282 Matamko Rasmi Juu ya Imani Katika Mungu
1
Sehemu ya msingi zaidi ya imani katika Mungu
ni kusoma maneno ya Mungu kila siku.
Na mazoezi yanayotakiwa ya kila siku
ni maombi kwa Mungu na kujitafakari.
Lengo kuu la imani ni kutenda ukweli
na kuwa na kanuni kwa matendo yako.
Dhamiri unayopaswa kuwa nayo katika imani katika Mungu
ni kuwa mwaminifu katika wajibu kukamilisha agizo la Mungu.
Unapokuwa na upendo kwa Mungu,
hiyo ndiyo imani ya kweli katika Mungu.
Kumpenda Mungu hukufanya uwe mwaminifu na mheshimiwa.
Ukiendelea kumpenda Mungu na kumwishia Mungu maisha yako,
hutawahi kujua hisia ya majuto.
Ni wale tu wanaompenda Mungu kwa dhati
ndio wawezao kumshuhudia na kumwinua.
Ni kweli: Hakuna kilicho na maana zaidi
na hakuna kilichobarikiwa Zaidi
kuliko kumpenda Mungu, kuliko kumpenda Mungu.
2
Njia ya kupata wokovu
ni kutii kazi ya Mungu, kufuatilia ukweli.
Kukubali kushughulikiwa naye na hukumu Yake
ndilo somo la msingi la imani katika Mungu.
Ukweli muhimu Zaidi
ni kuingia katika ukweli na kuwa mwaminifu.
Fanya utii kwa ukweli kuwa misheni yako ya maisha,
hiyo ndiyo kanuni ya juu kabisa ya kutenda ya imani katika Mungu.
Unapokuwa na upendo kwa Mungu,
hiyo ndiyo imani ya kweli katika Mungu.
Kumpenda Mungu kunakufanya uwe mwaminifu na mheshimiwa.
Ukiendelea kumpenda Mungu na kumwishia Mungu maisha yako,
hutawahi kujua hisia ya majuto.
Ni wale tu wanaompenda Mungu kwa dhati
ndio wawezao kumshuhudia na kumwinua.
Ni kweli: Hakuna kilicho na maana zaidi
na hakuna kilichobarikiwa Zaidi
kuliko kumpenda Mungu, kuliko kumpenda Mungu.
3
Kushindwa kukubwa katika imani kwa Mungu
ni kuwafuata au kuwaabudu watu.
Unapomwamini Mungu, kumbuka,
lazima usimsaliti au kumpinga.
Lazima umche na uepuke maovu,
hiyo ndiyo njia ya maisha ya imani katika Mungu.
Kusudi la msingi la imani katika Mungu
ni kujifunza kumjua Mungu na kumshuhudia.
Unapokuwa na upendo kwa Mungu,
hiyo ndiyo imani ya kweli katika Mungu.
Kumpenda Mungu kunakufanya uwe mwaminifu na mheshimiwa.
Ukiendelea kumpenda Mungu na kumwishia Mungu maisha yako,
hutawahi kujua hisia ya majuto.
Ni wale tu wanaompenda Mungu kwa dhati
ndio wawezao kumshuhudia na kumwinua.
Ni kweli: Hakuna kilicho na maana zaidi
na hakuna kilichobarikiwa zaidi
kuliko kumpenda Mungu, kuliko kumpenda Mungu.