Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)

Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, katika sehemu ya kwanza, tulijadili mamlaka ya Mungu. Katika sehemu ya pili, tulijadili tabia ya haki ya Mungu. Na tulijadili utakatifu wa Mungu katika sehemu ya tatu. Maudhui mahususi tuliyojadili kila mara yamewacha wazo kwako? Katika sehemu ya kwanza “mamlaka ya Mungu,” kitu kipi kimeacha wazo la kina sana kwako, ni sehemu gani imekuwa na matokeo makubwa kwako? (Mungu kwanza alizungumza juu ya mamlaka na nguvu ya neno la Mungu; Mungu ni mwema kama neno Lake na neno Lake litakuwa kweli. Hiki ndicho kiini cha asili cha Mungu.) (Maagizo ya Mungu kwa Shetani kwamba anaweza kumjaribu Ayubu, lakini hawezi kuchukua uhai wake. Kutokana na hili tunayaona mamlaka ya neno la Mungu.) Je, kuna kitu kingine cha kuongeza? (Mungu alitumia maneno kuumba mbingu na nchi na vitu vyote ndani yake, na anazungumza kuweka agano na mwanadamu na kuweka baraka Zake juu ya mwanadamu. Hii yote ni mifano ya mamlaka ya neno la Mungu. Kando na hayo, tunaona pale ambapo Bwana Yesu alimwamuru Lazaro kutoka kaburini kwamba uhai na kifo vipo chini ya udhibiti wa Mungu, ambavyo Shetani hana uwezo wa kudhibiti na kwamba haijalishi kazi ya Mungu inafanyika katika mwili au katika Roho, mamlaka Yake ni ya pekee.) Huu ni uelewa mlioupata baada ya kusikia ushiriki, sio? Tunapozungumza kuhusu mamlaka ya Mungu, mnaelewa nini kuhusu neno “mamlaka”? Ndani ya mawanda ya mamlaka ya Mungu, katika kile ambacho Mungu anafanya na kufichua, watu wanaona nini? (Tunauona ukuu na hekima ya Mungu.) (Tunaona kwamba mamlaka ya Mungu yapo siku zote na kwamba kweli, kweli yapo. Tunayaona mamlaka ya Mungu kwa upana kwenye utawala Wake juu ya mbingu, na tunayaona kwa ufinyu kadri anavyodhibiti maisha ya binadamu. Mungu kweli anapanga na kudhibiti awamu zile sita za maisha. Aidha, tunaona kwamba mamlaka ya Mungu yanamwakilisha Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, na hakuna viumbe vilivyoumbwa au ambavyo havijaumbwa vinaweza kuwa nayo. Mamlaka ya Mungu ni alama ya hadhi Yake.) “Alama za hadhi ya Mungu na nafasi ya Mungu,” mnaonekana kuwa na uelewa wa kimafundisho wa maneno haya. Je, mna ufahamu wowote wa maana kuhusu mamlaka ya Mungu? (Mungu ametuangalia na kutulinda tangu tukiwa wadogo, na tunayaona mamlaka ya Mungu katika hilo. Hatukujua kuhusu hatari zilizotupata, lakini Mungu siku zote alikuwa anatulinda kisiri; haya pia ni mamlaka ya Mungu.) Vizuri sana, imesemwa vyema.

Tunapozungumza kuhusu mamlaka ya Mungu, mkazo upo wapi, hoja kuu? Kwa nini tunahitaji kujadili maudhui haya? Kwanza, madhumuni ya kujadili maudhui haya ni kwa watu kuthibitisha hadhi ya Mungu kama Muumba na nafasi Yake miongoni mwa vitu vyote; hili ni jambo wanaweza kuelewa, jambo wanaloweza kuona na kuhisi. Kile unachokiona na kukihisi yote yanatokana na matendo ya Mungu, maneno ya Mungu na udhibiti wa Mungu wa ulimwengu. Hivyo, watu hupata ufahamu upi wa kweli kupitia yote wanayoona, kujifunza, na kujua kupitia mamlaka ya Mungu? Hili ndilo jambo la kwanza, ambalo tayari tumejadili. Pili, watu wanapoona yote ambayo Mungu amefanya na kusema na kuyadhibiti kupitia mamlaka Yake. Ni ili kukuruhusu uone jinsi Mungu alivyo mwenye nguvu na mwenye hekima katika kudhibiti Kwake kila kitu. Je, hili halikuwa lengo na hoja kuu ya mazungumzo yetu ya awali ya mamlaka ya pekee ya Mungu? Sio muda mrefu umepita na baadhi ya watu tayari wameshasahau hili, kitu kinachothibitisha kwamba hamjapata ufahamu wa kina wa mamlaka ya Mungu. Inaweza hata kusemwa kwamba mwanadamu hajayaona mamlaka ya Mungu. Sasa mnaelewa hili angalau kidogo? Unapoyaona mamlaka ya Mungu katika vitendo, utahisi nini hasa? Mmeihisi kweli nguvu ya Mungu? (Tumehisi.) Unaposoma maneno ya Mungu kuhusu uumbaji Wake wa ulimwengu unaihisi nguvu Yake, unauhisi uweza Wake. Unapoona utawala wa Mungu juu ya hatima ya wanadamu, unahisi nini? Je, unaihisi nguvu Yake na hekima Yake? Ikiwa Mungu hakuwa na nguvu hii, ikiwa hakuwa na hekima hii, je, Angekuwa na sifa za kutawala vitu vyote na juu ya hatima ya wanadamu? Mungu ana nguvu na hekima, na hivyo Ana mamlaka. Hili ni jambo la kipekee. Je, umewahi kumjua kiumbe yeyote au mtu ulimwenguni ambaye ana nguvu kama alizonazo Mungu? Je, kuna mtu yeyote au kitu chochote chenye nguvu za kuumba mbingu na nchi na vitu vyote vile vile kuvithibiti na kuvitawala? Je, kuna mtu yeyote au kitu chochote kinachoweza kutawala na kuwaongoza wanadamu wote na kuwapo siku zote na chenye uweza? (Hapana, hakuna.) Sasa unaelewa maana ya kweli ya yale yote yaliyomo katika mamlaka ya kipekee ya Mungu? Je, mna uelewa kiasi fulani? (Ndio, tunao.) Sasa tumemaliza kupitia hoja za mamlaka ya Mungu ya kipekee.

Katika sehemu ya pili, tulizungumza kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Hatukujadili mambo mengi kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Hii ni kwa sababu kazi ya Mungu katika hatua hii kimsingi ni ya hukumu na kuadibu. Tabia ya haki ya Mungu imefichuliwa wazi katika Enzi ya Ufalme, kwa umahususi kabisa. Amesema maneno ambayo hajawahi kuyasema kutoka wakati wa uumbaji; na katika maneno Yake watu wote, wote ambao wameliona neno Lake, na wote ambao wamepitia uzoefu wa neno Lake wameiona tabia Yake ya haki ikifichuliwa. Sasa hoja kuu ya kile tunachokijadili kuhusu tabia ya haki ya Mungu ni nini? Je, mmekuza ufahamu wa kina wa kile ambacho mmejifunza? Je, mmepata uelewa kutokana na uzoefu wenu wowote? (Mungu kuiteketeza Sodoma kwa moto ilikuwa ni kwa sababu watu wa wakati huo walikuwa waovu sana na hivyo wakaichochea ghadhabu ya Mungu. Ni kutokana na hili ndipo tunaiona tabia ya haki ya Mungu.) Kwanza, hebu tuangalie: Ikiwa Mungu asingeiangamiza Sodoma, je, ungeweza kuijua tabia Yake ya haki? Bado ungeweza kujua, siyo? Unaweza kuiona kupitia maneno Aliyoyaeleza katika Enzi ya Ufalme, na pia kwa hukumu Yake, kuadibu, na laana zilizotolewa dhidi ya mwanadamu. Je, mnaiona tabia ya haki ya Mungu kwa kuacha kuiangamiza Ninawi? (Ndiyo.) Katika enzi ya sasa, watu wanaweza kuona rehema, upendo na uvumilivu kiasi wa Mungu, na watu wanaweza pia kuiona mabadiliko ya moyo wa Mungu yanayofuata toa ya mwanadamu. Baada ya kutoa mifano hii miwili kuanzisha mjadala wetu wa tabia ya haki ya Mungu, iko wazi kabisa kuona kwamba tabia Yake ya haki imefichuliwa. Hata hivyo, katika uhalisia hii haiko tu kwa kile kilichorekodiwa katika visa viwili hivi vya Biblia. Kutokana na kile sasa umejifunza na kuona kupitia neno la Mungu na kazi Yake, kutokana na uzoefu wako wa sasa juu yao, tabia ya haki ya Mungu ni nini? Jadili kutokana na uzoefu wako binafsi. (Katika mazingira ambayo Mungu aliwatengenezea watu, pale wanapoweza kuutafuta ukweli na kutenda chini ya mapenzi ya Mungu, Mungu huwaongoza, huwapa nuru, na kuwafanywa wahisi mwangaza ndani yao. Watu wanapokwenda kinyume cha Mungu na kumpinga na kwenda kinyume cha mapenzi Yake, kunakuwa na giza ndani yao, kana kwamba Mungu amewatelekeza. Hata wanaomba lakini hawajui nini cha kumwambia, lakini pale ambapo wanaweka pembeni mawazo yao na kuweka pembeni dhana zao na kuwa tayari kushirikiana na Mungu na kujitahidi kujiboresha, ni hapa ndipo uso wa tabasamu wa Mungu unaanza kuonekana taratibu. Kutoka kwa hili tumepitia utakatifu wa tabia ya haki ya Mungu; Mungu huonekana katika ufalme mtakatifu na anafichika mahali penye uchafu.) (Ninaiona tabia ya haki ya Mungu kwa vile anavyowachukulia watu. Kaka zetu na dada zetu wanatofautiana katika kimo na ubora wa tabia, na kile ambacho Mungu anakitaka kutoka kwa kila mmoja wetu hutofautiana vile vile. Wote tunaweza kupokea nuru ya Mungu kwa viwango tofauti, na kwa namna hii ninaiona haki ya Mungu. Hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kumtendea mwanadamu kwa namna hii hii, ni Mungu pekee ndiye anaweza kufanya hivyo.) Nyote mmeongea maarifa ya kiutendaji.

Je, unaielewa hoja kuu kuhusu kuifahamu tabia ya haki ya Mungu? Kuna mengi yanayoweza kusemwa kutokana na uzoefu juu ya mada hii, lakini kwana kuna hoja chache ambazo lazima Niwaambie. Kuielewa tabia ya haki ya Mungu, kwanza mtu anapaswa kuelewa hisia za Mungu: kile Anachokichukia, kile Anachokichukia kabisa, kile Anachokipenda, ni mvumilivu na mwenye huruma kwa nani, na ni aina gani ya mtu anayepokea rehema hiyo. Hii ni hoja ya msingi kufahamu. Aidha, mtu anapaswa kuelewa kwamba haijalishi Mungu ni mwenye upendo kiasi gani, haijalishi ni Mwenye rehema na upendo kiasi gani kwa watu, Mungu hamvumilii mtu yeyote anayekosea hali na nafasi Yake, wala Hamvumilii mtu yeyote anayekosea heshima Yake. Ingawa Mungu anawapenda watu, Hawadekezi. Anawapatia watu upendo Wake, rehema Yake, na uvumilivu Wake, lakini hajawahi kuwakuwadia; Ana kanuni Zake na mipaka Yake. Bila kujali ni kwa kiwango gani umeuhisi upendo wa Mungu ndani yako, bila kujali upendo huo ni wa kina kiasi gani, hupaswi kamwe kumtendea Mungu kama ambavyo ungemtendea mtu mwingine. Ingawa ni kweli kwamba Mungu anawachukulia watu kama wako karibu Naye, ikiwa mtu anamwangalia Mungu kama mtu mwingine, kana kwamba ni kiumbe mwingine wa uumbaji, kama rafiki au kama kitu cha kuabudu, Mungu atawaficha uso Wake na kuwatelekeza. Hii ndiyo tabia Yake, na watu hawapaswi kulichukulia jambo hili kwa mzaha. Hivyo, mara nyingi sisi huona maneno kama haya yakinenwa na Mungu kuhusu tabia Yake: Haijalishi umesafiri njia nyingi kiasi gani, umefanya kazi kubwa kiasi gani au umevumilia kiasi gani, mara tu unapoikosea tabia ya Mungu, Atamlipa kila mmoja wenu kulingana na kile ulichokifanya. Hii ina maana kwamba Mungu huwaona watu kama wapo karibu na Yeye, lakini watu hawapaswi kumchukulia Mungu kama rafiki au ndugu. Usimchukulie Mungu kama rafiki yako. Haijalishi ni upendo kiasi gani umepokea kutoka Kwake, haijalishi Amekuvumilia kwa kiasi gani, hupaswi kabisa kumchukulia Mungu kama rafiki tu. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Unaelewa, sio? Je, kuna haja ya Mimi kusema zaidi kuhusu hili? Je, una uelewa wowote wa awali kuhusiana na suala hili? Kwa ujumla, hili ndilo kosa rahisi sana ambalo watu wanafanya bila kujali kama wanaelewa mafundisho, au kama hawajafikiria chochote kuyahusu hapo awali. Watu wanapomkosea Mungu, inaweza isiwe kwa tukio moja, au kitu kimoja walichokisema, bali ni kwa sababu ya mtazamo walionao na hali waliyomo. Hili ni jambo la kutisha sana. Baadhi ya watu wanaamini kwamba wana uelewa juu ya Mungu, kwamba wanamjua, hata wanaweza kufanya baadhi ya mambo ambayo yanaweza kumpendeza Mungu. Wanaanza kuhisi wako sawa na Mungu na kwamba kwa werevu wamekuwa na urafiki na Mungu. Aina hizi za hisia sio sahihi kabisa. Ikiwa huna uelewa wa kina juu ya hili, ikiwa huelewi vizuri hili, basi ni rahisi sana kumkosea Mungu na kukosea tabia Yake ya haki. Unalielewa hili sasa, siyo? Je, tabia ya haki ya Mungu sio ya kipekee? Je inaweza kamwe kuwa sawa na tabia ama maadili ya mwanadamu? Haiwezi kamwe. Hivyo, hupaswi kusahau kwamba haijalishi ni kwa namna gani Mungu anawachukulia watu, haijalishi ni namna gani Anafikiri juu ya watu, nafasi, tabia na hadhi ya Mungu kamwe havibadiliki. Kwa binadamu, Mungu siku zote ni Bwana wa vitu vyote na Muumbaji.

Umejifunza nini kuhusu utakatifu wa Mungu? Katika sehemu hiyo kuhusu “utakatifu wa Mungu,” kando na ukweli kwamba uovu wa Shetani unatumika kama foili[a], maudhui makuu ya mjadala wetu kuhusu utakatifu wa Mungu yalikuwa yapi? Je, sio kile ambacho Mungu anacho na alicho? Je, kile ambacho Mungu anacho na alicho ni vya kipekee kwa Mungu Mwenyewe? (Ndiyo.) Hakuna chochote katika viumbe vyake kina hii. Hivyo tunasema kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee. Hiki ni kitu ambacho unaweza kuelewa. Tulikuwa na mikutano mitatu juu ya utakatifu wa Mungu. Unaweza kufafanua kwa maneno yako mwenyewe, kwa uelewa wako mwenyewe, kile unachoamini ni utakatifu wa Mungu? (Mara ya mwisho ambapo Mungu aliwasiliana na sisi tulisujudu mbele Yake. Mungu aliwasiliana na sisi ukweli kuhusu kusujudu na kuinama kumwabudu, Tuliona kwamba haikuwa kulingana na mapenzi Yake kwamba tuliinama na kumwabudu wakati hatukuwa tumefikia matakwa Yake, na kutoka hili tuliona utakatifu wa Mungu.) Kweli kabisa, sio? Je, kuna kitu chochote kingine? (Katika neno la Mungu kwa mwanadamu, tunaona kwamba Anazungumza kwa wazi na kwa kueleweka, Analenga moja kwa moja kwenye hoja ya msingi. Shetani anazungumza kwa kuzungukazunguka na ni mwenye uongo mwingi. Kutokana na kile kilichotokea wakati uliopita wakati tuliposujudu kifudifudi mbele ya Mungu, tuliona kwamba maneno Yake na matendo Yake siku zote yanaongozwa na kanuni. Siku zote yupo wazi na wa kueleweka Anapotuambia jinsi gani tunavyopaswa kutenda, tunachopaswa kushikamana nacho, na jinsi gani tunavyopaswa kuchukua hatua. Lakini watu hawapo hivi; baada ya binadamu kuharibiwa na Shetani, watu walitafuta kufikia matakwa na nia zao binafsi, na tamaa zao binafsi katika matendo na maneno yao. Kutokana na namna ambayo Mungu anamwangalia binadamu, kutokana na uangalizi na ulinzi Anaowapatia, tunaona kwamba yote ambayo Mungu anafanya ni mazuri, na yako wazi kabisa. Ni kwa namna hii ndipo tunaona ufunuo wa kiini cha utakatifu wa Mungu.) Imesemwa vizuri! Je, kuna mtu yeyote aliye na jambo la kuongezea? (Kupitia kwa Mungu kufunua kiini kiovu cha Shetani, tunauona utakatifu wa Mungu, tunapata ufahamu zaidi wa wa uovu wa Shetani, na kuona chanzo cha mateso yote ya mwanadamu. Hapo nyuma, tulikuwa hatuna habari ya mateso chini ya utawala wa Shetani. Ni baada tu ya Mungu kufichua hili ndipo tuliona kwamba mateso yote yanayotokana na kufuatilia umaarufu na utajiri ni kazi ya Shetani. Ni hapo tu ndipo tulihisi kwamba utakatifu wa Mungu ndio wokovu wa kweli wa binadamu.) Kuna kitu chochote cha kuongezea hapo? (Watu wapotovu hawana maarifa ya kweli au upendo kwa Mungu. Kwa sababu hatuelewi kiini cha utakatifu wa Mungu, kuinama kwetu mbele Yake katika ibada kumeghushiwa, kuna makusudi yaliyofichika na kwa kukusudia, kitu kinachomfanya Mungu asiwe na furaha. Tunauona kwamba Mungu yupo tofauti sana na Shetani; Shetani anawataka watu kumsujudia na kujipendekeza kwake, kumwinamia na kumwabudu. Shetani hana kanuni. Kutokana na hili natambua utakatifu wa Mungu.) Vizuri sana! Kutokana na kile tulichoshiriki kuhusu utakatifu wa Mungu, je, mmeuona ukamilifu wa Mungu? Je, mnaona jinsi ambavyo Mungu ni chanzo cha mambo yote mazuri? Je, mnaweza kuona jinsi ambavyo Mungu ni mfano halisi wa ukweli na haki? Je, mnaona jinsi ambavyo Mungu ni chanzo cha upendo? Je, mnaona jinsi ambavyo yote ambayo Mungu anayafanya, yote ambayo anayatoa, na yote ambayo Anayafichua hayana makosa? (Tunaona hili.) Mifano hii kadhaa yote ni hoja kuu kuhusu utakatifu wa Mungu ambao Nauzungumzia kuhusu. Leo, maneno haya yanaweza kuonekana kama mafundisho tu kwako, lakini siku moja, utakapopita uzoefu na kumshuhudia Mungu wa kweli Mwenyewe kutoka katika neno Lake na kazi Yake, utasema kwa dhati kwamba Mungu ni mtakatifu, kwamba Mungu ni tofauti na binadamu, na kwamba moyo Wake, tabia Yake, na asili yote ni takatifu. Utakatifu huu unamruhusu mwanadamu kuuona ukamilifu Wake na vile vile humfanya mwanadamu kuona kwamba asili ya utakatifu wa Mungu haina mawaa. Asili ya utakatifu wake inaamua kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, na inamwonyesha mwanadamu, na kuthibitisha kwamba ni Mungu Mwenyewe wa kipekee. Je, hii si hoja kuu? (Ni hoja kuu.)

Leo tumefanya muhtasari wa sehemu kadhaa za maudhui kutoka katika mikutano iliyotangulia. Tutakamilisha muhtasari wetu hapa. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wenu ataweka moyoni hoja kuu za kila kipengele na mada. Usizifikirie tu kuwa ni mafundisho; zisome zote na jaribu kuzitafakari pale unapopata muda. Zikumbuke katika nyoyo zenu na mziweke katika uhalisi—kisha hakika utapitia yote ambayo Nimesema kuhusu uhalisi wa Mungu kufichua tabia Yake na kufichua kile Anacho na alicho. Hata hivyo hutaweza kuzielewa ikiwa utaziandika tu katika kitabu chako bila kuzisoma zote au kuzifikiria tena. Unaelewa, siyo? Baada ya kuviwasilisha vipengele hivi vitatu, watu watakuwa wamepata uelewa wa jumla au hata mahususi juu ya hadhi ya Mungu, asili Yake, na tabia Yake. Je, watakuwa na uelewa kamili juu ya Mungu lakini? (La.) Sasa, katika uelewa wenu binafsi juu ya Mungu, je, kuna maeneo mengine ambapo mnahisi mnahitaji uelewa wa kina? Hiyo ni kusema, baada ya kuwa umepata uelewa wa mamlaka ya Mungu, tabia Yake ya haki, na utakatifu Wake, pengine umeyakinisha katika akili yako mwenyewe utambuzi wa hadhi na nafasi Yake ya kipekee, lakini kupitia uzoefu wako unapaswa kufahamu na kutambua matendo Yake, uwezo Wake, na asili Yake kabla ya kuweza kupata uelewa wa kina. Sasa mmesikiliza ushirika huu hivyo mnaweza kuweka moyoni mwako makala haya ya imani: Mungu kweli yupo na ni ukweli kwamba Anaendesha vitu vyote. Hakuna mwanadamu anayepaswa kuikosea tabia Yake ya haki na utakatifu Wake ni hakika kiasi kwamba mwanadamu hawezi kuushuku. Huu ni ukweli. Ushirika huu unafanya hadhi na nafasi ya Mungu kuwa na msingi katika mioyo ya watu. Punde msingi huu kuanzishwa, watu lazima wajaribu kuelewa zaidi.

Hadithi ya 1: Mbegu, Ardhi, Mti, Mwanga wa Jua, Chiriku, na Mwanadamu

Leo Nitashiriki nawe mada mpya. Mada itakuwa ni nini? Kichwa cha mada kitakuwa “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.” Je, hii siyo mada kubwa kidogo kuweza kuijadili? Je, inaonekana kama kitu ambacho kidogo hakiwezi kufikika? Mungu kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote inaweza kuonekana ni mada ambayo watu wanahisi kutohusika nayo, lakini wote wanaomfuata Mungu wanapaswa kuielewa. Hii ni kwa sababu mada hii haihusiani kwa kuchanganulika na kila mtu anayemjua Mungu, kuweza kumridhisha na kumheshimu. Hivyo, mada hii inapaswa kuwasilishwa. Awali, pengine baadhi ya watu walikuwa na ufahamu wa msingi wa mada hii, au pengine baadhi ya watu waliifahamu. Wanaweza wakawa na ufahamu sahili kuhusu au ufahamu wa juu juu wa hii katika akili zao. Wengine wanaweza kuwa na ufahamu kiasi maalumu kuihusu; kutokana na uzoefu wao wa kipekee, mioyoni mwao wana uelewa wa kina juu ya mada hii. Lakini ama maarifa ya mada hii ni ya kina au ya juujuu, kwenu nyinyi ni ya upande mmoja na wala si mahususi vya kutosha. Hivyo, mada hii inapaswa kuwasilishwa, kusudi lake ni kuwapatia uelewa wa kina zaidi na mahususi. Nitatumia njia maalumu kushiriki na nyinyi mada hii, njia ambayo hatujawahi kuitumia hapo awali na njia ambayo kidogo mtaona si ya kawaida, au ambayo haifurahishi kidogo. Hata hivyo, baada ya kuisikia mtaijua, njia yoyote ile itakayotumika. Je, mnapenda kusikiliza hadithi? (Ndiyo.) Inaonekana kwamba Nilikuwa sahihi kuchagua njia ya kusimulia hadithi. Nyinyi nyote mnapenda kusikiliza hadithi. Sawa, hebu tuanze. Hamna haja ya kuandika hii kwenye matini zenu. Ninawaomba muwe watulivu, na msihangaike. Unaweza kufumba macho yako ikiwa unahisi kwamba kufumbua macho yako mazingira yanayokuzunguka au watu wanaokuzunguka wanaweza kukupotezea umakini. Nina hadithi ndogo nzuri ya kuwasimulia. Ni hadithi kuhusu mbegu, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu. Hadithi Ninayokwenda kuwasimulia ina wahusika gani wakuu ndani yake? (Mbegu, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu.) Mungu atakuwa ndani yake? (Hapana.) Lakini Nina uhakika kwamba baada ya hadithi kusimuliwa mtajihisi kuburudika na kuridhika. Sawa basi, unaweza kusikiliza kimya kimya.

Mbegu ndogo ilidondoka ardhini. Baada ya mvua kubwa kunyesha, mbegu ilianza kuchipuka na mizizi yake ikamea taratibu kwenda ardhini. Chipuko lilirefuka kadri muda ulivyozidi kwenda, yakivumilia upepo mkali na mvua kubwa, yakiangalia mabadiliko ya misimu kadri mwezi unavyopevuka na kufifia. Wakati wa kiangazi ardhi ilileta zawadi ya maji ili kwamba chipuko liweze kuhimili joto kali. Na kwa sababu ya ardhi, chipuko halikuhisi joto na hivyo lilihimili joto la kiangazi. Msimu wa baridi ulipokuja, ardhi ililifunika chipuko katika kumbatio la vuguvugu lake na kushikamana kwa nguvu. Na kwa sababu ya vuguvugu la ardhi, chipuko lilihimili baridi kali, likivuka bila kudhurika katika dhoruba ya msimu wa baridi na barafu za msimu. Likivikwa na ardhi, chipuko lilikua kwa ujasiri na lilikuwa na furaha. Lilirefuka na kujivunia malezi yasiyokuwa ya ubinafsi ambayo ardhi iliyatoa. Chipuko lilikua kwa furaha. Liliimba wakati mvua ilipokuwa ikinyesha na kucheza na kuyumba kadri upepo ulivyokuwa ukivuma. Na hivyo, chipuko na ardhi hutegemeana…

Miaka ilipita, na chipuko sasa lilikuwa mnara wa mti. Lilikuza matawi manene juu yake yaliyokuwa na majani yasiyohesabika na kusimama imara juu ya nchi. Mizizi ya mti ilimea aridhini kama ilivyomea hapo kabla, lakini sasa ilizama kabisa ardhini chini kabisa. Kile ambacho mwanzo kilililinda chipuko sasa kilikuwa msingi wa mti mkubwa sana.

Mwale wa mwanga wa jua ulimulika mti na shina likatikisika. Mti ulitoa nje matawi yake kwa upana na kufaidi sana kutoka kwenye mwanga. Ardhi chini ilipumua kwa wizani pamoja na mti, na ardhi ilihisi kufanywa upya. Baada ya hapo tu, upepo mwanana ulivuma ukitokea katika matawi, na mti ulifurahia sana, ukiwa na nguvu. Na hivyo, mti na mwanga wa jua vinategemeana …

Watu walikaa katika kivuli tulivu cha mti na wakafurahia hewa changamfu inayonukia vizuri. Hewa ilitakasa mioyo na mapafu yao, na ilitakasa damu ndani yao. Watu hawakuhisi tena kuchoka au kuelemewa. Na hivyo, watu na miti wanategemeana …

Kundi la chiriku waliimba kwa uchangamfu walivyokuwa wakitua kwenye matawi ya mti. Pengine walikuwa wanamwepuka adui fulani, au walikuwa wanazaliana na kuwalea watoto wao, au pengine walikuwa wanapata pumziko fupi. Na hivyo, ndege na mti wanategemeana …

Mizizi ya mti, ikiwa imesokotana na kusongamana, ilijikita chini kabisa ardhini. Shina lake liliifunika ardhi dhidi ya upepo na mvua na kuyatoa nje matawi yake makubwa na kuilinda ardhi chini yake, na mti ulifanya hivi kwa sababu ardhi ni mama yake. Yanatiana nguvu na kutegemeana, na kamwe hayataachana …

Na hivyo, hadithi hii imefikia mwisho. Hadithi ambayo Nimewasimulia ilikuwa kuhusu mbegu, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku na mwanadamu. Hadithi ina sehemu chache tu. Iliwapatia hisia gani? Baada ya kuwasimulia kwa namna hii, je, mmeielewa? (Tunaelewa.) Mnaweza kuzungumza kuhusu hisia zenu. Sasa, Mnahisi nini baada ya kusikia hadithi hii? Kwanza Nitawaambia kwamba vitu vyote Nilivyovitaja kwenu mnaweza kuviona na kuvishika; haya ni mambo halisi, sio sitiari. Ninawataka sasa mtafakari juu ya yale Niliyoyajadili. Hakuna Nilichokizungumza ambacho kilikuwa cha kina, na kuna sentensi chache ambazo zinatengeneza hoja kuu ya hadithi. (Hadithi tuliyoisikia inatoa picha nzuri: Mbegu inapata uhai na kadiri inavyokua inapitia misimu minne ya mwaka: majira ya kuchipua, kiangazi, kipupwe na baridi. Ardhi ni kama mama kwa namna ambavyo inalea. Inatoa vuguvugu wakati wa baridi ili kwamba chipuko lihimili baridi. Baada ya chipuko kukua na kuwa mti, mwale wa jua unagusa matawi yake, ukiupatia mti furaha zaidi. Tunaona kwamba miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu, ardhi pia ipo hai na kwamba hiyo na mti vinategemeana. Pia Ninaona joto jingi ambalo jua linaupa mti, na ingawa ndege ni vitu vya kawaida vya kuona, tunaona jinsi gani ndege, mti, na watu wote wanakuja pamoja kwa maafikiano. Tunaposikia hadithi hii, hii ndiyo hisia tuliyonayo mioyoni mwetu kwamba, kimsingi, vitu vyote vya uumbaji wa Mungu ni hai.) Imesemwa vizuri! Je, kuna mtu ana kitu chochote cha kuongeza? (Katika hadithi kadri mbegu inapokua na kuwa mti mrefu kabisa, naona maajabu ya uumbaji wa Mungu. Naonakwamba Mungu alifanya vitu vyote vihimiliane na kutegemeana, na vyote kuunganika pamoja na kuhudumiana. Tunaiona hekima ya Mungu, maajabu Yake, na tunaona kwamba Yeye ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.)

Mambo yote Niliyoyazungumzia ni mambo ambayo mmeshawahi kuyaona hapo awali, kama vile mbegu, mnajua kuhusiana na hili, sio? Mbegu kukua na kuwa mti unaweza usiwe mchakato unaouangalia katika maelezo ya kina, lakini unajua kwamba ni ukweli, sio? Unajua kuhusu ardhi na mwanga wa jua. Taswira ya chiriku wakitua mtini ni kitu ambacho watu wote wamekwishakiona, sio? Na watu kutuliza joto chini ya kivuli cha mti, wote mmekwishawahi kuona, sio? (Tumeona hilo.) Sasa, mnapata hisia gani mnapoona mifano yote hii katika taswira moja? (Upatanifu.) Je, mifano yote hii iliyopo katika taswira hii inatoka kwa Mungu? (Ndiyo.) Kwa kuwa inatoka kwa Mungu, Mungu anajua thamani na umuhimu wa mifano hii kadhaa inayokaa pamoja ardhini. Mungu alipoviumba vitu vyote, Alipofanya mpango na kuumba kila kitu, Alifanya hivyo kwa makusudi; na Alipoumba vitu hivyo, kila kimoja kilijazwa na uzima. Mazingira Aliyotengeneza kwa ajili ya kuwepo binadamu, ambayo yamejadiliwa katika hadithi tuliyoisikia. Imejadili hali ya kutegemeana baina ya mbegu na ardhi; ardhi inastawisha mbegu na mbegu inafungamana na ardhi. Uhusiano kati ya hivi vitu viwili uliamuliwa kabla na Mungu kuanzia mwanzoni kabisa. Mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu katika taswira hii ni mifano ya mazingira hai ambayo Mungu aliyaumba kwa ajili ya mwanadamu. Kwanza, mti hauwezi kuiacha ardhi, wala hauwezi kuishi bila mwanga wa jua. Kwa hivyo, kusudi la Mungu la kuumba mti lilikuwa ni nini? Je, tunaweza kusema kuwa ilikuwa tu ni kwa ajili ya ardhi? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya chiriku? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya watu? (Hapana.) Kuna uhusianao gani kati yao? Uhusianao kati yao ni wa kutiana nguvu, kutegemeana ambapo haviwezi kutengana. Yaani, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na watu wanategemeana kwa ajili ya kuishi na wanaleana. Mti unailinda ardhi wakati ardhi inaulea mti; mwanga wa jua unatoa huduma kwa mti, wakati mti unapata hewa nzuri kutoka katika mwanga wa jua unapunguza joto jingi la mwanga wa jua juu ya ardhi. Nani anayefaidika mwishoni? Mwanadamu ndiye anayefaidika, siyo? Na hii ndiyo kanuni juu ya kwa nini Mungu alifanya mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu na ambaye ndiye lengo kuu kwa ajili yake. Ingawa hii ni taswira rahisi, tunaweza kuona hekima za Mungu na nia yake. Binadamu hawezi kuishi bila ardhi, au bila miti, au bila chiriku na mwanga wa jua, sio? Ingawa ilikuwa ni hadithi, kile inachoonyesha ni mfano mdogo wa uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia na vitu vyote na zawadi Yake ya mazingira ambamo binadamu wanaweza kuishi.

Mungu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu na pia akafanya mazingira ya kuishi. Kwanza, hoja kuu tuliyoijadili katika hadithi ni mwingiliano wa mahusiano na hali ya kutegemeana ya vitu vyote. Chini ya kanuni hii, mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu yamelindwa, yanaendelea kuishi na kudumu; kwa sababu ya uwepo wa mazingira haya hai, mwanadamu anaweza akastawi na kuzaliana. Tuliona mti, ardhi, mwanga wa jua, na chiriku, na watu katika tukio. Mungu alikuwepo pia? Watu wanaweza wakose kuiona, sio? Lakini mtu aliweza kuona sheria ya kuhimizana na kutegemeana kati ya vitu katika tukio; ni kupitia kanuni hizi ndipo watu wanaweza kuona kwamba Mungu yupo na kwamba ni Mtawala. Mungu anatumia kanuni hizi na sheria kulinda uhai na uwepo wa vitu vyote. Ni kwa njia hii ndipo Anavikimu vitu vyote na Anamkimu binadamu. Je, hadithi hii ina uhusiano wowote na dhamira tuliyoijadili? Kwa juujuu inaonekana kama hakuna uhusiano, lakini kwa uhalisia, kanuni ambazo Mungu anazifanya kama Muumbaji na utawala Wake juu ya vitu vyote zinahusiana kwa karibu sana na Yeye kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote na zimeunganika bila kuachana. Umejifunza angalau kidogo, sio?

Mungu anaamuru sheria zinazoongoza uendeshaji wa vitu vyote; Anaamuru sheria zinazoongoza uwepo wa vitu vyote; Yeye hudhibiti vitu vyote, na huviweka kutiana nguvu na kutegemeana, ili visiangamie au kutoweka. Hivi tu ndivyo wanadamu wanaweza kuendela kuishi; ni hivyo tu ndivyo wanaweza kuishi chini ya mwongozo wa Mungu katika mazingira kama hayo. Mungu ndiye bwana wa sheria hizi za uendeshaji, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia. Ni lini miti itachipuka, ni lini mvua itanyesha, ni maji kiasi gani na virutubisho kiasi gani ardhi itaipatia mimea, ni katika msimu gani majani yatapukutika, ni katika msimu gani miti itazaa matunda,jua litaipa miti virutubisho vingapi; kile ambacho miti itatoa nje baada ya kulishwa na jua—vitu hivi vyote viliamuliwa kabla na Mungu alipoumba vitu vyote, kama sheria ambazo hakuna mtu anayeweza kuvunja. Vitu vilivyoumbwa na Mungu—ama ni hai au vinaonekana kwa watu si hai—vyote vipo mikononi mwa Mungu na chini ya utawala Wake. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuvunja kanuni hii. Hii ni kusema, Mungu alipoviumba vitu vyote Aliweka kanuni ya jinsi vinavyopaswa kuwa. Miti isingeweza kuzamisha mizizi, kuchipua na kukua bila ardhi. Ardhi isingekuwa na miti, ingekauka. Pia, mti ni makazi ya chiriku, ni sehemu ambapo wanapata kujikinga dhidi ya upepo. Je, mti unaweza kuishi bila dunia? La hasha. Je, unaweza kuishi bila jua au mvua. Hauwezi pia. Yote haya ni kwa ajili ya mwanadamu na kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Mwanadamu anapokea hewa safi kutoka kwenye miti, na anaishi katika ardhi inayomlinda. Mwanadamu hawezi kuishi bila mwanga wa jua, mwanadamu hawezi kuishi bila viumbe hai mbalimbali. Ingawa uhusiano baina ya vitu hivi ni changamani, mnapaswa kukumbuka kwamba Mungu alitengeneza kanuni ambazo zinaongoza vitu vyote ili kwamba viweze kuimarishana, kutegemeana na kuwepo pamoja. Kwa maneno mengine, kila kitu alichokiumba kina thamani na umuhimu. Ikiwa Mungu aliumba kitu bila kuwa na umuhimu, Mungu angeacha kipotee. Hii ni njia mojawapo Aliyoitumia katika kuvikimu vitu vyote. “Kukimu” kuna maana gani katika hadithi hii? Je, Mungu kila siku anatoka na kwenda kumwagilia mti maji? Je, mti unahitaji msaada wa Mungu ili uweze kupumua? (Hapana.) “Kukimu” hapa ina maana ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote baada ya uumbaji; Alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni sheria ili kufanya vitu kwenda vizuri. Mti ulikuwa wenyewe kwa kupandwa ardhini. Masharti ili uweze kukua yote yalitengenezwa na Mungu. Alitengeneza mwanga wa jua, maji, udongo, hewa, na mazingira, upepo, umande, barafu, na mvua, na misimu minne; haya ndiyo masharti ambayo mti huyahitaji ili uweze kukua, hivi ni vitu ambavyo Mungu aliviandaa. Kwa hiyo, Mungu ni chanzo cha mazingira haya hai? (Ndiyo.) Je, Mungu analazimika kwenda kila siku na kuhesabu kila jani kwa miti? Hakuna haja, sio? Mungu pia hahitaji kuusaidia mti ili uweze kupumua. Mungu pia hahitaji kuuamsha mwanga wa jua kila siku kwa kusema, “Ni muda wa kuiangazia miti sasa.” Hana haja ya kufanya hivyo. Mwanga wa jua humulika wenyewe wakati wake wa kumulika unapofika, kulingana na sheria; unaonekana na kumulika juu ya mti na mti unafyonza huo mwanga wakati unapohitaji, na wakati hauhitajiki, mti huo bado huishi ndani ya kanuni. Pengine hamwezi kuelezea jambo hili kwa uwazi, lakini ni ukweli ambao kila mtu anaweza kuona na kuukubali. Chote unachopaswa kufanya ni kutambua kwamba kanuni kwa ajili ya uwepo wa vitu vyote inatoka kwa Mungu na kujua kwamba Mungu ni mkuu juu ya ukuaji na kuishi kwa vitu vyote.

Je, istiari imetumika katika hadithi hii, kama watu wanavyoiita? Je, ni hadithi iliyopewa sifa za kibinadamu? (Hapana.) Kile Nilichokizungumza ni ukweli. Kila kitu ambacho ni hai, kila kitu ambacho kina uhai kipo chini ya utawala wa Mungu. Kilipewa uhai baada ya Mungu kukiumba; ni uhai uliotolewa kutoka kwa Mungu na unafuata sheria na njia Alizozitengeneza kwa ajili yake. Hii haihitaji kubadilishwa na mwanadamu, na haihitaji msaada kutoka kwa mwanadamu; hivi ndivyo Mungu anavyokimu vitu vyote. Unaelewa, sio? Je, unadhani ni lazima watu watambue hili? (Ndiyo.) Hivyo, hadithi hii ina uhusiano wowote na biolojia? Je, inahusiana kwa njia fulani nauwanja wa maarifa au tawi la kujifunza? Hatujadili biolojia hapa na hakika hatufanyi utafiti wa kibiolojia. Je, hoja kuu tunayoizungumzia hapa ni ipi? (Kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Mnaona nini miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji? Mmeiona miti? Mmeiona ardhi? (Ndiyo.) Mmeuona mwanga wa jua, sio? Mmewaona ndege wakikaa mtini? (Ndiyo.) Je, mwanadamu anafurahia kuishi mazingira kama hayo? (Anafurahia.) Yaani, Mungu anatumia vitu vyote—vitu alivyoviumba—kudumisha makazi ya binadamu kwa ajili ya kuishi na kulinda makazi ya binadamu, na hivi ndivyo Anavyomkimu mwanadamu na anavyokimu vitu vyote.

Je, mnapenda mtindo wa hotuba hii, namna Ninavyotoa ushirika? (Ni rahisi kuelewa na kuna mifano ya vitendo ambayo ni halisi.) Hii ni njia ya kweli ya kujadili mambo, sio? Hadithi hii ni ya lazima kuwasaidia watu kutambua kuwa Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Kama ni ya lazima, basi tutaendelea na hadithi inayofuata. Maudhui katika hadithi inayofuata ni tofauti kidogo na hoja kuu ni tofauti kidogo pia; mambo yaliyomo katika hadithi hii ni ambayo watu wanaweza kuona miongoni mwa uumbaji wa Mungu. Sasa, Nitaanza simulizi Yangu ya kufuatia. Tafadhali sikilizeni mkiwa kimya na mwone iwapo mnaweza kuelewa kile Ninachomaanisha. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi, nitawauliza maswali kuona mmeelewa kiasi gani. Wahusika wakuu katika hadithi ni mlima mkubwa, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa.

Hadithi ya 2: Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, “Tafadhali naomba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele.” Basi mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Swali ambalo kijito kililijibu, “Ninatafuta makazi yangu.” Mlima ukasema, “Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!” Lakini kwa sababu kijito kilikuwa dhaifu sana na kichanga sana, hakukuwa na namna kwake kutiririka juu ya mlima mkubwa hivyo, hivyo hakikuwa na uchaguzi bali kuendelea kutiririka chini ya mlima …

Upepo mkali ukavuma, ukiwa umekusanya mchanga na unga wa kusagika kwa mchanga kuelekea ambapo mlima ulikuwa umesimama. Upepo ukaungurumia mlima, “Hebu nipite!” Mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Upepo ukavuma kwa kujibu, “Ninataka kwenda upande ule wa mlima.” Mlima ukasema, “Sawa, kama unaweza kupenya katikati yangu, basi unaweza kwenda!” Upepo mkali ukavuma huku na kule, lakini haijalishi ulikuwa mkali kiasi gani, haukuweza kupenya katikati ya mlima. Upepo ukachoka na ukaacha ili upumzike. Hivyo katika upande ule wa mlima ni upepo dhaifu tu ndio ulivuma kwa vipindi, ambao uliwafurahisha watu waliopo kule. Hiyo ilikuwa ni salamu ambayo mlima ulikuwa unaitoa kwa watu …

Ufukweni mwa bahari, mawimbi tulivu ya bahari yalizunguka taratibu kwenye mwamba. Ghafula, wimbi kubwa likaja na likanguruma kuelekea kwenye mlima. “Pisha!” wimbi kubwa lilipiga kelele. Mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Wimbi kubwa halikusita, na likaendelea kutapakaa huku likijibu, “Ninapanua eneo langu na ninataka kunyoosha mikono yangu kidogo.” Mlima ukasema, “Sawa, kama utaweza kupita juu ya kilele changu, nitakupisha njia.” Wimbi kubwa likarudi nyuma kidogo, na kisha likavurumiza kuelekea mlimani. Lakini haijalishi lilijaribu kwa nguvu kiasi gani, halikuweza kufika juu ya mlima. Halikuwa na jinsi bali kurudi nyuma taratibu kurudi kule lilipotoka …

Kwa karne nyingi kijito kidogo kilichururika taratibu kuzunguka chini ya mlima. Kwa kufuata njia ambayo mlima uliifanya, kijito kidogo kilifanikiwa kufika nyumbani; kilijiunga na mto, na kutiririka kwenda baharini. Chini ya uangalizi wa mlima, kijito kidogo hakikuweza kupotea. Kijito na mlima ilihimiliana na kutegemeana; ilitiana nguvu, kutenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.

Kwa karne nyingi, upepo mkali haukuacha tabia yake ya kuvuma kwenye mlima. Upepo mkali ulivumisha kimbunga “ulipoutembelea” mlima kama ulivyofanya kabla. Uliutisha mlima, lakini haukuwahi kupenya katikati ya mlima. Upepo na mlima vilihimiliana na vilitegemeana; vilitiana nguvu, vilitenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.

Kwa karne nyingi, wimbi kubwa wala halikupumzika, na kamwe halikuacha kupanuka. Lingenguruma na kuvurumiza tena na tena kwenda kwenye mlima, lakini mlima haukuwahi kusogea hata inchi moja. Mlima uliilinda bahari, na kwa namna hii viumbe ndani ya bahari viliongezeka na kustawi. Wimbi na mlima mkubwa vilihimiliana na vilitegemeana; vilitiana nguvu, vilitenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.

Hadithi hii imeishia hapo. Kwanza, mnaweza kuniambia nini kuhusu hadithi hii, maudhui makuu yalikuwa ni nini? Kwanza kulikuwa na mlima, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa. Nini kilikitokea kijito kidogo na mlima mkubwa katika sehemu ya kwanza? Kwa nini tuzungumze juu ya mlima mkubwa na kijito kidogo? (Kwa sababu mlima ulikilinda kijito, kijito hakikuweza kupotea. Walitegemeana.) Unaweza kusema kuwa mlima ulikilinda au kukizuia kijito kidogo? (Ulikilinda.) Inawezekana kuwa ulikizuia? Mlima na kijito kidogo vilikuwa pamoja; ulikilinda kijito, na pia ulikuwa ni kizuizi. Mlima ulikilinda kijito ili kiweze kutiririka kwenda mtoni, lakini pia ulikizuia kutiririka kutapakaa kila sehemu ambapo kingeweza kufurika na kuwa majanga kwa watu. Hii ndiyo hoja kuu ya sehemu hii? Ulinzi wa mlima kwa kijito na kufanya kwake kazi kama kizuizi kulilinda makazi ya watu. Kisha unapata kijito kidogo kikiunganika na mto chini ya mlima na baadaye kutiririka kwenda baharini; je, huo si umuhimu wa kijito kidogo? Kijito kilipotiririka kwenda kwenye mto halafu kwenda baharini, kilikuwa kinategemea nini? Hakikuwa kinategemea mlima? Kilikuwa kinategemea ulinzi wa mlima na mlima kufanya kazi kama kizuizi; je, hii ndiyo hoja kuu? Je, mnauona umuhimu wa milima kwa maji katika tukio hili? Je, Mungu ana makusudi Yake ya kutengeneza milima mirefu na mifupi? (Ndiyo.) Hii ni sehemu ndogo ya hadithi, na kutoka tu katika kijito kidogo na mlima mkubwa tunaweza kuona thamani na umuhimu wa Mungu kuviumba vitu hivi viwili. Tunaweza pia kuona hekima Yake na makusudi katika jinsi ya kutawala vitu hivi viwili. Sivyo?

Sehemu ya pili ya hadithi inashughulika na nini? (Upepo mkali na mlima mkubwa.) Je, upepo ni kitu kizuri? (Ndiyo.) Sio lazima, kwa kuwa wakati mwingine ikiwa upepo ni mkali sana unaweza kuwa janga. Ungejisikiaje kama ungelazimika kukaa nje kwenye upepo mkali? Inategemea na ukali wake, sivyo? Kama ulikuwa upepo wa kiwango cha tatu au cha nne ungeweza kuvumilika. Kwa kiasi cha juu zaidi, mtu angeweza kupata shida kuendelea kuacha macho wazi bila kufumba. Lakini ungeweza kuvumilia kama upepo ungevuma kwa nguvu na kuwa kimbunga? Usingeweza kuvumilia. Hivyo, ni kosa watu kusema kwamba siku zote upepo ni mzuri, au kwamba siku zote ni mbaya kwa sababu inategemeana na upepo ni mkali kiasi gani. Hivyo mlima una matumizi gani hapa? Je, kwa kiasi fulani haufanyi kazi kama kichujio cha upepo? Mlima unachukua upepo mkali na kuutuliza na kuwa nini? (Upepo mwanana.) Watu wengi wanaweza kuugusa na kuuhisi katika mazingira ambamo wanaishi—je, wanachohisi ni upepo mkali au upepo mwanana? (Upepo mwanana.) Je, hili sio kusudi mojawapo la Mungu la kuumba milima?Ingekuwaje ikiwa watu wangeishi katika mazingira ambapo mchanga ulipeperuka sana katika upepo, bila kuzuiliwa na bila kuchujwa? Je, inaweza kuwa kwamba ardhi inayokabiliwa na mchanga na mawe yanayopeperuka haingeweza kukalika? Mawe yanaweza kuwapiga watu, na mchanga unaweza kuwapofusha. Upepo unaweza kuwaangusha watu au kuwabeba hewani. Je, upepo mkali una thamani? Niliposema kuwa ni mbaya, basi watu wangeweza kuhisi kwamba hauna thamani, lakini hiyo ni sahihi? Je, kubadilika kuwa upepo mwanana hakuna thamani? Watu wanahitaji nini zaidi kunapokuwa na unyevunyevu au kusongwa? Wanahitaji upepo mwanana kuwapepea, kuchangamsha na kusafisha vichwa vyao, kuamsha kufikiria kwao, kurekebisha na kuboresha hali zao za akili. Kwa mfano, nyote mmekaa chumbani kukiwa na watu wengi na hewa sio safi, ni kitu gani mtakihitaji zaidi? (Upepo mwanana.) Katika maeneo ambapo hewa imetibuliwa na imejaa uchafu inaweza kushusha uwezo wa kufikiri wa mtu, kupunguza mzunguko wao wa damu, na kuwafanya vichwa vyao visiwe vyepesi. Hata hivyo, hewa itakuwa safi ikiwa itapata nafasi ya kujongea na kuzunguka na watu watajihisi nafuu zaidi. Ingawa kijito kidogo na upepo mkali vingeweza kuwa janga, alimradi mlima upo utavibadilisha na kuwa vitu ambavyo kwa kweli vinawanufaisha watu; hiyo si kweli?

Sehemu ya tatu ya hadithi inazungumzia nini? (Mlima mkubwa na wimbi kubwa.) Mlima mkubwa na wimbi kubwa. Mandhari hapa ni mlima mkubwa uliopo kando ya bahari ambapo tunauona mlima, mawimbi tulivu ya bahari, na pia wimbi kubwa. Mlima ni nini kwa wimbi hapa? (Mlinzi na kinga.) Ni mlinzi na pia ni kinga. Lengo la kulinda ni kuilinda sehemu hii ya bahari isipotee ili kwamba viumbe vinavyoishi ndani yake viweze kuishi, kuongezeka na kustawi. Kama kinga, mlima hulinda maji ya bahari—chanzo hiki cha maji—yasifurike na kusababisha janga, ambalo linaweza kudhuru na kuharibu makazi ya watu. Hivyo tunaweza kusema kwamba mlima ni kinga na mlinzi. Hii inaonyesha hali ya kutegemeana kati ya mlima na kijito, mlima na upepo mkali, na mlima na wimbi kubwa, na jinsi vinavyozuiliana na kutegemeana, ambayo nimezungumzia.

Huu ni umuhimu wa muungano kati ya mlima mkuu na kijito kidogo, mlima mkuu na upepo mkali, na mlima mkuu na wimbi kubwa kabisa; huu ndio umuhimu wa kutiana nguvu na kuhimiliana, nay a kuwepo kwao pamoja. Vitu hivi ambavyo nimezungumzia. Kuna kanuni na sheria inayoongoza vitu hivi ambavyo Mungu aliviumba kuendelea kuishi. Mnaweza kuona kile ambacho Mungu alifanya kutokana na kile kilichotokea kwenye hadithi? Je, Mungu aliumba ulimwengu na kupuuzia kile kilichotokea baada ya hapo? Je, Alitoa kanuni na kuunda namna ambazo wao hufanya kazi na halafu kuwapuuza baada ya hapo? Je, hicho ndicho kilichotokea? (Hapana.) Ni nini hicho sasa? Mungu bado Anadhibiti maji, upepo na mawimbi. Haviachi bila kudhibitiwa, wala haviachi visababishe madhara au kuharibu nyumba ambamo watu wanaishi. Kwa sababu ya hili, watu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka na kusitawi katika nchi. Kitu kinachomaanisha kwamba Mungu alikwishapanga kanuni kwa ajili ya kuishi Alipofanya mbingu. Mungu Alipotengeneza vitu hivi, Alihakikisha kwamba vingewanufaisha binadamu, na pia Alividhibiti ili kwamba visiwe shida au majanga kwa binadamu. Ikiwa havingesimamiwa na Mungu, je, maji yangetiririka kila mahali? Je, upepo usingevuma kila sehemu? Yanafuata sheria? Ikiwa Mungu hakuvisimamia visingeongozwa na kanuni yoyote, na upepo ungevuma na maji yangeinuka na kutiririka kila sehemu. Ikiwa wimbi kubwa lingekuwa refu kuliko mlima, je, sehemu hiyo ya bahari ingekuwa bado ipo? Bahari isingeweza kuwepo. Ikiwa mlima haungekuwa mrefu kama wimbi, eneo la bahari lisingekuwepo na mlima ungepoteza thamani na umuhimu wake.

Je, unaiona hekima ya Mungu katika visa viwili hivi? Mungu aliumba ulimwengu na ni Bwana wake; Anaisimamia yote na Yeye huruzuku vyote, na ndani ya vitu vyote, Yeye huona na kuchunguza kila neno na tendo la kila kitu kilichopo. Vivyo hivyo, pia, ndivyo Mungu huona na kuchunguza kila kona ya maisha ya wanadamu. Hivyo, Mungu anajua kwa undani kila kipengele cha kila kitu kilichopo ndani ya uumbaji Wake, kutoka kwa kazi ya kila kitu, asili yake, na sheria zake za kuishi hadi kwa umuhimu wa maisha yake na thamani ya kuwepo kwake, yote haya Mungu anayajua kwa ukamilifu. Mungu Aliuumba ulimwengu; unadhani Anapaswa kufanya utafiti juu ya kanuni hizi zinazouongoza ulimwengu? Je, Mungu Anahitajika kusoma maarifa au sayansi ya kibinadamu kufanya utafiti na kuyaelewa? (Hapana.) Je, kuna yeyote miongoni mwa binadamu aliye na elimu na maarifa ya kuelewa mambo yote kama Mungu Anavyoelewa? Hakuna, sivyo? Je, kuna mamajusi au wanabiolojia ambao wanaelewa kweli sheria ambazo kwazo vitu vinaishi na kukua? Je, wanaweza kweli kuelewa thamani ya uwepo wa kila kitu? (Hawawezi.) Hii ni kwa sababu vitu vyote viliumbwa na Mungu, na haijalishi ni kwa kiasi kikubwa au kwa kina kiasi gani binadamu anajifunza maarifa haya, au ni kwa muda mrefu kiasi gani wanajitahidi kujifunza, hawataweza kuelewa siri na makusudi ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, hiyo si sahihi? Baada ya kujadili kwa kina hadi sasa, mnahisi kwamba mna ufahamu wa juujuu wa maana ya kweli ya kirai: “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? (Ndiyo.) Nilijua kwamba Nilipojadili mada hii watu wengi wangefikiri kwa haraka juu ya “Mungu ni ukweli, na Mungu hutumia neno Lake kutukimu,” lakini wangeifikiria tu katika kiwango hiki. Baadhi hata wangehisi kwamba Mungu kukimu maisha ya binadamu, kutoa chakula na kinywaji cha kila siku na mahitaji yote ya kila siku haihesabiki kama Yeye kumkimu mwanadamu. Je, baadhi ya watu hawahisi namna hii? Lakini, je, si nia ya Mungu katika uumbaji Wake ni wazi kabisa—kuwaruhusu binadamu wawepo na kuishi kwa kawaida? Mungu anadumisha mazingira ambamo watu wanaishi na anatoa vitu vyote ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi. Aidha, Anasimamia na kuwa mkuu juu ya vitu vyote. Haya yote yanamfanya binadamu kuishi na kusitawi na kuongezeka kwa kawaida; ni kwa njia hii ndipo Mungu Anavikimu vitu vyote na binadamu. Je, watu hahitaji kutambua na kuelewa mambo haya? Pengine baadhi wanaweza kusema, “Mada hii ipo mbali sana na maarifa yetu juu ya Mungu Mwenyewe wa kweli, na hatutaki kujua hili kwa sababu binadamu hawezi kuishi kwa mkate pekee, lakini badala yake anaishi kwa neno la Mungu.” Hili ni sahihi? (Hapana.) Kosa ni lipi hapa? Je, mnaweza kuwa na uelewa kamili juu ya Mungu ikiwa mnaelewa tu vitu ambavyo Mungu amesema? Ikiwa mnakubali tu kazi Yake na hukumu Yake na kuadibu, je, mtakuwa na uelewa kamili juu ya Mungu? Ikiwa mnaelewa sehemu ndogo tu ya tabia ya Mungu, sehemu ndogo ya mamlaka ya Mungu, hiyo inatosha kupata uelewa juu ya Mungu, sio? (Hapana.) Matendo ya Mungu yanaanza na uumbaji Wake wa ulimwengu na yanaendelea leo ambapo matendo yake ni dhahiri muda wote na kila wakati. Ikiwa watu wanaamini kwamba Mungu yupo kwa sababu tu Amewachagua baadhi ya watu ambao kwao Anafanya kazi Yake kuwaokoa watu hao, na kwamba hakuna kingine chochote kinachohusiana na Mungu, si mamlaka Yake, hadhi Yake, wala matendo Yake, basi, je, mtu anaweza kuchukuliwa kuwa aliye na umfahamu wa kweli kwa Mungu? Watu walio na haya yanayodaiwa kuwa “maarifa ya Mungu” wana ufahamu wa upande mmoja tu, ambao wanatumia kuzuia matendo Yake kwa kundi moja la watu. Je, haya ni maarifa ya kweli juu ya Mungu? Sio kwamba watu wenye aina hii ya maarifa juu ya Mungu wanakataa uumbaji Wake wa vitu vyote na utawala wao juu Yao? Baadhi ya watu hawatamani kujishughulisha na hili jambo, wakijiwazia badala yake: “Sioni utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, ni kitu ambacho kipo mbali sana na mimi na sitaki kukielewa. Mungu Anafanya kile anachotaka na wala hakinihusu. Ninakubali tu uongozi wa Mungu na neno Lake ili niweze kuokolewa na kufanywa mkamilifu na Mungu. Hakuna kingine kilicho na umuhimu kwangu. Sheria ambazo Mungu Alifanya Alipoviumba vitu vyote na kile ambacho Mungu Anafanya kuvikimu vitu vyote na kumkimu mwanadamu havinihusu.” Haya ni mazungumzo ya aina gani? Je, huu si uasi? Hii sio fedheha kabisa? Je, kuna mtu yeyote miongoni mwenu aliye na ufahamu kama huu? Ninajua kwamba kuna watu wengi sana wanaofikiri namna hii hata kama hamtasema. Aina ya mtu huyu wa kuamini katika maandiko anaweza kutumia kile kinachoitwa msimamo wao wa kiroho katika namna wanavyotazama kila kitu. Wanataka kumwekea Mungu mipaka katika Biblia, kumwekea Mungu mipaka kwa maneno Aliyoyazungumza, na kumwekea Mungu mipaka katika neno lilikoandikwa. Hawatamani kufahamu zaidi kuhusu Mungu na hawataki Mungu Aweke umakini zaidi katika kufanya mambo mengine. Aina hii ya kufikiri ni ya kitoto na ni ya kidini sana. Je, watu wenye mitazamo hii wanaweza kumjua Mungu? Wanaweza kuwa na wakati mgumu kumjua Mungu. Leo nimesimulia hadithi mbili, kila moja ikigusia kipengele tofauti. Mnaweza kuhisi kwamba ni za kina au hata ni za kidhahania kidogo na ngumu kutambua na kufahamu. Inaweza kuwa ni vigumu kuzihusianisha na matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, matendo yote ya Mungu na yote Aliyoyafanya miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa binadamu wote yanapaswa kueleweka kwa wazi na kwa usahihi kwa kila mtu na kwa kila mmoja ambaye anatafuta kumjua Mungu. Maarifa haya yatakupatia uthibitisho wa imani katika uwepo wa kweli wa Mungu. Pia yatakupatia maarifa sahihi juu ya hekima ya Mungu, nguvu Zake, na jinsi ambavyo anakimu vitu vyote. Itakufanya uelewe kwa wazi kabisa uwepo wa kweli wa Mungu na kuona kwamba siyo hadithi ya kubuni, na sio kisasili. Hii inakufanya uone kwamba si ya kidhahania, na sio tu nadharia, na kwamba Mungu hakika sio tu riziki ya kiroho, lakini ni kweli yupo. Aidha, itawaruhusu watu kujua kwamba Mungu daima amekimu viumbe na binadamu wote; Anafanya hivi kwa njia Yake mwenyewe na kulingana na wizani Wake mwenyewe. Hivyo mtu anaweza kusema kwamba ni kwa sababu Mungu Aliumba vitu vyote na Akavipatia kanuni kwamba kwa amri Yake kila kimoja kinafanya kazi zake kilizopangiwa, vinatimiza majukumu yao, na kutimiza jukumu ambalo lilipewa kila kimoja. Vitu vyote vinatimiza jukumu lao kwa ajili ya binadamu, na hufanya hivi katika sehemu, mazingira ambamo watu wanaishi. Ikiwa Mungu hangefanya mambo namna hii na mazingira ya binadamu hayangekuwa jinsi yalivyo, imani ya watu kwa Mungu au wao kumfuata Yeye—hakuna ambacho kingewezekana; yangekuwa tu mazungumzo ya bure, hii sio sahihi?

Hebu tuchukue mtazamo mwingine katika hadithi hii ambayo tumekwishaisikia—mlima mkubwa na kijito kidogo. Mlima una matumizi gani? Viumbe hai vinastawi juu ya mlima hivyo kuna thamani ya uwepo wake kwa wenyewe. Wakati huo huo, mlima unazuia kijito kidogo, unahakikisha kuwa hakitiririki kuelekea mahali popote kinapotaka na hivyo kuleta janga kwa watu. Hii sio sahihi? Uwepo tu wa mlima unaruhusu viumbe hai kama vile miti na majani na mimea yote mingine na wanyama mlimani kustawi huku pia ukiongoza kijito kidogo kinapopaswa kutiririka; mlima unakusanya maji ya kijito na kuyaongoza kiasili kuzunguka chini yake ambapo yanaweza kutiririka kuelekea mtoni na hatimaye baharini. Kanuni zilizopo hapa hazikutengenezwa na asili, badala yake zilipangwa mahususi na Mungu wakati wa uumbaji. Kuhusu mlima mkubwa na upepo mkali, mlima pia unahitaji upepo. Mlima unahitaji upepo ili kupapasa viumbe hai ambao wanaishi juu yake, na wakati huo huo mlima unazuia jinsi ambavyo upepo unaweza kuvuma kwa nguvu ili kwamba usiharibu na kuteketeza. Kanuni hii inashikilia wajibu wa mlima mkubwa, hivyo kanuni hii kuhusiana na wajibu wa mlima ilipata umbo yenyewe? (Hapana.) Badala yake ilitengenezwa na Mungu. Mlima mkubwa una wajibu wake na upepo mkali una wajibu wake pia. Sasa, kuhusu mlima mkubwa na wimbi kubwa, je, bila mlima kuwa pale maji yangepata mwelekeo wake wa kutiririka yenyewe? (Hapana.) Maji pia yangefurika. Mlima una thamani yake ya kuwepo kama mlima, na bahari ina thamani yake ya kuwepo kama bahari; hata hivyo, chini ya mazingira haya ambapo yanaweza kuwepo pamoja kwa kawaida na ambapo kila kimoja hakiingiliani na kingine, pia vinadhibitiana; mlima mkubwa unadhibiti bahari ili isiweze kufurika na hivyo unalinda makazi ya watu, na hii pia inaruhusu bahari kulea viumbe hai vinavyokaa ndani yake. Je, hii sura ya nchi ilipata umbo yenyewe? (Hapana.) Pia iliumbwa na Mungu. Tunaona katika taswira hizi kwamba Mungu Alipoiumba dunia, Alijua kabla mahali ambapo mlima ungesimama, mahali ambapo kijito kingetiririka, kutoka katika mwelekeo ambapo upepo mkali ungeanza kuvuma na kuelekea ambapo ungekwenda, vile vile kiwango cha urefu ambao wimbi lingekuwa. Nia na makusudi ya Mungu yamekumbatiwa ndani ya vitu vyote hivi na ni matendo Yake. Sasa, unaweza kuona kwamba matendo ya Mungu yapo katika vitu vyote? (Ndiyo.)

Kusudi la mjadala wetu wa haya mambo ni nini? Je, ni ili kwamba watu waweze kutafiti kanuni zilizopo kwenye uumbaji wa Mungu wa ulimwengu? Je, ni ili kwamba watu wavutiwe na falaki na jiografia? (Hapana.) Sasa ni nini? Ni ili kwamba watu wataelewa matendo ya Mungu. Katika matendo ya Mungu, watu wanaweza kukubali na kuthibitisha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kama unaweza kuielewa hoja hii, basi utaweza kuthibitisha kweli nafasi ya moyoni mwako na utaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, Muumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote. Hivyo, je, inasaidia katika uelewa wako juu ya Mungu kujua kanuni za vitu vyote na kujua matendo ya Mungu? (Ndiyo.) Inasaidiaje? Kwanza, utakapojua matendo haya ya Mungu, bado utavutiwa na falaki na jiografia? Bado utakuwa na moyo wa kushuku na mashaka kwamba Mungu ni Muumbaji wa vitu vyote? Bado utakuwa na moyo wa mtafiti na mashaka kwamba Mungu ni Muumbaji wa vitu vyote? (Hapana.) Utakapothibitisha kwamba Mungu ni Muumbaji wa ulimwengu na zaidi ujue kanuni zilizopo katika uumbaji Wake, moyoni mwako kweli utaamini kwamba Mungu anakimu ulimwengu? (Ndiyo.) Je, “kukimu” hapa lina maana mahsusi, au linarejelea hali mahsusi? Kwamba Mungu anakimu ulimwengu ina maana na matumizi mapana sana. Mungu hawakimu tu watu kwa kuwapatia mahitaji yao ya kila siku ya chakula na kinywaji, Anawapatia wanadamu kila kitu wanachohitaji, ikiwa ni pamoja na kila kitu ambacho watu wanakiona na vitu ambavyo haviwezi kuonekana. Mungu anatetea, anasimamia na anatawala mazingira ya kuishi ambayo binadamu anahitaji. Mazingira yoyote ambayo binadamu anayataka katika msimu wowote, Mungu ameyaandaa. Angahewa au halijoto yoyote ambayo inafaa kwa ajili ya uwepo wa binadamu pia ipo chini ya udhibiti wa Mungu na hakuna kati ya kanuni hizi ambayo inatokea yenyewe tu au bila utaratibu; ni matokeo ya kanuni ya Mungu na matendo Yake. Mungu Mwenyewe ni chanzo cha kanuni zote hizi na ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Huu ni ukweli uliothibitishwa na usioweza kushambuliwa na haijalishi unauamini au huuamini, haijalishi unaweza kuuona au huwezi kuuona, au haijalishi unaweza kuuelewa au huwezi kuuelewa.

Ninajua kwamba watu wengi wanaamini tu maneno na kazi ya Mungu ambayo yako katika Biblia. Kwa watu wachache, Mungu amefichua matendo Yake na akawawezesha watu waone thamani ya uwepo Wake. Pia anawawezesha wawe na ufahamu kiasi wa utambulisho Wake na Akathibitisha ukweli wa uwepo Wake. Hata hivyo, kwa watu wengi zaidi, ukweli kwamba Mungu Aliuumba ulimwengu na kwamba Anasimamia na kukimu vitu vyote unaonekana kuwa usio dhahiri au wenye utata na hata wanakuwa na mtazamo wa mashaka. Aina hii ya mtazamo inawafanya watu kuendelea kuamini kwamba sheria za ulimwengu asilia zilijitengeneza zenyewe, kwamba mabadiliko, mageuzi na ajabu ya ulimwengu asilia na sheria ambazo zinaongoza asili ziliibuka kwa hiari yao. Maana yake hii ni kwamba katika akili za watu, hawawezi kufikiri jinsi ambavyo Mungu alitengeneza kanuni juu ya vitu vyote, hawawezi kuelewa jinsi ambavyo Mungu anasimamia na kuvihudumia vitu vyote. Kwa sababu ya mipaka ya kigezo hiki, watu hawawezi kuamini kwamba Mungu aliumba, anatawala, na hukimu vitu vyote; hata wale wanaoamini wamewekewa mipaka katika imani yao katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme; wanaamini kwamba matendo ya Mungu na ruzuku Yake kwa binadamu ni kwa ajili tu ya wateule Wake. Hiki ni kitu ambacho Nachukia kukiona na kinaleta maumivu makali sana, kwa sababu binadamu hufurahia yote ambayo Mungu huleta, halafu wakati huohuo wanakana yote ambayo Anafanya na yote ambayo Anawapatia. Watu wanaamini tu kwamba mbingu na nchi na vitu vyote vinaongozwa na kanuni zao za asili na kwa sheria zao za asili na kwamba hazina mtawala wa kuvidhibiti au mtawala yeyote wa kuzikimu na kuzilinda. Hata kama unamwamini Mungu, unaweza usiamini yote haya kuwa ni maneno Yake; hili ni eneo kati ya maeneo ambayo hayajapewa uzito kwa kila anayemwamini Mungu, kwa kila mtu ambaye anakubali neno la Mungu, na kila mtu anayemfuata Mungu. Hivyo, Ninapoanza tu kujadili kitu fulani ambacho hakihusiani na Biblia au kile kinachodaiwa kuwa istilahi ya kiroho, baadhi ya watu wanasumbuliwa au wanachoshwa au hata kutofurahia. Wanahisi kwamba maneno Yangu yanaonekana yaliyotengana na watu wa kiroho na mambo ya kiroho. Hicho ni kitu kibaya. Linapokuja suala la kujua matendo ya Mungu, hata kama hatutaji falaki, jiografia, au biolojia, tunajua utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, tunajua kukimu Kwake vitu vyote, na kwamba Yeye ni chanzo cha vitu vyote. Hii ni kazi muhimu sana na ambayo inapaswa kuchunguzwa, mmeelewa?

Kuhusu hadithi mbili ambazo Nimezisema, ingawa zinaweza kuwa na maudhui ambayo si ya kawaida na zinaweza kuwa zimesimuliwa na kuwasilishwa kwako kwa mtindo wa kipekee, hata hivyo Nilitaka kutumia lugha ya moja kwa moja na njia rahisi ili kwamba ungeweza kukubali na kuelewa kitu ambacho ni cha kina zaidi. Hili ndilo lilikuwa lengo langu tu. Nilitaka mwone na kuamini kuwa Mungu ni Mtawala wa vitu vyote kutokana na hadithi hizi ndogo na matukio. Lengo la kusimulia hadithi hizi ni kuwafanya mwone na kujua matendo ya Mungu yasiyokuwa na kikomo ndani ya hadithi yenye kikomo. Kuhusu ni lini mtafikia kikamilifu matokeo haya ndani yenu inategemea uzoefu wako binafsi na maendeleo yako binafsi. Ukifuatilia ukweli na ikiwa unatafuta kumjua Mungu, basi mambo haya yatafanya kazi kama kumbusho lenye nguvu na imara kwako; yatakufanya uwe na utambuzi wa kina sana, ubayana katika uelewa wako, na polepole utasogea karibu na matendo ya kweli ya Mungu, ukaribu ambao utakuwepo bila umbali na bila hitilafu. Hata hivyo, kama hutafuti kumjua Mungu, basi hadithi hizo ulizozisikia haziwezi kukudhuru. Mnaweza kuzichukulia kama hadithi za kweli.

Je, mlielewa kitu chochote kwenye hadithi hizi mbili? Kwanza, je, hadithi hizi mbili zinajitenga na mjadala wetu wa awali kuhusu Mungu kumjali binadamu? Je, kuna uhusiano usioepukika? Je, ni kweli kwamba ndani ya hadithi hizi mbili tunaona matendo ya Mungu na kujali kwa kiwangi kikubwa Anakokipa kila kitu Anachopanga kwa ajili ya binadamu? Je, ni kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya na mawazo Yake yote yanaelekezwa kwa uwepo wa binadamu? (Ndiyo.) Je, sio kwamba fikra makini za Mungu na kujali kwake binadamu kuko dhahiri? Binadamu hana haja ya kufanya chochote. Mungu amewaandaliwa watu hewa—kile wanachohitaji kufanya ni kuivuta tu. Mboga na matunda wanayokula vinapatikana kwa urahisi. Kutoka kaskazini hadi kusini, kutoka mashariki hadi magharibi, kila kanda ina rasilimali zake asili na mazao na matunda tofauti na mboga zimeandaliwa na Mungu. Tukizungumza juu ya mazingira mapana, Mungu aliumba vitu vyote viimarishane, vitegemeane, vitiane nguvu, vishindane na viishi pamoja. Hii ni mbinu Yake na sheria Yake ya kudumisha kuendelea kuishi na kuwepo kwa vitu vyote; kwa njia hii, binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili. Kama kusingekuwa na udhibiti na ukuu wa Mungu, hakuna mwanadamu ambaye angeweza kudumisha na kuweka wiano katika mazingira, hata kama bado yangekuwa yaliumbwa na Mungu, bado yangukuwa zaidi ya uwezo wa mtu yeyote kuyalinda na kuyaweka katika usawa. Katika baadhi ya maeneo hakuna hewa, hivyo watu hawawezi kuishi hapo na Mungu hatakuruhusu uende kwa wao. Hivyo, usivuke mipaka inayostahili. Hili ni kwa ajili ya usalama wa binadamu—kuna siri ndani yake. Kila kipengele cha mazingira, urefu na upana wa dunia, na kila kiumbe hai duniani—vilivyo hai na vilivyokufa—viliandaliwa na Mungu na Alivifikiria: Kwa nini kitu hiki kinahitajika? Kwa nini sio cha lazima? Lengo la kuwa na kitu hiki hapa ni nini na kwa nini kiende hapo? Mungu alikuwa amekwishafikiria hii yote na hakuna haja ya watu kuyafikiria. Kuna baadhi ya watu wapumbavu ambao siku zote wanafikiri juu ya kuhamisha milima, lakini badala ya kufanya hivyo, kwa nini wasihamie kwenye tambarare? Kama huipendi milima, kwa nini unakwenda kuishi karibu nayo? Huu si upumbavu? Nini hutokea ikiwa utauhamisha mlima huo? Kimbunga kikali kitavuma au wimbi kubwa litapiga na makazi ya watu yataharibiwa. Je, hicho kisingekuwa kitu cha kipumbavu kufanya? Watu wanaweza tu kuharibu. Hawawezi hata kudumisha pahali pa pekee waliponapo pa kuishi, na ilhali wanataka kukimu vitu vyote. Hili haliwezekani.

Mungu anamwacha mwanadamu kusimamia vitu vyote na kuwa na utawala juu yao, lakini mwanadamu anafanya kazi nzuri? Mwanadamu ana tabia ya uharibifu; mwanadamu sio kwamba tu hawezi kutunza vitu kama Mungu alivyoviumba, kwa kweli ameviharibu. Binadamu ameifanya milima kuwa vifusi, ameijaza bahari kwa mchanga, na amezibadilisha tambarare kuwa majangwa ambapo hakuna kinachoweza kuishi. Halafu katika majangwa hayo mwanadamu amejenga viwanda na kujenga vinu vya nyuklia na uharibifu unaendelea katika pande zote. Mito si mito tena, bahari si bahari tena…. Binadamu anapovunja uwiano na kanuni za maumbile, siku yao ya maafa na kifo haipo mbali na haiepukiki. Maafa yanapokuja, watajua viumbe vya Mungu ni vya thamani kiasi gani jinsi vyote ni muhimu kwa binadamu. Mwanadamu kuishi katika mazingira yenye hali ya hewa nzuri ni sawa na kuwa peponi. Watu hawatambui baraka hii, lakini wakati ambapo wataipoteza yote ndipo watatambua ni jinsi gani yote ni adimu na ya thamani. Ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuirudisha hii yote? Watu wangefanyaje ikiwa Mungu Asingekuwa tayari kuitengeneza tena? Mngefanyaje? Kwa kweli, kuna kitu mnachoweza kufanya na ni rahisi sana na Nitakapowaambia ni nini, mara moja mtajua kwamba hiyo inawezekana. Kwa nini mwanadamu amejikuta katika mashaka yake ya kimazingira ya sasa? Je, ni kwa sababu ya tamaa na uharibifu wa mwanadamu? Ikiwa mwanadamu atasitisha uharibifu huu, je, mazingira ya kuishi hayatakuwa sawa taratibu yenyewe? Ikiwa Mungu hafanyi chochote, ikiwa Mungu hatamani tena kufanya kitu chochote kwa ajili ya binadamu—yaani, hataki kuingilia—njia bora zaidi ingekuwa ni binadamu kusitisha uharibifu huu na kurudisha vitu kuwa vile vilivyokuwa. Kusitisha uharibifu huu wote humaanisha kusitisha uporaji na uharibifu wa vitu ambavyo Mungu ameviumba. Hii itaruhusu mazingira ambamo mwanadamu anaishi kuboreka taratibu. Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha uharibifu zaidi wa mazingira na hali itakuwa mbaya zaidi. Je, mbinu Yangu ni rahisi? Ni rahisi na inawezekana, siyo? Ni rahisi kweli, na inawezekana kwa baadhi ya watu, lakini je, hii inawezekana kwa watu walio wengi duniani? (Haiwezekani.) Kwenu nyinyi, angalau inawezekana? (Ndiyo.) Chanzo cha “ndiyo” yenu ni nini? Je, mtu anaweza kusema kuwa inahusisha kuanzisha msingi wa uelewa kuhusu matendo ya Mungu? Je, mtu anaweza kusema inahusisha kushikilia kanuni na mpango wa Mungu? (Ndiyo.) Kuna njia ya kubadilisha haya yote, lakini hiyo siyo mada tunayoijadili sasa. Mungu anawajibika kwa kila uhai wa binadamu na anawajibika hadi mwisho. Mungu Anawakimu, hata kama umeugua kutokana na mazingira yaliyoharibiwa na Shetani, au kuathiriwa na uchafuzi au kupata madhara mengine, haijalishi; Mungu Anakukimu na Atakuacha uendelee kuishi. Mnapaswa kuwa na imani katika hili. Mungu hatamkubali mwanadamu afe kwa urahisi.

Mmehisi umuhimu wa kumtambua Mungu kama chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo, tumehisi.) Mna hisia gani? Endelea, nitasikiliza. (Hapo awali, hatukufikiria kamwe kuhusisha milima, bahari na maziwa na matendo ya Mungu. Haikuwa hadi tuliposikia ushirika wa Mungu leo ndipo tulielewa kwamba vitu hivi vina matendo na hekima ya Mungu ndani yavyo; tunaona kwamba hata wakati ambapo Mungu alianza kuumba vitu vyote, Alikuwa tayari amekijaza kila kitu na hatima na nia Yake njema. Vitu vyote vinaimarishana na kutegemeana na binadamu ndiye anayenufaika mwishowe. Tulichokisikia leo kinaonekana ni kipya na kigeni, na tumehisi jinsi ambavyo matendo ya Mungu ni halisi. Katika dunia halisi, katika maisha yetu ya kila siku, na katika mwingiliano wetu na vitu vyote, tunaona kwamba hili liko hivyo) Unaiona kabisa, sio? Mungu kumkimu binadamu sio bila msingi imara, hatamki tu maneno machache na kuishia hapo tu. Mungu anafanya mambo mengi, hata vitu ambavyo huvioni anafanya kwa manufaa yako. Mwanadamu anaishi katika mazingira haya, ulimwengu huu ambao Mungu Aliutengeneza, na ndani yake watu na vitu vingine vinategemeana, kama tu ambavyo gesi inayotoka kwenye mimea inaitakasa hewa na kuwanufaisha watu wanaoivuta. Hata hivyo, baadhi ya mimea ni yenye sumu kwa watu, ilhali mimea mingine inakinza mimea yenye sumu. Haya ni maajabu ya uumbaji wa Mungu! Lakini hebu tuiache mada hii kwa sasa; leo, mjadala wetu hasa ulihusu kuishi pamoja kwa mwanadamu na viumbe vingine, ambavyo mwanadamu hawezi kuishi bila. Ni nini umuhimu wa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote? Mwanadamu hawezi kuishi bila vitu vingine, kama ambavyo mwanadamu anahitaji hewa kuweza kuishi na namna ambavyo kama ungewekwa kwenye ombwe ungekufa upesi. Hii ni kanuni ya msingi sana kukufanya kuona kwamba mwanadamu anahitaji vitu vingine. Hivyo ni aina gani ya mtazamo ambao mwanadamu anapaswa kuwa nao kwa vitu vyote? Vithamini sana, vitunze, vitumie kwa ufanisi, usiviharibu, usivipoteze, na usivibadilishe kwa ghafula, maana vitu vyote vinatoka kwa Mungu na vinatolewa kwa binadamu na binadamu anapaswa kuvichukulia kwa uangalifu. Leo tumejadili mada hizi mbili, na mtarudi na kuzitafakari kwa kina. Wakati ujao tutajadili vitu vingi zaidi kwa kina. Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo. Kwa heri!

Januari 18, 2014

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Inayofuata: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp