982 Matokeo ya Makosa ya Mwanadamu

Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa makini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kuhusu hatima yako.

1 Kadri dhambi zako zilivyo nyingi, ndivyo nafasi zako za kupata hatima iliyo nzuri zilivyo chache. Kinyume chake, kadri dhambi zako zilivyo chache, ndivyo nafasi zako za kusifiwa na Mungu zilivyo nyingi. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi kiwango ambapo haiwezekani Mimi kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa jasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile kitakachokupata.

2 Kama wewe ni mtu mwenye ari anayetenda ukweli basi kwa hakika una fursa ya kusamehewa dhambi zako, na kiwango cha kutotii kwako kitakuwa kidogo zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu asiye radhi kutenda ukweli basi hakika dhambi zako mbele ya Mungu zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitakua zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeangamia kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kufurahisha ya kupokea baraka itaharibiwa.

3 Usizichukulie dhambi zako kama makosa ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu ubora wako wa tabia ulio duni ulifanya isiwezekane kuutenda, na hata zaidi, usizichukulie tu dhambi ulizofanya kama matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri zaidi. Kama unajua vizuri kujisamehe na unajua vizuri kujitendea kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hataupata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukusumbua, lakini zitakuzuia kuwahi kutosheleza madai ya ukweli na kukufanya milele kuwa mwenzi mwaminifu wa Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 981 Mungu Atumai Watu Wote Wapate Njia Ng’avu

Inayofuata: 983 Kila Siku Uishiyo Sasa ni Muhimu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp