1006 Masharti Manne ya Mungu Kumkamilisha Mwanadamu

1 Kuna masharti manne ya msingi ya watu kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu ufikiaji wa kufanywa mkamilifu: kutekeleza wajibu wako kwa kiwango kinachokubalika, kuwa na tabia ya utiifu, kimsingi kuwa mwaminifu, na kuwa na moyo unaotubu. Wakati masharti haya manne yanatimizwa, Mungu huanza kazi ya hukumu na kuadibu ndani ya watu. Kabla ya kutekeleza kazi ya hukumu na kuadibu ndani ya watu, Mungu atawapima na—na, je, Yeye huwapimaje? Mungu ana viwango kadhaa. Kwanza, Anaangalia mtazamo wa watu juu ya agizo ambalo Amewapa ni upi, ikiwa wana uwezo wa uaminifu, na ikiwa wanaweza kutoa moyo na nguvu zao zote. Kwa jumla, Anaangalia ikiwa una uwezo wa kutekeleza wajibu wako kwa kiwango kinachokubalika.

2 Pili, lazima uwe na mtazamo wa utiifu kwa Mungu. Kabla ufanikishe utiifu kamili, lazima uwe na mtazamo wa utiifu. Katika mtazamo wako kwa maagizo ambayo Mungu Anakupa, lazima—pamoja na kuyachukua kwa dhamiri na busara—pia uweze kutafuta ukweli, uelewe mapenzi ya Mungu, na lazima uweze kuwa na uwezo wa kuwa na tabia ya utiifu bila kujali aina ya mazingira uliyo ndani yake, bila kujali matukio yanayokupata. Yaani, unakubali kuwa maneno ya Mungu ni ya kweli, unayachukua maneno ya Mungu kama ukweli, unayachukua maneno ya Mungu kama kanuni ya utendaji wako, na hata ikiwa una ufahamu duni kuhusu kanuni hiyo, unaweza kuishika kana kwamba unayeshikilia mafundisho. Hii ni aina ya mtazamo.

3 Mara unapokuwa na mtazamo wa utiifu, mabadiliko zaidi katika maneno, mwenendo na tabia yako yatafuata hivi karibuni. Na mabadiliko haya yatakuwa yapi? Mungu atakuona kuwa mwaminifu kimsingi. Maneno na mienendo yako michache itahusisha uwongo wa kimakusudi; 80% ya unachosema kitakuwa kweli. Wakati mwingine, kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa sababu ya mazingira uliyomo, au sababu zingine, utasema uongo bila kutaka, na utahisi vibaya ndani, kisha utatubu na kukiri mbele za Mungu, na wakati mambo kama haya yanapokutendekea tena, hayatakuwa mabaya, hali yako itakuwa bora zaidi na zaidi, na Mungu atakuona kama mwaminifu kimsingi.

4 Mungu anahitaji watu wawe na moyo wa toba. Katika kila hatua—iwe ni wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukurudi, au Anapokukumbusha na kukusihi—ikiwa, wakati mgogoro utatokea kati yako na Mungu, unaendelea kushika maoni na fikira zako mwenyewe, na hakuna urekebishaji wa kuelewa kwako vibaya kwako, lawama, na kutomtii Mungu—usipojigeuza—basi Mungu atakukumbuka. Unapojigeuza, na kuweka kando maoni na nia zako, unapokuwa na moyo kama huu, basi huu pia kwa kawaida utakuwa mtazamo wa utiifu. Kwamba unaweza kujigeuza kunathibitisha kutambua kwako utambulisho wa Muumba, utambuzi wako wa kiini Chake. Mungu analiona hili kuwa muhimu hasa.

5 Wakati huishi kulingana na hisia zako mwenyewe, wakati huishi kulingana na falsafa zako za maisha, lakini uishi kulingana na maneno yaliyonemwa na Mungu, kulingana na kanuni ulizopewa na Mungu, kulingana na wajibu ulilopewa na Mungu, na njia ya vitendo, njia unayopaswa kuitembea, uliyoambiwa na Mungu, bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea au ikiwa Mungu anakusikiliza, ukifanya kile unachopaswa kufanya, basi Mungu atakutambua. Mara unapotimiza mambo haya—mara unapokuwa na utambuzi wako wa utambulisho wa Muumba, mtazamo wako wa uwajibikaji kuelekea wajibu wako mwenyewe, na mtazamo wa kuweza kujigeuza katika jinsi unavyouchukulia ukweli—Mungu atatekeleza kazi ya hukumu na kuadibu ndani yako, na ni kuanzia hapa ndipo wokovu wako unaanzia.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Wakati tu Unapotatua Dhana Zako Ndipo Unaweza Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Imani Katika Mungu III” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 1005 Mahitaji ya Mwisho ya Mungu kwa Mwanadamu

Inayofuata: 1007 Mpangilio wa Mungu wa Hatima ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp