labda wanaelewa. Hivyo bubujiko la hewa ni nini Mngesema kwamba kububujika kwa hewa kunaitwa “bubujiko la hewa.” Bubujiko la hewa ni upepo ambao jicho la mwanadamu haliwezi kuona. Pia ni njia ambayo gesi husonga. Lakini ni bubujiko la hewa gani tunalozungumzia hapa? Mtaelewa punde Nitakaposema. Dunia hubeba milima, bahari, na vitu vyote inapogeuka, na inapogeuka kuna spidi. Hata ikiwa huwezi kuhisi kuzunguka kokote, mzunguko wake upo kweli. Mzunguko wake huleta nini? Huwa kuna upepo kando ya masikio yako unapokimbia? Ikiwa upepo unaweza kuzalishwa unapokimbia, inawezekanaje kutokuwepo kwa nguvu za upepo dunia inapozunguka? Dunia inapozunguka, vitu vyote viko katika mwendo. Iko katika mwendo na kuzunguka katika spidi fulani, wakati vitu vyote duniani daima vinazaa na kukua. Kwa hiyo, kusonga kwa spidi fulani kwa kawaida kutaleta bubujiko la hewa. Hilo ndilo bubujiko la hewa. Bubujiko la hewa hilo litaathiri mwili wa mwanadamu kwa kiasi fulani? Unaona, tufani za kawaida hazina nguvu sana, lakini zinapotokea, watu hawawezi kusimama kwa utulivu na huona vigumu kutembea katika upepo huo. Ni vigumu hata kutembea hatua moja. Ina nguvu sana, baadhi ya watu wanasukumwa na upepo dhidi ya kitu na hawawezi kusonga. Hii ni mojawapo ya njia ambazo bubujiko la hewa linaweza kuathiri wanadamu. Ikiwa dunia nzima ingekuwa imejaa tambarare, ingekuwa vigumu mno kwa mwili wa binadamu kuhimili bubujiko la hewa ambalo lingezalishwa na mzunguko wa dunia na mwendo wa vitu vyote katika spidi fulani. Ingekuwa vigumu zaidi kustahimili. Ingekuwa hivyo, hili bubujiko la hewa halingeleta tu madhara kwa wanadamu, bali uharibifu. Hakuna ambaye angeweza kuendelea kuishi katika mazingira hayo. Ndio maana Mungu hutumia mazingira mbalimbali ya kijiografia kutatua aina hiyo ya mabubujiko ya hewa—katika mazingira tofauti, mabubujiko ya hewa hufifia, hubadili mwelekeo wake, hubadili kasi yake na hubadili nguvu yake. Ndio maana watu wanaweza kuona mazingira ya jiografia mbalimbali, kama vile milima, safu za milima, tambarare, vilima, vidimbwi, mabonde, uwanda wa juu, na mito. Mungu hutumia haya mazingira mbalimbali ya jiografia kubadilisha spidi, mwelekeo na nguvu za bubujiko la hewa, akitumia mbinu kama hiyo kupunguza au kuiendesha kuwa spidi ya upepo, mwelekeo wa upepo, na nguvu za upepo zinazofaa, ili wanadamu waweze kuwa na mazingira ya kuishi ya kawaida. Je, ni lazima kufanya hivyo? (Ndiyo.) Kufanya jambo kama hilo kunaonekana kuwa vigumu kwa wanadamu, lakini ni rahisi kwa Mungu kwa sababu Anaangalia kwa makini vitu vyote. Kwa Yeye kuumba mazingira yenye bubujiko la hewa linalofaa wanadamu ni kitu sahili sana, rahisi sana. Kwa hiyo, katika mazingira kama hayo yaliyoumbwa na Mungu, kila kitu na vitu vyote miongoni mwa vitu vyote ni vya lazima. Kuna thamani na umuhimu katika kila kuwepo kwa vitu hivyo. Hata hivyo, kanuni hii haieleweki na Shetani au kwa mwanadamu ambaye amepotoshwa. Wanaendelea kuharibu na kukuza, wakiota bure juu ya kugeuza milima kuwa ardhi tambarare, kujaza korongo kuu, na kujenga magorofa juu ya ardhi tambarare kuunda misitu ya saruji. Ni matumaini ya Mungu kwamba wanadamu wataishi kwa furaha, kukua kwa furaha, na kutumia kila siku kwa furaha katika mazingira ya kufaa zaidi Aliyowatayarishia. Ndiyo maana Mungu hajawahi kuwa mzembe inapohusu kushughulikia mazingira ya kuishi ya wanadamu. Kutoka kwa halijoto mpaka kwa hewa, kutoka kwa sauti mpaka kwa nuru, Mungu amefanya mipango na utaratibu tatanishi, ili mazingira ya kuishi ya wanadamu na miili yao visiweze kupatwa na kuharibiwa kokote kutoka kwa hali za asili, na badala yake wanadamu waweze kuishi na kuongezeka kawaida na kuishi na vitu vyote kawaida kwa kuishi pamoja kwa amani yenye kuridhisha. Hii yote inapeanwa na Mungu kwa vitu vyote na wanadamu.

Je, unaweza kuona, kutokana na jinsi Alishughulikia hali hizi tano za msingi za kuendelea kuishi kwa wanadamu, upeanaji wa Mungu kwa wanadamu? (Ndiyo.) Hiyo ni kusema kwamba Mungu aliumba msingi kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wakati huo huo, Mungu pia anasimamia na kudhibiti vitu hivi vyote, na hata sasa, baada ya wanadamu kuwepo kwa maelfu ya miaka, Mungu bado daima anabadilisha mazingira yao ya kuishi, kupeana mazingira ya kuishi yaliyo bora zaidi na ya kufaa zaidi kwa wanadamu ili maisha yao yaweze kudumishwa kwa kawaida. Haya yatadumishwa mpaka lini? Kwa maneno mengine, Mungu ataendelea kupeana mazingira kama haya kwa muda gani? Mpaka Mungu akamilishe kabisa kazi Yake ya usimamizi. Kisha, Mungu atabadilisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Huenda ikawa kupitia kwa mbinu zile zile, au huenda ikawa kupitia kwa mbinu tofauti, lakini kile ambacho watu wanahitaji kujua sasa ni kwamba Mungu daima anapeana mahitaji ya wanadamu, anasimamia mazingira ya kuishi ya wanadamu, na kutunza, kuhifadhi na kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Ni kwa sababu ya mazingira kama hayo ndiyo watu waliochaguliwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kawaida hivyo na kukubali wokovu wa Mungu na kuadibu na hukumu. Vitu vyote vinaendelea kuwepo kwa sababu ya kanuni ya Mungu, wakati wanadamu wote wanaendelea kusonga mbele kwa sababu ya upeanaji wa Mungu kwa jinsi hii.

Je, sehemu hii ambayo Nimewasilisha sasa hivi imewaletea mawazo yoyote mapya? Je, sasa mnahisi tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu? Nani hasa ndiye bwana wa vitu vyote? Ni mwanadamu? (La.) Basi ni nini tofauti kati ya vile Mungu na wanadamu hushughulikia vitu vyote? (Mungu hutawala na kupanga vitu vyote, ilhali mwanadamu hufurahia vitu hivyo vyote.) Je, mnakubaliana na maneno hayo? Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote. Yaani, vitu vyote vipo machoni mwa Mungu na katika eneo Lake la ukaguzi. Je, wanadamu wanaweza kuona vitu vyote? Kile ambacho wanadamu huona kimewekewa mipaka—ni tu kile wanachoona mbele ya macho yao. Ukiukwea mlima huu, unachoona ni mlima huu. Huwezi kuona kilicho upande mwingine wa mlima huo. Ukienda pwani, unaweza kuona upande huu wa bahari, lakini hujui upande ule mwingine wa bahari ulivyo. Ukiwasili katika msitu huu, unaweza kuona mimea iliyo mbele ya macho yako na inayokuzunguka, lakini huwezi kuona iliyo mbele zaidi. Wanadamu hawawezi kuona sehemu zilizo juu sana, mbali sana na kina sana. Kile wanachoweza kuona ni kilicho mbele ya macho yao na katika mpaka wa uwezo wao wa kuona. Hata kama wanadamu wanajua mpangilio wa misimu minne katika mwaka na mpangilio wa ukuaji wa vitu vyote, hawawezi kusimamia au kutawala vitu vyote. Kwa upande mwingine, vile Mungu aonavyo vitu vyote ni kama vile Mungu angeona mashine Aliyotengeneza binafsi. Angejua kila kijenzi vizuri kabisa. Kanuni zake ni zipi, mipangilio yake ni ipi, na kusudi lake ni lipi—Mungu anajua vitu hivi vyote wazi na dhahiri. Kwa hiyo Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu! Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo. Wanadamu wakichunguza kitu fulani kidogo ambacho Mungu alifanya, wangetumia maisha yao yote kukichunguza bila kupata matokeo yoyote ya kweli. Ndiyo maana ukitumia ufahamu na kile ulichojifunza kumsoma Mungu, hutaweza kamwe kujua au kuelewa Mungu. Lakini ukitumia njia ya kutafuta ukweli na kumtafuta Mungu, na kumtazama Mungu kutokana na mtazamo wa kuanza kumjua Mungu, basi siku moja utakubali kwamba matendo na hekima ya Mungu viko kila mahali, na utajua pia hasa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote na chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kadiri unavyokuwa na maarifa kama hayo, ndivyo utakavyoelewa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote. Vitu vyote na kila kitu, pamoja na wewe, daima vinapokea mtiririko thabiti wa upeanaji wa Mungu. Utaweza pia kuhisi dhahiri kwamba katika ulimwengu huu, na miongoni mwa wanadamu hawa, hakuna yeyote isipokuwa Mungu anayeweza kuwa na nguvu kama hizo na kiini kama hicho kutawala, kusimamia, na kudumisha kuwepo kwa vitu vyote. Ukitimiza ufahamu kama huo, utakubali kwa kweli kwamba Mungu ni Mungu wako. Ukifikia kiwango hiki, umemkubali Mungu kwa kweli na kumruhusu awe Mungu wako na Bwana wako. Ukiwa na ufahamu kama huo na maisha yako yakifikia kiwango kama hicho, Mungu hatakujaribu na kukuhukumu tena, wala Hatakushurutisha ufanye mambo, kwa sababu unamfahamu Mungu, unajua moyo Wake, na umemkubali Mungu kwa kweli ndani ya moyo wako. Hii ni sababu muhimu ya kuwasilisha mada hizi kuhusu utawala na usimamizi wa Mungu juu ya vitu vyote. Ni kuwapa watu maarifa na ufahamu zaidi; sio tu kukufanya ukubali, lakini kukupa maarifa zaidi na ufahamu wa utendaji wa matendo ya Mungu.

Chakula na Kinywaji cha Kila Siku Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu

Tulikuwa tumezungumza sasa hivi kuhusu sehemu ya mazingira ya jumla, yaani, hali zilizo muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu ambazo Mungu aliwatayarishia wanadamu tangu Alipoumba ulimwengu. Tumezungumza sasa hivi kuhusu vitu vitano, na vitu hivi vitano ndivyo mazingira ya jumla. Tunachoenda kuzungumzia baada ya hapo kinahusiana kwa karibu na kila maisha ya wanadamu katika mwili. Ni hali muhimu inayolingana zaidi na inayokubaliana zaidi na maisha ya mtu katika mwili. Kitu hiki ni chakula. Mungu alimuumba mwanadamu na akamweka ndani ya mazingira ya kuishi yanayofaa. Baadaye, mwanadamu alihitaji chakula na maji. Mwanadamu alikuwa na hitaji hilo, hivyo Mungu alimtengenezea mwanadamu matayarisho hayo. Kwa hiyo, kila hatua ya kazi ya Mungu na kila kitu Anachofanya sio maneno matupu tu, lakini vinafanyika kwa kweli. Je, chakula ni kitu ambacho watu hawawezi kukosa kuwa nacho katika maisha yao? Chakula ni muhimu zaidi kuliko hewa? Vyote ni muhimu kwa njia sawa. Vyote ni hali na vitu muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu na kuhifadhi mwendelezo wa maisha ya binadamu. Hewa ni muhimu zaidi au maji ni muhimu zaidi? Halijoto ni muhimu zaidi au chakula ni muhimu zaidi? Vyote ni muhimu. Watu hawawezi kuchagua kwa sababu hawawezi kuishi bila chochote kati ya hivyo vyote. Hili ni tatizo halisi, si kitu unachoweza kuchagua. Hujui, lakini Mungu anajua. Unapokiona chakula, utahisi, “Siwezi kuishi bila chakula!” Lakini baada tu ya wewe kuumbwa, je, ulijua kwamba ulihitaji chakula? Hungejua, lakini Mungu anajua. Ni wakati tu unapokuwa na njaa na kuona kuna matunda juu ya miti na nafaka juu ya ardhi ili uweze kula ndipo unatambua unahitaji chakula. Wakati unahisi kiu, unaona chemchemi ya maji mbele yako, na ni wakati tu unapokunywa maji ndipo unagundua unayahitaji. Maji yalitayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Kuhusu chakula, haijalishi ikiwa wewe hula milo mitatu kwa siku, milo miwili kwa siku, au hata zaidi ya hiyo; kwa ufupi, chakula ni kitu ambacho wanadamu hawawezi kukosa kuwa nacho katika maisha yao ya kila siku. Ni mojawapo ya vitu muhimu vya kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa binadamu. Hivyo chakula hasa hutoka wapi? Kwanza, kinatoka ndani ya udongo. Udongo ulitayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Udongo unafaa kwa kuendelea kuishi kwa mimea mbalimbali, sio tu kwa ajili ya miti au nyasi. Mungu aliwatayarishia wanadamu mbegu za kila aina ya nafaka na vyakula mbalimbali, na Akawapa wanadamu udongo na ardhi vinavyofaa ili wapande, na wakiwa na vitu hivi, wanadamu hupata chakula. Kuna aina gani za chakula? Mnapaswa kulijua hili vizuri, sivyo? Kwanza, kuna aina mbalimbali za nafaka. Ni nini kinahusishwa katika nafaka. Ngano, mtama wa mkia wa mbweha, mtama wa proso, mchele…, inayokuwa na maganda. Mazao ya nafaka pia yametenganishwa katika aina nyingi mbalimbali. Kuna aina nyingi za mazao ya nafaka kutoka kusini mpaka kaskazini, kama vile shayiri, ngano, oti, na nafaka inayofanana na ngano. Aina mbalimbali zinafaa kukuzwa katika maeneo mbalimbali. Pia kuna aina mbalimbali za mchele. Kusini ina aina zake za mchele, iliyo ndefu zaidi na inawafaa watu kutoka kusini kwa sababu si ya kunata sana. Kwa vile hali ya nchi ni joto zaidi kusini, wanahitajika kula aina mbalimbali kama vile mchele wa indica. Hautakiwi kunata sana la sivyo hawataweza kula na watapoteza hamu yao ya kula. Mchele unaoliwa na watu wa kaskazini ni wa kunata zaidi. Kwa vile kaskazini huwa na baridi zaidi kila mara, wanahitajika kula mchele wa kunata zaidi. Kuongezea, kuna aina mbalimbali za maharagwe. Haya yanakuzwa juu ya ardhi. Pia kuna vile vinavyokuzwa chini ya ardhi, kama viazi, viazi vitamu, jimbi, na vinginevyo. Viazi huota kaskazini. Sifa ya viazi vya kaskazini ni nzuri sana. Watu wakikosa nafaka za kula, viazi vinaweza kuwa chakula kikuu cha mlo wao ili waweze kudumisha milo mitatu kwa siku. Viazi pia vinaweza kuwa ugavi wa chakula. Viazi vitamu si vizuri kama viazi kulingana na sifa, lakini bado vinaweza kutumiwa na watu kama chakula cha kudumisha milo yao mitatu kwa siku. Ikiwa nafaka hazipatikani, watu wanaweza kutumia viazi vitamu kujaza matumbo yao. Jimbi, ambalo mara nyingi huliwa na watu wa kusini, inaweza kutumiwa kwa njia hiyo, na pia inaweza kuwa chakula kikuu. Hizi ni aina mbalimbali za nafaka, muhimu kwa chakula cha watu cha kila siku. Watu hutumia nafaka mbalimbali kutengeneza nudo, mkate mdogo wa mviringo uliopikwa kwa mvuke, mchele, na nudo za mchele. Mungu ametoa aina hizi mbalimbali za nafaka kwa wanadamu kwa wingi. Kwa nini kuna aina nyingi sana? Makusudi ya Mungu yanaweza kupatikana humo: Kwa upande mmoja, ni kwa ajili ya kufaa aina mbalimbali za udongo na hali ya nchi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi; kwa upande mwingine, vijenzi na kadiri mbalimbali vya nafaka hizi vinakubaliana na vijenzi na kadiri mbalimbali vya mwili wa mwanadamu. Watu wanaweza tu kudumisha virutubishi na vijenzi mbalimbali vinavyohitajika kwa miili yao kwa kula nafaka hizi. Ingawa chakula cha kaskazini na chakula cha kusini ni tofauti, vina mifanano mingi kuliko tofauti. Vyakula hivi vyote vinaweza kuridhisha mahitaji ya kawaida ya mwili wa mwanadamu na vinaweza kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa mwanadamu. Hivyo, sababu ya aina zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali kuwa nyingi mno ni kwamba mwili wa mwanadamu unahitaji kinachotolewa na vyakula hivyo. Wanahitaji kinachotolewa na vyakula mbalimbali vinavyokuzwa kutoka kwa udongo ili kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa mwanadamu na kutimiza maisha ya kawaida ya mwanadamu. Kwa ufupi, Mungu aliwafikiria sana wanadamu. Vyakula mbalimbali ambavyo Mungu aliwapa watu si vya kuchosha—ni vyenye maarifa mengi mno. Ikiwa watu wanataka kula nafaka wanaweza kula nafaka. Watu wengine hawapendi kula nudo, wanataka kula wali, na kisha wanaweza kula wali. Kuna aina nyingi za mchele—mchele mrefu, mchele mfupi, na yote inaweza kuridhisha ladha walizo nazo watu. Kwa hiyo, watu wakila nafaka hizi—bora tu si wa kuchaguachagua kuhusu vyakula vyao—hawatakosa lishe na wanahakikishiwa kuishi kwa afya nzuri mpaka umri wa uzeeni. Hilo lilikuwa wazo la asili ambalo Mungu alikuwa nalo akilini Alipowapa wanadamu chakula. Mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi bila vitu hivi—je, hiyo si kweli? Wanadamu hawawezi kutatua matatizo haya halisi, lakini Mungu alikuwa tayari ametayarisha na kulifikiria kabisa. Mungu alikuwa amewatayarishia wanadamu vitu zamani sana.

Mungu amempa mwanadamu zaidi ya vitu hivi tu—pia kuna mboga. Unapokula mchele, ikiwa mchele ndio kila kitu unachokula, huenda ukakosa lishe. Ikiwa kisha utakaanga kwa mafuta kidogo vyakula kadhaa kiasi kidogokidogo au uchanganye kachumbari ya kula na mlo huo, basi vitamini katika mboga hizo na kiasi kidogo cha vitu vya msingi au lishe zingine vitaweza kupeana mahitaji ya mwili wa mwanadamu kwa njia ya kawaida sana. Wakati watu hawali vyakula vikuu wanaweza pia kula matunda, sivyo? Wakati mwingine, watu wanapohitaji uowevu au lishe zingine au ladha tofauti, pia kuna mboga na matunda ya kuwapa vitu hivyo. Kwa vile udongo na hali ya nchi ya kaskazini, kusini, mashariki na magharibi ni tofauti, pia kuna aina mbalimbali za mboga na matunda. Kwa vile hali ya nchi ya kusini ni joto sana, matunda mengi na mboga ni vya aina ya kufanywa baridi vinavyoweza kusawazisha baridi na joto ndani ya miili ya watu wanapokula vitu hivyo. Kwa upande mwingine, kuna aina chache ya mboga na matunda kaskazini, lakini hata hivyo vinatosha kwa watu wa kaskazini kufurahia. Kwa hali yoyote, kwa sababu ya ustawi wa kijamii katika miaka ya hivi karibuni, kwa sababu ya kile kinachoitwa maendeleo ya kijamii, na vilevile maendeleo katika usafiri na mawasiliano vinavyounganisha kaskazini na kusini na mashariki na magharibi, watu walio kaskazini wanaweza pia kula baadhi ya matunda ya kusini na mboga, au bidhaa za mikoa kutoka kusini, hata katika mwaka mzima. Kwa njia hiyo, hata kama watu wanaweza kuridhisha hamu yao ya chakula na matamanio ya vitu vya mwili, miili yao bila kujua inapatwa na viwango mbalimbali vya madhara. Hii ni kwa sababu miongoni mwa vyakula ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu, kuna vyakula na matunda na mboga vinavyofaa watu walio kusini, na vilevile vyakula na matunda na mboga vinavyofaa watu walio kaskazini. Yaani, ikiwa ulizaliwa kusini, kula vitu kutoka kusini kunakufaa wewe sana. Mungu alitayarisha vyakula hivi na matunda na mboga kwa sababu kusini ina hali ya nchi mahsusi. Kaskazini ina vyakula vinavyohitajika kwa miili ya watu walio kaskazini. Lakini kwa vile watu wana hamu ya chakula ya ulafi, wamefagiliwa bila kujua katika mkondo wa maendeleo ya kijamii, na kuwafanya kukiuka sheria hizi bila kujua. Ingawa watu wanahisi kwamba maisha yao sasa ni bora zaidi, maendeleo ya kijamii kama hayo huleta madhara ya kufichika kwa miili ya watu wengi zaidi. Hiki si kile ambacho Mungu anataka kuona na vile vile si kile ambacho Mungu alikusudia alipompatia mwanadamu vyakula hivi, matunda na mboga. Wanadamu wenyewe wamesababisha hali ya sasa kwa kukiuka sheria ambazo Mungu aliweka.

Kuongezea, kile ambacho Mungu aliwapa wanadamu ni cha fahari na kingi, kila sehemu ikiwa na vitu maalum vya mahali maalum. Kwa mfano, sehemu nyingine zina utajiri wa tende nyekundu (zinazojulikana kwa kawaida kama jujubes), ilhali zingine zina utajiri wa jozi, na zingine zina utajiri kwa karanga, au aina zingine za njugu. Vitu hivi yakinifu vyote vinampa lishe inayohitajika na mwili wa mwanadamu. Lakini Mungu huwapa wanadamu vitu kulingana na misimu na wakati, na pia anawapa kiasi sahihi kwa wakati sahihi. Wanadamu hutamani kujifurahisha kwa kimwili na ni walafi, hiyo inafanya kuwa rahisi kukiuka na kuharibu sheria za kawaida za ukuaji wa mwanadamu tangu Alipowaumba wanadamu. Kama mfano, hebu tutazame matunda ya cheri, ambazo kila mtu anapaswa kuzijua, sivyo? Hizo huiva karibu Juni. Kwa kawaida, hizo huisha kabla ya Agosti. Cheri huwa mbichi kwa miezi miwili pekee, lakini kupitia mbinu za kisayansi watu sasa wanaweza kurefusha muda huo mpaka miezi 12, hata mpaka msimu wa cheri wa mwaka unaofuata. Hiyo inamaanisha cheri zipo kwa mwaka mzima. Je, jambo hili ni la kawaida? (La.) Basi msimu bora zaidi wa kula cheri ni upi? Ni kipindi cha kuanzia Juni mpaka Agosti. Zaidi ya kikomo hiki, haijalishi utaziweka mbichi vipi, hazitakuwa na ladha sawa, wala sio kile ambacho mwili wa mwanadamu unahitaji. Mara tu tarehe ya kuisha kutumika inapopita, haijalishi ni vitu vipi vya kemikali unatumia, hutaweza kuzifanya ziwe kama zinavyokuwa wakati zinakuzwa kwa kawaida. Zaidi, madhara ambayo kemikali huleta kwa wanadamu ni kitu ambacho hakuna anayeweza kufanya chochote kuyaondoa au kuyabadilisha. Basi, ni nini ambacho soko la uchumi la wakati huu linawaletea watu? Maisha ya watu yanaonekana kuwa mazuri zaidi, usafiri katika pande zote umekuwa wa kufikika kwa urahisi sana, na watu wanaweza kula aina zote za matunda katika msimu wowote kati ya misimu minne ya mwaka. Watu wa kaskazini mara kwa mara huweza kula ndizi na chakula chochote, vitu maalum vya mahali maalum au matunda kutoka kusini. Lakini haya si maisha ambayo Mungu anataka kuwapa wanadamu. Soko hili la uchumi huleta manufaa fulani kwa maisha ya wanadamu lakini pia linaweza kuleta madhara. Kwa sababu ya wingi wa vyakula sokoni, watu wengi hula chochote, wao hula bika kufikiria. Jambo hili hukiuka sheria za asili na lina madhara kwa afya yao. Hivyo, soko la uchumi haliwezi kuletea watu furaha ya kweli. Jioneenini wenyewe. Zabibu haziuzwi sokoni katika misimu yote mine? Kwa kweli, zabibu huwa mbichi tu kwa muda wa kipindi kifupi sana baada ya kuchumwa. Ukiziweka mpaka Juni inayofuata, bado zinaweza kuitwa zabibu? Je, unaweza kuziita takataka? Hazitakosa tu vijenzi vya asili vya zabibu, lakini pia zina kemikali zaidi juu yake. Baada ya mwaka mmoja, hazijapoteza tu ubichi wake, lakini pia lishe zake zimepotea kitambo. Watu wanapokula zabibu, wanahisi: “Ninafurahi sana! Je, tungeweza kula zabibu wakati wa msimu huu miaka 30 iliyopita? Hungeweza kuzila hata kama ungetaka. Maisha ni mazuri jinsi gani wakati huu!” Je, hii ni furaha kweli? Ukipenda, unaweza kwenda kusoma juu ya zabibu zilizohifadhiwa kwa kemikali na uone hasa vijenzi vyake ni vipi na iwapo vijenzi hivi vinaweza kuleta manufaa yoyote kwa wanadamu. Katika Enzi ya Sheria. Waisraeli walipokuwa njiani baada ya kuondoka Misri, Mungu aliwapa kware na mana. Je, Mungu aliwaruhusu watu kuvihifadhi? Wengine wao hawakufikiria mambo ya wakati ujao na waliogopa kwamba hakungekuwa na zaidi siku iliyofuata, hivyo walihifadhi nyingine iwapo wangehitaji baadaye. Kisha nini kilifanyika? Kufikia siku iliyofuata ilikuwa imeoza. Mungu hakuwaruhusu kuweka nyingine kama akiba kwa sababu Mungu alikuwa amefanya matayarisho fulani, yaliyohakikisha hawangekufa kwa njaa. Wanadamu hawana hakika hiyo, wala hawana imani ya kweli kwa Mungu. Kila mara wanaweka nyengine kando kwa ajili ya baadaye na hawawezi kamwe kuona utunzi wote na mawazo yaliyo ndani ya kile ambacho Mungu amewatayarishia wanadamu. Kila mara hawawezi kuhisi hasa, kila mara wanakosa kumwamini Mungu, kila mara wanafikiria: “Matendo ya Mungu si ya kutegemewa! Nani anajua iwapo Mungu atawapa wanadamu au ni lini Atawapa! Ikiwa nina njaa sana na Mungu hanipi, basi si nitakufa njaa? Si nitakosa lishe?” Ona jinsi hakika ya mwanadamu ni ndogo sana!

Nafaka, matunda na mboga, na kila aina ya njugu vyote ni vyakula vya wala mboga. Hata kama ni vyakula vya wala mboga, vina lishe za kutosha kuridhisha mahitaji ya mwili wa mwanadamu. Kwa hali yoyote, Mungu hakusema: “Kuwapa wanadamu hiki kunatosha. Wanadamu wanaweza tu kula vitu hivi.” Mungu hakuachia hapo na badala yake aliwatayarishia wanadamu vitu vyenye ladha nzuri zaidi. Vitu hivi ni gani? Ni aina mbalimbali ya nyama na samaki wengi wenu mnaweza kuona na kula kila siku. Kuna aina nyingi sana za nyama na samaki ambazo Mungu amemtayarishia mwanadamu. Samaki wote huishi majini; umbile asili la nyama yao ni tofauti na la nyama inayokuzwa juu ya ardhi na wanaweza kuwapa wanadamu lishe mbalimbali. Sifa za samaki zinaweza kubadilisha baridi na joto ndani ya mwili wa mwanadamu, kwa hiyo ni za manufaa makubwa sana kwa wanadamu. Lakini kilicho na ladha nzuri hakitakiwi kuliwa zaidi. Bado msemo ni huo huo: Mungu huwapa wanadamu kiasi sahihi kwa wakati sahihi, ili watu waweze kufurahia kwa kawaida na vizuri vitu hivi kulingana na msimu na wakati. Ndege wa kufugwa wanahusisha nini? Kuku, kware, njiwa, n.k. Watu wengi hula pia bata na bata bukini. Ingawa Mungu alitayarisha aina hizi za nyama, Alitoa masharti fulani kwa watu Wake aliowachagua na kuweka mipaka maalum kwa chakula chao wakati wa Enzi ya Sheria. Sasa eneo hili linatojkana na kupendelea kwa mtu binafsi na ufahamu wa mtu binafsi. Aina hizi mbalimbali za nyama hupatia mwili wa mwanadamu lishe mbalimbali, zinazoweza kusheheneza protini na madini ya chuma, kusitawisha damu, kuimarisha misuli na mifupa, na kupeana nguvu zaidi. Haijalishi ni mbinu gani watu hutumia kupika na kula vitu hivyo, kwa ufupi, vitu hivi vinaweza kwa upande mmoja kuwasaidia watu kuendeleza ladha na hamu ya chakula, na kwa upande mwingine kuridhisha matumbo yao. Kitu cha muhimu zaidi ni kwamba zinaweza kupatia mwili wa mwanadamu mahitaji yao ya lishe ya kila siku. Hizi ndizo fikira ambazo Mungu alikuwa nazo Alipowatayarishia wanadamu chakula. Kuna vyakula vya wala mboga na pia nyama—je, hiyo si ya fahari na nyingi? Lakini watu wanapaswa kuelewa kusudi la asili la Mungu lilikuwa gani Mungu alipowatayarishia wanadamu vyakula vyote. Je, ilikuwa ni kuwafanya wanadamu kutumia kupita kiasi hivi vyakula? Nini hutendeka wakati mtu hunaswa kwa kujaribu kuridhisha tamaa hizi za vitu? Je, hapati lishe ya kupita kiasi? Je, lishe ya kupita kiasi haidhuru mwili wa mwanadamu kwa njia nyingi? (Ndiyo.) Hiyo ndiyo maana Mungu hutoa kiasi sahihi kwa wakati sahihi na kuwaacha watu wafurahie vyakula mbalimbali kulingana na vipindi vya wakati na misimu. Kwa mfano, baada ya kuishi katika majira ya joto sana, watu watakusanya kiasi fulani cha joto, la kusababisha ukavu wa viini na unyevunyevu katika miili yao. Majira ya kupukutika kwa majani yakija, matunda ya aina nyingi sana yataiva, na watu watakapokula baadhi ya tunda unyevunyevu wao utaondolewa. Wakati huo huo, ng’ombe na kondoo watakuwa wamekua na kupata nguvu, ili watu wale nyama kiasi kama lishe. Baada ya kula aina mbalimbali za nyama, miili ya watu itakuwa na nguvu na joto la kuisaidia kustahimili baridi ya majira ya baridi, na kutokana na hayo wataweza kupita katika majira ya baridi kwa amani. Wakati upi wa kutayarisha vitu vipi kwa ajili ya wanadamu, na wakati upi wa kuacha vitu vipi vikue, vizae matunda na kuiva—yote haya yanadhibitiwa na kupangwa na Mungu kwa kupimwa kabisa. Hii ni mada kuhusu “jinsi Mungu alitayarisha chakula kilicho muhimu kwa maisha ya mwanadamu ya kila siku.” Mbali na aina zote za chakula, Mungu pia huwapa wanadamu vyanzo vya maji. Watu huhitaji kunywa maji kiasi baada ya kula. Je, kula matunda tu kunatosha? Watu hawataweza kustahimili kula matunda pekee, licha ya hayo, huwa hakuna matunda katika misimu mingine. Hivyo tatizo la wanadamu la maji litawezaje kutatuliwa? Kwa Mungu kutayarisha vyanzo vingi vya maji juu ya ardhi na chini ya ardhi, ikiwemo maziwa, mito, na chemchemi. Vyanzo hivi vya maji vinaweza kunywewa maji katika hali ambazo hakuna kuchafuliwa kokote, au maendeleo ya wanadamu au uharibifu. Yaani, kuhusu vyanzo vya chakula kwa maisha ya miili ya wanadamu, Mungu amefanya matayarisho sahihi sana, yasiyo na hitilafu yoyote na ya kufaa sana, ili maisha ya watu yawe ya fahari na yenye wingi na yasiyokosa chochote. Hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kuhisi na kuona.

Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote Mungu aliumba baadhi ya mimea, wanyama, na mitishamba mbalimbali ambayo hususan hukusudiwa kuponya majeraha ama kutibu magonjwa katika mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka au kuungua kiajali na maji moto? Je, unaweza kufoka kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote. Kuna mimea inayoendeleza mzunguko wa damu kuondoa ukwamaji, kutuliza maumivu, kukomesha kutokwa na damu, kutia ganzi, kuwasaidia watu kupata tena ngozi ya kawaida, kuondoa ukwamaji wa damu mwilini, na kuondoa sumu mwilini. Kwa ufupi, yote inaweza kutumiwa katika maisha ya kila siku. Ni ya kufaa watu na imetayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwili wa mwanadamu iwapo inahitajika. Baadhi ya hiyo iliruhusiwa na Mungu kugunduliwa bila uangalifu na mwanadamu, ilhali mingine iligunduliwa na watu ambao Mungu aliwachagua kufanya hivyo, ama kama matokeo ya matukio maalum Aliyoyapanga. Baada ya ugunduzi wao, wanadamu wangeipitisha kwa wengine, na halafu watu wengi wangejua kuihusu. Kwa njia hii, uumbaji wa Mungu wa mimea hii unakuwa na thamani na maana. Kwa ufupi, vitu hivi vyote vinatoka kwa Mungu na vilitayarishwa na kupandwa Alipowaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Vitu hivi vyote ni muhimu sana. Je, fikira Zake Mungu zilifikiriwa vizuri sana kuliko za wanadamu? Unapoona yote ambayo Mungu amefanya, unaweza kuhisi upande wa Mungu wa vitendo? Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi kwa furaha katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote. Wanadamu wanaendelea kuzaa na kuendelea kuishi katika mazingira hayo.

Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hapana shaka juu ya hili! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingeweza kutangulia? Kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Baada ya siku 21, kuku huangua na huyo kuku hutaga mayai zaidi, na kuku zaidi huangualiwa kutoka kwa hayo mayai. Hivyo kuku alitangulia au yai lilitangulia? Mnajibu “kuku” kwa uhakika. Kwa nini? (Biblia inasema Mungu aliumba ndege na wanyama wa mwitu.) Hiyo ina msingi katika Biblia. Ninataka mzungumze kuhusu maarifa yenu wenyewe kuona iwapo mna maarifa ya kweli ya matendo ya Mungu. Je, mna hakika kuhusu jibu lenu au la? (Mungu aliumba kuku, halafu akampa uwezo wa kuzaa, yaaniuwezo wa kuatamiza mayai) Maelezo haya yanakaribia kuwa sahihi. Kuku alikuwa wa kwanza, na kisha yai. Huo ndio utaratibu. Kuku alitangulia. Hili ni hakika. Si fumbo la maana sana, lakini watu wa dunia huliona kuwa la maana sana na hutumia falsafa kwa utoaji hoja. Mwishowe, bado huwa hawana hitimisho. Jambo hili ni kama wakati watu hawajui kwamba Mungu aliwaumba. Hawajui kanuni hii muhimu, wala hawana uhakika kuhusu iwapo yai au kuku anapaswa kutangulia. Hawajui ni nini kinapaswa kutangulia, hivyo kila mara wao hushindwa kupata jibu. Ni kawaida kabisa kwamba kuku alitangulia. Ikiwa yai lingetangulia kabla ya kuku, basi hiyo haingekuwa kawaida! Bila shaka kuku alitangulia. Hiki ni kitu rahisi sana. Hakiwahitaji nyinyi kuwa wenye maarifa mengi. Mungu aliumba hivi vyote. Kusudi Lake la mwanzo lilikuwa ni mwanadamu kuvifurahia. Kuku akiwepo, yai linakuja kwa kawaida. Je, hili si suluhisho rahisi? Ikiwa yai lingeumbwa kwanza, je, bado halingehitaji kuku kuliatamiza? Kuumba kuku moja kwa moja ni suluhisho rahisi zaidi. Kwa njia hii, kuku angezaa mayai na kuatamiza vifaranga walio ndani, na watu wangeweza kuwa na kuku wa kula. Jambo la kufaa kweli! Vile Mungu afanyavyo mambo ni kwa maneno machache ya wazi na sio kwa usumbufu. Yai linatoka wapi? Linatoka kwa kuku. Hakuna yai bila kuku. Alichoumba Mungu ni kiumbe chenye uhai! Wanadamu ni wa upuuzi na wa dhihaka, kila mara wanajitatanisha katika mambo haya rahisi, na mwishowe hata wanafikia kifungu kizima cha hoja za uwongo. Hayo ni ya kitoto! Uhusiano kati ya yai na kuku ni dhahiri: Kuku alitangulia. Hayo ndiyo maelezo sahihi kabisa, njia sahihi kabisa ya kulielewa, na jibu sahihi kabisa. Hii ni ya kweli.

Tumetoka kuzungumzia nini? Hapo mwanzo, tulizungumza kuhusu mazingira ya kuishi ya wanadamu na kile Mungu alifanya, alitayarisha, na kushughulikia kwa ajili ya mazingira haya, na vilevile mahusiano kati ya vitu vyote ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu na jinsi Mungu alishughulikia mahusiano haya yote kuzuia vitu vyote kuleta madhara kwa wanadamu. Mungu pia alitatua athari hasi katika mazingira ya wanadamu zilizosababishwa na vitu mbalimbali vya asili ambavyo vinaletwa na mambo yote, Akaruhusu vitu vyote kuongeza hadi upeo shughuli za vitu hivyo, na Akawaletea wanadamu mazingira ya kufaa na vitu vyote vya asili vyenye manufaa, kuwawezesha wanadamu kuwa wepesi kubadilika kwa mazingira hayo na kuendelea na mfuatano wa kuzaa na wa maisha kwa kawaida. Kilichofuata kilikuwa chakula kilichohitajika na mwili wa mwanadamu—chakula cha kila siku na kinywaji. Hii pia ni hali muhimu ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Hiyo ni kusema, mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi tu kwa kupumua, kuwa na mwangaza wa jua au upepo pekee, au halijoto za kufaa tu. Wanahitaji pia kujaza matumbo yao. Vitu hivi vya kujaza matumbo yao vyote vimetayarishwa pia na Mungu kwa ajili ya wanadamu—hiki ni chanzo cha chakula cha wanadamu. Baada ya kuona mazao haya ya fahari na mengi—vyanzo vya chakula cha wanadamu na kinywaji—unaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha kupeana wanadamu na vitu vyote? Ikiwa Mungu angeumba tu miti na nyasi au hata viumbe mbalimbali vyenye uhai Alipoumba vitu vyote, ikiwa hivyo viumbe mbalimbali vyenye uhai vyote vingekuwa vya ng’ombe na kondoo kula, au vingekuwa vya pundamilia, paa na aina nyingine mbalimbali za wanyama,kwa mfano, simba walipaswa kula vitu kama pundamilia na paa, na chui wakubwa wenye milia walipaswa kula vitu kama kondoo na nguruwe—lakini kusiwe na hata kitu kimoja cha kufaa wanadamu kula, je, hilo lingefaulu? Halingefaulu. Wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi. Na je, wanadamu wangekula tu majani ya miti? Hilo lingefaulu? Wanadamu wangeweza kula nyasi ambayo kondoo hutayarishiwa? Huenda ikawa sawa wakijaribu kidogo tu, lakini wakiendelea kula kwa muda mrefu, matumbo ya wanadamu hayataweza kustahimili tena na hawatadumu kwa muda mrefu. Na hata kuna vitu vingine ambavyo vinaweza kuliwa na wanyama, lakini wanadamu wakivila watapata sumu. Kuna vitu vingine vyenye sumu ambavyo wanyama wanaweza kuvila bila kuathiriwa, lakini wanadamu hawawezi kufanya vivyo hivyo. Kwa maneno mengine, Mungu aliwaumba wanadamu, hivyo Mungu anajua vizuri sana kanuni na muundo wa mwili wa mwanadamu na wanachohitaji wanadamu. Mungu ana hakika kamili kuhusu sehemu na vijenzi vyake, na inachohitaji, vilevile jinsi sehemu za ndani ya mwili wa mwanadamu hufanya kazi, hufyonza, huondosha, na kuvunjavunja kemikali mwilini. Watu hawana hakika kuhusu hili na wakati mwingine hula na kujaliza bila kujua. Wao hujaliza kupita kiasi na mwisho husababisha kutolingana nguvu. Ukila na kufurahia vitu hivi alivyokutayarishia Mungu kwa kawaida, hutakuwa na shida yoyote. Hata kama wakati mwingine una hali mbaya ya moyo na una ukwamaji wa damu, haidhuru. Unahitaji tu kula aina fulani ya mmea na ukwamaji utatatuliwa. Mungu ametayarisha vitu hivi vyote. Kwa hivyo, machoni mwa Mungu, wanadamu wako juu zaidi ya kiumbe chochote kingine chenye uhai. Mungu alitayarishia kila aina ya mimea mazingira ya kuishi na Akatayarishia kila aina ya wanyama chakula na mazingira ya kuishi, lakini mahitaji ya wanadamu pekee kwa mazingira yao ya kuishi ndiyo makali zaidi na yasiyostahamili kutotunzwa. La sivyo, wanadamu hawangeweza kuendelea kukua na kuzaa na kuishi kwa kawaida. Mungu anajua hili vizuri zaidi moyoni Mwake. Mungu alipofanya hili, alilipa umuhimu zaidi kuliko kitu chengine chochote. Labda huwezi kuhisi umuhimu wa kitu fulani kisicho na maana unachokiona na kufurahia au kitu unachohisi ulizaliwa nacho na unaweza kufurahia, ilhali kisiri, au pengine muda mrefu uliopita, Mungu alikuwa tayari amekutayarishia hekima Yake. Mungu ameondoa na kutatua kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo vipengele vyote hasi visivyofaa kwa wanadamu na vinavyoweza kudhuru mwili wa mwanadamu. Nini ambacho hiki kinaweka wazi? Je, kinahakikisha mtazamo wa Mungu kwa wanadamu Alipowaumba wakati huu? Mtazamo huo ulikuwa upi? Mtazamo wa Mungu ulikuwa wa msimamo na maana kubwa, na Hakustahimili kuingilia kati kwa vipengele au hali au nguvu zozote za adui isipokuwa Mungu. Kutokana na hili, unaweza kuona mtazamo wa Mungu alipoumba wanadamu na katika usimamizi Wake wa wanadamu wakati huu. Mtazamo wa Mungu ni upi? Kupitia kwa mazingira ya kuishi na kuendelea kuishi ambayo wanadamu wanafurahia pamoja na chakula chao cha kila siku na kinywaji na mahitaji ya kila siku, tunaweza kuona mtazamo wa Mungu wa wajibu kwao wanadamu ambao Anao tangu Awaumbe, na vilevile uamuzi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu wakati huu. Je, tunaweza kuona uhalisi wa Mungu kupitia kwa haya yote? Tunaweza kuona ustaajabishaji wa Mungu? Tunaweza kuona kutoweza kueleweka kwa Mungu? Tunaweza kuona kudura ya Mungu? Mungu anatumia tu njia Zake za uweza na hekima kuwapa wanadamu wote, na vilevile kuvipa vitu vyote. Licha ya hayo, baada ya Mimi kusema mengi sana, mnaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Hili ni hakika. Je, mna shaka yoyote? (La.) Upeanaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa kutosha kuonyesha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, kwa sababu Yeye ni chanzo cha ruzuku ambao umewezesha vitu vyote kuwepo, kuishi, kuzaa, na kuendelea, na hakuna chanzo kingine ila Mungu Mwenyewe. Mungu huruzuku mahitaji yote ya vitu vyote na mahitaji yote ya wanadamu, bila kujali iwapo ni mazingira ya msingi kabisa ya watu kuishi, wanachohitaji watu kila siku, au upeanaji wa ukweli kwa roho za watu. Katika kila namna, utambulisho wa Mungu na hadhi Yake ni vyenye umuhimu mkubwa kwa Mungu; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Yaani, Mungu ni Mtawala, Bwana, na mwenye kukimu dunia hii, dunia hii ambayo watu wanaweza kuiona na kuihisi. Kwa wanadamu, je, huu si utambulisho wa Mungu? Hii ni kweli kabisa. Hivyo unapoona ndege wakiruka angani, unapaswa kujua kwamba Mungu aliumba vitu vinavyoweza kuruka. Lakini kuna viumbe vyenye uhai vinavyoogelea majini, navyo pia huendelea kuishi kwa njia mbalimbali. Miti na mimea inayoishi ndani ya udongo huchipuka katika majira ya kuchipuka na huzaa matunda na kupoteza majani katika majira ya kupukutika kwa majani, na ifikapo wakati wa majira ya baridi majani yote huwa yameanguka na kupitia katika majira ya baridi. Hiyo ni njia yao ya kuendelea kuishi. Mungu aliumba vitu vyote, na kila kimojawapo huishi kupitia taratibu mbalimbali na njia mbalimbali na hutumia mbinu mbalimbali kuonyesha nguvu zake na taratibu ya maisha. Haijalishi ni mbinu gani, yote iko chini ya utawala wa Mungu. Ni nini kusudi la Mungu la kutawala taratibu zote mbalimbali za maisha na viumbe vyenye uhai? Je, ni kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu? Anadhibiti sheria zote za maisha kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hii inaonyesha hasa vile kuendelea kuishi kwa wanadamu ni muhimu kwa Mungu.

Wanadamu kuweza kuendelea kuishi na kuzaa kwa kawaida ni jambo la muhimu zaidi kwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu daima huwapa wanadamu na vitu vyote. Anapeana vitu vyote kwa njia mbalimbali, na chini ya hali za kudumisha kuendelea kuishi kwa vitu vyote, Anawawezesha wanadamu kuendelea kusonga mbele ili Aweze kudumisha kuwepo kwa kawaida kwa wanadamu. Hivi ndivyo vipengele viwili tunavyowasiliana leo. Vipengele hivi ni vipi? (Kutokana na mtazamo mkubwa, Mungu aliwaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Hicho ni kipengele cha kwanza. Pia, Mungu alitayarisha hivi vitu yakinifu ambavyo wanadamu wanahitaji na wanaweza kuona na kugusa.) Tumewasilisha mada yetu kuu kupitia vipengele hivi viwili. Mada yetu kuu ni gani? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Mnapaswa sasa kuwa na ufahamu fulani wa mbona Niliwasilisha maudhui haya chini ya mada hii. Je, kumekuwa na majadiliano yoyote yasiyohusiana na mada kuu? Hakuna, sivyo? Labda baada ya kusikia mambo haya, wengine wenu hupata ufahamu fulani na kuhisi kwamba maneno haya ni muhimu sana, lakini wengine huenda wakapata tu ufahamu kidogo wa kawaida na kuhisi kwamba maneno haya hayana maana. Haijalishi vile nyinyi mnaelewa hili wakati huu, mnapoendelea kupitia matukio itafika siku ambayo ufahamu wenu utafikia kiwango fulani, yaani, wakati maarifa yenu ya matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe yatafikia kiwango fulani, mtatumia maneno yenu wenyewe ya kiutendaji kuwasilisha ushuhuda wa maana na wa kweli kuhusu matendo ya Mungu.

Ninafikiri ufahamu wenu sasa bado ni sahili na wa kawaida, lakini mnaweza angaa, baada ya kunisikiliza Nikiwasilisha vipengele hivi viwili, kutambua ni mbinu zipi Mungu hutumia kuwapa wanadamu au ni vitu vipi Mungu huwapa wanadamu? Je, mna wazo la msingi na vilevile ufahamu wa msingi? (Ndiyo.) Lakini vipengele hivi viwili Nilivyowasilisha vinahusiana na Biblia? Vinahusiana na hukumu na kuadibu kwa Mungu katika Enzi ya Ufalme? (La.) Basi kwa nini Niliwasilisha vipengele hivi? Je, ni kwa sababu watu ni lazima wavielewe ili kumjua Mungu? (Ndiyo.) Ni muhimu sana kuvijua na pia ni muhimu sana kuvielewa. Usizuiwe tu kwa Biblia, na usizuiwe tu kwa Mungu kuhukumu na kuadibu wanadamu ili kuelewa kila kitu kuhusu Mungu. Ni nini kusudi la Mimi kusema hili? Ni ili kuwafanya watu wajue kwamba Mungu si Mungu wa watu Wake wateule pekee. Wewe sasa unamfuata Mungu, na Yeye ni Mungu wako, lakini kwa wale walio nje ya watu wanaomfuata Mungu, je, Mungu ni Mungu wao? Je, Mungu ni Mungu wa watu wote walio nje ya wale wanaomfuata Yeye? Mungu ni Mungu wa vitu vyote? (Ndiyo.) Basi Mungu hutenda kazi Yake na kutekeleza matendo Yake kwa wale tu wanaomfuata Yeye? (La.) Mawanda ya kazi Yake na matendo Yake ni yapi? Kwa kiwango kidogo zaidi, mawanada ya kazi Yake na matendo Yake yanajumuisha wanadamu wote na vitu vyote vya uumbaji. Kwa kiwango cha juu inajumuisha ulimwengu wote ambao watu hawawezi kuuona. Hivyo tunaweza kusema kwamba Mungu hufanya kazi Yake na kutekeleza matendo Yake miongoni mwa wanadamu wote. Hili ni la kutosha kuwafanya watu wajue yote kuhusu Mungu Mwenyewe. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Wewe unamwona Mungu kitu kidogo Ni jinsi gani kufanya hivyo kungeathiri watu? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako wa Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kupeana vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na upeanaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote. Vitu vyote viko chini ya mamlaka ya sheria zao, ambazo ziko chini ya utawala wa Mungu, na vitu vyote vina sheria zao za kuendelea kuishi, ambazo pia ziko chini ya utawala wa Mungu, huku majaliwa ya wanadamu na wanachohitaji pia vikihusiana kwa karibu na utawala wa Mungu na upeanaji Wake. Ndiyo maana, chini ya utawala wa Mungu na uongozi, wanadamu na vitu vyote vinahusiana, vinategemeana, na vinafumana. Hili ni kusudi na thamani ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote.

Februari 2, 2014

Iliyotangulia: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Inayofuata: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp