Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX
Mungu ni Chanzo cha Uzima kwa Vitu Vyote (III)
Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya hii. Ni mada gani? (Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Inaonekana yale mambo na mada niliyoyazungumzia yaliwachia kila mtu wazo dhahiri. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu. Matendo haya yanayofanywa na Mungu hayakomei tu kwenye maandalizi Yake ya mazingira kwa ajili ya watu kuendelea kuishi na riziki zao za kila siku—yana mawanda mapana zaidi kuliko hayo. Licha ya aina mbili hizi za kazi, pia Anaandaa mazingira mengi na hali kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni lazima kwa ajili ya maisha ya mwanadamu. Hii ndiyo mada ambayo tutajadili leo. Pia inahusiana na matendo ya Mungu; vinginevyo, kuizungumzia hapa isingekuwa na maana. Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu lakini wana maana ya moja kwa moja ya “Mungu,” ya neno hilo, au ya vipengele vyote vya kile Mungu anacho na alicho, huo sio uelewa wa kweli. Sasa, njia kwa ajili ya maarifa ya Mungu ni ipi? Ni kumjua Yeye, kujua kila kipengele Chake kupitia matendo Yake. Kwa hiyo, kinachofuata tunapaswa kushiriki kuhusu matendo ya Mungu pale alipoumba vitu vyote.
Tangu Mungu alipoviumba, kulingana na sheria ambazo Aliziamua, vitu vyote vimekuwa vikitenda kazi na vimekuwa vikiendelea kukua kwa kawaida. Chini ya uangalizi Wake, chini ya kanuni Yake, vitu vyote vimekuwa vikiendelea kwa kawaida sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu. Hakuna kitu hata kimoja kinaweza kubadilisha sheria hizi, na hakuna hata kitu kimoja kinachoweza kuziharibu sheria hizi. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu ndipo viumbe vyote vinaweza kuongezeka, na kwa sababu ya kanuni na usimamizi Wake ndipo vitu vyote vinaweza kuendelea kuishi. Hii ni kusema kwamba chini ya kanuni ya Mungu, viumbe vyote vinakuwepo, vinastawi, vinatoweka, na kuzaliwa upya kwa namna ya mpangilio. Msimu wa machipuo unapowadia, mvua ya manyunyu huleta hisia hiyo ya machipuo na kuipatia nchi unyevunyevu. Ardhi huanza kuyeyuka, na majani huota na kujipenyeza juu ya udongo na kuanza kuchipuka, ilihali miti kwa utaratibu hubadilika kuwa ya kijani. Viumbe hai hivi vyote vinaleta uzima mpya katika dunia. Hii ndiyo picha ya viumbe vyote kuwepo na kustawi. Wanyama wa kila aina pia hutoka matunduni mwao ili kupata uvuguvugu wa msimu wa machipuo na kuanza mwaka mpya. Viumbe vyote vinaota jua kwenye joto wakati wa kiangazi na kufurahia uvuguvugu unaoletwa na msimu huu. Vinakua haraka; miti, nyasi, na aina zote za mimea inakua haraka sana, kisha inachanua na kuzaa matunda. Viumbe vyote vinakuwa vimetingwa sana wakati wa kiangazi, binadamu wakiwemo. Katika msimu wa majani kupukutika, mvua inaleta utulivu wa msimu wa majani kupukutika, na aina zote za viumbe hai vinaanza kuhisi majilio ya msimu wa kiangazi. Viumbe vyote vinazaa matunda, na binadamu wanaanza kuvuna matunda haya ya aina mbalimbali ili kuwa na chakula kwa ajili ya msimu wa baridi. Katika msimu wa baridi viumbe vyote taratibu vinaanza kupumzika katika ubaridi, kuwa kimya, na watu pia wanachukua pumziko wakati wa msimu huu. Mabadiliko haya kutoka msimu wa machipuo kwenda msimu wa kiangazi kwenda msimu wa mapukutiko na kwenda msimu wa baridi—mabadiliko haya yote yanatokea kulingana na sheria zilizoanzishwa na Mungu. Anaongoza vitu vyote na wanadamu kwa kutumia sheria hizi na amebuni maisha yenye utajiri na ya kupendeza kwa ajili ya mwanadamu, akiandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo yana halijoto tofautitofauti na misimu tofautitofauti. Chini ya mazingira haya yaliyopangiliwa kwa ajili ya kuendelea kuishi, binadamu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka kwa namna ya mpangilio. Wanadamu hawawezi kuzibadilisha sheria hizi, na hakuna mtu hata mmoja au kiumbe ambacho kinaweza kuzivunja. Ingawa mabadiliko yasiyohesabika yametokea—bahari zimekuwa mbuga, ilhali mbuga zimekuwa bahari—sheria hizi zinaendelea kuwepo. Sheria hizi zipo kwa sababu Mungu yupo, na kwa sababu ya sheria na usimamizi Wake. Kwa aina hii ya mpangilio, mazingira makubwa, maisha ya watu yanaendelea ndani ya sheria na kanuni hizi. Sheria hizi ziliendeleza kizazi baada ya kizazi cha watu na kizazi baada ya kizazi cha watu wameendelea kuishi ndani ya sheria hizi. Watu wamefurahia mazingira haya ya mpangilio kwa ajili ya kuendelea kuishi vilevile vyote miongoni mwa vingi vilivyoumbwa na Mungu kwa ajili ya kizazi baada ya kizazi cha binadamu. Ingawa watu wanahisi kwamba aina hii ya sheria ni za kiasili, ingawa wanazipuuza kabisa sheria hizo, na ingawa hawawezi kuhisi kuwa Mungu ndiye anaweka utaratibu wa sheria hizi, kwamba Mungu anatawala sheria hizi, haijalishi, Mungu siku zote anajihusisha katika kazi hii isiyobadilika. Kusudi lake katika kazi hii isiyobadilika ni kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na ili binadamu waweze kuendelea.
Mungu Huweka Mipaka kwa ajili ya Vitu Vyote ili Kuwalea Binadamu Wote
Leo Mimi nitazungumzia mada ya jinsi ambavyo hizi kanuni ambazo Mungu amezileta kwa vitu vyote hulea wanadamu wote. Hii ni mada kubwa, kwa hiyo tunaweza kuigawanya katika sehemu kadhaa na kuzijadili moja baada ya nyingine ili ziweze kufafanuliwa vizuri kwenu. Kwa njia hii itakuwa rahisi kwenu kupata maana na taratibu mnaweza kuielewa.
Sehemu ya Kwanza: Mungu Aweka Mipaka kwa Ajili ya Mandhari ya Kila Aina
Kwanza, Mungu alipoviumba vitu vyote, Aliweka mipaka kwa ajili ya milima, tambarare, majangwa, vilima, mito, na maziwa. Duniani kuna milima, tambarare, majangwa, vilima, vilevile vyanzo mbalimbali vya maji. Je, hayo si mandhari tofautitofauti? Mungu aliweka mipaka kati ya mandhari haya yote tofautitofauti. Tunapozungumza juu ya kuweka mipaka, ina maana kwamba milima ina mipaka yake, tambarare zina mipaka yake, majangwa yana mawanda fulani, na vilima vina eneo mahususi. Pia kuna kiwango mahususi cha vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Yaani, Mungu alipoumba vitu vyote aligawanya kila kitu vizuri kabisa. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha mlima ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha tambarare ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Alipokuwa anaumba viumbe vyote, Aliamua pia mipaka ya majangwa, vilevile masafa ya vilima na uwiano wao, na vile vilivyopakana navyo—pia Aliamua yote haya. Aliamua mawanda ya mito na maziwa Alipokuwa anaviumba—vyote vina mipaka yao. Kwa hiyo ina maana gani tunaposema “mipaka”? Tulizungumza tu kuhusu ambavyo Mungu huongoza vitu vyote kwa kuanzisha sheria kwa vitu vyote. Yaani, masafa na mipaka ya milima havitaongezeka au kupungua kwa sababu ya mzunguko wa dunia au muda kupita. Hizi ni thabiti, hazibadiliki na ni Mungu ambaye huamrisha kutobadilika kwayo. Kwa maeneo ya tambarare, masafa yao, kile kilichopakana nayo, hii imewekwa na Mungu. Yana mipaka, na tuta haliwezi kutokea tu bila mpangilio, katikati ya tambarare. Tambarare haiwezi tu kubadilika na kuwa mlima—hii haitatokea. Sheria na mipaka tuliyoizungumzia inarejelea hili. Kwa jangwa, hatutataja wajibu wa jangwa au mandhari nyingineyo au eneo la kijiografia hapa, ni mipaka yake tu. Chini ya kanuni ya Mungu mawanda ya jangwa nayo pia hayatapanuka. Hii ni kwa sababu Mungu amelipatia sheria yake, mawanda yake. Eneo lake ni kubwa kiasi gani na wajibu wake ni upi, kile kilichopakana nalo, na lipo mahali gani—hii imeshawekwa na Mungu tayari. Halitazidisha mawanda yake, kuhamisha sehemu yake, na halitaongeza eneo lake kiholela tu. Ingawa mtiririko wa maji kama vile mito na maziwa yote yapo katika mpangilio na mwendelezo, hayajawahi kwenda nje ya mawanda yao au kwenda zaidi ya mipaka yao. Yote yanafuata mwelekeo mmoja kwa namna ya mpangilio, yakitiririka kuelekea mwelekeo yanaopaswa kwenda. Kwa hiyo chini ya sheria ya kanuni ya Mungu, hakuna mto au ziwa ambalo litakauka kiholela tu, au kubadilisha mwelekeo au kiwango cha kutiririka kwake kiholela tu kwa sababu ya mzunguko wa dunia au kupita kwa muda. Hii yote ipo ndani ya maarifa ya Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu miongoni akiwemo binadamu, vina sehemu zao, maeneo yao, na mipaka yao. Yaani, Mungu alipoviumba viumbe vyote, mipaka yao ilianzishwa na hii haiwezi kugeuzwa kiholela tu, kufanywa upya au kubadilishwa. “Kiholela” inamaanisha nini? Ina maana kwamba havitahama, kupanuka, au kubadilisha umbo lao asilia bila mpangilio kwa sababu ya hali ya hewa, halijoto, au kasi ya mzunguko wa dunia. Kwa mfano, mlima una kimo fulani, kitako chake ni cha eneo fulani, una mwinuko fulani, na una kiasi fulani cha uoto. Hii yote imepangwa na kukokotolewa na Mungu na haitabadilishwa kiholela. Kwa tambarare, idadi kubwa ya binadamu wanaishi katika tambarare, na hakuna mabadiliko ya hali ya hewa yatakayoathiri maeneo yao au thamani ya uwepo wao. Sio hata kile ambacho kimejumuishwa katika mandhari haya na mazingira ya kijiografia ambayo yaliumbwa na Mungu yatabadilika kiholela. Kwa mfano, vipengele vya jangwa ni vipi, ni aina gani ya madini yaliyopo chini ya ardhi, yanajumuisha mchanga kiasi gani na rangi ya mchanga, upana wake—haya hayatabadilika kiholela. Kwa nini hayatabadilika kiholela? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Ndani ya mandhari haya yote tofautitofauti na mazingira ya kijiografia yaliyoumbwa na Mungu, Anasimamia kila kitu kwa njia iliyopangwa na kwa mpangilio. Kwa hiyo mazingira haya yote ya kijiografia bado yapo kwa miaka elfu kadhaa, makumi elfu ya miaka baada ya kuwa yameumbwa na Mungu. Bado yanatimiza kila wajibu wao. Ingawa wakati wa vipindi fulani volkano hulipuka, wakati wa vipindi fulani matetemeko ya ardhi hutokea, na kuna mabadiliko makubwa ya ardhi, hakika Mungu hataruhusu aina yoyote ya mandhari kupoteza kazi yake ya asili. Ni kwa sababu tu ya usimamizi huu unaofanywa na Mungu, utawala Wake na udhibiti wa sheria hizi, kwamba yote haya—yote haya yanayofurahiwa na binadamu na kuonwa na binadamu—yanaweza kuendelea kuishi duniani kwa njia ya mpangilio. Sasa kwa nini Mungu anasimamia mandhari yote haya yaliyopo duniani kwa njia hii? Kusudi ni ili viumbe hai vinavyoendelea kuishi katika mazingira mbalimbali ya kijiografia yote yatakuwa na mazingira imara, na kwamba wataweza kuendelea kuishi na kuongezeka katika mazingira hayo imara. Vitu hivi vyote—vile vinavyotembea na vile ambavyo havitembei, vile ambavyo vinapumua kupitia mapua yao na vile ambavyo havitumii mapua—vinaunda mazingira ya tofauti kabisa kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ni aina hii tu ya mazingira ndiyo inaweza kulea kizazi baada ya kizazi cha binadamu, na ni aina hii tu ya mazingira inaweza kuruhusu binadamu kuendelea kuishi kwa amani, kizazi baada ya kizazi.
Yale nimetoka tu kuyazungumzia ni mada kubwa kiasi, kwa hivyo labda inaonekana imeondolewa maishani mwenu, lakini naamini nyote mnaweza kuyaelewa, sivyo? Yaani, sheria za Mungu katika utawala wake wa vitu vyote ni muhimu sana—muhimu sana! Je, masharti ya awali ni yapi kwa viumbe vyote kukua ndani ya sheria hizi? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu. Ni kwa sababu ya kanuni Yake ndipo vitu vyote vinafanya kazi zao ndani ya kanuni Yake. Kwa mfano, milima inalea misitu, halafu misitu inalea na kuwalinda ndege mbalimbali na wanyama wanaoishi ndani yake. Tambarare ni jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya binadamu kupanda mazao vilevile kwa ajili ya ndege na wanyama mbalimbali. Zinaruhusu idadi kubwa ya binadamu kuishi katika ardhi tambarare na kutoa hali isiyo na taabu katika maisha ya binadamu. Na tambarare pia zinajumuisha ukanda wa mbuga—malundo ya ukanda wa mbuga. Ukanda wa mbuga ni uoto wa nchi. Unalinda ardhi na kuwalea ng’ombe, kondoo na farasi wanaoishi katika ukanda wa mbuga. Jangwa pia linafanya kazi yake. Sio sehemu kwa ajili ya binadamu kuishi; jukumu lake ni kufanya hali ya hewa ya unyevunyevu kuwa kavu. Mitiririko ya mito na maziwa kunaleta hali isiyo ya usumbufu kwa ajili ya watu kunywa maji. Mahali popote yanapotiririka, watu watakuwa na maji kwa ajili ya kunywa, na mahitaji ya maji ya vitu vyote yataridhishwa kwa urahisi. Hii ni mipaka iliyochorwa na Mungu kwa ajili ya mandhari mbalimbali.
Sehemu ya Pili: Mungu Aweka Mipaka kwa Ajili ya Kiumbe Hai wa Kila Aina
Kwa sababu ya mipaka hii ambayo Mungu ameichora, mandhari mbalimbali yamezalisha mazingira tofautitofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na mazingira haya kwa ajili ya kuendelea kuishi yamekuwa na hali isiyokuwa na usumbufu kwa ajili ya aina tofautitofauti ya ndege na wanyama na vilevile kuleta nafasi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kutokana na hili, mipaka kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa viumbe hai mbalimbali imeendelezwa. Hii ndiyo hoja ya pili tutakayokwenda kuzungumzia baadaye. Kwanza kabisa ni aina gani ya mazingira ambamo ndege na wanyama na wadudu wanaishi? Je, wanaishi katika misitu na vijisitu? Haya ndiyo makazi yao. Kwa hivyo, kando na kuanzisha mipaka kwa ajili ya mazingira mbalimbali ya kijiografia, Mungu pia Aliweka mipaka kwa ajili ya ndege na wanyama, samaki, wadudu mbalimbali, na mimea yote. Pia alianzisha sheria. Kwa sababu ya tofauti za mazingira mbalimbali ya kijiografia na kwa sababu ya uwepo wa mazingira tofauti ya kijiografia, aina tofautitofauti za ndege na wanyama, samaki, wadudu, na mimea vina mazingira tofauti kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ndege na wanyama na wadudu wanaishi miongoni mwa mimea, samaki wanaishi majini, na mimea inakua kwenye nchi kavu. Nchi kavu inajumuisha maeneo mbalimbali kama vile milima, tambarare, na vilima. Punde tu ndege na wanyama wanapokuwa na makazi yao yasiyobadilika, hawataweza kuzungukazunguka wakielekea njia yeyote. Makazi yao ni misitu na milima. Ikiwa, siku moja makazi yao yataharibiwa, mpangilio utakuwa machafuko. Mara tu mpangilio huo unapokuwa machafuko, madhara yake ni yapi? Wa kwanza kuumizwa ni akina nani? Ni binadamu. Ndani ya sheria na mipaka hii ambayo Mungu ameianzisha, je, mmewahi kuona tukio lolote la ajabu? Kwa mfano, tembo wakitembea jangwani kwa kawaida. Mmewahi kuona tukio hilo? Kama ingekuwa hivyo, lingekuwa ni tukio la ajabu sana, kwa sababu tembo wanaishi msituni, na ni mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliwaandalia. Wana mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi na wana makazi yao yasiyobadilika, sasa kwa nini watangetange? Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuona simba au duma wakitembea ufuoni? Hapana, hamjawahi. Makazi ya simba na duma ni msituni na kwenye milima. Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kumwona nyangumi au papa wa bahari akiogelea kupitia jangwani? Hakuna ambaye ameona hayo, siyo? Nyangumi na papa makazi yao ni baharini. Katika mazingira ya kuishi ya binadamu, je, kuna watu ambao wanaishi pamoja na dubu wa kahawia? Je, kuna watu ambao siku zote wamezungukwa na tausi au ndege wengineo, ndani au nje ya makazi yao? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaona tai au bata bukini wa mwituni wakicheza na tumbili? (Hakuna.) Haya yatakuwa ni matukio ya pekee sana. Sababu Ninazungumza juu ya vitu hivi ambavyo vinaonekana kuwa vya kipekee masikioni mwenu ni kuwafanya muelewe kwamba vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu—haijalishi kama vimewekwa katika sehemu moja au iwapo vinapumua kupitia mapuani—vina sheria zao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Zamani kabla Mungu hajaumba viumbe hai hivi Alikuwa ameviandalia makazi yao, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai hivi vilikuwa na mazingira yao yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi, chakula chao, makazi yao yasiyobadilika, sehemu zao zisizobadilika zinazowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, maeneo yenye halijoto inayowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa njia hiyo wasingezungukazunguka au kuhafifisha hali ya mwanadamu kuendelea kuishi au kuathiri maisha yao. Hivi ndivyo Mungu anavyoongoza vitu vyote, akiwaandalia wanadamu mazingira mazuri kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai chini ya vitu vyote kila kimoja kina chakula chao kinachokimu maisha yao wenyewe ndani ya mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa chakula hicho, vinajifunga katika mazingira yao ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi. Katika aina hiyo ya mazingira bado vinaendelea kuishi, kuzaliana, na kuendelea kulingana na sheria za Mungu alizozianzisha kwa ajili yao. Kwa sababu ya aina hizi za sheria, kwa sababu ya majaaliwa ya Mungu, vitu vyote vinaishi kwa upatanifu na wanadamu, na wanadamu huishi pamoja na vitu vyote kwa kutegemeana.
Sehemu ya Tatu: Mungu Aendeleza Mazingira na Ekolojia ili Kumkuza Mwanadamu
Mungu aliviumba vitu vyote na akaanzisha mipaka kwa ajili yao; miongoni mwao Akalea aina zote za viumbe hai. Wakati huo, pia Aliandaa mbinu tofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, hivyo unaweza kuona kwamba binadamu hawana njia moja tu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Pia hawana aina moja tu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hapo kabla tulizungumza juu ya Mungu kuandaa aina mbalimbali za chakula na vyanzo vya maji kwa ajili ya binadamu, kitu ambacho ni muhimu sana kufanya uhai wa binadamu katika mwili kuendelea. Hata hivyo, miongoni mwa binadamu huyu, sio watu wote wanaishi kwa kula nafaka. Watu wana mbinu tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa sababu ya tofauti za mazingira ya kijiografia na mandhari. Mbinu hizi za kuendelea kuishi zote zimeandaliwa na Mungu. Hivyo si binadamu wote wanajihusisha na kilimo. Yaani, si watu wote wanapata chakula chao kwa kulima mazao. Hii ni hoja ya tatu ambayo tutakwenda kuizungumzia. Mipaka imetengenezwa kutokana na mitindo mbalimbali ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ni aina nyingine ipi ya mtindo wa maisha ambayo binadamu wanayo? Kwa suala la vyanzo tofauti vya vyakula, ni aina gani nyingine ya vyakula ambavyo wanadamu wanavyo? Kuna aina za msingi kadhaa.
Ya kwanza ni mtindo wa maisha wa uwindaji. Kila mmoja anajua hiyo ni nini. Watu wanaoishi kwa kuwinda wanakula nini? (Windo.) Wanakula ndege na wanyama wa mwituni. “Windo” ni neno la kisasa. Wawindaji hawaoni kwamba ni mchezo, wanaona kama chakula, kama riziki yao ya kila siku. Kwa mfano, wangepata paa. Wanapopata paa huyu ni sawa tu na mkulima kupata mazao kutoka ardhini. Mkulima hupata mazao kutoka ardhini, na anapoona mazao yake anakuwa na furaha na anahisi amani. Familia haitakuwa na njaa ya mazao ya kula. Moyo wake una amani na anahisi kuridhika. Na mwindaji pia anahisi amani na kuridhika akiangalia kile ambacho amekamata kwa sababu hana haja ya kuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula. Kuna kitu cha kula kwa ajili ya mlo unaofuata, hakuna haja ya kuwa na njaa. Huyu ni mtu ambaye anawinda kwa ajili ya kuishi. Wengi wa wale ambao hutegemea uwindaji wanaishi katika misitu ya milima. Hawalimi. Sio rahisi kupata ardhi inayolimika hapo, kwa hiyo wanaishi kwa kutegemea viumbe hai mbalimbali, aina mbalimbali za mawindo. Hii ni aina ya kwanza ya mtindo wa maisha ambao ni tofauti na ule wa watu wa kawaida.
Aina ya pili ni mtindo wa maisha wa ufugaji. Je, wale ambao wanafuga kwa ajili ya kuishi wanalima? (La.) Kwa hiyo sasa wanafanya nini? Wanaishije? (Kwa sehemu kubwa, wanafuga ng’ombe na kondoo kwa ajili ya kuishi, na msimu wa baridi wanawachinja na kuwala mifugo wao. Chakula chao cha msingi ni nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, na wanakunywa chai ya maziwa. Ingawa wafugaji ni wenye shughuli misimu yote minne, wanakula vizuri. Wana kiwango kikubwa cha maziwa, bidhaa za maziwa, na nyama.) Watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi kimsingi hula nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, hunywa maziwa ya kondoo na ng’ombe, na wanaendesha madume ya ng’ombe na farasi uwandani na upepo kwenye nywele zao, jua usoni pao. Hawana msongo wa mawazo juu ya maisha ya kisasa. Siku nzima wanaona tu upana wa wingu la bluu na tambarare za majani. Wengi wa watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi wanaishi kwenye uwanda wa mbuga na wanaweza kuendelea na mtindo wao wa maisha ya kuhamahama kwa kizazi baada ya kizazi. Ingawa maisha katika uwanda wa mbuga ni ya upweke kidogo, pia ni maisha ya furaha. Si mtindo mbaya wa maisha!
Aina ya tatu ni mtindo wa maisha ya uvuvi. Kuna sehemu ndogo ya binadamu wanaoishi pembezoni mwa bahari au kwenye visiwa vidogo. Wamezungukwa na maji, wakikabiliana na bahari. Watu hawa huvua kwa ajili ya kuishi. Ni nini chanzo cha chakula kwa wale wanaovua kwa ajili ya kuishi? Vyanzo vyao vya vyakula ni pamoja na aina zote za samaki, vyakula vya baharini, na mazao mengine ya baharini. Watu wanaovua kwa ajili ya kuishi hawalimi mashamba, lakini badala yake wao huenda kuvua kila siku. Chakula chao cha msingi kinajumuisha aina mbalimbali za samaki, na bidhaa za vyakula vya baharini. Mara chache waliweza kubadilishana bidhaa hizi na mchele, unga, na mahitaji ya kila siku. Huu ni mtindo tofauti wa maisha wa watu wanaoishi karibu na maji. Wale wanaoishi karibu na maji wanayategemea kwa ajili ya chakula chao, na uvuvi ni riziki yao. Ni chanzo cha riziki yao vilevile chanzo chao cha chakula.
Licha ya wale ambao hulima kwa ajili ya kuishi, kimsingi kuna aina tatu tofauti za mtindo wa maisha zilizotajwa hapo juu. Licha ya wale ambao wanaishi kwa kutegemea ufugaji, uvuvi, na kuwinda, idadi kubwa ya watu hulima kwa ajili ya chakula. Na watu wanaolima kwa ajili ya kuishi wanahitaji nini? Wanahitaji udongo. Wao wanategemea kupanda mazao kwa vizazi. Haijalishi wanapanda mbogamboga, matunda au nafaka, wanapata chakula chao na mahitaji yao ya kila siku kutoka ardhini.
Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Yaani, ikiwa wale wanaotegemea uwindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, chanzo cha riziki yao kingepotea. Mwelekeo ambao kabila hili na watu wa aina hii wanapaswa kuchukua ungekuwa wa mashaka, na hata huenda wakatoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao hutegemea nini? Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo yao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi—uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng’ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama hawangekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Yaani, kama kuna tatizo na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi, na zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, kama hawangeweza kupanda vitu, na kupata vyakula vyao kutoka kwa mimea mbalimbali, matokeo yake yangekuwa nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali. Mungu ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira—ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.
Ikiwa vitu vyote vya uumbaji vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za vitu vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa vitu vyote visingeweza kuendelea. Wanadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wangepoteza hayo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya wanadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia wanadamu viumbe vyote vya uumbaji kuvilea, kuwalea wanadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo. Kwa aina hiyo ya mazingira yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni ya kufaa na yapo katika mpangilio, aina zote za watu duniani, aina zote za jamii zinaweza kuishi ndani ya mawanda yao husika. Hakuna anayeweza kwenda zaidi ya mawanda haya au mipaka hii kwa sababu ni Mungu ambaye ameichora. Kwa nini Mungu aichore kwa namna hii? Hii ni muhimu sana kwa binadamu wote—ni muhimu sana! Mungu alichora mawanda ya kila aina ya kiumbe hai na aliweka mbinu ya kuendelea kuishi kwa kila aina ya binadamu. Pia aligawanya aina mbalimbali za watu na jamii mbalimbali duniani na akaweka mawanda yao. Hiki ndicho tunachotaka kujadili wakati ujao.
Sehemu ya Nne: Mungu Aweka Mipaka Kati ya Jamii Tofauti za Ulimwengu
Nne, Mungu alichora mipaka kati ya jamii za rangi tofautitofauti. Duniani kuna watu weupe, watu weusi, watu wa kahawia na watu wa njano. Hawa ni aina tofauti za watu. Mungu pia aliweka mawanda kwa ajili ya maisha ya aina hizi tofauti za watu, na bila kutambua, watu wanaishi ndani ya mazingira yao stahiki kwa kuendelea kuishi chini ya usimamizi wa Mungu. Hakuna anayeweza kwenda nje ya hapa. Kwa mfano, wazungu, ni maeneo gani ambayo wanaishi kwa kiasi kikubwa? Kwa kiasi kikubwa wanaishi Ulaya na Marekani. Watu weusi kimsingi wanaishi Afrika. Na watu wa rangi ya kahawia wanaishi ndani ya eneo gani? Hasa wanaishi Kusini-mashariki mwa Asia na Asia Kusini, kama vile Tailandi, Bara Hindi, Myanmar, Vietnam na Laos. Watu wenye rangi ya hudhurungi kimsingi wanaishi Asia, yaani, China, Japan, Korea ya Kusini na nchi nyinginezo kama hizo. Mungu amegawanya aina hizi tofautitofauti za jamii kwa usawa kiasi kwamba jamii hizi tofautitofauti zimegawanywa katika sehemu tofautitofauti za dunia. Katika sehemu tofautitofauti hizi za dunia, Mungu aliandaa zamani sana mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yanayofaa kwa ajili ya kila jamii tofauti ya binadamu. Ndani ya aina hizi za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi, Mungu amewaandalia rangi na vijenzi vya udongo. Kwa maneno mengine, vijenzi katika miili ya watu weupe havifanani na vile vilivyo ndani ya miili ya watu weusi, na pia ni tofauti na vijenzi vya miili ya watu wa jamii nyinginezo. Mungu alipoumba vitu vyote, tayari Alikuwa ameandaa mazingira ya namna hiyo kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa jamii hiyo. Lengo Lake katika hili lilikuwa kwamba pale ambapo aina hiyo ya watu inaanza kuongezeka, watakapoanza kuongezeka kwa idadi, wangeweza kuwekwa ndani ya mawanda hayo. Kabla Mungu hajawaumba binadamu alikuwa amekwishatafakari yote—Angeweza kutoa Ulaya na Amerika kwa watu weupe na kuwaruhusu kuliendeleza na kuendelea kuishi. Kwa hiyo Mungu alipokuwa anatengeneza dunia tayari Alikuwa na mpango, alikuwa na nia na kusudi katika kile alichokuwa anakiweka katika kipande hicho cha ardhi, na kile ambacho kingelelewa katika kipande hicho cha ardhi. Kwa mfano, Mungu zamani sana aliandaa mlima upi, tambarare ngapi, vyanzo vya maji vingapi, ni aina gani ya ndege na wanyama, samaki gani, na mimea gani ingeweza kuwepo katika ardhi hiyo. Alipokuwa anaandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina ya binadamu, kwa ajili ya jamii, Mungu aliangalia vipengele vingi vya masuala: mazingira ya kijiografia, vijenzi vya udongo, aina ya ndege na wanyama, ukubwa wa aina tofautitofauti za samaki, vijenzi katika samaki, ubora tofauti wa maji, vilevile aina tofauti za mimea…. Mungu alikuwa ameandaa yote hayo zamani sana. Mazingira ya aina hiyo ni mazingira ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaumba na kuyaandaa kwa ajili ya watu weupe na kwa hivyo ni yao kiasili. Mmeweza kuona kwamba Mungu alipoviumba vitu vyote Alitafakari sana na Alitenda kwa mpango? (Ndiyo, tumeona kwamba fikira za Mungu kwa aina mbalimbali za watu zilikuwa ni za uangalifu sana. Kwa mazingira aliyoyaumba kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina tofautitofauti za binadamu, aliandaa aina za ndege na wanyama na aina za samaki, milima mingapi na tambarare ngapi zitakuwepo. Yote haya yalifikiriwa kwa uangalifu sana na kwa usahihi.) Kwa mfano, vyakula wanavyokula wazungu hasa ni vipi? Vyakula ambavyo watu weupe wanakula ni tofauti sana na vyakula ambavyo watu wa Asia wanakula. Vyakula vikuu ambavyo watu weupe wanakula hasa ni nyama, mayai, maziwa, na kuku. Nafaka kama vile mkate na mchele kwa ujumla sio chakula kikuu ambacho kinawekwa pembeni mwa sahani. Hata pale wanapokula kachumbari ya mboga, wanaweka kiasi cha nyama ya kukaanga au kuku ndani yake. Hata kama wanakula vyakula vinavyotokana na ngano, wanaongeza siagi, mayai, au nyama kwenye chakula hicho. Hiyo ni kusema, vyakula vyao vikuu havijumuishi hasa vyakula vinavyotokana na ngano au mchele; wanakula sana nyama na siagi. Mara nyingi wanakunywa maji ya barafu kwa sababu wanakula vyakula vyenye kalori ya juu sana. Kwa hiyo watu weupe ni wenye afya kweli. Hivi ndivyo vyanzo vya maisha yao, mazingira yao kwa ajili ya kuishi yaliandaliwa na Mungu kwa ajili yao, yanawafanya wawe na aina hiyo ya mtindo wa maisha. Mtindo huo wa maisha ni tofauti na mitindo ya maisha ya watu wa jamii nyingine. Hakuna baya au zuri katika mtindo huu wa maisha—ni wa kuzaliwa, uliamuliwa kabla na Mungu na kwa sababu ya kanuni ya Mungu na mipangilio Yake. Aina hii ya mbari ina mtindo fulani wa maisha na vyanzo fulani vya riziki zao kitu ambacho ni kwa sababu ya mbari yao, vilevile ni kwa sababu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoandaliwa na Mungu kwa ajili yao. Mngeweza kusema kwamba mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili ya watu weupe na chakula cha kila siku wanachokipata kutoka katika mazingira hayo ni kingi na kimejaa tele.
Mungu pia aliandaa mazingira yanayofaa kwa ajili ya mbari nyingine kuendelea kuishi. Pia kuna watu weusi—watu weusi wanapatikana wapi? Hasa wanapatikana katikati na kusini mwa Afrika. Mungu aliwaandalia nini kwa ajili ya kuishi katika aina hiyo ya mazingira? Misitu ya kitropiki, aina zote za ndege na wanyama, pia majangwa, na aina zote za mimea ambayo inaambatana nao. Wana vyanzo vya maji, riziki zao, na chakula. Mungu hakuwabagua. Bila kujali kile walichowahi kukifanya, kuendelea kuishi kwao hakujawahi kuwa tatizo. Pia wanachukua mahali fulani maalumu na eneo fulani katika sehemu ya dunia.
Sasa, hebu tuzungumze kidogo kuhusu watu wa njano. Watu wa njano hasa wanapatikana nchi za Mashariki. Kuna tofauti gani kati ya mazingira na sehemu za kijiografia za nchi za Mashariki na nchi za Magharibi? Katika nchi za Mashariki, eneo kubwa la ardhi ni la rutuba, na zina hazina kubwa ya vitu na madini. Yaani, aina zote za rasilimali za juu ya ardhi na za chini ya ardhi zimejaa tele. Na kwa kundi hili la watu, kwa mbari hii, Mungu pia aliandaa udongo, hali ya hewa inayofanana nao, na mazingira mbalimbali ya kijiografia ambayo yanawafaa. Ingawa kuna tofauti kubwa kati ya mazingira hayo ya kijiografia na mazingira ya nchi za Magharibi, chakula cha lazima cha watu, riziki, na vyanzo kwa ajili ya kuendelea kuishi viliandaliwa na Mungu. Ni mazingira tofauti tu kwa ajili ya kuishi kuliko yale ambayo watu weupe wanayo katika nchi za Magharibi. Lakini ni kitu kipi kimoja ambacho Ninahitaji kuvuta usikivu wenu, ambacho Ninahitaji kuwaambia? Idadi ya mbari ya Mashariki kiasi fulani ni kubwa, hivyo Mungu aliongeza vipengele vingi katika kipande hicho cha ardhi ambavyo ni tofauti na vya Magharibi. Katika upande huo wa dunia, Aliongeza mandhari mengi mbalimbali na aina zote za vitu vingi. Huko rasilimali za asili ni tele; mandhari pia yanatofautiana na anuwai, yanatosha kwa ajili ya kulea idadi kubwa ya mbari ya Mashariki. Kitu fulani ambacho ni tofauti na Magharibi ni kwamba Mashariki—kutoka kusini kwenda kaskazini, kutoka mashariki kwenda magharibi—hali ya hewa ni nzuri kuliko ya Magharibi. Misimu minne imeoneshwa kinaganaga, hali ya joto ni nzuri, rasilimali za asili zipo tele, mazingira ya asili na aina za mandhari ni mazuri zaidi kuliko ya Magharibi. Kwa nini Mungu alifanya hivi? Mungu alitengeneza uwiano razini kabisa kati ya watu weupe na watu wa njano. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa kila kipengele cha chakula chao, vitu ambavyo wanatumia, kile ambacho watu weupe wanacho cha kujifurahisha ni kizuri zaidi kuliko kile ambacho watu wa njano wanaweza kukifurahia. Hata hivyo, Mungu habagui mbari yoyote. Mungu aliwapatia watu wa njano mazingira mazuri na bora zaidi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hii ni uwiano.
Mungu amjalia kabla ni aina gani ya watu wanastahili kuishi katika sehemu ipi ya dunia; je, wanadamu wanaweza kupita hii mipaka? (La.) Kitu cha ajabu kweli! Hata kama kuna vita au uvamizi katika enzi mbalimbali au nyakati fulani, vita hivi, uvamizi huu, hakika hauwezi kuharibu mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaamua kabla kwa ajili ya kila mbari. Yaani, Mungu amewaweka aina fulani ya watu katika eneo fulani la dunia na hawawezi kwenda nje ya mawanda hayo. Hata kama watu wana lengo la kubadilisha au kuongeza eneo lao, bila ruhusa ya Mungu, hii itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Kwa mfano, watu weupe walitaka kuongeza maeneo yao na wakazitawala kwa mabavu baadhi ya nchi. Wajerumani walivamia baadhi ya nchi, Uingereza waliitwaa India. Matokeo yalikuwa ni nini? Mwishowe walishindwa. Tunaona nini kutokana na kushindwa huku? Kile ambacho Mungu amekiamua kabla hakiwezi kuharibiwa. Kwa hiyo, haijalishi ni nguvu kubwa kiasi gani ambayo umeweza kuiona katika upanuzi wa Uingereza, mwishowe walitakiwa bado kuondoka, na kuacha ardhi hiyo ikiwa bado ni ya India. Wale ambao wanaishi katika ardhi hiyo bado ni Wahindi, na si Waingereza. Hii ni kwa sababu ni kitu ambacho Mungu haruhusu. Baadhi ya wale ambao wanatafiti historia au siasa wametoa tasnifu juu ya hili. Wanatoa sababu kwa nini Uingereza ilishindwa, wanasema kwamba pengine ilikuwa ni kwa sababu mbari fulani isingeweza kushindwa, au pengine ni kwa sababu ya sababu nyinginezo za kibinadamu.… Hizi sio sababu za kweli. Sababu ya kweli ni kwa sababu ya Mungu—Haruhusu hilo! Mungu anaamua mbari waishi katika nchi fulani na Anawaweka hapo, na kama Mungu hawaruhusu kuhama hawataweza kuhama kamwe. Ikiwa Mungu ataamua mawanda kwa ajili yao, wataishi ndani ya mawanda hayo. Binadamu hawezi kuvunja bure au kwenda nje ya mawanda haya. Hii ni hakika. Haijalishi nguvu za wavamizi ni kubwa kiasi gani, au jinsi gani wale wanaovamiwa ni dhaifu, mafanikio yao mwishowe yanamtegemea Mungu. Ameshaliamua hili tayari na hakuna anayeweza kulibadilisha.
Haya ya juu ndivyo Mungu alivyogawanya mbari mbalimbali. Ni kazi gani ambayo Mungu amefanya kuzigawanya mbari? Kwanza, aliandaa mazingira makubwa ya kijiografia, Akiwapa watu maeneo tofautitofauti, na kisha kizazi baada ya kizazi kinaendelea kuishi pale. Hii imeamuliwa—mawanda ya kuendelea kuishi kwao yameamuliwa. Na maisha yao, kile wanachokula, kile wanachokunywa, riziki zao—Mungu aliamua hayo yote zamani sana. Na Mungu alipokuwa anaumba vitu vyote, Alifanya maandalizi tofautitofauti kwa ajili ya aina tofauti za watu: Kuna vijenzi tofautitofauti vya udongo, hali ya hewa tofauti, mimea tofauti, na mazingira tofauti ya kijiografia. Maeneo tofautitofauti yana hata ndege na wanyama tofauti, maji tofauti yana aina tofauti za samaki wao spesheli na bidhaa za majini. Hata aina ya wadudu inaamuliwa na Mungu. Kwa mfano, vitu ambavyo vinakua katika bara la Marekani vyote ni vikubwa sana, virefu sana na vyenye nguvu sana. Mizizi ya miti kwenye mlima wa msitu yote haina kina kirefu kabisa, lakini inakua mirefu sana. Inaweza kurefuka hadi kimo cha mita mia moja au zaidi, lakini miti katika misitu ya Asia kwa kiasi kikubwa siyo mirefu sana. Chukua mimea ya mshubiri kwa mfano. Nchini Japani, mimea hii ni midogo sana na miembamba sana, lakini mimea ya mshubiri nchini Marekani ni mikubwa mno. Hii ni tofauti. Ni aina ile ile ya mmea ikiwa na jina lile lile, lakini katika bara la Marekani ni kubwa hasa. Tofauti katika vipengele hivi tofautitofauti zinaweza zisionekane au kufahamika kwa watu, lakini Mungu alipokuwa anaumba vitu vyote, alivionyesha kinaganaga na aliandaa mazingira tofauti ya kijiografia, mandhari tofauti, na viumbe hai tofauti kwa ajili ya mbari mbalimbali. Hiyo ni kwa sababu Mungu aliumba aina tofautitofauti za watu, na Anajua kile ambacho kila mmoja anahitaji na mitindo yao ya maisha ni nini.
Mungu Atawala Vitu Vyote na Kuruzuku Vitu Vyote, Yeye Ndiye Mungu wa Vitu Vyote
Baada ya kuzungumza juu ya baadhi ya vitu hivi, sasa mna uelewa fulani wa mada kuu ambayo tumeijadili hivi punde? Je, mmeielewa kwa kiasi fulani? Kuna sababu ambayo nimeongea kuhusu mambo haya ndani ya mada pana—sasa mnapaswa kuwa mmeelewa angalau kwa muhtasari, sivyo? Mnaweza kuniambia mmeelewa kwa kiasi gani. (Binadamu wote wamelelewa kwa sheria ambazo ziliamuliwa na Mungu kwa ajili ya vitu vyote. Mungu alipokuwa anaamua sheria hizi, Aliandaa mbari tofautitofauti zikiwa na mazingira tofauti, mitindo tofauti ya maisha, vyakula tofauti, na hali ya hewa na halijoto tofauti. Hii ilikuwa hivyo ili binadamu wote waweze kuishi duniani na kuendelea kuishi. Kutokana na hili naweza kuona mipango ya Mungu ya kuendelea kwao kuishi yako dhahiri sana na ninaweza kuona hekima Yake na ukamilifu Wake, na upendo Wake kwa sisi binadamu.) (Sheria na mawanda yaliyoamuliwa na Mungu hayawezi kubadilishwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Yote ipo chini ya kanuni Yake.) Tukiangalia kwa mtazamo wa sheria zilizoamriwa na Mungu kwa ukuaji wa vitu vyote, yote hii si kwa ajili ya mwanadamu, haijalishi ni wa aina gani, anaishi chini ya uangalizi wa Mungu—je, wote hawaishi chini ya malezi Yake? Ikiwa sheria hizi zingeharibiwa au Mungu hakuanzisha aina hizi za sheria kwa ajili ya binadamu, majaliwa yao yangekuwa ni nini? Baada ya binadamu kupoteza mazingira yao ya msingi kwa ajili ya kuendelea kuishi, je, wangekuwa na chanzo chochote cha chakula? Inawezekana kwamba vyanzo vya chakula vingekuwa tatizo. Ikiwa watu wangepoteza vyanzo vyao vya chakula, yaani, ikiwa hawangeweza kupata kitu chochote cha kula, ni siku ngapi wangeweza kuvumilia? Pengine wasingeweza kuvumilia hata kwa mwezi mmoja, na kuendelea kuishi kwao kungekuwa ni tatizo. Kwa hiyo kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa ajili ya watu kuendelea kuishi, kwa ajili ya wao kuendelea kuwepo, kuongezeka, na ruzuku ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya miongoni mwa vitu vyote vinahusiana kwa karibu na haviwezi kutenganishwa na watu kuendelea kuishi. Ikiwa kuendelea kuishi kwa binadamu kulikuwa tatizo, je, usimamizi wa Mungu ungeweza kuendelea? Je, usimamizi wa Mungu bado ungekuwepo? Usimamizi wa Mungu unakwenda sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu wote ambao Anawalea, kwa hivyo haijalishi Mungu anaandaa kitu gani kwa ajili ya vitu vyote na kile Anachofanya kwa ajili ya binadamu, hii yote ndiyo lazima Kwake, na ni muhimu sana kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ikiwa sheria zote hizi ambazo Mungu aliziamua kwa ajili ya vitu vyote zingekuwa zimeachwa, ikiwa sheria hizi zingekuwa zimevunjwa au zimeharibiwa, vitu vyote visingeweza kuwepo, mazingira ya binadamu ya kuendelea kuwepo yasingekuwepo, na wala riziki zao za kila siku, na wala wao wenyewe. Kwa sababu hii, Usimamizi wa Mungu wa wokovu wa binadamu wala nao usingekuwepo pia.
Kila kitu ambacho tumejadili, kila kitu, kila kipengele kimeungana kikamilifu na kuendelea kuishi kwa kila mtu. Mnaweza kusema, “Unachokizungumzia ni kikubwa sana, hatuwezi kukiona,” na pengine kuna watu ambao wangeweza kusema “Unachokizungumzia hakinihusu.” Hata hivyo, usisahau kwamba unaishi kama sehemu tu ya vitu vyote; wewe ni mshirika wa vitu vyote ndani ya kanuni ya Mungu. Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake. Baadhi ya watu wanasema: “Mimi sio mkulima, sipandi mazao kwa ajili ya kuishi. Sitegemei mbingu ili nipate chakula changu, kwa hiyo siendelei kuishi katika mazingira ambayo aliyaanzisha Mungu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Aina hiyo ya mazingira haijanipatia kitu chochote.” Hii ni kweli? Unasema kwamba hupandi mazao kwa ajili ya kuishi, lakini huli nafaka? Huli nyama na mayai? Je, huli mbogamboga na matunda. Kila kitu unachokula, vitu hivi vyote unavyovitaka havitenganishwi na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoanzishwa na Mungu kwa ajili ya binadamu. Na chanzo cha kila kitu ambacho binadamu anahitaji hakiwezi kutenganishwa na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, aina hizo za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Maji unayokunywa, nguo unazovaa, na vitu vyote unavyotumia—ni kitu gani kati ya hivi ambacho hakipatikani kutoka katika vitu hivi vyote? Baadhi ya watu husema: “Kuna baadhi ya vitu ambavyo havipatikani kutoka katika vitu vyote hivi. Unaona, plastiki haitokani na vitu vyote hivi. Ni kitu cha kemikali, kitu kilichotengenezwa na mwanadamu.” Hii ni sahihi? Plastiki imetengenezwa na mwanadamu, ni kitu cha kemikali, lakini vijenzi asilia vya plastiki vilitoka wapi? Vijenzi asilia vilipatikana kutoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu. Vitu ambavyo unavifurahia, ambavyo unaona, kila kitu ambacho unatumia, vyote vinapatikana kutoka katika vitu vyote ambavyo vilitengenezwa na Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, haijalishi ni mbari gani, haijalishi ni riziki gani, au ni katika aina gani ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo watu wanaishi, hawawezi kujitenganisha na uangalizi wa Mungu. Kwa hiyo mambo haya tuliyoyajadili leo yanahusiana na mada yetu ya “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? Je, vitu tulivyovijadili leo vinaangukia chini ya mada hii kubwa? (Ndiyo.) Pengine baadhi ya ambayo nimeyazungumzia leo ni ya kidhahania kidogo na ni vigumu kidogo kuweza kuyajadili. Hata hivyo, Nadhani kwamba sasa mnaelewa vizuri kidogo.
Nyakati chache hizi katika ushirika, kiwango cha mada ambazo tumekuwa nazo katika ushirika ni kipana sana, na mawanda yao ni mapana, kwa hiyo unapaswa uwe na jitihada kiasi fulani ili uweze kuzielewa zote. Hii ni kwa sababu mada hizi ni vitu ambavyo watu hawajawahi kukabiliana navyo katika imani yao kwa Mungu. Baadhi ya watu wanaisikia kama muujiza na baadhi ya watu wanaisikia kama hadithi—mtazamo gani ni sahihi? Unasikia haya yote kutoka katika mtazamo gani? (Tumeona jinsi Mungu amepanga vitu vyote kwa mbinu yenye mpangilio na kwamba vitu vyote vina sheria hizi na kupitia maneno haya tunaweza kuelewa zaidi juu ya matendo ya Mungu na mpangilio wake angalifu na sahihi kwa ajili ya kumwokoa binadamu.) Kupitia nyakati hizi katika ushirika, Mmeona mawanda ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote ni nini? (Binadamu wote, kila kitu.) Je, Mungu ni Mungu wa mbari moja? Je, ni Mungu wa aina moja ya watu? Je, ni Mungu wa eneo dogo la binadamu? (Hapana, hayupo hivyo.) Kwa kuwa Hayupo hivyo, katika maarifa ya watu juu ya Mungu, ikiwa angekuwa ni Mungu wa sehemu ndogo tu ya binadamu, au ikiwa unaamini kwamba Mungu ni Mungu wako tu, je, mtazamo huu upo sahihi? Kwa kuwa Mungu anasimamia na kutawala vitu vyote, watu wanapaswa kuona matendo Yake, hekima Yake, na ukuu Wake ambavyo vimefunuliwa katika utawala Wake wa vitu vyote. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kufahamu. Ikiwa unasema kwamba Mungu anasimamia vitu vyote, na Anatawala juu ya vitu vyote, lakini kama huna uelewa wowote au umaizi katika utawala Wake kwa binadamu, je, unaweza kutambua kwamba Anatawala vitu vyote? Unaweza kufikiri moyoni mwako, “Ninaweza, kwa sababu ninaona kwamba maisha yangu haya yote yanatawaliwa na Mungu.” Je, kweli Mungu ni mdogo kiasi hicho? Hayupo hivyo! Unaona tu wokovu wa Mungu kwa ajili yako na kazi yake kwako, na kutokana na vitu hivi unauona utawala Wake. Hayo ni mawanda finyu sana, na yana athari katika maarifa yako halisi juu ya Mungu. Pia yanaweka mipaka kwenye maarifa yako halisi juu ya utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Ikiwa unayawekea mipaka maarifa yako kuhusu Mungu kwenye mawanda ya kile ambacho Mungu anatoa kwa ajili yako na wokovu Wake kwa ajili yako, hutaweza kutambua kwamba anatawala kila kitu, kwamba anatawala vitu vyote, na anatawala binadamu wote. Unaposhindwa kutambua haya yote, je, kweli unaweza kutambua ukweli kwamba Mungu anatawala majaliwa yako? Huwezi. Moyoni mwako hutaweza kutambua kipengele hicho—hutoweza kutambua kiwango hicho. Unaelewa, siyo? Kwa kweli, Ninajua ni kwa kiwango gani mnaweza kuelewa mada hizi, maudhui haya ninayoyazungumzia, sasa kwa nini Naendelea kuizungumzia? Ni kwa sababu mada hizi ni mambo ambayo yanapaswa kueleweka kwa kila mfuasi wa Mungu, kila mtu ambaye anataka kuokolewa na Mungu—anapaswa kuelewa mada hizi. Ingawa, kwa kipindi hiki ambacho huzielewi, siku moja, ambapo maisha yako na uzoefu wako wa ukweli utafikia kiwango fulani, pale ambapo mabadiliko yako ya tabia yako ya maisha yanafikia kiwango fulani na kimo chako kinaongezeka kwa kiwango fulani, ni wakati huo tu ndio mada hizi ambazo naziwasilisha kwako katika ushirika zitakimu na kuridhisha utafutaji wako wa maarifa ya Mungu. Kwa hiyo maneno haya yalikuwa ni kwa ajili ya kuweka msingi, kuwaandaa kwa ajili ya uelewa wenu wa baadaye kwamba Mungu anatawala vitu vyote na kwa ajili ya uelewa wenu wa Mungu Mwenyewe.
Vyovyote vile uelewa juu ya Mungu ulivyo mkubwa katika mioyo ya watu, unaamua nafasi kubwa kiasi gani Anachukua katika mioyo yao. Vyovyote vile kiwango cha maarifa ya Mungu kilivyo katika mioyo yao ndivyo kwa kiwango kikubwa Mungu alivyo katika mioyo yao. Ikiwa Mungu unayemfahamu yupo tupu na ni yule asiye yakini, basi yule Mungu unayemwamini pia ni tupu na ni yule asiye yakini. Mungu unayemfahamu anaishia ndani ya mipaka ya upeo wa maisha yako binafsi, na hahusiani na Mungu wa kweli Mwenyewe. Kwa hiyo, kuyajua matendo ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote—haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya yana uhusiano wa moja kwa moja na iwapo watu wanaweza kuingia kwa uhalisi wa ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba yule Mungu unayemwamini si Mungu Mwenyewe wa kweli kabisa, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini ni Mungu wa fikira tu, si Mungu wa kweli. Hii ni kwa sababu Mungu wa kweli ni Yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote. Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaelekeza wanadamu, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Lengo Langu la kusema haya yote ni lipi? Iko hivyo ili usiweze kulichukulia hili kirahisi, ili msiamini kwamba mada hizi Nilizozizungumzia hazina uhusiano na kuingia kwenu binafsi katika maisha, na ili msichukue mada hizi kama tu aina ya maarifa au mafundisho. Ikiwa unasikiliza ukiwa na mtazamo kama huo, hutapata kitu hata kimoja. Mtapoteza fursa kubwa hii ya kumjua Mungu.
Lengo Langu la kuzungumza juu ya mambo haya yote ni nini? Lengo langu ni kuwafanya watu wamjue Mungu, kuwafanya watu waelewe matendo halisi ya Mungu. Mara utakapomuelewa Mungu na ukaelewa matendo Yake, ni baada ya hapo tu ndipo utakuwa na fursa au uwezekano wa kumjua Mungu. Kwa mfano, ikiwa unataka kumwelewa mtu, ni jinsi gani unaweza kumwelewa? Je, inaweza kuwa kupitia kuangalia umbo lao la nje? Je, inaweza kuwa kupitia kile wanachokivaa, jinsi wanavyovaa? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia jinsi wanavyotembea? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia mawanda ya maarifa yao? (Hapana.) Kwa hiyo unamwelewaje mtu? Unafanya hukumu kupitia maneno na tabia ya mtu, kupitia mawazo zake, kupitia kile anachokionyesha na kile anachokifichua. Hivyo ndivyo unavyomjua mtu, unavyomwelewa mtu. Kwa njia ile ile, ikiwa mnahitaji kumjua Mungu, ikiwa mnataka kuelewa upande Wake wa vitendo, upande Wake wa kweli, mnapaswa kumjua Yeye kupitia matendo Yake na kupitika kila kitu halisi Anachofanya. Hii ndiyo njia bora zaidi na ndiyo njia pekee.
Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi
Mungu anadhihirisha matendo Yake miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa vitu vyote Anavyovitawala na Anashikilia sheria za vitu vyote. Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao. Hii pia ni mada kubwa sana kwenu. Kuweka uwiano wa uhusiano kati ya vitu vyote—je, hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kufanya? Binadamu wenyewe hawawezi. Watu wanaweza tu kuharibu. Hawawezi kuweka uwiano wa uhusiano kati ya vitu vyote; hawawezi kuvisimamia, wala hawana mamlaka makubwa hayo au nguvu. Ni Mungu Mwenyewe ndiye ana aina ya nguvu kuweza kufanya kitu cha aina hii. Kusudi la Mungu la kufanya kitu cha aina hii—kinamsaidia nini? Ni vilevile, inafanana kwa ukaribu na kuendelea kuishi kwa binadamu. Kila kitu ambacho Mungu anataka kufanya ni cha lazima—hakuna kitu ambacho Anaweza au asiweze kufanya. Ili Yeye alinde kuendelea kuishi kwa binadamu na kuwapatia watu mazingira yanayofaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, kuna vitu fulani vya lazima, vitu fulani vya muhimu sana ambavyo ni lazima Afanye kulinda kuendelea kuishi kwao.
Kutokana na maana ya moja kwa moja ya kirai “Mungu anaweka uwiano kwa vitu vyote,” ni mada pana sana; kwanza inakupatia dhana ili uweze kujua kwamba kuweka uwiano kwa vitu vyote ni utawala wa Mungu kwa vitu vyote. Neno hili “uwiano” linamaanisha nini? Kwanza, “uwiano” unamaanisha kutoruhusu kitu fulani kutoka nje ya uwiano. Ni kama kutumia mizani kupima vitu. Ili kuweka uwiano kwenye mizani, uzito wa kila upande lazima uwe sawa. Mungu aliumba vitu vingi miongoni mwa vitu vyote—Aliumba vitu ambavyo havibadiliki, vitu ambavyo vinajongea, vitu ambavyo vinaishi, na vitu ambavyo vinapumua, vilevile vile ambavyo havipumui. Je, ni rahisi kwa vitu hivi vyote kupata uhusiano wa kutegemeana, wa kusaidiana na kuzuiana, wa kuingiliana? Kwa hakika kuna kanuni fulani ndani ya jambo hili. Inatatiza sana, siyo? Sio vigumu kwa Mungu, lakini kwa watu, inatatia sana kufanya utafiti. Ni neno rahisi sana—uwiano. Hata hivyo, ikiwa watu wangelitafiti, ikiwa watu wangehitaji kutengeneza uwiano, basi hata kama wanataaluma wangekuwa wanalifanyia kazi—wanabiolojia wa kibinadamu, mamajusi, wanafizikia, wakemia na hata wanahistoria—matokeo ya mwisho ya utafiti huo yangekuwa ni yapi? Matokeo yake yasingekuwa chochote. Hii ni kwa sababu uumbaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa ajabu sana na binadamu kamwe hataweza kufungua siri zake. Mungu alipoviumba vitu vyote, Alianzisha kanuni kati yao, Alianzisha njia tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa ajili ya kuzuiana, kukamilishana, kuheshimiana, na riziki. Mbinu hizi mbalimbali zinatatiza sana; si rahisi au za kuelekea upande mmoja. Watu wanapotumia akili zao, maarifa ambayo wamepata, na matukio ambayo wameona kuthibitisha au kutafiti kanuni zinazoongoza udhibiti wa Mungu wa vitu vyote, vitu hivi ni vigumu sana kuvigundua, na pia ni vigumu sana kupata matokeo yoyote. Inaweza ikasemwa kwamba ni vigumu sana watu kupata matokeo yoyote. Ni vigumu sana kwa watu kupata matokeo yoyote; ni vigumu sana kwa watu kudumisha uwiano wao wanapoongoza vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu kwa kutegemea fikira na maarifa ya kibinadamu. Hii ni kwa sababu kama watu hawafahamu kanuni za kuendelea kuishi kwa vitu vyote, hawatajua jinsi ya kulinda aina hii ya uwiano. Kwa hiyo, ikiwa watu wangeweza kusimamia na kuongoza vitu vyote vya Mungu, kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kuharibu uwiano. Mara tu utakapoharibiwa, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi yangeweza kuharibiwa, na hiyo inapotokea, ingeweza kufuatiwa na mgogoro kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao. Ingesababisha janga. Binadamu anapoishi katikati ya janga, nini kingeweza kutokea mbele yao? Yangekuwa ni matokeo ambayo ni vigumu kuyakisia, vigumu kuyabashiri.
Basi ni jinsi gani Mungu anaweka uwiano kwenye uhusiano kati ya vitu vyote? Kwanza, kuna baadhi ya maeneo duniani ambayo yamefunikwa na barafu na theluji kwa mwaka mzima, wakati katika baadhi ya maeneo, misimu yote minne ni kama msimu wa machipuo. Hutoweza kabisa kuona kipande cha barafu au chembe ya theluji—hakuna msimu wa baridi. Hii ni njia moja—ni kutokana na mtazamo mkubwa wa hali ya hewa. Njia ya pili ni hii: Safu ya milima iliyofunikwa na uoto uliostawi sana, ambapo aina zote za mimea inafunika ardhi; kuna malundo ya msitu na unapotembea katikati yao huwezi hata kuona jua. Katika milima mingine nyasi hata hazioti—kuna safu na safu za milima yenye ukame, isiyokaliwa. Ukiangalia kwa nje, yote ni milima yenye mchanga uliorundikana. Kundi moja la milima limejaa uoto uliositawi, na kundi jingine halina hata nyasi. Hii ni aina ya pili. Katika aina ya tatu, unaweza kuona tabaka la mbuga lisilokuwa na kikomo, uwanda wa kijani unaopunga. Au unaweza kuona jangwa kadri jicho linavyoweza kuona; huoni kiumbe hai yeyote, wala chanzo chochote cha maji, ni sauti tu ya upepo pamoja na mchanga. Katika aina ya nne, sehemu moja imefunikwa na bahari, ambayo imeundwa na eneo kubwa la maji, wakati katika sehemu nyingine unahangaika sana kutafuta chemchemi ya maji. Katika aina ya tano, katika nchi moja mvua ya manyunyu inanyesha mfululizo na ina ukungu na unyevunyevu, wakati kwenye nchi nyingine siku za jua kali ni za kawaida sana na hutaona hata tone moja la mvua. Katika aina ya sita, aina moja ya sehemu ni nchi tambarare ambapo hewa ni finyu sana na ni vigumu kwa binadamu kupumua, na katika aina nyingine ya eneo kuna kinamasi na nyanda za chini, ambayo yanatumika kama makazi ya aina mbalimbali ya ndege wahamao. Hizi ni aina tofautitofauti za tabia ya nchi, au tabia za nchi au mazingira ambayo yanaitikia mazingira tofautitofauti ya kijiografia. Hiyo ni sawa na kusema, Mungu anaweka uwiano kwenye mazingira ya msingi ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi kutoka katika mtazamo wa mazingira makubwa, kutoka katika tabia ya nchi kwenda katika mazingira ya kijiografia, kutoka katika vijenzi tofauti vya udongo kwenye kiwango cha vyanzo vya maji ili kupata uwiano kwenye hewa, halijoto na unyevunyevu wa mazingira ambamo watu wanaendelea kuishi. Kwa tofauti hizi za mazingira tofauti ya kijiografia, watu watakuwa na hewa imara na halijoto na unyevunyevu katika misimu tofautitofauti vitakuwa imara. Hii inawaruhusu watu kuendelea kuishi katika aina hiyo ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi siku zote. Kwanza, mazingira makubwa yanapaswa kuwekewa uwiano. Hii inafanyika kupitia kutumia kikamilifu maeneo mbalimbali ya kijiografia na muundo na vilevile muachano kati ya hali za nchi tofautitofauti kwa ajili ya kuzuiana ili kupata uwiano ambao Mungu anataka na ambao binadamu anahitaji. Hii ni kutokana na mtazamo wa mazingira makubwa.
Ukiangalia kwenye maelezo, kama vile uoto, inawezekanaje kuifanya hiyo ipate uwiano? Yaani, ni jinsi gani uoto unaweza kuruhusiwa kuendelea kuishi ndani ya mazingira yenye uwiano kwa ajili ya kuendelea kuishi? Ni kwa kusimamia urefu wa maisha, viwango vya ukuaji, na viwango vya kuzaliana vya aina mbalimbali za mimea ili kulinda mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Chukulia nyasi dogo kama mfano—wakati wa machipuo linachipua, wakati wa kiangazi linatoa maua, na wakati wa majira ya kupukutika majani linatoa matunda. Tunda linaanguka kwenye ardhi. Mwaka ujao, mbegu kutoka kwenye tunda inachipua na kukua kulingana na sheria zile zile. Urefu wa maisha ya nyasi ni mafupi sana. Kila mbegu inaanguka ardhini, inakuza mizizi na kuchipuka, inaweka maua na kuzaa matunda—hatua hii inatokea tu wakati wa machipuo, kiangazi na kupukutika, Aina zote za miti pia zina urefu wao wa maisha na vipindi tofauti kwa ajili ya kuchipua na kuzaa matunda. Baadhi ya miti hufa baada tu ya miaka 30 hadi 50—ina urefu wa maisha ya kuanzia miaka 30 hadi 50, lakini matunda yao huanguka ardhini, ambayo kisha hukuza mizizi na machipuko, maua na kuzaa tunda, na kuishi kwa miaka mingine 30 hadi 50. Hiki ndicho kiwango cha kujirudia kwake. Mti mzee unakufa na mti mdogo unakua—hii ndio maana siku zote unaona miti inaendelea kukua msituni. Lakini pia ina mzunguko wao mzuri na mchakato ama kuzaliwa na kufa. Baadhi ya miti inaweza kuishi kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu moja, na baadhi inaweza kuishi kwa hata miaka elfu tatu. Haijalishi ni aina gani ya mmea au urefu wao wa maisha ni mrefu kiasi gani, nikizungumza kwa ujumla, Mungu anasimamia uwiano wake kulingana na kipindi unachoishi, uwezo wake wa kuzaliana, kasi yake ya kuzaliana vilevile kiasi na kiwango chake cha kuzaliana. Hii inawaruhusu, kuanzia majani hadi miti, kuweza kuendelea kusitawi, kukua ndani ya mazingira ya kiikolojia yenye uwiano. Kwa hiyo unapoangalia msitu duniani, haijalishi kama ni miti au majani, unaendelea kujizalisha na kukua kulingana na sheria zake. Haihitaji msaada wa binadamu; haihitaji kazi yoyote ya ziada kutoka kwa binadamu. Ni kwa sababu tu wana aina hii ya uwiano ndipo wana uwezo wa kudumisha mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ni kwa sababu tu wana mazingira yanayofaa kwa ajili ya kuendelea kuishi ndipo misitu hii, kanda hizi za mbuga zinaweza kuendelea kuishi duniani. Uwepo wao unalea kizazi baada ya kizazi cha watu vilevile kizazi baada ya kizazi cha aina zote za viumbe hai vyenye makazi misituni na kwenye kanda za mbuga—ndege na wanyama, wadudu, na aina zote za vijiumbe.
Mungu pia anadhibiti uwiano wa aina zote za wanyama. Anadhibiti vipi uwiano huu? Ni sawa na kwenye mimea—anasimamia uwiano wao na anaamua idadi yao kulingana na uwezo wao wa kuzaliana, ukubwa na kiwango cha kuzaliana kwao na wajibu wanaoufanya miongoni mwa wanyama. Kwa mfano, simba hula pundamilia, kwa hiyo ikiwa idadi ya simba ingezidi idadi ya pundamilia, hatima ya pundamilia ingekuwaje? Wangepotea kabisa. Na ikiwa kuzaliana kwa pundamilia kungekuwa kwa idadi ndogo kuliko idadi ya simba, hatima yao ingekuwaje? Vilevile wangepotea kabisa. Kwa hiyo, idadi ya pundamilia inapaswa kuwa kubwa kuliko idadi ya simba. Hii ni kwa sababu pundamilia hawaishi tu kwa ajili yao; wanaishi pia kwa ajili ya simba. Unaweza pia kusema kwamba kila pundamilia ni sehemu moja ya pundamilia, lakini pia ni chakula katika kinywa cha simba. Kasi ya simba ya kuzaliana haiwezi kamwe kuiacha ile ya pundamilia, kwa hiyo idadi yao haiwezi kuwa kubwa kuliko idadi ya pundamilia. Ni kwa njia hii tu ndipo chanzo cha chakula cha simba kinaweza kuhakikishwa. Na kwa hivyo, ingawa simba ni maadui wa asili wa pundamilia, watu mara kwa mara huwaona wakiwa wamepumzika kwa kustarehe katika eneo moja. Pundamilia hawatapungua idadi au kupotea kabisa kwa sababu simba wanawawinda na kuwala, na simba hawataongezeka idadi yao kwa sababu ya hadhi yao kama “mfalme.” Uwiano huu ni kitu ambacho Mungu alikianzisha zamani sana. Yaani, Mungu alianzisha sheria za uwiano kati ya wanyama wote ili kwamba waweze kupata uwiano, na hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi huona. Je, simba ni adui pekee wa asili wa pundamilia? La, mamba pia hula pundamilia. Pundamilia anaonekana kuwa mnyama asiyekuwa na msaada kabisa. Hawana ukali kama wa simba, na wanapomkabili adui huyu wa kutisha, wanaweza kukimbia tu. Hawawezi hata kutoa upinzani. Wakati ambapo hawawezi kumshinda mbio simba, wanaweza kujiruhusu tu waliwe naye. Hii inaweza kuonekana mara kwa mara katika ulimwengu wa wanyama. Mnapata wazo gani mnapoona kitu cha namna hii? Je, unamhurumia pundamilia? Je, unamchukia simba? Pundamilia wanaonekana wazuri sana. Lakini simba, siku zote wanawaangalia kwa tamaa. Na kwa upumbavu, pundamilia hawakimbii mbali sana. Wanawaangalia simba pale wakiwasubiri, kwa kawaida wakiwasubiri chini ya kivuli cha mti. Nani anajua ni wakati gani atawala. Wanajua hili mioyoni mwao, lakini hawatalihama eneo hilo. Hili ni jambo la ajabu. Jambo hili la ajabu linajumuisha majaliwa ya Mungu, kanuni Yake. Unamhurumia pundamilia lakini huna uwezo wa kumsaidia, na unahisi kwamba simba ni wa kuchukiwa lakini huwezi ukamwepuka. Pundamilia ni chakula ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya simba, lakini haijalishi ni kwa namna gani simba wanawala, pundamilia hawatamalizwa. Idadi ya watoto ambao simba wanazaa ni ndogo sana, na wanazaa polepole sana, kwa hiyo haijalishi ni pundamilia ngapi wanakula, idadi zao haziwezi kuzidi za pundamilia. Hii ni aina ya uwiano.
Lengo la Mungu ni lipi katika kudumisha aina hii ya uwiano? Hii inahusiana na mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi vilevile kuendelea kuishi kwa binadamu. Ikiwa pundamilia au mawindo mengine ya simba—paa au wanyama wengineo—watazaliana taratibu sana na idadi ya simba ikaongezeka haraka, ni aina gani ya hatari ambayo binadamu wangepata? Simba kuyala mawindo yao ni tukio la kawaida, lakini simba kumla mtu ni janga. Janga hili sio kitu ambacho kilipangwa kabla na Mungu, halipo ndani ya sheria Yake, wala kile ambacho amekileta kwa ajili ya binadamu. Badala yake, ni kile ambacho watu wamejiletea wenyewe. Kwa hiyo kama Mungu aonavyo, uwiano kati ya vitu vyote ni muhimu kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Iwe ni mimea au wanyama hawawezi kupoteza uwiano wao sahihi. Mimea, wanyama, milima, na maziwa—Mungu amewaandalia binadamu mazingira ya kawaida ya kiikolojia. Hadi pale tu ambapo watu watakuwa na aina hii ya mazingira ya kiikolojia—yenye uwiano—ndipo kuendelea kuishi kwao kutakuwa salama. Ikiwa miti au nyasi ingekuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha au kasi yake ya uzalishaji ingekuwa ya taratibu sana, je, udongo ungepoteza unyevunyevu wake? Ikiwa udongo ungepoteza unyevunyevu wake, je, bado ungekuwa na afya? Ikiwa udongo ungepoteza uoto wake na unyevunyevu wake, ungemomonyoka haraka sana, na mchanga ungetokea badala yake. Wakati udongo ulipoharibika, mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi pia yangeharibika. Pamoja na uharibifu huu majanga yangeweza kutokea. Bila aina hii ya uwiano wa kiikolojia, bila aina hii ya mazingira ya kiikolojia, watu wangeendelea kuathirika na majanga kwa sababu ya kukosa uwiano baina ya vitu hivi vyote. Kwa mfano, wakati kunapokuwa na kukosekana kwa uwiano wa kimazingira hadi kusababisha uharibifu wa mazingira ya ikolojia ya vyura, wote wanakusanyika pamoja, idadi yao inaongezeka haraka sana na watu hata wanaona idadi kubwa ya vyura wanapita mtaani mijini, na idadi kubwa ya vyura barabarani. Ikiwa idadi kubwa ya vyura ingechukua sehemu kubwa ya mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi, hiyo ingeitwaje? Janga. Kwa nini liitwe janga? Wanyama hawa wadogo ambao wana manufaa kwa binadamu wana faida kwa watu wanapobaki katika eneo ambalo linafaa kwao; wanadumisha uwiano wa mazingira ya watu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Mara tu wanapokuwa janga, wataathiri mpangilio wa maisha ya watu. Vitu vyote na vipengele vyote ambavyo chura wanavileta vinaweza kuathiri ubora wa maisha ya watu. Hata ogani zao za kimwili zinaweza kushambuliwa—hii ni moja ya aina ya majanga. Aina nyingine ya janga, ambalo ni kitu ambacho binadamu wamepitia mara kwa mara—ni kutokea kwa idadi kubwa ya nzige. Hili si janga? Hili ni janga la kutisha. Haijalishi binadamu wana uwezo kiasi gani—watu wanaweza kutengeneza ndege, mizinga, na mabomu ya atomiki—lakini pale ambapo nzige wanawavamia binadamu, wanakuwa na suluhisho gani? Je, wanaweza kuwashambulia kwa mizinga? Je, wanaweza kuwafyatulia risasi kwa bunduki? Hawawezi. Basi wanaweza kuwanyunyizia dawa ya kuua wadudu ili kuwafukuza? Hiyo si rahisi pia. Hao nzige wadogo wanakuja kufanya nini? Wao haswa hula mimea na nafaka. Popote pale nzige wanapokwenda, mazao yanafutiliwa mbali kabisa. Kwa hivyo, chini ya uvamizi wa nzige, kufumba na kufumbua, chakula cha mwaka mmoja ambacho wakulima wanakitegemea kinaweza kuliwa kabisa na nzige. Kwa binadamu, ujio wa nzige sio tu kero—ni janga. Kutokea kwa nzige wengi ni aina ya janga, sasa vipi kuhusu panya? Ikiwa hakuna ndege wowote mbua wa kula panya, watazaliana haraka sana, haraka kuliko unavyoweza kufikiri. Na ikiwa kuenea kwa panya hakutadhibitiwa, je, binadamu wanaweza kuishi maisha mazuri? Kwa hivyo ni kitu gani ambacho binadamu wangekabiliana nacho? (Tauni.) Tauni tu? Panya watatafuna kila kitu. Watatafuna hata mbao. Ikiwa kuna panya wawili tu katika nyumba, kila mtu kwenye nyumba yote atachukizwa. Wakati mwingine wanaiba mafuta na kula, wakati mwingine wanakula nafaka. Na vitu ambavyo hawali wanavitafuna tu na kuvivuruga kabisa. Wanatafuna nguo, viatu, fanicha—wanatafuna kila kitu. Wakati mwingine watapanda kwenye kabati la vyombo—je, vyombo hivyo bado vinaweza kutumiwa baada ya kukanyagwa na panya? Hata kama utavisafisha hutahisi una amani, kwa hiyo unavitupa tu nje. Hii ndiyo shida ambayo panya wanawapatia watu. Ni panya wadogo tu, lakini watu hawana namna ya kushughulika nao. Wamefanyiwa hata udhalimu na hao panya. Hakuna haja ya kuzungumzia kundi lote la panya—panya wawili tu wanatosha kufanya uharibifu. Kama wangekuwa janga, madhara yake hayawezi kufikirika. Na ikiwa mchwa wadogo wangekuwa janga, yale madhara ambayo wangefanya kwa binadamu pia yasingeweza kupuuzwa. Mchwa wanaweza kusababisha madhara kwa nyumba hadi zianguke. Uwezo wao haufai kupuuzwa. Halitakuwa jambo la kuogofya ikiwa aina tofauti za ndege wangesababisha janga? (Ndiyo.) Kusema vingine, haijalishi wao ni aina gani ya wanyama au viumbe hai, mara tu watakapopoteza uwiano wao, watakua, kuzaliana, na kuishi ndani ya mawanda yasiyokuwa ya kawaida, mawanda yasiyofuata kanuni. Hiyo ingeweza kuleta madhara yasiyoweza kufikirika kwa binadamu. Hiyo isingeweza kuathiri kuendelea kuishi na maisha ya watu tu, bali pia ingeleta janga kwa binadamu, hata kufikia hatua ambapo watu watapatwa na maangamizo, watapatwa na hatma ya kufa.
Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha. Hakuna hata kimoja katika viumbe wote kinachoweza kwenda nje ya sheria, na sheria haziwezi kuvunjwa. Ni ndani ya aina hii tu ya mazingira ya msingi ndipo binadamu wanaweza kuendelea kuishi kwa usalama na kuongezeka, kizazi baada ya kizazi. Ikiwa kiumbe yeyote anakwenda zaidi ya ukubwa au mawanda yaliyoanzishwa na Mungu, au ikiwa anazidi kiwango cha ukuaji, marudio, au idadi chini ya utawala Wake, mazingira ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yangepata uharibifu wa viwango vinavyotofautiana. Na wakati uo huo, kuendelea kuishi kwa binadamu kungetishiwa. Ikiwa aina moja ya kiumbe hai ni kubwa sana kwa idadi, itawanyang’anya watu chakula chao, kuharibu vyanzo vya maji ya watu, na kuharibu makazi yao. Kwa njia hiyo, kuzaliana kwa binadamu au hali ya kuendelea kuishi ingeathiriwa mara moja. Kwa mfano, maji ni muhimu sana kwa vitu vyote. Ikiwa kuna idadi kubwa sana ya panya, siafu, nzige, na vyura, au wanyama wengine wa kila aina, watakunywa maji zaidi. Kadri kiwango cha maji wanachokunywa kinaongezeka, ndani ya mawanda haya yasiyobadilika ya vyanzo vya maji ya kunywa na maeneo ya majimaji, maji ya kunywa ya watu na vyanzo vya maji vitapungua, na watapungukiwa maji. Ikiwa maji ya kunywa ya watu yataharibiwa, kuchafuliwa au kukatwa kwa sababu aina zote za wanyama zimeongezeka kwa idadi, chini ya aina hiyo ya mazingira katili kwa ajili ya kuendelea kuishi, kuendelea kuishi kwa binadamu hakika kutakuwa kumetishiwa vikali. Ikiwa kuna aina moja au aina kadhaa za viumbe hai ambavyo vinazidi idadi yao inayofaa, hewa, halijoto, unyevunyevu, na hata vijenzi vya hewa ndani ya eneo la binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi litakuwa na sumu na kuharibiwa kwa viwango vinavyotofautiana. Hali kadhalika, chini ya mazingira haya, kuendelea kuishi kwa binadamu na hatma bado vitakuwa chini ya tishio la aina hiyo ya mazingira. Kwa hiyo, ikiwa watu watapoteza uwiano huu, hewa wanayovuta itaharibiwa, maji wanayokunywa yatachafuliwa, na halijoto ambayo wanahitaji pia itabadilika, itaathiriwa kwa viwango tofautitofauti. Ikiwa hiyo itatokea, mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo kiasili ni ya wanadamu yataandamwa na madhara na changamoto kubwa. Chini ya aina hii ya mazingira ambapo mazingira ya msingi ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yameharibiwa, hatma na matarajio ya binadamu yatakuwa ni nini? Ni tatizo kubwa sana! Kwa sababu Mungu anajua vitu vyote ni nini kwa binadamu, wajibu wa kila aina ya kitu Alichokiumba, aina gani ya athari kinacho kwa watu, na faida kubwa kiasi gani kinaleta kwa binadamu—katika moyo wa Mungu kuna mpango kwa ajili ya haya yote na Anasimamia kila kipengele cha vitu vyote alivyoviumba, kwa hiyo kwa binadamu, kila kitu Anachofanya ni muhimu sana—vyote ni lazima. Kwa hiyo wakati unaona baadhi ya matukio ya kiikolojia miongoni mwa vitu vyote, au baadhi ya sheria za asili miongoni mwa vitu vyote, hutashuku tena ulazima wa kila kitu ambacho kiliumbwa na Mungu. Hutatumia tena maneno ya kijinga kufanya hukumu zisizokuwa na msingi juu ya mipangilio ya Mungu juu ya vitu vyote na njia zake mbalimbali za kuwakimu binadamu. Pia hutafanya mahitimisho yasiyokuwa na msingi juu ya sheria za Mungu kwa ajili ya vitu vyote ambavyo Aliviumba. Je, hii haiko hivyo?
Je, haya yote tuliyoyazungumza ni nini? Yafikirie. Mungu ana nia Yake katika kila kitu anachofanya. Ingawa binadamu hawawezi kuona nia hiyo, siku zote inahusiana na kuendelea kuishi kwa binadamu. Inahusiana bila kutenganishwa nayo—ni ya lazima. Hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kufanya kitu ambacho hakina manufaa. Kwa kila kitu ambacho Anafanya, mpango Wake upo ndani ya nadharia na kanuni zake, ambazo zinajumuisha hekima Yake. Lengo na nia ya mpango huo ni kwa ajili ya ulinzi wa binadamu, kumsaidia binadamu kuzuia janga, uvamizi wa kiumbe chochote hai, na aina yoyote ya madhara kwa binadamu yasababishwayo na vitu vyote. Kwa hiyo kutokana na matendo ya Mungu ambayo tumeyaona kutoka katika mada hii ambayo tunaijadili, tungeweza kusema kwamba Mungu anawakimu binadamu kwa njia nyingine? Je, tungeweza kusema kwamba Mungu anawalisha na kuwachunga binadamu kwa njia hii? (Ndiyo.) Je, kuna uhusiano mkubwa kati ya mada hii na anwani ya ushirika wetu, “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? (Ndiyo.) Kuna uhusiano mkubwa, na mada hii ni kipengele kimoja chake. Kabla ya kuzungumza kuhusu mada hizi, watu walikuwa tu na fikra zisizo dhahiri juu ya Mungu, Mungu Mwenyewe na matendo Yake—hawakuwa na uelewa wa kweli juu ya vitu hivi. Hata hivyo, watu wanapoambiwa kuhusu matendo Yake na vitu ambavyo Amefanya, wanaweza kuelewa na kufahamu kanuni za kile ambacho Mungu anafanya na wanaweza kupata kuzielewa na kuzikaribia—hivyo sivyo ilivyo? Ingawa katika moyo wa Mungu, nadharia Zake, kanuni Zake, na Sheria Zake zinatatiza sana Anapokuwa anafanya kitu chochote, Alipotengeneza vitu vyote, na Anapotawala vitu vyote, ikiwa kitu kimoja kimechukuliwa kushiriki na nyinyi katika ushirika, je, hamtaweza kuelewa mioyoni mwenu kwamba haya ni matendo ya Mungu, na yapo thabiti sana? (Ndiyo.) Basi ni kwa jinsi gani uelewa wenu wa sasa juu ya Mungu ni tofauti na ulivyokuwa kabla? Ni tofauti kwa asili yake. Mlichokielewa kabla kilikuwa tupu, kisicho dhahiri sana, na kila mnachokielewa sasa kinajumuisha kiasi kikubwa cha ushahidi thabiti kushikilia matendo ya Mungu, kulinganisha na kile Mungu anacho na alicho. Kwa hiyo, yote ambayo nimeyasema ni nyenzo nzuri sana kwa ajili ya uelewa wa Mungu.
Februari 9, 2014