Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

59 Ulimwengu Unatoa Sauti ya Sifa kwa Mungu

1

Ulimwengu ni bahari ya sifa, iliyojaa nyimbo na dansi.

Tunacheza, nyota zinaruka, mwezi watabasamu; sifa zinaujaza ulimwengu.

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, Amekuja duniani,

Akinena ukweli, akitikisa mataifa na dini zote.

Wateule wanaisikia sauti ya Mungu, wanageuka na kumwabudu.

Huko Sayuni Mungu amegeuka kuutazama ulimwengu,

Akifichua haki Yake, utakatifu Wake.

Watu wa Mungu wamejaa furaha, wakimsifu milele.

Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni Mungu)!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni na msifuni)!

2

Kumpenda Mungu, kutekeleza wajibu wetu, kujali mapenzi Yake.

Mioyo ya ndugu zetu wote imeungana kwa karibu.

Wanaume na wanawake wote, wazee na vijana, msifuni Mungu kwa pamoja.

Imbeni, mimi nitacheza; mshuhudieni Mungu, mimi nitajiunga nanyi.

Tunaliaibisha pepo joka kuu jekundu, kuliheshimu jina la Mungu wa kweli.

Tumeiona tabia ya haki ya Mungu kupitia kazi Yake!

Watu wa Mungu wanauona uso Wake mtukufu, wanatafuta kumpenda, kumridhisha.

wakiwa tayari kuwa waaminifu Kwake milele.

Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni Mungu)!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni na msifuni)!

3

Mungu anapata utukufu duniani, watu wote wana furaha.

Maisha katika ufalme ni ya kupendeza sana.

Kuna mbingu mpya, dunia mpya, ufalme mpya.

Tunacheza na kumwimbia Mungu, na tuna furaha sana.

Nyimbo nzuri zaidi tunazojua zinaimbiwa Mungu,

dansi nzuri zaidi, huchezwa kwa ajili Yake.

Tunampa Mungu mioyo yetu ya kweli; upendo wetu ni safi, mwaminifu.

Watu wa Mungu, viumbe wote, humsifu milele,

Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni Mungu)!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni na msifuni)!

Ee Sayuni, utukufu ulioje! Makao ya Mungu yanang’aa sana.

Nuru yake tukufu yaiangaza ulimwengu wote.

Mwenyezi Mungu sasa anatabasamu akiketi kwenye kiti Chake

na kuangalia kufanywa upya kwa ulimwengu.

(Wajua unapaswa kusifu.)

Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni Mungu)!

(Fanya hima na umsifu.)

Msifuni Mungu (Haleluya! Msifuni Mungu!

Msifuni na msifuni, msifuni na msifuni)!

Msifuni Mungu, Msifuni Mungu! Haleluya!

Msifuni Mungu (msifuni na msifuni, msifuni Mungu)!

Msifuni Mungu! Haleluya! Haleluya!

Iliyotangulia:Msifuni Mungu kwa Kupata Utukufu

Inayofuata:Mwimbie Mungu Nyimbo za Sifa Milele

Maudhui Yanayohusiana