954 Una Uwezekano wa Kumwasi Mungu Unapokuwa na Madai Kwake

1 Hakuna kilicho kigumu kushughulikia kuliko madai ya watu kwa Mungu. Ikiwa hakuna chochote afanyacho Mungu kinacholingana na mawazo yako, na ikiwa Hatendi kulingana na mawazo yako, basi wewe unaweza kupinga—ambayo inaonyesha kwamba, kwa asili, mwanadamu hupingana na Mungu. Lazima utumie ufuatiliaji wa ukweli kujua na kutatua tatizo hili. Wale wasio na ukweli hufanya madai mengi kwa Mungu, ilhali wale wanaoelewa ukweli kweli hawana madai; wanahisi tu kuwa hawajamridhisha Mungu vya kutosha, na kwamba si watiifu vya kutosha.

2 Kwamba watu daima hufanya madai kwa Mungu wanapomwamini huonyesha asili yao potovu. Usipolichukulia hili kama tatizo kubwa, usipolichukua kama jambo muhimu, basi kutakuwa na maangamizo na hatari zilizofichika katika njia yako. Unaweza kuvishinda vitu vingi, lakini majaliwa, matarajio, na hatima vinapohusika, huwezi kushinda. Wakati huo, ikiwa huna ukweli, unaweza kurudi kwenye njia zako za zamani, na hivyo utakuwa mmoja wa wale watakaongamizwa.

3 Watu wengi daima wamefuata hivi; wametenda vyema wakati ambao wamefuata, lakini hili haliamui kitakachotokea katika siku zijazo: Hii ni kwa sababu hujawahi kujua udhaifu wako, au vitu vinavyofunuliwa kutoka katika asili yako na vinavyoweza kumpinga Mungu, na kabla vikuletee msiba, unabaki bila kujua, na kwa uwezekano wowote, safari yako imalizikapo na kazi ya Mungu imekamilika, utafanya kile kimpingacho Mungu zaidi na ndiyo kufuru isikitishayo zaidi dhidi Yake.

Umetoholewa kutoka kwa “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 953 Vigezo vya Utiifu wa Mwanadamu kwa Mungu

Inayofuata: 955 Kanuni za Msingi za Kutatua Asili ya Mtu

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki