Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)

Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila muumini, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo anapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Mnadhani mambo ambayo tumekuwa tukiyafanyia ushirika hivi karibuni kuhusu kumjua Mungu yanawezekana? Ni haki kusema kuwa ni nje ya uwezo wa watu wengi. Mwaweza kukosa kusadiki maneno haya. Kwa nini Ninasema hili? Kwa sababu mlipokuwa mkisikiliza Niliyokuwa nikisema awali, haijalishi Niliyasema vipi, au ni kwa maneno gani, moja kwa moja na kinadharia mlikuwa mnatambua Nilichokuwa nikisema, lakini tatizo lenu kubwa ni kwamba, hamkuelewa ni kwa nini Niliyasema mambo haya, ni kwa nini nilizizungumzia hizi mada. Hiki ndicho kiini cha hili suala. Na kwa hiyo, japo kusikia kwenu haya mambo kuliongeza na kuimarisha uelewa wenu kuhusu Mungu na matendo Yake, bado mnapata ugumu kumjua Mungu. Baada ya kusikia Nilichokisema, wengi wenu hawaelewi ni kwa nini Nilisema hili, na lina uhusiano gani na kumjua Mungu. Sababu ya nyinyi kutoweza kuelewa uhusiano wake na kumjua Mungu ni uzoefu wenu wa kimaisha ni wa juujuu sana. Ikiwa ufahamu na uzoefu wa watu kuhusu maneno ya Mungu utabaki kuwa wa juujuu, basi ufahamu wao mkubwa kumhusu Mungu utakuwa si yakini na wa kidhahania;wote utakuwa wa jumla, wa kimafundisho, na wa kinadharia. Kinadharia, yanaonekana au kusikika kuwa na mantiki na razini, ila ufahamu kuhusu Mungu utokao vinywani mwa watu ni mtupu. Na mbona Ninasema kuwa ni mtupu? Kwa sababu, kwa hakika, moyoni mwako hauko wazi kama maneno kuhusu kumjua Mungu yatokayo kinywani mwako ni sawa au la, ikiwa ni sahihi au la. Hivyo basi, japo watu wengi wamesikia taarifa na mada nyingi kuhusu kumjua Mungu, ufahamu wao kuhusu Mungu haujatoka nje ya nadharia na zaidi ya kanuni ambayo ni sio wazi na dhahania. Jinsi gani, basi, hili tatizo linaweza kusuluhishwa vipi? Je, mmewahi kuliwazia hilo? Ikiwa watu hawautafuti ukweli, wanaweza kuwa na uhalisi? Ikiwa watu hawautafuti ukweli, basi bila shaka hawana uhalisi, na hivyo, kwa hakika hawana ufahamu au uzoefu wa maneno ya Mungu. Je, yawezekana wasioyafahamu maneno ya Mungu wamfahamu Mungu? Hawawezi Kabisa. Haya mawili yameshikamana. Hivyo, watu wengi husema, “Kumjua Mungu kwawezaje kuwa kugumu hivi? Ninapozungumzia kujijua mimi mwenyewe, naweza kuzungumza kwa saa nyingi, ila inapofika kumjua Mungu nakoswa maneno. Hata ninapoweza kusema machache, ni kwa kushurutishwa, yanakosa uchangamfu—hata yanasikika ya kufedhehesha ninapojisikia nikiyasema.” Hiki ndicho chanzo. Ukihisi kwamba kumjua Mungu ni kugumu sana, kwamba kunakuchosha, kwamba huna la kuzungumzia—huna chochote cha kufanya ushirika na kuwapa wengine, na kujipa wewe mwenyewe—basi hili linathibitisha kwamba hujayapitia maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu ni nini? Je, maneno ya Mungu sio maonyesho ya kile Mungu anacho na alicho? Ikiwa hujapitia uzoefu wa maneno ya Mungu, unaweza kuwa na ufahamu wowote kuhusu anacho na alicho. Kwa hakika siyo. Vitu hivi vyote vimeshikamana. Ikiwa huna uzoefu wa maneno ya Mungu, basi huwezi kuelewa mapenzi ya Mungu, na hutajua tabia Yake ni nini, Anachokipenda, Anachokichukia, mahitaji Yake kwa mwanadamu ni yapi, mtazamo Wake kwa walio wazuri, na kwa wale walio waovu ni upi—kwa hakika haya yote yatakuwa tata na yenye mashaka kwako. Ikiwa mnamwamini Mungu katikati ya haya mashaka, basi wakati unapodai kuwa miongoni mwa wale wanaoufuatilia ukweli na kumfuata Mungu, je, haya maneno yana uhalisi? Hayana! Hivyo tuendelee kufanya ushirika kuhusu kumjua Mungu.

Nyinyi nyote mna shauku ya kuisikia mada tutakayoifanyia ushirika, sivyo? Mada tutakayowasiliana kwa karibu leo pia inahusiana na mada ya “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ambayo tumekuwa tukizungumzia hivi karibuni. Tumeongea mengi kuhusu jinsi “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” kutumia njia na mitazamo mbalimbali kuwaarifu watu jinsi Mungu anatawala juu ya vitu vyote, ni kwa njia gani Anavitawala vitu vyote, na ni kwa kanuni gani anavisimamia vitu vyote, ili kwamba viweze kuishi katika hii sayari Aliyoumba Mungu. Tulizungumza pia mengi kuhusu jinsi ambavyo Mungu anamkimu mwanadamu: ni kwa njia gani Mungu anamkimu mwanadamu, ni mazingira ya kuishi ya aina gani Mungu anampa mwanadamu, na ni kwa njia zipi na kuanzia wapi Anampa mwanadamu mazingira thabiti ya kuishi. Japo Sikuzungumzia moja kwa moja uhusiano baina ya utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, uendeshaji Wake wa vitu vyote na usimamizi Wake, kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja Nilisema ni kwa nini Anaviendesha vitu vyote namna hii, na ni kwa nini Anamkimu na kumlisha mwanadamu namna hii—yote ambayo yanahusu usimamizi wa Mungu. Maudhui tuliyoyazungumzia yalikuwa mengi na mapana—kuanzia mazingira makubwa hadi vitu vidogo zaidi kama mahitaji na lishe ya msingi ya wanadamu; kuanzia jinsi Mungu anaviongoza vitu vyote na kuvifanya vitende kazi kwa utaratibu, hadi kwenye mazingira ya kuishi sahihi na ya kufaa Aliyoyaumba kwa ajili ya watu wa kila jamii, na kadhalika. Haya maudhui mapana yanahusu jinsi mwanadamu anaishi katika mwili. Hivi ni kusema, yote yanahusiana na vitu katika ulimwengu halisi vinavyoonekana kwa macho ya kawaida, na ambavyo mwanadamu anaweza kuvihisi, kwa mfano, milima, mito, bahari, tambarare… Hivi vyote ni vitu vinavyoweza kuonekana na kuguswa. Nizungumzapo kuhusu hewa na halijoto, mnaweza kutumia pumzi zenu kuhisi moja kwa moja uwepo wa hewa, na miili yenu kuhisi kama halijoto iko juu au chini. Miti, nyasi, na ndege na wanyama porini, vitu vinavyopaa angani, na kutembea ardhini, na wanyama wadogo mbalimbali watokezao kutoka matunduni, vyote vinaweza kuonekana kwa wanadamu kwa macho yao wenyewe na kusikika kwa masikio yao wenyewe. Japo mawanda ya vitu kama hivyo ni mapana, miongoni mwa vitu vyote vinawakilisha tu ulimwengu halisi. Vitu yakinifu ni vitu ambavyo watu wanaweza kuviona na kuvihisi, yaani, ukivigusa, utavihisi, na macho yako yakiviona, ubongo wako utakupatia umbo, picha. Ni vitu ambavyo ni halisi na kweli; kwako si dhahania, bali vina umbo; vinaweza kuwa mraba, au duara, au virefu au vifupi; na kila kimoja kinakupa taswira tofauti. Vitu hivi vyote vinawakilisha sehemu ile yakinifu ya vitu vyote. Na hivi, “vitu vyote” katika “utawala wa Mungu juu ya vitu vyote” vinajumuisha nini kwa Mungu? Havijumuishi tu vitu ambavyo watu wanaweza kuona na kugusa, bali, vilevile, visivyoonekana na visivyoshikika. Hii ni mojawapo ya maana za kweli za utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Hata kama vitu hivi havionekani na havishikiki kwa watu, kwa Mungu, alimradi vinaweza kuonekana kwa jicho Lake na vipo ndani ya ukuu Wake, kwa hakika vipo. Hata kama, kwa mwanadamu, ni dhahania na visivyofikirika—na hata kama, aidha, havionekani na havishikiki—kwa Mungu kwa kweli na kwa uhalisi vipo. Huo ndio ulimwengu mwingine wa vitu vyote ambavyo Mungu anatawala, na ni sehemu nyingine ya mawanda mengine ambayo Anatawala. Hii ndiyo mada ambayo tutaifanyia ushirika leo—jinsi Mungu anatawala na kuuongoza ulimwengu wa kiroho. Kwa kuwa mada hii inagusia jinsi Mungu anatawala na kusimamia vitu vyote, inahusiana na ulimwengu ulio nje ya ulimwengu yakinifu—ulimwengu wa kiroho—na kwa hivyo ni muhimu sana kwetu kuuelewa. Ni baada tu ya ushirika huu umetolewa na ni wakati tu watu wameuelewa ndipo wataweza kuelewa kwa hakika maana ya kweli ya maneno “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Hii ndiyo maana tutazungumzia mada hii. Na shabaha ya mada hii ni kukamilisha dhamira ya “Mungu anavitawala vitu vyote, na Mungu anavisimamia vitu vyote.” Pengine, mtakapoisikia mada hii, inaweza kuonekana ni ya ajabu na isiyoaminika kwenu—lakini bila kujali mnavyohisi, kwa kuwa ulimwengu wa kiroho ni sehemu moja ya vitu vinavyotawaliwa na Mungu, ni sharti mjifunze kitu kuhusu mada hii. Baada ya kujifunza, mtakuwa na ufahamu wa kina, uelewa na maarifa kuhusu maneno “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.”

Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho

Kwa ulimwengu yakinifu, watu wakikosa kuelewa vitu au jambo fulani, wanaweza kutafuta taarifa mwafaka, vinginevyo wanaweza kutumia njia mbalimbali kubaini asili ya habari kuvihusu. Lakini inapokuja kwa ulimwengu huu mwingine ambao tunauzungumzia leo—ulimwengu wa kiroho ulio nje ya ulimwengu yakinifu—watu hawana hasa mbinu au njia za kujifunzia chochote kuuhusu. Mbona Ninasema hivi? Kwa sababu, katika ulimwengu wa mwanadamu, kila kitu cha ulimwengu yakinifu hakijitengi na uwepo wa kimwili wa mwanadamu, na kwa sababu watu wanahisi kwamba kila kitu katika ulimwengu yakinifu hakitenganishwi na maisha yao ya kimwili na uhai wao wa kimwili, watu wengi wanafahamu tu kuhusu, au kuona, vitu yakinifu mbele ya macho yao, vitu vinavyoonekana kwao. Bali inapokuja katika ulimwengu wa kiroho—yaani, kila kilicho cha ule ulimwengu mwingine—ni haki kusema kuwa watu wengi hawaamini. Kwa sababu watu hawawezi kuuona, wanaamini kuwa hakuna haja ya kuuelewa au kujua kitu chochote kuuhusu, sembuse jinsi ulimwengu wa kiroho ni ulimwengu tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu na kutoka kwa mtazamo wa Mungu, uko wazi—ingawa kwa wanadamu, ni wa siri na umefungwa—kwa hivyo watu huona ikiwa vigumu sana kupata njia ya kuelewa vipengele mbalimbali vya ulimwengu huu. Vipengele tofauti ambavyo nitazungumzia kuhusu ulimwengu wa kiroho vinahusu utawala na ukuu wa Mungu tu. Sifichui miujiza, wala Siwaambii siri zozote mnazotaka kugundua, kwani hili linahusu ukuu wa Mungu, utawala wa Mungu, na riziki ya Mungu, na kwa hivyo Sitazungumzia tu sehemu ambayo ni muhimu nyinyi kuijua.

Kwanza, hebu Niwaulize swali: katika mawazo yenu, ulimwengu wa kiroho ni nini? Kuzungumza kwa ujumla, ni ulimwengu ulio nje ya ulimwengu yakinifu, ambao hauonekani na haushikiki na watu. Lakini kwa fikra zenu, ulimwengu wa kiroho unafaa uwe ulimwengu wa aina gani? Pengine, kwa sababu ya kutoweza kuuona, mnaweza kushindwa kuufikiria. Lakini mtakaposikia hadithi kuuhusu, bado mtafikiri, hamtaweza kujizuia nyinyi wenyewe. Na kwa nini Ninasema hili? Kuna kitu kinachowatokea watu wengi wanapokuwa wachanga: mtu akiwasimulia hadithi ya kuogofya—juu ya mazimwi, na roho—wanaogopeshwa kabisa. Na kwa nini wanaogopeshwa? Ni kwa kuwa wanavifikiria vitu hivyo; hata japo hawawezi kuviona, wanahisi kuwa vipo kila pembe ya chumba chao, vimejificha sehemu fulani, au sehemu fulani yenye giza, na wanaogopa sana kiasi kwamba hawawezi kuthubutu kulala. Hasa wakati wa usiku, hawathubutu kuwa chumbani peke yao, au uani peke yao. Huo ndio ulimwengu wa kiroho wa fikra zenu, na ni ulimwengu ambao watu hudhani unaogofya. Kwa kweli, kila mtu ana fikra fulani, na kila mtu anaweza kuhisi kitu.

Hebu tuanze na ulimwengu wa kiroho. Ulimwengu wa kiroho ni nini? Hebu Niwape maelezo mafupi na rahisi. Ulimwengu wa kiroho ni sehemu muhimu, ambayo ni tofauti na ulimwengu yakinifu. Na mbona Ninasema kwamba ni muhimu? Tutalizungumzia hili kwa kina. Uwepo wa huu ulimwengu wa kiroho umeungana na ulimwengu yakinifu wa mwanadamu kwa njia isiyoweza kufumbulika. Una jukumu katika mzunguko wa uhai na mauti wa mwanadamu katika utawala wa Mungu juu ya vitu vyote; hili ndilo jukumu lake, na sababu mojawapo inayofanya uwepo wake kuwa muhimu. Kwa sababu ni mahali ambapo hapawezi kutambuliwa kwa milango mitano ya fahamu ya mwanadamu, hakuna anayeweza kubaini kwa hakika kuwepo au kutokuwepo kwake. Shughuli za ulimwengu wa kiroho zimeunganika kikamilifu na uwepo wa mwanadamu, na kwa sababu hiyo mpango wa maisha ya wanadamu pia unaathiriwa kwa kiwango kikubwa na ulimwengu wa kiroho. Je, hili linahusiana na ukuu wa Mungu? Linahusiana. Nisemapo hili, unaelewa ni kwa nini Ninajadili mada hii; Kwa sababu inahusu ukuu wa Mungu, na utawala Wake. Katika ulimwengu kama huu—ulimwengu ambao hauonekani kwa watu—kila sheria yake ya peponi, amri na mfumo wake wa utawala ni wa juu zaidi kuliko sheria na mifumo ya nchi yoyote katika ulimwengu yakinifu, na hakuna kiumbe aishiye katika ulimwengu huu anaweza kuzivunja au kujitwalia bila haki. Je, hili linahusiana na ukuu na utawala wa Mungu? Katika ulimwengu huu kuna amri wazi za utawala, sheria wazi za mbinguni, na masharti wazi. Katika viwango tofauti na katika mawanda tofauti, wasimamizi huzingatia kikamilifu katika wajibu wao na kufuata sheria na masharti, kwa kuwa wanajua matokeo ya kukiuka sheria ya mbinguni ni yapi, wanafahamu wazi jinsi ambavyo Mungu anaadhibu maovu na kutuza mazuri, na kuhusu jinsi Anavyoviendesha vitu vyote, jinsi Anavyotawala vitu vyote, na zaidi, wanaona wazi ni jinsi gani Mungu anaendesha sheria za mbinguni na masharti Yake. Je, hizi ni tofauti na ulimwengu yakinifu unaokaliwa na wanadamu? Ni tofauti kwa kiasi kikubwa. Ni ulimwengu ambao ni tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu. Kwa kuwa kuna sheria na masharti ya mbinguni, inahusu ukuu wa Mungu, utawala, aidha, tabia ya Mungu ya kile Anacho na alicho. Baada ya kusikia hili, hamhisi kwamba ni muhimu sana Mimi kuzungumzia hii mada? Hamtaki kujifunza siri zilizomo? (Ndiyo, tunataka.) Hiyo ndiyo dhana ya ulimwengu wa kiroho. Japo unapatikana sambamba na ulimwengu yakinifu, na wakati ule ule ukiwa chini ya utawala na ukuu wa Mungu, utawala na ukuu wa Mungu ya huu ulimwengu ni makali zaidi kuliko ulivyo ulimwengu yakinifu. Ikija katika maelezo, tunafaa tuanze na jinsi ulimwengu wa kiroho unawajibikia kazi ya mzunguko wa uhai na mauti ya mwanadamu, kwa kuwa kazi hii ni sehemu kuu ya viumbe wa ulimwengu wa kiroho.

Miongoni mwa wanadamu, Ninawaainisha watu katika aina tatu. Aina ya kwanza ni wasioamini, wale wasio na imani za kidini. Wanaitwa wasioamini. Wengi wa wasioamini wanaamini tu katika pesa, wanatafuta tu maslahi yao wenyewe, wana tamaa ya vitu, na wanaamini katika ulimwengu yakinifu, si katika mzunguko wa uhai na mauti au katika semi za miungu na mapepo. Ninawaainisha kama wasioamini na ni wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni watu mbalimbali wenye imani tofauti na wasioamini. Miongoni mwa wanadamu, Ninawagawa hawa wenye imani katika aina kuu kadhaa: Ya kwanza ni Wayahudi, wa pili ni Wakatoliki, ya tatu ni Wakristo, ya nne ni Waislamu, na ya tano ni wafuasi wa Budha—kuna aina tano. Hizi ndizo aina mbalimbali za watu wenye imani. Aina ya tatu ni wale wanaomwamini Mungu, inayohusiana nanyi. Waumini kama hawa ni wale wanaomfuata Mungu leo. Hawa watu wamegawanyika katika aina mbili. Wateule wa Mungu na watendaji huduma. Hizi aina kuu zimebainishwa wazi. Basi sasa, akilini mwenu mnaweza kutofautisha wazi aina na madaraja ya binadamu, siyo? Ya kwanza ni wasioamini—nimesema wasioamini ni watu gani. Je, wale wanaomwamini Mtu Mzee aliye Angani wanahesabika kama wasioamini? Wengi wa wasioamini wanamwamini yule Mzee aliye Angani; wanaamini kuwa upepo, mvua na radi, na kadhalika vyote vinadhibitiwa na huyu mtu ambaye wanamtegemea kwa upanzi wa mimea na uvunaji wa mazao—lakini wakati imani katika Mungu inatajwa, hawataki kumwamini. Je, hii yaweza kuitwa imani katika Mungu? Watu kama hao wanahesabiwa katika wasioamini. Mnaelewa hili, siyo? —Msifahamu visivyo vikundi hivi. Aina ya pili ni watu wa imani. Aina ya tatu ni wale wanaomfuata Mungu leo. Na kwa nini Nimewagawa wanadamu wote katika aina hizi? (Kwa sababu aina kadhaa za watu wana vituo na hatima tofautitofauti.) Hicho ni kipengele kimoja. Kwa sababu, wakati haya matabaka na aina mbalimbali za watu wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, kila mmoja atakuwa na sehemu tofauti ya kuenda, watapitia sheria ya mzunguko tofauti wa uhai na mauti na hii ndiyo sababu Nimewaainisha wanadamu katika hizi aina kuu.

a. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, akithibitisha majina yao, anwani, umri, na uzoefu wao wote. Kila kitu walichofanya walipokuwa hai kinanakiliwa kwenye kitabu na usahihi wake unahakikishwa. Baada ya kukaguliwa, matendo na mienendo ya mtu maishani mwake vinatumika kuamua ikiwa ataadhibiwa au ataendelea kupata mwili kama mwanadamu, ambayo ni hatua ya kwanza. Je, hii hatua ya kwanza inaogofya? Haiogopeshi sana, kwani kitu cha pekee kilichofanyika ni kwamba mtu amewasili katika mahali pa giza na pageni.

Katika hatua ya pili, ikiwa mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya maishani mwake, kama ametenda vitendo vingi viovu, basi atapelekwa mahali pa adhabu ili kuadhibiwa. Hiyo ndiyo itakuwa mahali ambapo kwa hakika ni kwa ajili ya adhabu ya watu. Maelezo kuhusu jinsi watakavyoadhibiwa yanategemea dhambi ambazo wamezitenda, pia ni vitendo vingapi viovu walitenda kabla hawajafa—hili ni tukio la kwanza ambalo linatokea katika hatua hii ya pili. Kwa sababu ya mambo mabaya waliyoyafanya, na maovu waliyoyafanya kabla hawajafa, wapatapo mwili baada ya adhabu yao—wazaliwapo upya tena katika ulimwengu yakinifu—watu wengine wataendelea kuwa wanadamu, na wengine watakuwa wanyama. Yaani, baada ya mtu kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanaadhibiwa kwa sababu ya maovu waliyotenda; zaidi, kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya, watakapozaliwa tena katika mwili mpya huenda hawawi wanadamu, ila watakuwa mnyama. Baadhi ya wanyama watakaokuwa ni ng’ombe, farasi, nguruwe, na mbwa. Watu wengine wanaweza kuwa ndege kule angani, au bata au bata bukini.… Baada ya kupata mwili kama mnyama, wanapokufa wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na sawa na mara ya kwanza, kutegemea mienendo yao kabla hawajafa, ulimwengu wa kiroho utaamua kama wapate mwili kama mwanadamu au la. Watu wengi hutenda maovu mengi sana, dhambi zao ni nzito sana, na kwa hivyo wapatapo mwili wanakuwa wanyama mara saba hadi mara kumi na mbili. Mara saba hadi mara kumi na mbili—hilo linaogopesha? (Linaogopesha.) Ni nini kinawaogopesha? Mtu kuwa mnyama, hilo linaogopesha. Na kwa mwanadamu, ni kipi cha uchungu zaidi kuhusu kuwa mnyama? Kutokuwa na lugha, kuwa tu na mawazo sahili, kuweza tu kufanya vitu ambavyo wanyama hufanya na kula vitu ambavyo wanyama hula, na kuwa na fikira sahili na kuwa na viziada lugha vya mnyama, kutoweza kutembea wima, kutoweza kuwasiliana na wanadamu, na mienendo yoyote na vitendo vya wanadamu kutokuwa na uhusiano na wanyama. Yaani, miongoni mwa vitu vyote, kuwa mnyama kunakufanya kuwa chini zaidi ya viumbe hai wote, na ni kuchungu zaidi kuliko kuwa mwanadamu. Hiki ni kipengele kimoja cha adhabu ya ulimwengu wa kiroho kwa wale waliofanya maovu mengi na kutenda dhambi kubwa. Ukali wa adhabu utakavyokuwa, hili hubainishwa na aina ya mnyama ambaye mtu anakuwa. Kwa mfano, kuwa nguruwe ni bora kuliko kuwa mbwa? Je, nguruwe huishi vizuri au vibaya kuliko mbwa? Vibaya zaidi, siyo? Watu wakiwa ng’ombe au farasi, je, wataishi vizuri zaidi au vibaya kuliko jinsi wangesishi kama nguruwe? (Vizuri zaidi.) Je, mtu atakuwa wa faraja zaidi kama mtu angezaliwa kama paka? Angekuwa mnyama sawa tu, na kuwa paka ingekuwa rahisi zaidi kuliko kuwa ng’ombe au farasi, kwa sababu paka huweza kuupitisha muda wao mwingi kulala. Kuwa ng’ombe au farasi ni kazi nzito. Hivyo basi, iwapo mtu atapata mwili na kuwa ng’ombe au farasi, wanapaswa kutia bidii—ambayo ni sawa na adhabu nzito. Kuwa mbwa kungekuwa ni afadhali kidogo kuliko kuja kuwa ng’ombe au farasi, kwa kuwa mbwa ana uhusiano wa karibu na bwana wake. Baadhi ya mbwa, baada ya kuwa kipenzi kwa miaka mingi, wanaweza kuelewa mengi ya yale bwana wao wanasema! Wakati mwingine na mahitaji yake na bwana anamtunza mbwa vyema, na mbwa anakula na kunywa vyema, na akiwa na maumivu anatunzwa zaidi. Je, mbwa basi hapati maisha ya furaha? Hivyo basi, kuwa mbwa ni bora kuliko kuwa ng’ombe au farasi. Katika hili, ukali wa adhabu ya mtu unaamua ni mara ngapi mtu hupata mwili kuwa mnyama, pia wa aina gani.

Kwa sababu walitenda dhambi nyingi sana walipokuwa hai, watu wengine wataadhibiwa kwa kupatiwa miili kama wanyama mara saba hadi kumi na mbili. Baada ya kuadhibiwa vya kutosha, wanaporudi katika ulimwengu wa kiroho wanapelekwa mahali pengine. Roho mbalimbali mahali hapa zimeadhibiwa tayari, na ni aina ya roho ambazo ziko tayari kupata mwili kama wanadamu. Mahali hapa panaziainisha roho katika makundi kulingana na aina ya familia watakamozaliwa, ni aina gani ya nafasi watashikilia baada ya kupata mwili, na kadhalika. Kwa mfano, watu wengine watakuwa waimbaji wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa waimbaji; wengine watakuwa wafanyabiashara wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa wafanyabiashara; na ikiwa mtu atakuwa mtafiti wa kisayansi akiwa mwanadamu, basi anawekwa miongoni mwa watafiti wa kisayansi. Baada ya kuwekwa katika makundi, kila mmoja anatumwa kulingana na wakati tofauti na tarehe iliyowekwa, sawa tu na jinsi watu hutuma barua pepe siku hizi. Katika hili kutakuwa kumekamilika mzunguko mmoja wa uhai na mauti. Tangu siku mtu anapowasili katika ulimwengu wa kiroho hadi mwisho wa adhabu yake, ama hadi anapozaliwa upya kama mnyama mara nyingi na anajitayarisha kuzaliwa upya kama mwanadamu, huu ni mchakato mzima.

Na wale waliokamilisha adhabu yao, na hawajapata mwili kuwa wanyama, je, watapelekwa kwa haraka katika ulimwengu yakinifu kuwa wanadamu? Au watachukua muda gani ndipo waje miongoni mwa wanadamu? Hili linaweza kurudiwa mara ngapi? Kwa hili kuna mipaka ya wakati. Kila kitu kinachofanyika katika ulimwengu huu wa kiroho kinapitia mipaka ifaayo kwa wakati na sheria—ambayo, Nikiieleza kutumia tarakimu, mtaelewa. Kwa wapatao mwili baada ya muda mfupi, wakati wanapokufa kuzaliwa kwao upya kama wanadamu kutatayarishwa. Wakati mfupi zaidi ni siku tatu. Kwa watu wengine, ni miezi mitatu, kwa wengine ni miaka mitatu, kwa wengine ni miaka thelathini, kwa wengine ni miaka mia tatu, kwa wengine hata ni miaka elfu tatu, na kadhalika. Hivyo basi ni nini kinaweza kusemwa kuhusu hizi sheria za wakati, na vipimo vyake ni vipi? Vinalingana na ulimwengu yakinifu, ulimwengu wa mwanadamu unahitaji kutoka kwa roho, na nafasi itakayochukuliwa na hii roho duniani. Watu wakipata mwili kama wanadamu wa kawaida, wengi wao wanapewa mwili haraka sana, kwa sababu dunia ya wanadamu ina uhitaji mkubwa wa watu wa kawaida kama hao, na kwa hiyo siku tatu baadaye wanatumwa tena katika familia ambayo ni tofauti kabisa na ile waliyokuwa kabla hawajafa. Lakini wapo ambao wana nafasi maalum katika ulimwengu huu. “Maalum” inamaanisha kuwa hakuna uhitaji mkubwa wa hawa watu katika ulimwengu wa wanadamu; si watu wengi wanaohitajika kuishikilia nafasi hiyo, kwa hiyo basi inaweza kuwa miaka mia tatu kabla hawajapata mwili. Ambako ni kusema, hii roho itakuja mara moja tu katika kila miaka mia tatu, au hata mara moja kila baada ya miaka elfu tatu. Na ni kwa nini hivi? Ni kwa sababu kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu, nafasi hiyo haihitajiki katika dunia ya mwanadamu, na kwa hiyo wanatunzwa mahali fulani katika ulimwengu wa kiroho. Tazama Confucius, kwa mfano. Alikuwa na athari kubwa katika utamaduni wa jadi wa Uchina. Kuwasili kwake kulikuwa na athari kubwa kwenye utamaduni, elimu, desturi, na kufikiri kwa watu wa wakati ule. Lakini mtu kama huyu hahitajiki katika kila enzi, na kwa hiyo alilazimika kubaki katika ulimwengu wa kiroho, akisubiri huko kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu kabla ya kupata mwili. Kwa kuwa ulimwengu wa mwanadamu haukuhitaji mtu kama huyu, alilazimika kusubiri bila kufanya chochote, kwa kuwa kulikuwa na nafasi chache sana kama yake, kulikuwa na machache ya yeye kufanya, na hivyo basi alitunzwa sehemu fulani katika ulimwengu wa kiroho kwa muda mrefu, bila kufanya chochote, na kutumwa wakati ambapo ulimwengu wa mwanadamu ulimhitaji. Hizo ndizo sheria za wakati za milki ya kiroho kuhusu haraka ambayo watu wengi wanapata miili. Iwe ni mtu wa kawaida au maalum, ulimwengu wa kiroho una sheria mwafaka na desturi sahihi kwa utayarishaji wa watu kuzaliwa katika mwili mpya, na hizi sheria na desturi zinatumwa kutoka kwa Mungu, na haziamuliwi au kudhibitiwa na msimamizi yeyote au kiumbe chochote katika ulimwengu wa kiroho. Sasa mnaelewa, naam?

Kwa nafsi yoyote, kuzaliwa kwake katika mwili mpya, nafasi yake ni ipi katika haya maisha, atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Watu wa kila aina huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanakuja kulipa deni. Katika maisha haya Wakati uleule, watu wengine, wamekuja kuchukua madeni yao: Walitapeliwa vitu vingi sana, na pesa nyingi sana katika maisha yao yaliyopita, na kwa hiyo, baada ya kuwasili katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapa haki na kuwapa fursa ya kukusanya madeni yao katika maisha haya. Watu wengine wamekuja kulipa deni la shukrani: katika maisha yao yaliyopita—kabla hawajafa—mtu alikuwa mkarimu kwao, na katika maisha haya wamepatiwa fursa nzuri kupata mwili ili kwamba waweze kuzaliwa upya ili kulipa upya deni hili la shukrani. Wakati uleule, wengine wamezaliwa upya katika haya maisha ili kudai uhai. Na wanadai uhai wa nani? Uhai wa mtu aliyewaua katika maisha yao yaliyopita. Kwa ujumla, maisha ya sasa ya kila mtu yana uhusiano mkubwa na maisha yao yaliyopita, yameungana kwa njia isiyoachana. Yaani, maisha ya sasa ya kila mtu yanaathiriwa pakubwa na maisha yao yaliyopita. Kwa mfano, kabla ya kufariki, Zhang alimtapeli Li kiwango kikubwa cha pesa. Je, Zhang ana deni la Li? Kwa kuwa analo, ni kawaida kwamba Li anapaswa kuchukua deni lake kutoka kwa Zhang? Hivyo basi baada ya wao kufa, kuna deni kati yao ambalo linatakiwa kulipwa. Wakati wanapata mwili mpya na Zhang anakuwa mwanadamu, je, Li anapataje deni hili kutoka kwake? Mbinu moja ni kwamba Li anapata deni lake kwa kuzaliwa upya kama mwana wa Zhang, Zhang anapata pesa nyingi, na zinaliwa na Li. Haijalishi Zhang anapata pesa nyingi kiasi gani, mwana wa Li anazitumia ovyo. Haijalishi Zhang anapata kiasi gani cha pesa, katu hazitoshi, wakati uleule, mwanawe, kwa namna fulani daima anazitumia pesa za babake kupitia njia na mbinu mbalimbali. Zhang anachanganyikiwa: “Kwa nini mwanangu daima amekuwa kisirani? Mbona wana wa watu wengine ni wema sana? Ni kwa nini mwanangu hana lengo, ni kwa nini hana maana na hana uwezo wa kuchuma pesa zozote, kwa nini daima ninapaswa kumsaidia? Kwa kuwa ni lazima nimsaidie, nitamsaidia, ila kwa nini hata nimpe pesa kiasi gani, daima anataka zaidi? Ni kwa nini asifanye kazi halali, lakini atafanya chochote—kuzurura, kula, kunywa, kuzini, na kucheza kamari? Nini kinaendelea?” Halafu Zhang anafikiria kidogo: “Inaweza kuwa ni kwa sababu nilikuwa na deni lake katika maisha ya zamani. Sawa basi, nitalilipa! Haya hayataisha hadi nilipe kikamilifu!” Inaweza kufika siku ambayo Li anafidia deni lake, na akiwa na umri wa miaka arobaini au hamsini, itafika siku ambayo atajitambua: “Sijafanya kitu kizuri hata kimoja katika hii nusu ya kwanza ya maisha yangu! Nimefuja pesa zote alizozipata baba—ninapaswa kuwa mtu mwema! Nitajikakamua: nitakuwa mtu ambaye ni mwaminifu, na anayeishi ipasavyo, na sitamletea babangu huzuni tena!” Kwa nini anafikiria hivi? Mbona anageuka kuwa mwema ghafla? Kuna sababu ya hili? Ni sababu gani? (Kwa sababu Li amepokea deni lake; Zhang amelipa deni lake.) Katika hili, kuna chanzo na matokeo. Kisa kilianza zamani sana, kabla hawa wawili hawajazaliwa, na hiki kisa cha maisha yao ya zamani kimeletwa katika maisha yao ya sasa, na hakuna anayeweza kumlaumu mwingine. Haijalishi Zhang alimfundisha nini mwanake, mwanake hakumsikiliza, na hakufanya kazi halali hata ya siku—lakini siku ambayo deni lilipwa, hapakuwa na haja ya kumfundisha; mwanake alielewa kiasili. Huu ni mfano rahisi. Kuna mifano mingine mingi kama huu? (Ndiyo.) Na unawafunza watu kitu gani? (Wanapaswa kuwa wema na hawapaswi kutenda maovu.) Kwamba hawapaswi kutenda maovu, na kutakuwa na adhabu kwa maovu yao! Wengi wa wasioamini, hutenda maovu mengi na utendaji maovu wao umekutwa na adhabu, sawa? Je, hii adhabu ni ya kinasibu? Kila linalokutwa na adhabu lina asili na sababu. Unadhani hakuna litakalotendeka baada ya kumlaghai mtu pesa? Unadhani baada ya kuwatapeli pesa zao hakutakuwa na matokeo kwako baada ya kuchukua pesa zao? Hilo halitawezekana, na kutakuwa na athari! Bila kujali yeye ni nani, au kama anaamini ama haamini kuwa kuna Mungu, kila mtu ni lazima atawajibikia mienendo yake na kubeba matokeo ya matendo yake. Kwa kurejelea huu mfano rahisi—Zhang kuadhibiwa, na Li kulipwa—je hii si haki? Watu wakifanya vitu kama hivyo, kuna aina hiyo ya matokeo. Haitenganishwi na utawala wa ulimwengu wa kiroho. Licha ya kuwa wasioamini, wale wasiomwamini Mungu, uwepo wao uko chini ya amri za peponi na sheria ambazo haziwezi kuepukika na yeyote na hakuna mtu anayeweza kuuepuka ukweli huu.

Wale ambao hawana imani huamini kuwa kila kitu ambacho kinaweza kuonekana kipo, ilhali kila kitu kisichoonekana, au ambacho kiko mbali sana na watu, hakipo. Wanapenda kuamini kuwa hakuna “mzunguko wa uhai na mauti,” na hakuna “adhabu,” na kwa hiyo wanatenda dhambi na kufanya maovu bila majuto—ambayo baadaye wataadhibiwa kwayo, au watapata miili kama mnyama. Wengi wa watu mbalimbali miongoni mwa Wasioamini wanapatikana katika mzunguko huu. Ni kwa sababu hawajui kuwa ulimwengu wa kiroho ni mkali katika kuviendesha viumbe hai wote. Ikiwa unaamini au la, huu ukweli upo, na hakuna mtu hata mmoja au chombo chochote kinaweza kuepuka mawanda ya ambacho kinaonwa na macho ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja au chombo kinachoweza kuepuka sheria na mipaka ya sheria za peponi na amri za Mungu. Na hivyo basi mfano huu rahisi unamwambia kila mtu kwamba haijalishi kama unamwamini au humwamini Mungu, haikubaliwi kutenda dhambi na kufanya maovu, na kuna matokeo. Wakati mtu aliyemlaghai mwingine pesa anaadhibiwa hivyo, hiyo adhabu ni ya haki. Mienendo inayoonekana ya kawaida kama hii inaadhibiwa na ulimwengu wa kiroho, inaadhibiwa na amri na sheria za mbinguni za Mungu, na vivyo hivyo uhalifu mkubwa na matendo maovu—ubakaji na unyang’anyi, ulaghai na udanganyifu, wizi na ujambazi, mauaji na uchomaji, na kadhalika—yanapitia adhabu za aina zenye ukali wa viwango mbalimbali. Na hizi adhabu zenye ukali wa viwango mbalimbali zinajumuisha nini? Baadhi yake zinatumia muda kufikisha kiwango cha ukali, na nyingine hufikiwa kwa mbinu mbalimbali, na nyingi hufikiwa kupitia mahali mtu aendapo akipata mwili. Kwa mfano, watu wengine wana maneno machafu. Kuwa na “maneno machafu” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwaapiza wengine mara kwa mara, na kutumia lugha chafu, lugha inayowalaani watu wengine. Lugha yenye nia mbaya inaashiria nini? Inaashiria kuwa mtu ana roho mbaya. Lugha yenye nia mbaya inayowalaani watu wengine mara nyingi inatoka vinywani mwa watu kama hao, na lugha yenye nia mbaya kama hiyo mara nyingi inaandamana na matokeo makali. Baada ya hawa watu kufa na kupokea adhabu stahili, wanaweza kuzaliwa kama mabubu. Watu wengine ni wajanja sana wakiwa hai, mara kwa mara wanawatumia watu wengine kwa manufaa yao, njama zao huwa zimepangwa barabara, na wanafanya mengi yanayowadhuru wengine. Wakizaliwa upya, wanaweza kuwa wazimu au punguani. Watu wengine mara nyingi huwachungulia watu wengine wakiwa faraghani; macho yao huona mengi ambayo hawakutakiwa kuona, na hujua mengi ambayo hawakupaswa kujua, hivyo basi wazaliwapo upya, wanaweza kuwa vipofu. Watu wengine ni hodari sana wakiwa hai, wanapigana mara kwa mara, na kufanya mengi ambayo ni maovu, na kwa hiyo wanapozaliwa upya, wanaweza kuwa vilema au wakakosa mkono, vinginevyo wanaweza kuwa vibyongo, au wenye shingo iliyopinda, huenda wakatembea wakichechemea, au wakawa na mguu mmoja mfupi kuliko mwingine, na kadhalika. Katika hali hii, wanapewa adhabu mbalimbali kutegemea kiwango cha maovu waliyotenda walipokuwa hai. Mwasemaje, kuhusu ni kwa nini watu huwa na makengeza? Je, kuna watu wengi wa hivyo? Kuna wengi wao siku hizi. Watu wengine wana makengeza kwa sababu waliyatumia macho yao sana katika maisha yao yaliyopita, walifanya mambo mengi mabaya, na kwa hiyo wazaliwapo katika haya maisha macho yao hupata makengeza, na katika hali mbaya, hata huwa vipofu. Haya ni malipo! Watu wengine wanaelewana vizuri na wengine kabla hawajafa, wanafanya mambo mengi mazuri kwa wapendwa wao, marafiki, wenza, au watu wanaohusiana nao. Wanatoa hisani na matunzo kwa wengine, au kuwasaidia kifedha, wengine wanawaheshimu sana, na watu kama hao warudipo katika ulimwengu wa kiroho hawaadhibiwi. Kwa asiyeamini kukosa kuadhibiwa kwa njia yoyote inamaanisha alikuwa mtu mzuri sana. Badala ya kuamini katika uwepo wa Mungu, wanaamini tu katika Mzee aliye Angani. Wanaamini tu kuwa kuna roho juu yao akitazama yote wafanyayo—hayo tu ndiyo wanaamini. Na matokeo ni kwamba wanakuwa na mwenendo mzuri zaidi. Hawa watu ni wenye huruma na wakarimu, na mwishowe wakirudi katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapokea vizuri sana na watapata mwili na kuzaliwa upya mapema. Wanapozaliwa tena, watafikia katika familia za aina gani? Japo familia yake haitakuwa ya kitajiri, itakuwa tulivu, kutakuwa na maelewano miongoni mwa wanafamilia, watakuwa na siku mwanana, za kupendeza, kila mmoja atafurahia, na watakuwa na maisha mazuri. Naye atakapokuwa mtu mzima, atakuwa na familia kubwa na jamaa wengi, watoto wake watakuwa na vipawa na kufanikiwa, na familia yake watakuwa na bahati nzuri—na matokeo kama hayo yanahusiana kwa kiasi kikubwa na maisha ya zamani ya mtu. Yaani, mahali mtu huenda baada ya kufa na kupata mwili, wawe wanaume au wanawake, wito wao ni upi, watapitia nini maishani, vikwazo vyao, watapata baraka gani, watakutana na nani, ni nini kitawatokea—hakuna awezaye kulitabiri hili, kuliepuka, au kujificha kutokana nalo. Yaani, baada ya maisha yako kupangwa, kitakachokutokea, hata ujaribu namna gani kukikwepa, hata ukitumia mbinu gani kukiepuka, huna njia ya kuvuruga mkondo wa maisha uliopangiwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho. Kwani upatapo mwili, majaaliwa yako tayari huwa yameishapangwa, ikiwa yatakuwa mazuri au mabaya, kila mtu anapaswa kuyakubali yalivyo, na anapaswa kusonga mbele; hili ni jambo ambalo hakuna mtu aishiye katika maisha haya anaweza kuliepuka, na huu ndio uhalisia. Sawa, umeyaelewa haya yote, naam?

Baada ya kulielewa hili, mnaona kwamba Mungu ana uangalizi unaolipiza sana na mkali pamoja na utawala kwa mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini? Kwanza, Mungu ameweka sheria mbalimbali za mbinguni, amri, na mifumo katika milki ya kiroho, na baada ya kutangazwa kwa hizi sheria za mbinguni, amri na mifumo, ambazo zinatekelezwa kabisa, kama zilivyopangwa na Mungu, na viumbe wenye nyadhifa rasmi mbalimbali katika ulimwengu wa kiroho, na hakuna anayethubutu kuzikiuka. Na kwa hivyo, katika Mzunguko wa uhai na mauti wa wanadamu katika dunia ya mwanadamu, mtu awe amepata mwili kama mwanadamu au mnyama, kuna sheria kwa yote mawili. Kwa kuwa sheria hizi zinatoka kwa Mungu, hakuna anayethubutu kuzivunja, wala hakuna awezaye kuzivunja. Ni kwa sababu tu ya huo ukuu wa Mungu, na kwa sababu kuna sheria hizo, ndiyo ulimwengu yakinifu uonekanao kwa mwanadamu ni wa kawaida na wenye mpangilio; ni kwa sababu tu ya ukuu wa Mungu ndipo mwanadamu anaweza kuishi kwa amani pamoja na ulimwengu mwingine ambao hauonekani kabisa kwa mwanadamu, na kuweza kuishi nao kwa amani—vitu ambavyo vyote haviwezi kutenganishwa na mamlaka ya Mungu. Baada ya maisha ya mtu ya kimwili kufa, roho bado huwa na uhai, basi ni nini kingetendeka ikiwa roho ingekosa utawala wa Mungu? Roho ingezurura kila mahali, ikiingia kila sehemu, na hata kudhuru viumbe hai katika ulimwengu wa wanadamu. Madhara hayo hayangekuwa tu kwa mwanadamu bali pia kwa mimea na wanyama—ila wa kwanza kudhuriwa wangekuwa watu. Kama hili lingetukia—roho kama hiyo ingekosa uendeshaji, na kuwadhuru watu kwa hakika, na kufanya mambo maovu kwa hakika—basi pia kungekuwa na ushughulikiaji ufaao wa roho hii katika ulimwengu wa kiroho: Ikiwa mambo yangekuwa mabaya, roho haingeendelea kuwepo, ingeangamizwa; ikiwezekana, ingewekwa mahali fulani halafu ipatiwe mwili. Yaani, utawala wa ulimwengu wa kiroho kwa roho mbalimbali umepangiliwa, na kutekelezwa kulingana na hatua na sheria. Ni kwa sababu tu ya utawala huo ndiyo ulimwengu yakinifu wa mwanadamu haujatumbukia kwenye machafuko, ndiyo mwanadamu wa ulimwengu wa kuonekana ana akili ya kawaida, urazini wa kawaida, na maisha ya kimwili yenye mpangilio. Ni baada tu ya mwanadamu kuwa na maisha ya kawaida ndiyo wale wanaoishi katika mwili wanaweza kuendelea kufanikiwa na kuzaana katika vizazi vyote.

Mnafikiri nini kuhusu maneno ambayo mmesikia hivi punde? Je, ni mageni kwenu? Na mnahisi nini baada ya Mimi kuwasiliana maneno haya leo? Licha ya kwamba ni mapya, mnahisi kitu kingine chochote? (Ni lazima watu wawe na tabia nzuri, na ninaona Mungu ni mkubwa na wa kuogopwa.) (Baada ya kusikia kuwasiliana kwa karibu kwa Mungu kuhusu jinsi Mungu hupanga hatima za aina mbalimbali za watu, kwa upande mmoja ninahisi kuwa tabia ya Mungu haikubali kosa lolote, na kwamba ninapaswa kumheshimu sana; na kwa upande mwingine, ninafahamu Mungu anapenda aina gani ya watu, na ni aina gani hapendi, kwa hivyo ninataka kuwa mmoja wa wale ambao Mungu anapenda.) Je, mnaona kwamba Mungu ni mwenye kanuni katika matendo Yake katika mambo haya? Anatenda kulingana na kanuni gani? (Anapanga hatima za watu kulingana na yote wanayoyafanya.) Hii inahusu hatima mbalimbali za wasioamini ambao tumezungumzia. Ikija kwa wasioamini, je, kanuni iongozayo matendo ya Mungu ni ile ya kutuza mazuri na kuadhibu mabaya? Kuna upekee wowote? (La.) Je, mnaona kwamba kuna kanuni katika matendo ya Mungu? Wasioamini kwa hakika hawamwamini Mungu, hawatii mipango ya Mungu, na hawafahamu ukuu wa Mungu, na hawamtambui Mungu hata kidogo. Zito zaidi, wanamkufuru Mungu, na kumlaani, na ni mahasimu wa wale wanaomwamini Mungu. Japo watu hawa wana mwelekeo huo kwa Mungu, bado uongozi wa Mungu kwao hauachani na kanuni Zake; Anawaongoza kwa njia ya utaratibu kulingana na kanuni Zake na tabia Yake. Je, Mungu anauchukuliaje uhasama wao? Kama ujinga! Na kwa hiyo Amewasababisha hawa watu—wengi wa wasioamini—wakati mmoja kuwahi kupata mwili kama wanyama. Basi wasioamini ni nini machoni mwa Mungu? Wao ni mifugo. Mungu anaongoza mifugo na kwa watu kama hao Ana kanuni sawa. Hata kwa utawala wa Mungu kwa watu hawa, tabia Yake kwao, bado inaweza kuonekana, kama inavyowezekana sheria Zake kama chanzo cha utawala Wake juu ya vitu vyote. Hivyo basi, unaona mamlaka ya Mungu katika kanuni ambazo kwazo Anawaongoza wasioamini ambao Nimezungumzia hivi punde? Je, mnaona tabia ya haki ya Mungu? (Tunaona.) Yaani, haijalishi Anashughulikia kitu gani kati ya vitu vyote Anavyoshughulikia, Mungu anatenda kulingana na kanuni na tabia Yake. Hiki ndicho kiini cha Mungu. Hangeweza kujitenga kiholela na amri au sheria za mbinguni Alizozipanga kwa sababu Anamwona mtu wa aina hii kama mfugo. Mungu anatenda kulingana na kanuni, bila kuzivuruga hata kidogo, matendo Yake hayaathiriwi na jambo lolote, na haijalishi Anafanya nini, yote ni kulingana na kanuni Zake mwenyewe. Hili ni kwa sababu Mungu ana kiini cha Mungu Mwenyewe, ambacho ni kipengele cha kiini Chake ambacho hakimo kwenye kiumbe yeyote. Mungu ni Mwangalifu na Anawajibika katika kushughulikia Kwake, njia Zake, usimamizi, uongozi, na utawala wa kila chombo, mtu, na kiumbe hai miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba, na Hajawahi kuwa mzembe katika hili. Yeye ni mwenye neema na mkarimu kwa wale walio wazuri; Kwa wale waovu, Anawapa adhabu bila huruma; na kwa viumbe hai mbalimbali, Anafanya mipango ifaayo kwa wakati na kwa njia ya kawaida kulingana na mahitaji mbalimbali ya ulimwengu wa wanadamu katika nyakati mbalimbali, kiasi kwamba hawa viumbe hai mbalimbali wanapata miili kulingana na nafasi wanayochukua kwa njia ya utaratibu, na kuhama kati ya ulimwengu yakinifu na ulimwengu wa kiroho kwa njia ya utaratibu.

Kifo cha kiumbe hai—kuondokewa na uhai wa kimwili—kinaashiria kwamba kiumbe hai huyu ametoka katika ulimwengu yakinifu hadi ulimwengu wa kiroho, ilhali kuzaliwa kimwili kunaashiria kwamba kiumbe hai ametoka ulimwengu wa kiroho na kuja ulimwengu yakinifu kuanza kufanya kazi yake, kuchukua nafasi yake. Iwe ni kuondoka au kuwasili kwa kiumbe, vyote havitenganishwi na kazi ya ulimwengu wa kiroho. Mtu akija katika ulimwengu yakinifu, mipango kabambe na fafanuzi huwa tayari imetengenezwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho kuhusu atakwenda katika familia gani, atafikia enzi gani, atawasili saa ngapi, na nafasi yake. Hivyo basi, maisha yote ya mtu huyu—mambo afanyayo, na njia azichukuazo—yanasonga kulingana na mipango ya ulimwengu wa kiroho, bila hitilafu hata kidogo. Wakati ambapo maisha ya kiroho yanaisha, wakati huo, na namna na mahali ambapo yanaishia, ni wazi na yanaonekana katika ulimwengu wa kiroho. Mungu anatawala ulimwengu yakinifu, na Anatawala ulimwengu wa kiroho, na Hawezi kuchelewesha mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti wa roho, wala Hawezi kufanya makosa katika mpangilio wa mzunguko wa uhai na mauti wa roho. Kila msimamizi katika nyadhifa rasmi katika ulimwengu wa kiroho anafanya majukumu yake na kufanya ambacho anapaswa kufanya, kulingana na maelezo na sheria za Mungu. Na kwa hiyo, katika ulimwengu wa wanadamu, kila tukio la kuonekana lishuhudiwalo na binadamu lina utaratibu, na halina vurugu yoyote. Haya yote ni kwa sababu ya utawala uliopangiliwa wa Mungu juu ya vitu vyote, hali kadhalika kwa sababu mamlaka ya Mungu yanatawala kila kitu, na kila kitu Anachokitawala kinajumuisha ulimwengu yakinifu ambamo mwanadamu anaishi, aidha, ulimwengu wa kiroho usioonekana nyuma ya mwanadamu. Na kwa hiyo, ikiwa mwanadamu anataka kuwa na maisha mazuri, na anataka kuishi katika mazingira mazuri, hali kadhalika kupewa ulimwengu yakinifu mzima, mwanadamu sharti pia apatiwe ulimwengu wa kiroho, ambao hauwezi kuonekana kwa yeyote, ambao unaongoza kila kiumbe hai kwa niaba ya mwanadamu, na ambao una utaratibu. Basi, inaposemwa kwamba Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote, je, hatujakuza ufahamu na uelewa wetu wa “vitu vyote”? (Ndiyo.)

b. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani

Tumemaliza kujadili mzunguko wa uhai na mauti wa kundi la kwanza, wasioamini. Hebu sasa tujadili ule wa kundi la pili, watu mbalimbali wenye imani. “Mzunguko wa uhai na mauti wa watu mbalimbali wenye imani” vilevile ni mada muhimu sana, na inafaa kwamba muwe na kiasi fulani cha uelewa wake. Kwanza, hebu tuseme ni imani gani “imani” kwa watu wa imani inaashiria: dini tano kuu za Uyahudi, Ukristo, Ukatoliki, Uisilamu, na Ubudha. Pamoja na wasioamini, watu ambao ni waumini katika hizi dini tano wanajumuisha idadi kubwa ya watu duniani. Miongoni mwa dini hizi tano, wale ambao wametengeneza ajira kutokana na imani yao ni wachache, lakini hizi dini zina waumini wengi. Waumini wake huenda sehemu tofauti wanapokufa. “Tofauti” na nani? Na wasioamini, watu wasiokuwa na imani, ambao tumemaliza kuzungumzia. Baada ya kufa, waumini wa hizi dini tano huenda mahali pengine, mahali tofauti na wasioamini. Lakini ni mchakato sawa. Ulimwengu wa kiroho pia utafanya uamuzi juu yao kutegemea yale yote waliyoyafanya kabla wafe, baadaye watatayarishwa ipasavyo. Lakini mbona hawa watu wanawekwa sehemu tofauti kutayarishwa? Kuna sababu muhimu ya hili. Na hii sababu ni gani? Nitawaambia kutumia mfano. Lakini kabla nifanye hivyo, mnaweza kuwa mkijiwazia: “Labda ni kwa sababu wana imani ndogo katika Mungu! Wao si wasioamini kabisa.” Hii ndiyo sababu mbona. Kuna sababu muhimu sana kwa wao kuwekwa mahali pengine.

Chukua Ubudha: Hebu Niwaambie ukweli. Mfuasi wa Budha, kwanza kabisa, ni mtu aliyebadili dini kwenda Ubudha, na ni mtu ajuaye imani yake ni nini. Mfuasi wa Budha akinyoa nywele zake na kuwa mtawa wa kiume au mtawa wa kike, hii inamaanisha kuwa amejitenga na mambo ya kidunia na kuacha nyuma ghasia ya dunia ya mwanadamu. Kila siku anakariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha, na kula chakula bila nyama, anaishi maisha ya kujinyima anasa za kimwili, na kupitisha siku zake ndani ya mwangaza baridi, na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi. Anaishi maisha yake yote kwa njia hii. Maisha yake ya kimwili yaishapo, anatengeneza muhtasari wa maisha yake, ila mioyoni mwake hajui atakapoenda baada ya kufa, atakutana na nani, na atakuwa na hatima ya aina gani—mioyoni mwake hana uhakika na haya mambo. Hajafanya chochote zaidi ya kuishi bila mwelekeo maisha yake yote akiambatana na imani, baadaye anaondoka duniani akiambatana na matamanio na maadili asiyoyafahamu. Hiyo ndiyo tamati ya maisha yake ya kimwili anapoiaga dunia ya walio hai, na baada ya hapo, anarudi katika sehemu yake asilia katika ulimwengu wa kiroho. Kama mtu hutu atapata mwili na kurudi duniani kuendelea na kujikuza kwake kunategemea mienendo na kujikuza kwake kabla ya kifo chake. Ikiwa hakufanya kitu kibaya wakati wa uhai wake, atapata mwili haraka na kurudishwa duniani, ambapo atakuwa mtawa wa kiume au mtawa wa kike tena. Kulingana na utaratibu wa mara ya kwanza, mwili wake unajikuza wenyewe, baada ya hapo anakufa na kurudi katika ulimwengu wa kiroho, ambapo anatathminiwa, na baada ya hapo—ikiwa hakuna shida—anaweza kurudi tena katika ulimwengu wa wanadamu, na kuweza kubadili dini hadi Ubudha tena na kuendelea kujikuza. Baada ya kupata mwili mara tatu hadi mara saba, atarudi tena katika ulimwengu wa kiroho, ambapo anakwenda kila mara ambapo maisha yake ya kimwili yanamalizika. Ikiwa viwango na mienendo yake mbalimbali katika ulimwengu wa wanadamu inaambata na sheria za mbinguni za ulimwengu wa kiroho, basi atabaki huko kutoka wakati huu kuendelea; hatapata mwili tena kama mwanadamu; wala hakutakuwa na tishio la yeye kuadhibiwa kwa kutenda maovu duniani. Hatawahi kupitia tena mchakato huu. Badala yake, kulingana na hali zake, atachukua nyadhifa katika milki ya kiroho. Hili ndilo wafuasi wa Budha wanaliita “kufikia hali ya Ubudha.” Kufikia hali ya Ubudha hasa kunamaanisha kufanikiwa kama afisa wa ulimwengu wa kiroho, na baada ya hapo kutozaliwa tena katika mwili mpya ama kuwa katika hatari ya kuadhibiwa. Aidha, kunamaanisha kwamba hakuna kupata taabu tena ya kuwa mwanadamu baada ya kuzaliwa upya. Hivyo basi, bado kuna uwezekano wake kupata mwili tena kama mnyama? (La.) Hili linamaanisha kwamba anabaki kushika nafasi katika ulimwengu wa kiroho, na kamwe hatazaliwa upya. Huu ni mfano mmoja wa kufanikiwa kufikia hali ya Ubudha katika dini ya Ubudha. Na kuhusu wale ambao hawafanikiwi, baada ya wao kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanachunguzwa na kuthibitishwa na ofisa mhusika, ambaye anagundua kuwa ingawa wako hai, hawakujikuza kwa makini au kuwa makini katika kukariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha kama inavyotakiwa na dini ya Ubudha, na badala yake, walikuwa wametenda matendo mengi maovu na kujihusisha katika mienendo mingi mibaya. Basi katika ulimwengu wa kiroho hukumu inatolewa juu ya uovu wao, na baada ya hapo wana hakika ya kuadhibiwa. Hakuna vighairi katika hili. Basi, mtu kama huyu atafanikiwa lini? Katika maisha ambamo hakutenda maovu yoyote—wakati, baada ya kurudi katika ulimwengu wa kiroho, inaonekana hakufanya chochote kibaya kabla afariki. Basi anaendelea kuzaliwa upya, akiendelea kukariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha, akipitisha siku zake ndani ya mwangaza baridi na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi, bila kuua chochote chenye uhai, bila kula nyama, na hafurahii ulimwengu wa mwanadamu, akiachana na vurugu zake kabisa, na kuepuka migogoro na wengine. Katika mchakato huu, hafanyi maovu, na kufuatia hayo anarudi katika ulimwengu wa kiroho, na baada ya matendo na mienendo yake yote kutathminiwa, anatumwa tena katika ulimwengu wa wanadamu, kwa mzunguko unaojirudia mara tatu au saba. Ikiwa hakuna kikwazo wakati huu, basi kupata kwake Ubudhaa hakutaathiriwa, na hakutacheleweshwa. Hii ni sifa ya mzunguko wa uhai na mauti wa watu wote wenye imani: Wanaweza “kufanikiwa” na kushikilia wadhifa katika ulimwengu wa kiroho; hili ndilo linawafanya kuwa tofauti na wasioamini. Kwanza kabisa, wanapokuwa hai duniani, matendo ya wale wanaoweza kushika wadhifa katika ulimwengu wa kiroho ni yapi? Ni sharti wasifanye kabisa ovu lolote: ni lazima wasifanye mauaji, uchomaji, ubakaji, au wizi; wakifanya hila, udanganyifu, au ujambazi, basi hawawezi kufanikiwa. Yaani, wakiwa na uhusiano au ushirikishaji wowote na uovu, hawataweza kuepukana na adhabu ya ulimwengu wa kiroho. Ulimwengu wa kiroho unafanya mipango inayofaa kwa wafuasi wa Budha wanaofikia hali ya Ubudha: wanaweza kuteuliwa kusimamia wale ambao wanaonekana kuamini katika Ubudha, na yule Mzee aliye Angani, na wafuasi wa Budha watapewa mamlaka, wanaweza tu kuteuliwa kuwasimamia wasioamini, vinginevyo wanaweza kuwa wasimamizi wadogo sana. Ugavi huo unalingana na asili ya hizi roho. Huu ni mfano wa Ubudha.

Miongoni mwa dini tano tulizozungumzia, Ukristo ni maalum kiasi fulani. Ni nini maalum kuhusu Ukristo? Hawa ni watu wanaomwamini Mungu wa kweli. Je, inawezekanaje wale wanaomwamini Mungu wa kweli waorodheshwe hapa? Kwa sababu Ukristo ni aina ya imani, basi, bila shaka, unahusiana tu na imani—ni aina ya sherehe, aina ya dini, na kitu tofauti na imani ya wale wanaomfuata Mungu kweli. Kilichonifanya kuuorodhesha miongoni mwa hizi dini tano ni kwa sababu Ukristo umeshushwa hadi kiwango sawa na Uyahudi, Ubudha, Uislamu. Wakristo wengi hawaamini kuna Mungu, au kwamba Anatawala juu ya vitu vyote, seuze kuamini katika uwepo Wake. Badala yake, wanatumia tu Maandiko Matakatifu kuzungumza kuhusu elimu ya dini, wakitumia elimu ya dini kuwafundisha watu kuwa wema, kuvumilia mateso, na kufanya vitu vizuri. Ukristo ni wa aina hiyo ya dini: Unazingatia tu nadharia za mafundisho ya kidini, hauna kabisa uhusiano wowote na kazi ya Mungu ya kusimamia na kuokoa wanadamu, ni dini ya wale wanaomfuata Mungu ambayo haitambuliwi na Mungu. Lakini pia Mungu ana kanuni kuhusu mtazamo Wake kwao. Hawatendei na kuwashughulikia wapendavyo bila mpango, njia sawa na wasioamini. Mtazamo Wake kwao ni sawa na Alio nao kwa wafuasi wa Budha: Ikiwa, angali hai, Mkristo anajiheshimu, anaweza kuzifuata kabisa Amri Kumi za Mungu na kuzingatia sheria na amri katika mahitaji yao kwa tabia zao wenyewe—na ikiwa wanaweza kufanya hivi katika maisha yao yote—basi pia watalazimika kuchukua muda sawa kupitia mzunguko wa uhai na mauti kabla hawajaweza kweli kupata huko kuitwako kuchukuliwa kuenda mbinguni. Baada ya kupata huku kunyakuliwa wanabaki katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanashika wadhifa na kuwa miongoni mwa wasimamizi. Vivyo hivyo, wakifanya maovu duniani, ikiwa ni watenda dhambi na kufanya dhambi nyingi, basi haiepukiki kwamba wataadhibiwa kwa ukali unaotofautiana. Katika Ubudha, kufanikiwa kunamaanisha kufika kwa Nchi Safi ya Furaha Kubwa Sana, lakini hii inaitwaje katika Ukristo? Inaitwa “kuingia mbinguni” na “kunyakuliwa.” Wale ambao kwa kweli “wananyakuliwa” pia wanapitia mzunguko wa uhai na mauti mara tatu hadi saba, halafu, wakiwa wamekufa, wanaingia katika ulimwengu wa kiroho, kana kwamba walikuwa usingizini. Ikiwa walikuwa wanafaa wanaweza kusalia kushika wadhifa, na tofauti na watu walio duniani, hawatapata mwili kwa njia rahisi, au kulingana na mazoea.

Miongoni mwa dini hizi zote, mwisho zinaozungumzia na ambao zinajitahidi kufikia ni sawa na kufanikiwa katika Ubudha; ni vile tu “kufanikiwa” huku kunatimizwa kwa njia tofauti. Wote ni wa aina moja. Kwa hili kundi la watu wa dini hizi ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini katika tabia zao, Mungu huwapa hatima nzuri, sehemu nzuri ya kwenda, na kuwatendea inavyofaa. Haya yote ni sawa, ila si jinsi ambavyo watu wanadhani, sawa? Sasa, baada ya kusikia kuhusu yanayowatokea watu katika Ukristo, mnahisi vipi? Je, mnahisi kwamba shida zao si za haki? Mnawahurumia? (Kidogo.) Hakuna kitu kinachoweza kufanywa; watajilaumu wenyewe. Kwa nini Ninasema hivi? Kazi ya Mungu ni ya kweli; Yeye yu hai na kweli, na kazi Yake inawalenga wanadamu wote na kila mmoja. Kwa nini basi wasikubali hili? Ni kwa nini wanampinga kwa nguvu na kumtesa Mungu? Wana bahati hata kuwa na mwisho kama huu, basi mbona mnawaonea huruma? Kwa wao kutendewa namna hii kunaonyesha uvumilivu mkubwa. Kulingana na kiasi ambacho wanampinga Mungu, wanapaswa kuangamizwa—bali Mungu hafanyi hili, anaushughulikia Ukristo sawa tu na dini ya kawaida. Sasa kuna haja ya kutoa maelezo ya kina kuhusu dini nyinginezo? Maadili ya dini zote hizi ni kuwa watu wapitie shida zaidi, wasifanye maovu, watende mambo mema, wasiwaapize watu wengine, wasiwahukumu wengine, wajitenge na ugomvi, na wawe watu wazuri—mafundisho ya kidini mengi ni ya aina hii. Na kwa hiyo, kama hawa watu wa imani—hawa watu wa dini na madhehebu mbalimbali—wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, basi hawatafanya makosa au dhambi nyingi wakati wangali duniani, na baada ya kupata mwili mara tatu hadi saba, basi kwa jumla watu hawa, watu ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, watabaki kushikilia wajibu katika ulimwengu wa kiroho. Na je, kuna watu wengi wa aina hii? (La, hakuna wengi.) Jibu lako linategemea nini? Si rahisi kutenda mazuri, au kufuata amri na sheria. Ubudha hauwaruhusu watu kula nyama—unaweza kufanya hilo? Ungepaswa kuvaa kanzu za kijivu na kukariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha katika hekalu la wafuasi wa Budha siku nzima, ungeweza kufanya hivyo? Haingekuwa rahisi. Ukristo una Amri Kumi za Mungu, amri na sheria, je, ni rahisi kufuata? Si rahisi! Chukua mfano wa kutowaapia wengine: Watu hawawezi kufuata hii amri. Kwa kushindwa kujizuia wenyewe, wanaapa—na baada ya kuapa hawawezi kurudisha kiapo, basi wanafanya nini? Usiku wanakiri dhambi zao. Wakati mwingine baada ya kuwaapia wengine, bado kuna chuki mioyoni mwao, na hata wanazidi zaidi na kupanga ni lini watawadhuru. Kwa jumla, kwa wale wanaoishi katika hii imani iliyokufa, si rahisi kukosa kufanya dhambi au kutenda maovu. Na kwa hiyo, katika kila dini, ni watu wachache sana tu ndio wanaweza kufanikiwa kweli. Unadhani kwamba kwa sababu watu wengi sana wanafuata hizi dini, wengi wataweza kubaki kuchukua nafasi katika milki ya kiroho. Lakini si wengi hivyo, ni wachache tu ndio wanaweza kulifikia hili. Kwa jumla ni hayo tu kwa mzunguko wa uhai na mauti wa watu wenye imani. Kinachowatofautisha ni kwamba wanaweza kufanikiwa, na hiki ndicho kinawatofautisha na wasioamini.

c. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wafuasi wa Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na wanaitwa tu “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni maalum kwa vile ilizuiliwa kwa wachache waliochaguliwa, ambao ni lazima waje Anapofanya kazi muhimu. Na umuhimu ni upi? Kwa kuwa wao ni kikundi kilichochaguliwa na Mungu, umuhimu ni mkubwa. Yaani, Mungu anataka kuwakamilisha watu hawa, na kuwafanya wawe wakamilifu, na baada ya kazi Yake ya usimamizi kuisha, Atawachukua watu hawa. Je, umuhimu huu si mkubwa? Kwa hiyo, hawa wateule ni wa umuhimu mkubwa kwa Mungu, kwa kuwa ni wale ambao Mungu anakusudia kuwapata. Lakini watendaji huduma—vyema, hebu tuachane na uamuzi uliokwisha kufanywa na Mungu, na kwanza tuzungumzie asili yao. Maana ya kawaida ya “mtendaji huduma” ni mtu anayehudumu. Wanaohudumu ni wa kupita; hawahudumu kwa muda mrefu, au milele, ila wanaajiriwa au kuandikwa kwa muda mfupi. Wengi wao wanachaguliwa kutoka miongoni mwa wasioamini. Wajapo duniani ndipo inapoamriwa kwamba watachukua nafasi ya watendaji huduma katika kazi ya Mungu. Wanaweza kuwa walikuwa mnyama katika maisha yao yaliyopita, lakini pia wanaweza kuwa walikuwa mmoja wa wasioamini. Hiyo ndiyo asili ya watendaji huduma.

Hebu turejee kwa wateule wa Mungu. Wanapokufa, wateule wa Mungu huenda sehemu fulani tofauti kabisa na wasioamini na watu mbalimbali wenye imani. Ni sehemu ambayo wanaambatana na malaika na wajumbe wa Mungu, na ambayo inaendeshwa na Mungu binafsi. Japo katika sehemu hii, wateule wa Mungu hawawezi kumwona Mungu kwa macho yao wenyewe, si kama sehemu nyingine yoyote katika milki ya kiroho; ni sehemu ambayo hili kundi la watu huenda baada ya kufa. Wakifa, wao pia hupitia uchunguzi mkali kutoka kwa wajumbe wa Mungu. Na ni nini kinachochunguzwa? Wajumbe wa Mungu huchunguza njia zilizopitiwa na hawa watu katika maisha yao yote katika imani yao kwa Mungu, ikiwa waliwahi au hawakuwahi kumpinga Mungu wakati huo, au kumlaani, na ikiwa walitenda au hawakutenda dhambi mbaya au maovu. Uchunguzi huu unajibu swali la ikiwa mtu fulani ataondoka au atabaki. “Kuondoka” kunarejelea nini? Na “kubaki” kunarejelea nini? “Kuondoka” kunarejelea ikiwa, kulingana na mienendo yao, watabaki miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu. “Kubaki” kunarejelea kuwa wanaweza kubaki miongoni mwa watu ambao wanafanywa na Mungu kuwa kamili katika siku za mwisho. Mungu ana mipango maalum kwa wale wanaobaki. Katika kila kipindi cha kazi Yake, Mungu atatuma watu kufanya kazi kama mitume au kufanya kazi ya kuyaamsha makanisa, au kuyahudumia. Lakini watu ambao wana uwezo wa kazi kama hizo hawapati miili mara kwa mara kama wasioamini, ambao wanazaliwa upya tena na tena; badala yake, wanarudishwa duniani kulingana na mahitaji na hatua ya kazi ya Mungu, na si wale wapatao mwili mara kwa mara. Je, kuna amri kuhusu ni lini wapate mwili? Je, wanakuja mara moja baada ya kila miaka michache? Je, wanakuja na hiyo haraka? Hawafanyi hivyo. Hii inategemea kazi ya Mungu, hatua ya kazi ya Mungu, na mahitaji Yake, na hakuna amri. Amri moja tu ni kwamba Mungu akifanya hatua ya mwisho ya kazi Yake katika siku za mwisho, wateule hawa wote watakuja. Wakija wote, hii itakuwa mara ya mwisho ambapo wanapata mwili. Na kwa nini hivyo? Hii inategemea matokeo yatakayopatikana katika hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu—kwani katika hatua hii ya mwisho ya kazi, Mungu atawafanya wateule hawa kuwa kamili kabisa. Hili linamaanisha nini? Ikiwa, katika hii awamu ya mwisho, watu hawa watafanywa kuwa kamili, na kufanywa wakamilifu, basi hawatapata mwili kama awali; mchakato wa kuwa wanadamu utakamilika kabisa, sawa na mchakato wa kuzaliwa katika mwili mpya. Hili linawahusu wale watakaobaki. Je, wale ambao hawawezi kubaki huenda wapi? Wasioweza kubaki wanakuwa na sehemu mwafaka ya kwenda. Kwanza kabisa kwa sababu ya maovu yao, makosa waliyofanya, na dhambi walizofanya, wao pia wanaadhibiwa. Baada ya kuadhibiwa, Mungu atafanya mpango wawe miongoni mwa wasioamini, vinginevyo miongoni mwa watu mbalimbali wenye imani, kulingana na hali. Yaani, kuna hali mbili kwao: Moja ni, baada ya kuadhibiwa, labda kuishi miongoni mwa watu wa dini fulani wanapopata mwili tena, na nyingine ni kuwa wasioamini. Kama watakuwa wasioamini, basi watapoteza kila fursa. Lakini wakiwa watu wa imani—kwa mfano, wakiwa Wakristo—bado wangali na nafasi ya kurudi miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu; kwa hili kuna uhusiano changamano sana. Kwa ufupi, ikiwa mmoja wa wateule wa Mungu atafanya kitu kitakachomkosea Mungu, wataadhibiwa sawa tu na watu wengine. Chukulia Paulo, kwa mfano, ambaye tulizungumzia awali. Paulo ni mfano wa wale wanaoadhibiwa. Je, mnapata picha ya yale ninayozungumzia? Je, mipaka ya wateule wa Mungu ni ya kudumu? (Kwa kiasi kikubwa ni ya kudumu.) Kiasi kikubwa chake ni cha kudumu, lakini sehemu ndogo si ya kudumu. Kwa nini hivyo? Nimerejelea hapa sababu moja dhahiri: kutenda maovu. Wanapotenda maovu, Mungu hawataki, na wakati Mungu hawataki, anawatupa miongoni mwa makabila na aina mbalimbali za watu, kitu ambacho kinawaacha bila tegemeo na kufanya kurudi kwao kuwe kugumu. Haya yote yanahusu mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wa Mungu.

Kinachofuata ni mzunguko wa uhai na mauti wa watendaji huduma. Tulizungumzia tu asili za watendaji huduma, yaani, walipata mwili kutoka kwa wasioamini na wanyama katika maisha yao ya awali. Na ujio wa hatua ya mwisho ya kazi, Mungu amechagua kundi la watu hawa kutoka kwa wasioamini, na ni kundi ambalo ni maalum. Nia ya Mungu ya kuchagua watu hawa ni kuhudumia kazi Yake. “Huduma” si neno la jamala kutamka, wala si kitu ambacho mtu yeyote angependa, lakini tunapaswa kuona ambao linawalenga. Kuna umuhimu maalum katika uwepo wa watendaji huduma wa Mungu. Hamna mwingine awezaye kuchukua nafasi yao, kwa kuwa walichaguliwa na Mungu. Na ni ipi nafasi ya watendaji huduma? Kuwahudumia wateule wa Mungu. Kwa ujumla, kazi yao ni kuihudumia kazi ya Mungu, kushirikiana na kazi ya Mungu, na kushirikiana na ukamilisho wa Mungu wa wateule Wake. Haijalishi kama wanafanya kazi ngumu, wanafanya kazi fulani, au wanajiandaa kufanya kazi fulani, ni yapi mahitaji ya Mungu kwa hawa watu? Je, anawadai sana kwa masharti Yake kwao? (La, Mungu anawataka wawe waaminifu.) Watendaji huduma pia wanapaswa kuwa waaminifu. Haijalishi asili zako, au kwa nini Mungu alikuchagua, ni lazima uwe mwaminifu kwa Mungu, kwa kile anachokuagiza, na vilevile kazi unayoiwajibikia na jukumu unalolifanya. Ikiwa watendaji huduma wanaweza kuwa waaminifu, na kumridhisha Mungu, basi hatima yao itakuwaje? Wataweza kubaki. Je, ni baraka kuwa mtendaji huduma anayebaki? Kubaki kunamaanisha nini? Hii baraka inamaanisha nini? Kihadhi, hawafanani na wateule wa Mungu, wanaonekana tofauti. Kwa hakika, hata hivyo, wakipatacho katika maisha haya siyo sawa na wakipatacho wateule wa Mungu? Angalau, katika haya maisha ni sawa. Hamlipingi hili, naam? Matamko ya Mungu, neema ya Mungu, riziki ya Mungu, baraka za Mungu—ni nani hafurahii vitu hivi? Kila mtu anafurahia wingi wa haya. Kitambulisho cha mtendaji huduma ni mtendaji huduma, lakini kwa Mungu, ni miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba—tofauti ni kwamba tu nafasi yao ni ile ya watendaji huduma. Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, kuna tofauti kati ya watendaji huduma na wateule wa Mungu? Kwa hakika, hakuna. Kwa mazungumzo ya kawaida, kuna tofauti, katika kiini kuna tofauti, kwa kurejelea nafasi wanazoshika kuna tofauti, ila Mungu hawabagui hawa watu. Hivyo ni kwa nini hawa watu wanatambuliwa kama watendaji huduma? Unapaswa kuelewa hili. Watendaji huduma wanatokana na wasioamini. Kutaja wasioamini kunatuambia kuwa maisha yao ya awali ni mabaya: Wote ni wakana Mungu, katika maisha yao ya nyuma walikuwa wakana Mungu, hawakumwamini Mungu, na walikuwa mahasimu wa Mungu, wa ukweli, na vitu vizuri. Hawakumwamini Mungu, hawakuamini kuwa kuna Mungu, hivi wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu? Ni haki kusema kwamba, kwa kiwango kikubwa, hawana. Sawa tu na wanyama wasivyo na uwezo wa kuelewa maneno ya mwanadamu, watendaji huduma hawaelewi Mungu anasema nini, Anahitaji nini, kwa nini Ana mahitaji kama hayo—hawaelewi, hivi vitu havieleweki kwao, wanabaki bila nuru. Na kwa sababu hii, watu hawa hawana uhai tuliouzungumzia. Je, bila uhai, watu wanaweza kuelewa ukweli? Je, wana ukweli? Je, wana uzoefu na ufahamu wa maneno ya Mungu? (La.) Hizo ndizo asili za watendaji huduma. Lakini kwa kuwa Mungu anawafanya hawa watu watendaji huduma, bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo; Hawadharau, na Hawachukulii kwa uzembe. Japo hawaelewi maneno yake, na hawana uhai, bado Mungu ni mwema kwao, na bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo. Mmevizungumzia hivi viwango hivi karibuni: Kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya Asemacho. Katika huduma yako ni lazima uhudumu unapohitajika, na ni lazima uhudumu hadi mwisho. Ikiwa unaweza kuwa mtendaji huduma mwaminifu, unaweza kuhudumu hadi mwisho, na unaweza kutimiza agizo uliloaminiwa na Mungu kikamilifu, basi utaishi maisha ya thamani, na utaweza kubaki. Ukitia bidii kidogo, ukijaribu kwa nguvu, ukiongeza maradufu jitihada zako za kumjua Mungu, ukiweza kuongea kidogo kuhusu ufahamu wa Mungu, ukiweza kumshuhudia Mungu, na zaidi, ukielewa kitu kuhusu mapenzi ya Mungu, ukiweza kushirikiana katika kazi ya Mungu, na ukiyazingatia kidogo mapenzi ya Mungu, basi wewe, mtendaji huduma, utapata bahati. Na hili litakuwa badiliko gani katika bahati? Hutaweza kubaki tu. Kutegemea tabia yako na malengo na juhudi zako binafsi, Mungu atakufanya mmoja wa wateule. Hii itakuwa bahati yako. Kwa watendaji huduma, ni nini kizuri kuhusu hili? Ni kwamba unaweza kuwa mmoja wa wateule wa Mungu. Wakiwa mmoja wa wateule wa Mungu, inamaanisha kuwa hawatapata tena mwili kama wanyama au wasioamini. Je, hiyo ni habari njema? Ndiyo, na ni habari njema. Inamaanisha, watendaji huduma wanaweza kufinyangwa. Si kwamba kwa mtendaji huduma, Mungu akimpangia awali kuhudumu, daima atahudumu; si lazima iwe hivyo. Kutegemea tabia yake binafsi, Mungu atamtendea tofauti, na kumjibu tofauti.

Lakini kuna watendaji huduma ambao hawana uwezo wa kumtumikia Mungu hadi mwisho; wakati wa huduma yao, kuna wale ambao wanajitoa nusu na kutelekeza Mungu, kuna wale ambao hufanya mambo mengi mabaya, na hata wale ambao wanasababisha madhara makubwa na kufanya uharibifu mkubwa kwa Kazi ya Mungu, kuna hata watendaji huduma ambao humlaani Mungu, na kadhalika—na ni nini maana ya matokeo haya yasiyorekebishika? Matendo maovu yoyote kama hayo humaanisha kufikia mwisho kwa huduma yao. Kwa sababu matendo yako wakati wa huduma yamekuwa maovu sana, kwa sababu umevuka mipaka yako, wakati Mungu anaona huduma yako haijafikia kiwango Atakutoa ustahiki wa kutoa huduma, Hatakubali ufanye huduma, Atakutoa mbele ya macho Yake, na kutoka katika nyumba ya Mungu. Au ni kwamba hutaki kufanya huduma? Je, siku zote hutamani kufanya maovu? Je, siku zote wewe si mwaminifu? Sawa basi, kuna suluhisho rahisi: Utanyang’anywa ustahiki wako wa kuhudumu. Kwa Mungu, kunyang’anya mtendaji huduma ustahiki wa kufanya huduma kuna maana kuwa mwisho wa mtendaji huduma huyu umetangazwa, na hatakuwa anastahili kufanya huduma kwa Mungu tena, Mungu hahitaji huduma zake tena, na haijalishi ni vitu vipi vizuri atasema, maneno haya yatabaki ya bure. Mambo yanapofikia kiwango hiki, hii hali itakuwa isiyorekebishika; watendaji huduma kama hawa hawana njia ya kurudi nyuma. Na Mungu huwafanyia nini watendaji huduma kama hawa? Anawaachisha tu kutoa huduma? La! Je, Anawazuia tu wasibaki? Au anawaweka katika upande mmoja. Na kuwangoja wabadilike? Hafanyi hivyo. Kwa kweli Mungu hana upendo sana kwa watendaji huduma. Iwapo mtu ana aina hii ya mwelekeo katika huduma yake kwa Mungu, Mungu, kutokana na matokeo ya mwelekeo huu, Atamnyang’anya ustahiki wake wa kutoa huduma, na kwa mara nyingine tena kumtupa miongoni mwa wasioamini. Na ni ipi hatima ya watendaji huduma waliorudishwa tena kati ya wasioamini? Ni sawa na ile ya wasioamini; kupata mwili kama wanyama na kupokea adhabu ya wasioamini katika ulimwengu wa kiroho. Na Mungu hatakuwa na maslahi ya kibinafsi katika adhabu yao, kwa kuwa hawana umuhimu wowote tena katika kazi ya Mungu. Huu si mwisho tu wa maisha yao ya imani kwa Mungu, ila mwisho wa hatima yao pia, kutangazwa kwa hatima yao. Kwa hiyo watendaji huduma wakihudumu vibaya, watapata matokeo wao wenyewe. Kama mtendaji huduma hana uwezo wa kufanya huduma hadi mwisho kabisa, au amenyang’anywa ustahiki wake wa kutoa huduma katikati ya njia, basi watatupwa miongoni mwa wasioamini—na kama watatupwa miongoni mwa wasioamini watashughulikiwa sawa na jinsi mifugo wanavyoshughulikiwa, sawa na watu wasio na akili au urazini. Ninapoielezea namna hiyo, unaelewa, naam?

Ilivyo hapo juu ndivyo Mungu anavyoushughulikia mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wake na watendaji huduma. Mnajihisi vipi baada ya kusikia haya? Nimewahi kuzungumza kuhusu mada ambayo Nimeitaja sasa hivi, mada ya wateule wa Mungu na watendaji huduma? Kwa kweli Nimewahi, lakini hamkumbuki. Mungu ni mwenye haki kwa wateule wake na watendaji huduma. Kwa vyovyote vile Yeye ni mwenye haki, siyo? Kuna mahali popote unaweza kupata makosa? Wapo watu ambao watasema: “Kwa nini Mungu ni mvumilivu sana kwa wateule? Na kwa nini anawavumilia kidogo sana watendaji huduma?” Kuna yeyote angependa kuwatetea watendaji huduma? “Je, Mungu anaweza kuwapa watendaji huduma muda zaidi, na kuwa mstahimilivu na mvumilivu zaidi kwao?” Haya maneno yako sahihi? (Hapana, hayapo sahihi.) Na ni kwa nini hayapo sahihi? (Kwa kuwa tumeonyeshwa neema kweli kwa kufanywa kuwa watendaji huduma.) Watendaji huduma wameonyeshwa neema kwa kuruhusiwa kufanya huduma! Bila ya dhana “watendaji huduma,” na bila Kazi ya watendaji huduma, hawa watendaji huduma wangekuwa wapi? Miongoni mwa wasioamini, wakiishi na kufa pamoja na mifugo. Ni neema kubwa wanayoifurahia leo, kuruhusiwa kuja mbele za Mungu, na kuja katika nyumba ya Mungu! Hii ni neema kubwa! Kama Mungu hakukupa nafasi ya kutoa huduma, usingekuwa na nafasi ya kuja mbele za Mungu. Kwa kusema machache, hata kama wewe ni Mbudha na umefanikiwa, sanasana wewe ni mtumwa katika ulimwengu wa kiroho; hutaweza kamwe kumwona Mungu, au kusikia sauti Yake, au kusikia maneno Yake, au kuhisi upendo Wake na baraka Zake kwako, na hata isingewezekana kamwe kuonana na Yeye uso kwa uso. Kilicho tu mbele ya wafuasi wa Budha ni kazi rahisi. Hawawezi kamwe kumjua Mungu, na wanaitikia na kutii kiupofu tu, wakati ambapo watendaji huduma wanafaidi mengi sana katika hatua hii ya kazi. Kwanza, wanaweza kuonana na Mungu uso kwa uso, kusikia sauti Yake, kuyasikia maneno Yake, na kupitia neema na baraka Anazowapa watu. Aidha, wanaweza kufurahia maneno na ukweli unaopewa na Mungu. Watendaji huduma kwa kweli hupata mengi zaidi! Basi, kama mtendaji huduma, huwezi hata kutia juhudi inayofaa, je, Mungu bado atakuweka? Hawezi kukuweka. Hataki mengi kutoka kwako lakini hufanyi chochote Anachotaka vizuri, hujawajibika ipasavyo—na kwa hivyo, bila shaka, Mungu hawezi kukuweka. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Mungu hakudekezi, lakini wala Hakubagui. Mungu anafanya kazi na kanuni hizo. Mungu hutekeleza mambo jinsi hii kwa watu na viumbe wote.

Inapokuja katika ulimwengu wa kiroho, kama viumbe mbalimbali waliomo watafanya kitu kibaya, kama hawafanyi kazi yao inavyostahili, Mungu pia ana sheria za peponi na amri zifaazo kuwashughulikia—hili halipingwi. Basi, katika maelfu kadhaa ya miaka ya kazi ya usimamizi ya Mungu, wasimamizi wengine ambao walifanya maovu wameangamizwa, wengine, leo, wangali wanazuiliwa na kuadhibiwa. Hili ndilo linafaa kukabiliwa na kila kiumbe aliye katika ulimwengu wa kiroho. Akifanya kitu kibaya au kutenda maovu, anaadhibiwa—ambayo ni sawa na jinsi Mungu anavyotenda kwa wateule Wake na watendaji huduma. Na kwa hivyo, iwe ni katika ulimwengu wa kiroho au ulimwengu yakinifu, kanuni ambazo Mungu hutekeleza matendo hazibadiliki. Bila kujali kama unaweza kuona matendo ya Mungu au la, kanuni zao hazibadiliki. Daima, Mungu amekuwa na kanuni sawa kwa jinsi Anavyotekeleza matendo kwa vitu vyote na kuvishughulikia vitu vyote. Hili halibadiliki. Mungu atakuwa mkarimu kwa wale walio miongoni mwa wasioamini ambao angalau wanaishi ipasavyo, na kuwapa nafasi wale walio katika kila dini ambao wana tabia nzuri na hawatendi maovu, kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao katika vitu vyote vinavyosimamiwa na Mungu, na kufanya kile ambacho wanafaa kufanya. Vivyo hivyo, kati ya wale wanaomfuata Mungu, kati ya wateule Wake, Mungu habagui mtu yeyote kulingana na kanuni Zake hizi. Ni mwema kwa kila mtu anayeweza kumfuata kwa dhati, na kupenda kila mtu anayemfuata kwa dhati. Ni kwamba tu kwa aina hizi mbalimbali za watu—wasioamini, aina tofauti za watu wenye imani, na wateule wa Mungu—anachowazawadia wao ni tofauti. Chukulia wasioamini: hata kama hawamwamini Mungu, na Mungu huwaona kama mifugo, miongoni mwa kila kitu kila mmoja wao ana chakula, mahali pao wenyewe, na mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti. Wanaotenda maovu wanaadhibiwa, na wanaofanya mazuri wanabarikiwa na hupokea wema wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo? Kwa watu wenye imani, kama wanaweza kutii hasa maadili ya kidini, kizazi baada ya kizazi, basi baada ya hivi vizazi vyote Mungu hatimaye atatoa uamuzi Wake kwao. Vivyohivyo, kwa wewe leo, awe mmoja wa wateule wa Mungu au mtendaji huduma, Mungu vilevile atakuwazisha na kuamua mwisho wako kulingana na kanuni na amri za utawala ambazo Ameziweka. Miongoni mwa aina hizi kadhaa za watu—aina tofauti za watu wa imani, walio katika dini tofauti—je, Mungu amewapa nafasi ya kuishi? Uko wapi Uyahudi? Mungu ameingilia katika imani yao? Hajaingilia, siyo? Na vipi kuhusu Ukristo? Hajaingilia pia? Anawaruhusu kufuata mipangilio yao wenyewe, na Hasemi nao, au kuwapa nuru yoyote, na, zaidi ya hayo, Hawafichulii kitu chochote: “Kama unafikiria ni sahihi, basi amini hivyo.” Wakatoliki wanamwamini Maria, na kwamba ni kupitia kwa Maria ambapo habari zilimfikia Yesu; hiyo ndiyo aina yao ya imani. Na Mungu amewahi kurekebisha imani yao? Mungu huwapa uhuru, Mungu hawasikizi, na huwapa sehemu fulani ambapo wataishi. Na kwa Waisilamu na wafuasi wa Budha, je, Yuko hivyo pia? Ameweka mipaka kwa ajili yao, pia, na kuwaruhusu kuwa na mahali pao wenyewe pa kuishi, bila ya kuingilia imani zao. Yote yamepangwa vizuri. Na unaona nini katika haya yote? Kwamba Mungu ana mamlaka, lakini hatumii vibaya mamlaka Yake. Mungu hupanga vitu vyote katika mpangilio taratibu, na ni mwenye utaratibu, na katika hili busara na kudura Zake vinadhihirika.

Leo tumezungumzia mada mpya na maalum, ambayo inahusu masuala ya ulimwengu wa kiroho, ambayo ni sehemu mojawapo ya uendeshaji na utawala wa Mungu juu ya ulimwengu wa kiroho. Mlipokuwa hamyaelewi mambo haya, huenda mlisema; “Chochote kinachohusiana na haya ni mafumbo, na hayahusiani na kuingia kwetu katika uhai; mambo haya yametenganishwa na jinsi watu wanaishi hasa, na hatutaki kuyaelewa, wala hatutamani kuyasikia. Hayana uhusiano wowote na kumfahamu Mungu.” Sasa, mnafikiria kuna shida na aina hiyo ya mawazo? Ni sahihi? (La.) Mawazo kama hayo sio sahihi, na yana matatizo makubwa. Hii ni kwa sababu, kama unatamani kujua jinsi Mungu anatawala juu ya vitu vyote, huwezi tu kuelewa kile ambacho unaweza kuona na kile unachokipata kutoka kwa mawazo yako. Ni lazima pia ufahamu ya ulimwengu ule mwingine ambao hauonekani kwako, ambao umeunganishwa kwa njia isiyochanganulika na huu ulimwengu ambao unaweza kuuona. Haya yanahusu ukuu wa Mungu, yanahusu mada ya “Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote”; ni taarifa kuhusu hayo. Bila ya hii taarifa, kungekuwepo na dosari na upungufu katika ufahamu kuhusu jinsi Mungu alivyo chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hivyo, kile ambacho tumeongea leo kinaweza kusemwa kuwa kimetamatisha yale tuliyoyaongelea kabla, pamoja na maudhui ya “Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Baada ya kuelewa haya, mna uwezo wa kumjua Mungu kupitia maudhui haya? Na kilicho muhimu zaidi ni kwamba leo, Nimewapitisha ujumbe muhimu sana: kuhusu watendaji huduma. Ninajua mnapenda sana kusikia mada kama hizi, kwamba mnayatilia maanani sana mambo haya, basi mnahisi mmeridhika na yale Nimezungumzia leo? (Ndiyo, tumeridhika.) Mwaweza kuwa hamvutiwi sana na vitu vingine, lakini haswa mnavutiwa na mazungumzo kuhusu watendaji huduma, kwa kuwa hii mada inagusia kila moyo wa mmoja wenu.

Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu

a. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe

Tumefikia mwisho wa mada ya “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” vilevile na ile ya “Mungu ni wa kipekee Mungu Mwenyewe.” Baada ya kufanya hivyo, tunahitaji kufanya muhtasari. Muhtasari wa aina gani? Unaomhusu Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa ni kumhusu Mungu Mwenyewe, basi lazima ugusie kila kipengele cha Mungu, vilevile aina ya imani ya watu kwa Mungu. Na kwa hiyo, kwanza lazima Niwaulize: Baada ya kusikia mahubiri, Mungu ni nani katika jicho la mawazo yako? (Muumbaji.) Mungu katika jicho la mawazo yako ndiye Muumbaji. Kuna kitu kingine chochote? Mungu ni Bwana wa vitu vyote. Maneno haya yanafaa? (Yanafaa.) Mungu ndiye mtawala wa vitu vyote, na anayeendesha vitu vyote. Aliumba vitu vyote, Anaendesha vitu vyote, na pia Anatawala vitu vyote na kukimu vitu vyote. Hii ndiyo hadhi ya Mungu, na utambulisho wa Mungu. Kwa vitu vyote na vyote vilivyopo, utambulisho wa kweli wa Mungu ni Muumbaji, na Mtawala wa vitu vyote. Huo ni utambulisho unaomilikiwa na Mungu, na ni wa kipekee miongoni mwa vitu vyote. Hakuna Kati ya viumbe wa Mungu—wawe miongoni mwa wanadamu, au katika ulimwengu wa kiroho—ambao wanaweza kutumia namna yoyote au kisingizio kuiga au kuchukua nafasi ya utambulisho wa Mungu na hadhi Yake, kwa kuwa kuna mmoja tu kati ya vitu vyote anayemiliki huu utambulisho, nguvu, mamlaka, na uwezo wa kutawala vitu vyote: Mungu wetu wa kipekee Mwenyewe. Anaishi na kutembea miongoni mwa vitu vyote; Anaweza kufikia palipo mbali zaidi, juu ya vitu vyote; Anaweza kunyenyekea kwa kuwa mwanadamu, kuwa mmoja wa wenye mwili na damu, kuonana ana kwa ana na watu na kushiriki na wao dhiki na faraja; wakati huo huo, Anaamuru vitu vyote, na Huamua hatima ya vitu vyote, na njia itakayofuata, zaidi na hayo, Anaongoza hatima za wanadamu wote, na njia za wanadamu. Mungu kama huyu anastahili kuabudiwa, kuheshimiwa, na kujulikana na viumbe wote. Na hivyo, pasipo kujali uko katika kundi na aina gani ya wanadamu, kumwamini Mungu, kumfuata Mungu, kumheshimu Mungu sana, kukubali utawala wa Mungu, na kukubali mipango ya Mungu katika hatima yako ndio uamuzi wa pekee, na uamuzi unaofaa, kwa mtu yeyote, kwa kiumbe chochote kinachoishi. Katika upekee wa Mungu, watu huona kwamba mamlaka Yake, tabia Yake ya haki, kiini Chake, na namna ambazo Anakirimia vitu vyote ni za kipekee; upekee Wake unabainisha utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, na unabaini hadhi Yake. Na kwa hivyo, miongoni mwa viumbe vyote, kama kuna kiumbe anayeishi katika ulimwengu wa kiroho au miongoni mwa wanadamu angetamani kusimama badala ya Mungu, haingewezekana, sawa na kujaribu kumuiga Mungu. Huu ni ukweli. Ni mahitaji yapi kwa mwanadamu aliyonayo Muumbaji na Mtawala kama huyu, ambaye Aliye na utambulisho, nguvu, na hadhi ya Mungu Mwenyewe? Hili linapaswa kuwa wazi kwa kila mtu, na linapaswa kukumbukwa nanyi, na ni muhimu sana kwa Mungu na mwanadamu!

b. Mielekeo Mbalimbali ya Wanadamu kwa Mungu

Jinsi watu wamtendeavyo Mungu huamua hatima yao, na huamua jinsi Mungu anavyowatendea na kuwashughulikia. Kufikia sasa nitawapa mifano kadhaa ya jinsi watu wanavyotenda mbele za Mungu. Hebu tusikie kitu kuhusu ama mienendo na tabia ambazo kwazo wanamtendea Mungu ni sahihi au la. Hebu tuangalie mwenendo wa aina saba za watu wafuatao:

1) Kuna aina moja ya watu ambao mwelekeo wao kwa Mungu haswa ni wa kipuuzi. Wanafikiria kuwa Mungu ni kama Bodhisattva au kiumbe takatifu wa masimulizi ya kibinadamu, na kuwataka watu kusujudu mara tatu wanapokutana na kuchoma ubani baada ya kula. Kwa hivyo, katika mioyo yao, wanapomshukuru Mungu kwa neema Yake, na kuwa wenye shukrani kwa Mungu, mara nyingi wana msukumo kama huo. Hivyo wanatamani Mungu wanaomwamini leo, kama kiumbe takatifu wanayemtamania ndani ya mioyo yao, anaweza kukubali mienendo yao Kwake ambapo wanasujudu mara tatu wanapokutana, na kuchoma ubani baada ya kula.

2) Watu wengine wanamwona Mungu kama Budha anayeishi, mwenye uwezo wa kutoa wanaoishi wote kutoka kwenye mateso, na kuwaokoa; wanaona Mungu kama Budha anayeishi mwenye uwezo wa kuwatoa kwenye mateso mengi. Imani ya watu hawa kwa Mungu ni kumwabudu Mungu kama Buddha. Ijapokuwa hawachomi ubani, kusujudu, au kutoa sadaka, katika nyoyo zao Mungu ni kama tu Buddha, na huwataka tu wawe wema na wenye huruma, kuwa wasiue chochote kilicho hai, wasiwaapie wengine, waishi maisha yanayoonekana kuwa manyoofu, na wasifanye chochote kibaya—vitu hivi tu. Huyu ndiye Mungu mioyoni mwao.

3) Watu wengine humwabudu Mungu kama mtu mkubwa au maarufu. Kwa mfano, kwa namna yoyote mtu huyu mkubwa hupenda kuongea, kwa kiimbo chochote huongea, maneno na msamiati anaotumia, kiimbo chake, ishara zake za mikono, maoni na matendo yake, ukali wake—wanaiga yote, na hivi ndivyo vitu ambavyo ni lazima watavisababisha katika mwendo wa imani yao kwa Mungu.

4) Watu wengine wanamwona Mungu kama mfalme, wanahisi kuwa Yuko juu ya vitu vyote vingine, na hakuna anayejaribu kumkosea—na wakifanya hivyo, wataadhibiwa. Wanaabudu mfalme kama huyo kwa sababu wafalme huwa wanashikilia sehemu fulani kwenye mioyo yao. Mawazo, tabia, mamlaka, na asili ya wafalme—hata na maslahi na maisha yao ya kibinafsi—yote huwa kitu ambacho watu hawa lazima waelewe, masuala na mambo ambayo wanashughulika nayo, na hivyo wanamwabudu Mungu kama mfalme. Imani ya namna hiyo inachekesha.

5) Watu wengine wana imani fulani katika uwepo wa Mungu, ambayo ni kubwa na isiyotingishika. Kwa sababu ufahamu wa Mungu kwao ni wa juujuu mno na hawana mazoea ya maneno ya Mungu, wanamwabudu kama sanamu. Sanamu hii ni Mungu aliye ndani ya mioyo yao, ni kitu ambacho wanafaa kuogopa na kusujudia, na ambayo wanalazimika kufuata na kuiga. Wanamwona Mungu kama sanamu, ambayo wanafaa kufuata maisha yao yote. Wanaiga sauti ambayo kwayo Mungu huzungumza, na kwa nje wanaiga wale ambao Mungu anapenda. Aghalabu wanafanya mambo ambayo yanaonekana kuwa manyoofu, safi, na ya kweli, na wanafuata hii sanamu kama mwenzao au mwandani wao ambaye wanaweza kushirikiana. Hiyo ndiyo aina ya imani yao.

6) Kuna watu ambao, kando na kusoma maneno mengi ya Mungu na kuwa wameyasikia mahubiri mengi, wanahisi ndani ya nyoyo zao kuwa msimamo tu wa mienendo yao kwa Mungu ni kuwa kila wakati wanafaa wawe watiifu na kujipendekeza, la sivyo wanafaa kumsifu Mungu na kumwabudu kwa njia isiyo halisi. Wanaamini kuwa Mungu ni Mungu anayewahitaji kutenda hivyo, na wanaamini kuwa wasipofanya hivyo, basi wakati wowote wanaweza kuchochea hasira Yake au kumtenda dhambi, na kwamba kwa sababu ya kutenda dhambi Mungu atawaadhibu. Huyo ndiye Mungu mioyoni mwao.

7) Kisha kuna watu wengi, wanaotafuta riziki ya kiroho katika Mungu. Kwa sababu wanaishi katika ulimwengu huu, hawana amani au furaha, na hakuna wanapopata faraja. Baada ya kumpata Mungu, wanapokuwa wameona na kusikia maneno Yake, ndani ya mioyo yao wanafurahi na kusisimka kisiri. Hii ni kwa sababu wanaamini kuwa tayari wamepata mahali ambapo patawapa furaha, kwamba hatimaye wamepata Mungu ambaye atawapa riziki ya kiroho. Baada ya kukubali Mungu na kuanza kumfuata, wanakuwa wenye furaha, maisha yao yanakamilishwa, hawako kama wengine wasioamini tena, wanaotembea usingizini maishani mwao kama wanyama, na wanahisi kuwa kuna kitu cha kutamania katika maisha. Kwa hivyo, wanafikiri kuwa huyu Mungu anaweza kuwatimizia mahitaji yao ya kiroho na kuleta furaha kubwa katika mawazo na Roho. Bila ya kujua, wanakuwa hawawezi kumwacha huyu Mungu anayewapa riziki ya kiroho, Anayeleta furaha katika Roho na familia zao. Wanaamini kuwa imani katika Mungu haihitaji zaidi ya kuwapa riziki ya kiroho.

Je, mielekeo kumwelekea Mungu ya watu hawa wa aina mbalimbali waliotajwa hapo juu ipo miongoni mwenu? (Ipo.) Kama, katika imani yao katika Mungu, moyo wa mtu una mwelekeo wowote kati ya hii, je, kweli wanaweza kuja mbele za Mungu? Kama watu wana mwelekeo wowote kati ya hii katika mioyo yao, je, wanamwamini Mungu? Je, wanamwamini Mungu Mwenyewe yule wa kipekee? (La.) Kwa kuwa humwamini Mungu wa kipekee Mwenyewe, unamwamini nani? Kama unachoamini si Mungu Mwenyewe wa kipekee, kuna uwezekano unaamini katika sanamu, mtu maarufu, au Bodhisattva, kuwa unamwabudu Budha moyoni mwako. Zaidi ya hayo, kuna uwezekano unaamini katika mtu wa kawaida. Kwa muhtasari, kwa sababu ya aina tofautitofauti za imani za watu na mielekeo kwa Mungu, watu humweka Mungu wa utambuzi wao wenyewe katika nyoyo zao, wanamlazimishia Mungu fikira zao, wanaweka fikira na mielekeo yao kuhusu Mungu sambamba na Mungu Mwenyewe wa kipekee, na baadaye wanayadhihirisha ili yafanywe kuwa takatifu. Ina maana gani watu wakiwa na mielekeo hiyo isiyofaa kwa Mungu? Ina maana kuwa wamemkataa Mungu wa kweli Mwenyewe na kuabudu Mungu bandia, na ina maana kuwa wakati uleule wanapomwamini Mungu, wanamkataa Mungu, wanampinga, na kuwa wanakana uwepo wa Mungu wa kweli. Kama watu watazidi kushikilia imani za aina hiyo, matokeo yao yatakuwa gani? Kwa aina hiyo ya imani, je, wanaweza kufikia karibu na kutimiza matakwa ya Mungu? (La, hawawezi.) Kinyume cha hayo, kwa sababu ya dhana na fikira zao, watu watazidi kuwa mbali na njia ya Mungu, kwa kuwa njia wanayoifuata ni kinyume cha njia ambayo Mungu anawahitaji waifuate. Umekwisha kusikia hadithi ya “kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini”? Hii yaweza kuwa ni mfano wa kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini. Watu wakimwamini Mungu kwa njia hii ya kipumbavu, basi kadiri unavyojaribu kwa nguvu, ndivyo utakavyokuwa mbali zaidi na Mungu. Na kwa hiyo nakuonya hivi: Kabla ya kufunga safari, ni lazima kwanza ujue kama unaenda njia iliyo sawa. Lenga katika juhudi zako, kuwa na uhakika na kujiuliza, “Je, Mungu ninayemwamini ni Mtawala wa vitu vyote? Je, huyu Mungu ninayemwamini ni mtu tu wa kunipa riziki ya kiroho? Ni sanamu yangu? Je, huyu Mungu ninayemwamini anataka nini kutoka kwangu? Mungu huwa anakubali chochote ninachokifanya? Je, kila kitu ninachokifanya na kutafuta kinalingana na kazi ya kumjua Mungu? Je, kinalingana na mahitaji ya Mungu kwangu? Je, njia ninayoifuata inajulikana na kukubaliwa na Mungu? Je, Mungu anaridhishwa na imani yangu?” Aghalabu na mara kwa mara unafaa ujiulize haya maswali. Kama ungetaka kuutafuta ufahamu wa Mungu, basi lazima uwe na dhamiri safi na malengo wazi ndipo uweze kumridhisha Mungu.

Inawezekana kuwa, kutokana na ustahimilivu Wake, Mungu anaweza kukubali mielekeo hii hasi ambayo Nimeizungumzia shingo upande? Mungu anaweza kuipongeza mielekeo ya watu hawa? (La.) Ni mahitaji yapi ya Mungu kwa wanadamu na wale ambao wanamfuata? Je, mnajua ni mwelekeo gani anaouhitaji kwa watu? Leo, nimezungumza mengi, nimezungumzia mengi kuhusu mada ya Mungu Mwenyewe, pamoja na matendo ya Mungu na kile Anacho na alicho. Sasa unajua ni kitu gani Mungu anatamani kupata kutoka kwa watu? Unajua ni kitu gani Mungu anataka kutoka kwako? Zungumzeni. Kama bado ufahamu wako kutokana na mazoea na matendo yako unakosa au ni wa juujuu sana, unaweza kusema kitu kuhusu ufahamu wako juu ya maneno haya. Una ufahamu kwa muhtasari? Ni kitu gani Mungu anahitaji kwa wanadamu? (Wakati wa huu ushirika mbalimbali, Mungu ametoa mkazo wa kututaka tumjue Mungu, tujue matendo Yake, tujue kuwa ni Yeye chanzo cha uhai kwa vitu vyote, tujue hadhi na utambulisho Wake.) Na ni nini matokeo ya mwisho Mungu anapohitaji watu wamjue? (Wajue kwamba Mungu ndiye Muumbaji, na kuwa watu ni viumbe walioumbwa.) Wanapopata ufahamu kama huu, ni mabadiliko yapi yanakuwepo katika mitazamo yao kwa Mungu, katika utekelezaji wao wa wajibu, au katika tabia zao? Umewahi kuwaza kuhusu hili? Inaweza kusemwa kuwa, baada ya kumjua Mungu na kumfahamu, wanakuwa watu wazuri? (Imani katika Mungu sio kwa ajili ya kuwa mtu mzuri. Bali, ni kutafuta kuwa kiumbe wa Mungu ambaye anafikia kiwango kilichotengwa, na kuwa mtu mwaminifu.) Kuna kitu kingine chochote? (Baada ya kumjua Mungu kweli na kwa usahihi, tunaweza kumtendea Mungu kama Mungu, tunajua kuwa Mungu daima ni Mungu, kuwa sisi ni viumbe walioumbwa, tunapaswa kumwabudu Mungu, na kusimama katika nafasi sahihi.) Vizuri sana! Hebu tusikie kutoka kwa wengine. (Tunamjua Mungu, na hatimaye tunaweza kuwa watu ambao wanamtii Mungu kweli, kumheshimu Mungu sana, na kuepuka maovu.) Huo ni ukweli.

c. Mwelekeo Ambao Mungu Anahitaji Mwanadamu Awe Nao Kwake

Kwa kweli, Mungu hana mahitaji sana kwa wanadamu—au angalau, hana mahitaji kama watu wanavyodhani. Ikiwa Mungu hangetamka maneno yoyote, ikiwa hangeonyesha tabia Yake au matendo yoyote, basi kumjua Mungu kungekuwa kugumu sana kwenu, kwa sababu watu wangelazimika kukisia nia ya Mungu na mapenzi Yake, kitu ambacho ni kigumu sana kwao. Lakini katika hatua ya mwisho ya Kazi Yake, Mungu amenena maneno mengi, kufanya kiwango kikubwa cha kazi, na kufanya mahitaji mengi kwa wanadamu. Katika maneno Yake, na kiwango kikubwa cha kazi Yake, amejulisha watu anachokipenda, anachokichukia, na wanafaa kuwa aina gani ya watu. Baada ya kuelewa vitu hivi, ndani ya nyoyo watu wanafaa kuwa na maelezo sahihi ya mahitaji ya Mungu, kwa kuwa hawamwamini Mungu wakiwa katika hali isiyo dhahiri na ya kinadharia, nahawamwabudu tena yule Mungu asiye yakini, au kumfuata Mungu katika ukosefu uyakini na udhahania na utupu; badala yake, watu wanaweza kusikia maneno ya Mungu, wanaweza kuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, na kuvifikia, na Mungu hutumia lugha ya wanadamu kuwaambia watu yale yote wanafaa kujua na kulewa. Leo, kama watu bado hawamjui Mungu na kile Anachohitaji kutoka kwao; ikiwa hawajui kwa nini mtu anapaswa kumwamini Mungu, wala jinsi ya kumwamini ama kumtendea—basi kuna shida na hili. Sasa hivi tu kila mmoja wenu amezungumza kuhusu kipengele kimoja; mnafahamu kuhusu mambo fulani, yawe ni mambo mahususi au ya jumla—lakini Ningependa kuwaambia mahitaji ya Mungu ya kweli, kamili, na mahususi kwa wanadamu. Ni maneno machache tu, na rahisi sana. Yawezekana tayari mnayajua haya maneno. Mahitaji sahihi ya Mungu kwa wanadamu na wale ambao wanamfuata ni kama ifuatavyo. Mungu anahitaji mambo matano kutoka kwa wale wanaomfuata; imani ya kweli, ufuasi wenye uaminifu, utiifu kamili, ufahamu wa kweli na heshima za kutoka moyoni.

Katika mambo haya matano, Mungu anahitaji kuwa watu wasimshuku tena, wala kumfuata wakitumia fikira zao au mitazamo ikosayo uyakini na iliyo dhahania; Ni lazima wamfuate Mungu bila fikira au dhana zozote. Mungu anahitaji kuwa wote wanaomfuata wafanye hivyo kwa uaminifu, sio kwa shingo upande au bila kujizatiti. Mungu anapokupa mahitaji yoyote, au kukujaribu, kukuhukumu, kukushughulikia na kukupogoa, au kukuadhibu na kukuangamiza, unapaswa kuwa mtiifu kabisa Kwake. Hufai kuuliza kilichosababisha, au kuweka masharti, au hata uongee kuhusu sababu. Utiifu wako lazima uwe usio na shaka. Maarifa ya Mungu ni kipengele ambacho watu wengi wanakosea. Mara kwa mara wanamlazimishia Mungu misemo, matamshi, na maneno ambayo hayahusiani na Yeye, wakiamini kuwa haya maneno ndiyo ya kweli kuhusu kumfahamu Mungu. Kumbe hawajui kuwa hii misemo, ambayo inatoka kwa fikira za watu, ung'amuzi wao, na busara zao, havina uhusiano wowote na kiini cha Mungu. Na kwa hiyo, Ninataka kukwambia kuwa, katika ufahamu wa watu unaotamaniwa na Mungu, Mungu haulizi tu kwamba umtambue Mungu na maneno Yake, lakini kuwa ufahamu wako juu ya Mungu ni sahihi. Hata kama unaweza kusema sentensi moja tu, au una ufahamu mdogo tu, huu ufahamu mdogo ni sahihi na wa kweli, na unalingana na kiini cha Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hapendi sifa na wao kumtukuza Yeye kwa hali isiyo halisi na yenye nia mbaya. Zaidi ya hayo, Anachukia watu wanapomchukulia kama hewa. Anachukia ambapo, wakati wa majadiliano juu ya mada kuhusu Mungu, watu wanazungumza kimzaha, wakiongea kwa hiari bila ya kujali, wakiongea wapendavyo; zaidi ya hayo, anawachukia wale wanaojifanya wanamjua Mungu, na wanaringa kuhusu ufahamu wa Mungu, wakijadili mada kuhusu Mungu bila mipaka au kipimo. La mwisho Kati ya yale mahitaji matano lilikuwa ni kumheshimu Mungu kutoka moyoni. Hili ndilo hitaji kuu la Mungu kwa wale wote wanaomfuata. Wakati mtu ana ufahamu wa kweli na sahihi kumhusu Mungu, anaweza kumheshimu Mungu na kuepuka maovu. Heshima hii hutoka ndani ya moyo wake, ni ya hiari, na sio kwa sababu Mungu amemshurutisha. Mungu hataki utoe zawadi ya mwelekeo wowote wa kupendeza, au tabia, au mienendo ya nje Kwake; badala yake, anataka kwamba umheshimu na umwogope kutoka ndani ya moyo wako. Heshima hii inaafikiwa kutokana na mabadiliko katika tabia ya maisha yako, kwa sababu una ufahamu juu ya Mungu, kwa sababu unaelewa matendo ya Mungu, kwa sababu ya uelewa wako wa kiini cha Mungu, na kwa sababu umetambua ukweli kuwa wewe ni mmoja wa viumbe wa Mungu. Na kwa hiyo, nia yangu ya kutumia neno “kutoka moyoni” kwa kurejelea heshima hapa ni kwamba wanadamu waelewe kuwa heshima ya watu kwa Mungu inapaswa kutoka ndani ya mioyo yao.

Sasa yafikirie hayo matakwa matano: kuna yeyote kati yenu anaweza kupata matatu ya kwanza? Ambapo Ninamaanisha uaminifu wa kweli, ufuasi wenye uaminifu, na utiifu kamili. Kuna wowote kati yenu wanaoweza mambo haya? Najua Nikisema yote matano, basi bila kuuliza hapatakuwa na hata mmoja kati yenu anayeweza—lakini nimeyapunguza hadi matatu. Tafakari kama umeyapata au la. Je, “uaminifu wa kweli” ni rahisi kuupata? (La, sio rahisi.) Sio rahisi, kwa kuwa mara nyingi watu humtilia Mungu mashaka. Na, je, “ufuasi wenye uaminifu”? Huu “uaminifu” una maana gani? (Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote.) Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote. Mmegonga ndipo! Kwa hiyo, je, mna uwezo wa kupata hili hitaji? Inabidi mjitahidi zaidi—siyo? Kwa sasa bado hamjapata hili hitaji. Kuhusu “utiifu kamili”—je, mmepata hilo? (Hapana.) Bado hamjapata hilo, pia. Mara nyingi nyinyi si watiifu na ni waasi, mara nyingi hamsikilizi, au kupenda kutii, au kutaka kusikia. Haya ndiyo mahitaji matatu ya msingi wanayopata watu baada ya kuingia katika maisha yao, na bado hamjayapata. Kwa hiyo, kwa wakati huu, mna uwezo mkubwa? Leo, baada ya kunisikia nikisema maneno haya, mna wasiwasi? (Ndiyo.) Ni sawa kuwa mna wasiwasi. Msiwe na wasiwasi Ninahisi wasiwasi kwa niaba yenu. Sitakwenda katika mahitaji hayo mengine mawili; bila shaka, hakuna anayeweza kuyafikia. Mna shauku. Kwa hivyo mmebaini malengo yenu? Malengo yapi, kuelekeza upande gani, mnapaswa kuyafuata, na kujitolea jitihada zenu? Mna lengo? Hebu niongee waziwazi: mnapofikia mahitaji haya matano, mtakuwa mmemridhisha Mungu. Kila mojawapo ni ishara, ishara ya watu wakiingia katika maisha wakiwa wamefikia ukomavu, na lengo la mwisho la hii. Hata kama Ningechukua moja kati ya mahitaji na kuongea kwa kina kulihusu na kinachohitajika, haiwezi kuwa rahisi kupata; ni lazima mpitie kiwango fulani cha matatizo na kufanya kiasi fulani cha juhudi. Na ni aina gani ya mawazo mnapaswa kuwa nayo? Yanapaswa kuwa sawa na yale ya mgonjwa wa saratani anayesubiri kwenda kwenye meza ya upasuaji. Na ni kwa nini Ninasema haya? Kama ungependa kumwamini Mungu, na kumpata Mungu na kupata ridhaa Yake, basi kama hutapitia katika kiasi fulani cha shida, au kufanya kiwango fulani cha juhudi, hutaweza kupata vitu hivi. Umesikia mahubiri mengi, lakini kuyasikia hakumaanishi kuwa haya mahubiri ni yako; ni lazima uyachukue na kuyageuza yawe kitu ambacho ni chako, ni lazima uyasimilishe maishani mwako, na kuyaleta katika uwepo wako, ukiyaruhusu maneno na mahubiri haya yakuongoze katika maisha yako, na kuleta dhamana na maana ya uhai katika maisha yako—na hivyo basi itakuwa ni thamani kuwa uliyasikia maneno haya. Kama maneno haya Ninayoyanena hayaleti mabadiliko yoyote katika maisha yenu, au thamani yoyote katika uwepo wako, basi hakuna haja ya kuyasikiliza. Mnaelewa haya, ndiyo? Baada ya kuelewa haya, basi kilichobaki ni juu yenu wenyewe. Ni lazima mfanye kazi! Ni lazima muwe na bidii katika kila jambo! Msiwe huku na kule—wakati unapita upesi! Wengi wenu wamemwamini Mungu kwa zaidi ya miaka kumi. Fikiria nyuma kwa hii miaka kumi: Umenufaika kiasi gani? Na mmesalia na miongo mingapi ya haya maisha? Sio mirefu. Sahau kuhusu iwapo kazi ya Mungu inakusubiri, iwapo Amekuachia nafasi, iwapo Atafanya kazi ile ile tena; usizungumze kuhusu hili. Unaweza kurudisha nyuma miaka yako kumi iliyopita? Kwa kila siku inayopita, na kila hatua unayochukua, siku ambazo unazo hupunguzwa kwa siku moja. Muda haumsubiri mwanadamu yeyote! Utanufaika tu kutokana na imani kwa Mungu kama utaichukulia kama kitu kikubwa zaidi maishani mwako, muhimu zaidi kuliko chakula, mavazi, au kitu kingine chochote! Kama huwa unaamini tu unapokuwa na wakati, na huwezi kutoa umakini wako wote kwa imani yako, kama siku zote umetatizwa na vurugu, basi hutafaidi chochote. Unaelewa hili, ndio? Tutaishia hapa kwa leo. Tuonane wakati ujao!

Februari 15, 2014

Iliyotangulia: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp