Hatima na Matokeo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 580)

Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oo, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu? Wanawezaje, katika mwanga, kukosa kuendeleza kazi zao? Dunia si kimya na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena. Mbingu na nchi, bila kutenganishwa na utupu tena, zimeungana kama kitu kimoja, kamwe kutotenganishwa tena. Wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo, haki Yangu na utakatifu Wangu umeenea kila mahali katika ulimwengu, na binadamu wote wanavisifu bila kikomo. Miji yote ya mbingu inacheka kwa furaha, na falme zote za nchi zinacheza kwa shangwe. Ni nani wakati huu ambaye haonyeshi furaha? Na ni nani wakati huu ambaye halii? Nchi katika hali yake ya asili ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wake, kwa ajili yake kufanywa upya, mbingu haijafichwa tena kutoka kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu. Nyuso za binadamu zimezingirwa na tabasamu za shukurani, na nyoyo zao zinadondokwa na utamu usiokuwa na kifani. Mwanadamu hagombani na mwanadamu, wala binadamu kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kunao wale ambao, katika mwanga Wangu, hawaishi kwa furaha na wenzao? Kunao wale ambao, katika siku Yangu, hufedhehesha jina Langu? Binadamu wote huelekeza macho yao ya heshima Kwangu, na wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao. Nimechunguza kila kitendo cha binadamu: Miongoni mwa wanadamu waliotakaswa, hakuna yeyote aliye mkaidi Kwangu, hakuna anayenielekezea hukumu. Binadamu wote umejawa na tabia Yangu. Kila mtu anakuja kunijua, ananijongelea, na ananiabudu. Msimamo wangu ni mmoja katika roho ya mwanadamu, Nimetukuzwa kwa kiwango cha juu zaidi kwa macho ya mwanadamu, na hububujika katika damu ya mishipa yake. Nderemo za furaha katika nyoyo za wanadamu huenea kila sehemu ya uso wa nchi, hewa ni ya kuchangamsha na bichi, ukungu mzito hauitandai ardhi tena, na mwangaza wa jua huvutia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 18

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 581)

Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; binadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtasimama imara na thabiti katika nchi ya Sinimu. Kupitia katika mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 19

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 582)

Kwa kuwa maneno Yangu yametimilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu. Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida. Leo hii, nyote mko hai mbele Yangu; kesho nyote mtakua hai ndani ya ufalme Wangu. Je, si hii ndiyo baraka kubwa zaidi ambayo Nimempa mwanadamu? Kwa sababu ya gharama ambayo mnalipa leo, mtarithi baraka za wakati ujao na mtaishi ndani ya utukufu Wangu. Je, si bado mnataka kujihusisha na kiini cha Roho Wangu? Je, bado mnataka kujiua wenyewe? Watu wako tayari kufuata ahadi ambazo wanaweza kuziona, hata kama ni za muda mfupi, lakini hakuna aliye tayari kukubali ahadi za kesho, hata kama ni za milele. Vitu vinavyoonekana kwa mwanadamu ni vitu ambavyo Nitaangamiza, na vitu visivyoweza kushikika na mwanadamu ndivyo Nitakavyotimiza. Hii ndiyo tofauti ya Mungu na mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 20

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 583)

Katika nuru Yangu, watu wanaiona nuru tena. Katika neno Langu, watu wanapata mambo ambayo wanafurahia. Nimekuja kutoka Mashariki, Ninatoka Mashariki. Utukufu Wangu unapoangaza, mataifa yote yanatiwa nuru, vitu vyote vinaletwa kwenye mwanga, hakuna kitu hata kimoja kinachobaki gizani. Katika ufalme, maisha ambayo watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu ni yenye furaha kupita kiasi. Maji yanacheza kwa furaha katika maisha ya watu yenye baraka, milima inafurahia pamoja na watu katika wingi Wangu. Wanadamu wote wanajitahidi, wakifanya bidii, wakionyesha uaminifu wao katika ufalme Wangu. Katika ufalme, uasi haupo tena, upinzani haupo tena; mbingu na dunia zinategemeana, Mimi na mwanadamu tunakaribiana katika hisia ya kina, katika furaha kuu tamu ya maisha, tukiegemeana…. Wakati huu, Ninayaanza rasmi maisha Yangu mbinguni. Usumbufu wa Shetani haupo tena, na watu wanaingia katika pumziko. Ulimwenguni kote, watu Wangu wateule wanaishi ndani ya utukufu Wangu, wakiwa wamebarikiwa sana, si kama watu wanaoishi kati ya watu, lakini kama watu wanaoishi na Mungu. Binadamu wote wamepitia upotovu wa Shetani, na kuishi maisha ya mateso makubwa. Sasa, mtu anawezaje kutofurahia akiishi katika nuru Yangu? Mtu anawezaje kuuachilia wakati huu mzuri umponyoke? Enyi watu! Imbeni wimbo ulio mioyoni mwenu na mnichezee kwa furaha! Iinueni na mnitolee mioyo yenu ya dhati! Pigeni ngoma zenu na mnichezee kwa furaha! Ninaangaza furaha Yangu ulimwenguni kote! Naufichua uso Wangu mtukufu kwa watu! Nitaita kwa sauti kubwa! Nitaupita ulimwengu wote! Tayari Ninatawala kati ya watu! Ninatukuzwa na watu! Ninapeperuka kwenye mbingu zenye rangi ya samawati na watu wanakwenda wakitembea pamoja nami. Ninatembea kati ya watu na watu Wangu wananizunguka! Mioyo ya watu ni yenye furaha, nyimbo zao zinautikisa ulimwengu, zikiipasua mbingu! Ulimwengu haujafunikwa kwa ukungu tena; hakuna matope tena, hakuna mkusanyiko wa maji machafu tena. Watu watakatifu wa ulimwengu! Mnaonyesha nyuso zenu za kweli chini ya ukaguzi Wangu. Ninyi sio watu mliofunikwa na uchafu, lakini ni watakatifu walio safi kama jiwe la thamani lenye rangi ya kijani kibichi, ninyi nyote ni wapendwa Wangu, ninyi nyote ni furaha Yangu! Vitu vyote vinafufuka! Watakatifu wote wamerejea ili kunitumikia mbinguni, wakiingia katika kumbatio Langu lililo changamfu, hawalii tena, hawana wasiwasi tena, wakijitoa Kwangu, wakirudi nyumbani Kwangu, nao watanipenda bila kukoma katika nchi yao! Wasibadilike kamwe milele! Huzuni iko wapi! Machozi yako wapi! Mwili uko wapi! Dunia inapita, lakini mbingu ni za milele. Ninawaonekania watu wote, na watu wote wananisifu. Maisha haya, uzuri huu, tangu zama za kale hadi mwisho wa dahari, havitabadilika. Haya ndiyo maisha ya ufalme.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Furahini, Enyi Watu Wote!

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 584)

Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimenena baadhi ya matamshi pia. Hata hivyo Sina budi kuhisi kwamba maneno Yangu na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ili kufafanua tabia Yangu ya asili. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—watu hawajapata ufahamu wowote kunihusu kutokana na tabia Yangu. Kwa hivyo, Ninaanza mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, na kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale wanaoniona watajipiga kifuani na kulilia na kuombolezea bila kukoma kwa sababu ya uwepo Wangu. Hii ni kwa sababu Ninaleta mwisho wa wanadamu duniani, na kuanzia sasa na kuendelea, Ninaweka wazi tabia Yangu yote mbele ya wanadamu, ili wote wanijuao na wale wote wasionijua waweze kuyafurahisha macho yao na kuona kwamba kweli, Nimekuja katika ulimwengu wa kibinadamu, Nimekuja duniani ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, na “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Niwaumbe wanadamu. Nawaomba mzingatie kwa makini kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinawakaribia wanadamu tena, kwa wale wote wanaonipinga.

Pamoja na mbingu, Ninaanza kazi ambayo ni lazima Niifanye. Na kwa hiyo Ninapenya kati ya misururu ya watu na kupita kati ya mbingu na ardhi, bila ya yeyote kutambua miendo Yangu au kuyatambua maneno Yangu. Kwa hivyo, mpango Wangu unaendelea kusonga mbele kwa urahisi. Ni kwamba hisia zenu zote zimekufa ganzi kiasi kwamba hamtambui hatua za kazi Yangu. Lakini kwa kweli siku moja itakuja ambapo mtatambua nia Zangu. Leo, Ninaishi pamoja nanyi, na Ninasumbuka pamoja nanyi, na kwa muda mrefu Nimekuja kuelewa mtazamo walio nao wanadamu kunielekea. Nisingependa kuzungumza zaidi kuhusu jambo hili, sembuse kutoa mifano zaidi ya suala hili linaloumiza. Natumai tu kwamba mtayakumbuka yale yote ambayo mmeyafanya, ili tuweze kulinganisha maelezo yetu siku tutakapokutana tena. Nisingependa kumshutumu yeyote miongoni mwenu kwa njia isiyo ya kweli, kwa sababu daima Nimekuwa Nikitenda kwa njia ya haki, bila upendeleo, na kwa heshima. Bila shaka, Natumai pia kwamba nyinyi mnaweza kuwa wazi waadilifu, na kutofanya lolote lililo kinyume na mbingu na ardhi na dhamiri yenu. Hili ndilo jambo la pekee Ninalowaomba mfanye. Watu wengi huhisi kusumbuka na kuona haya kwa sababu wametenda makosa mabaya, na wengi wanajionea aibu kwa sababu hawajawahi kutenda tendo lolote zuri. Tena wapo pia wengi ambao, mbali na kutahayari kwa ajili ya dhambi zao, wanakuwa wabaya zaidi, wakiitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—ambayo haikuwa bado imewekwa wazi kikamilifu—ili kujaribu tabia Yangu. Sijali, wala sitilii maanani yoyote matendo ya mtu yeyote. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, iwe kukusanya habari, kuzunguka katika nchi au kufanya jambo ambalo linanipendeza. Katika nyakati muhimu, Mimi huendelea na kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama ilivyopangwa awali, bila kuchelewa au kuwa mapema hata kidogo, na kwa urahisi na kwa makini. Hata hivyo, katika kila hatua ya kazi Yanu, watu wengine wanawekwa pembeni, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali yao ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaonichukiza sana hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ningependa wale wote Ninaowadharau wawe mbali sana Nami. Ni dhahiri kwamba, Sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika nyumba Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, Sina haraka ya kuzitupa nje zile nafsi zote zinazostahili dharau kutoka katika nyumba Yangu, kwa kuwa Nina mpango Wangu mwenyewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 585)

Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, bali si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya lingine, njia ambayo kwayo wameitumia kunifuata, sifa zao asilia, na hatimaye jinsi ambavyo wamejistahi. Kwa njia hii, haijalishi ni mtu wa aina gani, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu, na wote watakuwa pamoja na wa aina yake kama Nilivyopanga. Ninaamua hatima ya kila mtu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anataka huruma, bali kulingana na ikiwa anao ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili. Sharti mtambue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa pia. Huu ni ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu. Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu uanzishwe. Ni kwamba tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wanaonekana kupungua kwa idadi, sawa na wale Ninaowakubali kwa kweli. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambavyo hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba kuna uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitupa nje. Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto, hadi pale Nitakapohisi kuchukizwa na karaha, na hatimaye kutoa adhabu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu yenu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona tena. Kwa kuwa maisha miongoni mwenu yameshakuwa ya kuchosha na ya taabuKwangu, basi, ni wazi kwamba Nimechagua mazingira tofauti ya kuishi, afadhali kuepuka kuumizwa na maneno yenu maovu na kuwa mbali na tabia zenu mbovu kwa namna isiyovumilika, ili msinipumbaze au kunitendea kwa namna ya uzembe tena. Kabla Sijawaacha, lazima bado Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na ukweli. Badala yake, mnafaa kufanya kile ambacho kinawapendeza wote, kile kilicho na manufaa kwa wote, na kile kinachofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule anayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 586)

Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia matendo yake maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha watu ambao wanafikiria kama Mimi. Wale ambao hawana fikira sawa na Zangu, wakati ule ule, Siwasahau kamwe; Ninawachukia kabisa moyoni Mwangu daima, Nikisubiri nafasi ya kutoa adhabu kwao, jambo ambalo Nitafurahia kuona. Sasa siku Yangu imefika hatimaye, na Sihitaji kusubiri zaidi!

Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 587)

Katika upana mkubwa wa dunia hii, mabadiliko yasiyohesabika yamefanyika, bahari kujaa hadi kuziba mashamba, mashamba kufurika hadi baharini, tena na tena. Isipokuwa Yule ambaye anatawala kila kitu katika ulimwengu, Hakuna anayeweza kuongoza na kuelekeza jamii hii ya wanadamu. Hakuna yeyote hodari kufanya kazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya jamii hii ya binadamu, sembuse yule anayeweza kuiongoza jamii hii ya wanadamu hadi hatima ya mwanga na kuikomboa kutokana na udhalimu wa duniani. Mungu hulalamikia wakati ujao wa wanadamu, huhuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu na anaumizwa kwamba binadamu wanatembea, hatua baada ya nyingine hadi kuoza na katika njia ambayo hawawezi kurudi. Wanadamu ambao wameuvunja moyo wa Mungu na wakamkana kumfuata yule mwovu: je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaza kuhusu mwelekeo ambao wanadamu wa aina hii huenda wanafuata? Ni kwa sababu hii haswa kwamba hakuna anayehisi hasira ya Mungu, hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu au kujaribu kuja karibu na Mungu na isitoshe, hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu. Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu, binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mwenyewe, anazidi kwenda mbali na Mungu, kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli Wake, akiona heri kujiuza kwa Shetani, adui wa Mungu. Na ni nani amefikiri—iwapo mwanadamu ataendelea kuwa mkaidi—jinsi Mungu atakavyowatendea wanadamu hawa ambao wamempuuza bila kusita? Hakuna anayejua kwamba maana ya ukumbusho wa mara kwa mara na kusihi kwa Mungu ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake maafa yasiyokuwa ya kawaida ambayo ameandaa, maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili. Maafa haya siyo tu adhabu ya mwili bali pia ya roho. Unafaa kujua hili: Mpango wa Mungu utakaposhindikana na wakati makumbusho Yake na kusihi Kwake hakutapata majibu yoyote, atatoa hasira ya aina gani? Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali au hata kusikika na viumbe vyovyote. Na hivyo Nasema, majanga haya hayana mengine ya kulinganishwa nalo awali na kamwe hayatawahi kurudiwa. Hii ni kwa sababu ni mpango wa Mungu kuumba wanadamu mara hii moja tu na kuwaokoa wanadamu mara hii moja tu. Hii ndiyo mara ya kwanza na pia ni ya mwisho. Kwa hivyo, hakuna anayeweza kuelewa nia za bidii na hamu ya ari ambazo kwazo Mungu huokoa wanadamu wakati huu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 588)

Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo; mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kusimamia vitu mwenyewe, na huna ustadi juu yako mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinashikiliwa katika mikono Yake. Kama kazi ya Mungu ilimkimu mwanadamu kwa kumpa hatima, hatima ya ajabu, kabla ya wakati, na kama Mungu alitumia hii kumshawishi mwanadamu na kusababisha mwanadamu kumfuata Yeye—kama Yeye alifanya mpango na mwanadamu—basi huu haungekuwa ni ushindi, wala haingekuwa kufanya kazi katika maisha ya binadamu. Kama Mungu angetumia hatima ya mambo kumtawala au kumdhibiti mwanadamu na kupata moyo wake, basi kwa hii Hangekuwa anamkamilisha mwanadamu, wala Hangeweza kumpata mwanadamu, lakini badala yake angekuwa akitumia hatima kumdhibiti. Mwanadamu anajali tu kuhusu hatima ya siku zijazo, hatima, na kama kuna ama hamna kitu kizuri cha kutumainia. Iwapo mwanadamu angepewa matumaini mazuri wakati wa kazi ya ushindi, na kama, kabla ya kushindwa kwa mwanadamu, yeye angepewa hatima ifaayo ya kufuata, basi kushindwa kwa mwanadamu kusingekosa kuwa na athari tu, bali athari za kushindwa zingeshawishika pia. Hivi ni kusema kwamba, kazi ya ushindi inafanikisha mazao yake kwa kuchukua hatima na matarajio ya mwanadamu na kuhukumu na kuadibu uasi wa tabia ya mwanadamu. Haifanikishwi kwa kufanya mpango na mwanadamu, yaani, kwa kumpa mwanadamu baraka na neema, lakini ni kwa kufichua uaminifu wa mwanadamu kwa kumnyang’anya “uhuru” wake na kukomesha matarajio yake. Hiki ni kiini cha kazi ya ushindi. Kama mtu angepewa matumaini mazuri hapo mwanzoni sana, na kazi ya kuadibu na hukumu zingefanywa baadaye, basi mwanadamu angekubali kuadibu huku na hukumu kwa msingi kwamba alikuwa na matarajio, na mwishowe, utiifu na ibada ya Muumba isiyo na masharti ya viumbe vyote vyake haingetimizika; kungekuwepo tu na utiifu wenye upofu na wa ujinga, au pengine mwanadamu angetoa madai yasiyo na msingi kwa Mungu, na ingekuwa ni vigumu kushinda moyo wa mwanadamu. Kwa hivyo, kazi kama hii ya ushindi haingekuwa na uwezo wa kumpata mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Viumbe kama hawa hawangeweza kutekeleza jukumu lao, na wangeweza tu kufikia makubaliano na Mungu; hii haitakuwa ushindi, lakini huruma na baraka. Tatizo kubwa mno kwa mwanadamu ni kuwa yeye hufikiria tu kuhusu hatima yake na matarajio, na kuyaabudu. Mwanadamu humfuata Mungu kwa ajili ya hatima yake na matarajio; yeye hamwabudu Mungu kwa sababu ya upendo wake kwake. Na kwa hivyo, katika ushindi kwa mwanadamu, ubinafsi wa mwanadamu, uroho na vitu ambavyo sana sana huzuia ibada yake kwa Mungu ni sharti vishughulikiwe na hapo viondolewe. Kwa kufanya hivyo, matokeo ya ushindi kwa mwanadamu yatatimizwa. Hivyo, katika ushindi wa kwanza wa mwanadamu ni muhimu kuondoa matarajio makubwa na udhaifu mkubwa kabisa wa mwanadamu, na, kupitia hili, kufichua upendo wa mwanadamu kwa Mungu, na kubadilisha maarifa yake kuhusu maisha ya binadamu, mtazamo wake kwa Mungu, na maana ya kuwepo kwake. Kwa njia hii, upendo wa mwanadamu kwa Mungu unatakaswa, ambapo ni kusema, moyo wa binadamu unashindwa. Lakini katika mtazamo wake wa viumbe vyote, Mungu hashindi kwa sababu ya kushinda; badala yake, Yeye anashinda ili kumpata mtu, kwa sababu ya utukufu wake mwenyewe, na ili kuokoa ufanano wa kwanza wa awali wa mwanadamu. Kama angeshinda kwa ajili ya kushinda, basi umuhimu wa kazi ya ushindi ungepotea. Hiyo ni kusema kuwa ikiwa, baada ya kumshinda mwanadamu, Mungu alikata tamaa kwa ajili ya mwanadamu, na hakuzingatia maisha au kifo chake, basi hii haitakuwa usimamizi wa mwanadamu, wala kumshinda mwanadamu haitakuwa ni kwa ajili ya wokovu wake. Ni upato wa mwanadamu tu kufuatia ushindi wake na ujio wake wa mwisho katika hatima ya ajabu ndiyo yaliyomo katika kiini cha kazi yote ya wokovu, na ni hii tu ndio inayoweza kufikia lengo la wokovu wa mwanadamu. Kwa maneno mengine, ni ufikaji wa mwanadamu katika hatima nzuri na kuingia kwake katika mapumziko tu ndiyo matarajio ambayo yanatakiwa yamilikiwe na viumbe vyote, na kazi ambayo lazima ifanywe na Muumba. Kama mwanadamu ndiye ambaye angefanya kazi hii, basi kazi hii ingekuwa kidogo sana. Ingemchukua mwanadamu hadi kiwango fulani, lakini haingekuwa na uwezo wa kumleta mwanadamu katika hatima ya milele. Mwanadamu hana uwezo wa kuamua hatima ya mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, hana uwezo wa kuhakikisha matarajio na hatima ya baadaye ya binadamu. Kazi inayofanywa na Mungu, hata hivyo, ni tofauti. Tangu Yeye amuumbe mwanadamu, Yeye anamwongoza; kwa sababu Yeye humwokoa mwanadamu, atamwokoa mwanadamu kwelikweli, na atampata kikamilifu; kwa kuwa Yeye humwongoza mwanadamu, atamleta kwenye hatima inayofaa; na kwa kuwa Yeye alimuumba mwanadamu na humsimamia mwanadamu, ni sharti Achukue jukumu la hatima ya mwanadamu na matarajio yake. Ni hii ndio kazi ambayo hufanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inatimizwa kwa kutakasa matarajio ya mwanadamu, hatimaye ni lazima mwanadamu aletwe kwenye hatima ifaayo aliyotengenezewa na Mungu kwa ajili yake. Ni kwa sababu hasa kuwa Mungu hufanya kazi katika mwanadamu ndiyo maana mwanadamu ana hatima na hatima yake ni ya uhakika. Hapa, hatima ifaayo inayoangaziwa sio matumaini na matarajio yaliyotakaswa katika nyakati za zamani, hizi mbili ni tofauti. Kitu ambacho mwanadamu hutumainia na kufuata ni tamaa za harakati ya hamu ya kimwili iliyo badhirifu, badala ya hatima ya mwanadamu anayotazamiwa. Kile ambacho Mungu amemwandalia mwanadamu, wakati huo huo, ni baraka na ahadi alizoandaliwa mwanadamu mara baada ya kutakaswa, ambayo Mungu alimtayarishia mwanadamu baada ya kuumba ulimwengu, na ambayo haitiwi doa na uchaguzi, dhana, mawazo au mwili wa mwanadamu. Hatima hii haitayarishwi kwa ajili ya mtu fulani, lakini ni mahali pa kupumzikia pa wanadamu wote. Na kwa hivyo, hii hatima ni hatima inayofaa zaidi kwa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 589)

Muumba anakusudia kupanga viumbe vyote. Wewe ni lazima usitupe au kutokaidi chochote ambacho Yeye anakifanya, wala usiwe na uasi kwake. Wakati ambapo kazi ambayo Yeye hufanya hatimaye inatimiza nia Yake, katika hii atapata utukufu. Leo, ni kwa nini haisemwi kwamba nyinyi ni wa uzao wa Moabu, au watoto wa joka kuu jekundu? Je, ni kwa nini hakuna mazungumzo ya wateule, na mazungumzo pekee ni ya viumbe? Kiumbe—hili lilikuwa jina la asili la mwanadamu, na ni hili ndilo utambulisho wake wa asili. Majina yanatofautiana tu kwa sababu nyakati na vipindi ni tofauti; kwa kweli, mwanadamu ni kiumbe wa kawaida. Viumbe wote, ikiwa ni wapotovu zaidi ama ni watakatifu sana, ni lazima watekeleze wajibu wa kiumbe. Wakati Yeye anafanya kazi ya ushindi, Mungu hakudhibiti kwa kutumia matarajio yako, majaliwa au hatima. Kwa kweli hakuna haja ya kufanya kazi kwa namna hii. Lengo la kazi ya ushindi ni kumfanya mwanadamu atekeleze wajibu wa kiumbe, kumfanya aabudu Muumba, na ni baada ya hii tu ndivyo ataweza kuingia kwenye hatima ya kustaajabisha. Majaliwa ya mwanadamu yanadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe? Kwa kifupi, bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi, kazi yote yake ni kwa ajili ya mwanadamu. Chukua, kwa mfano, mbingu na nchi na vitu vyote ambavyo Mungu aliviumba ili kumhudumia mwanadamu: mwezi, jua, na nyota ambazo Yeye alimuumbia mwanadamu, wanyama na mimea, majira ya machipuko, majira ya joto, vuli na baridi, na kadhalika—yote yametengenezwa kwa ajili ya kuwepo kwa mwanadamu. Na kwa hivyo, bila kujali ni jinsi gani anavyoadibu na kuhukumu mwanadamu, yote ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Japokuwa yeye humnyang’anya mwanadamu matumaini yake ya kimwili, ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, na utakaso wa mwanadamu ni kwa ajili ya kuishi kwake. Hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Muumba, hivyo ni jinsi gani mwanadamu anaweza kujidhibiti mwenyewe?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 590)

Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu. Lakini ahadi hii haiwezi timika mara moja: Mwanadamu ataingia katika hatima ya mbeleni punde tu kazi ya siku za mwisho zitakapokuwa zimemalizika na yeye amekwisha kushindwa kikamilifu, yaani, punde tu Shetani atakapokuwa ameshindwa kabisa. Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera. Ni kama tu vikosi vya uhasama wa giza vitakuwa vimefungwa ndipo mwanadamu atakuwa huru kokote aendako, na bila uasi au upinzani. Shetani ni sharti afungwe katika utumwa, and kila kitu kitakuwa sawa kwa mwanadamu; hali ya sasa ipo kwa sababu Shetani bado huchochea shida kila mahali hapa duniani, na kwa sababu kazi nzima ya usimamizi wa Mungu bado haijafika mwisho wake. Punde tu Shetani anaposhindwa, mwanadamu atakuwa amekombolewa kikamilifu; wakati mwanadamu anampata Mungu na anatoka katika kumilikiwa na Shetani, atatazama jua ya haki. Maisha atakayolipwa mwanadamu wa kawaida yatarejeshwa; yote yale ambayo ni lazima yamilikiwe na mwanadamu wa kawaida—kama uwezo wa kupambanua mema na mabaya, na kufahamu jinsi ya kula na kujivisha mwenyewe, na uwezo wa kuishi kama kawaida—yote haya yatarejeshwa. Hata kama Hawa hakuwa amejaribiwa na nyoka, mwanadamu ni lazima angekuwa na maisha kama haya ambayo ni ya kawaida baada ya kuumbwa hapo mwanzo. Ni lazima angekula, angevishwa, na kuendelea na maisha ya mwanadamu wa kawaida hapa duniani. Ila baada ya mwanadamu kupotoshwa, maisha haya yakawa ndoto, na hata leo mwanadamu hathubutu kufikiri mambo kama haya. Kwa kweli, maisha haya ya kupendeza ambayo mwanadamu anatamani ni haja yake: Iwapo mwanadamu angekuwa hana hatima kama hii, basi maisha yake ya duniani yaliyopotoshwa kamwe hayangekoma, na kama hakungekuwepo na maisha yakupendeza kama haya, basi hakungekuwa na hitimisho la majaliwa ya Shetani au kwa enzi ambayo Shetani ana utawala duniani kote. Mwanadamu ni sharti awasili kwenye ufalme ambao huwezi kufikiwa na nguvu za giza, na wakati atawasili, hii itathibitisha ya kwamba Shetani amekwisha shindwa. Kwa njia hii, punde tu hakuna usumbufu wa Shetani, Mungu mwenyewe atamdhibiti mwanadamu, na Yeye ataamuru na kudhibiti maisha yote ya mwanadamu; hii tu ndiyo itahesabika kama kushindwa kwa Shetani. Maisha ya mwanadamu leo ni sanasana maisha ya uchafu, na bado ni maisha ya kuteseka na mateso. Hii haingeitwa kushindwa kwa Shetani; mwanadamu bado hajatoroka kutoka katika bahari ya mateso, bado hajatoroka kutoka katika ugumu wa maisha ya mwanadamu, ama ushawishi wa Shetani, na bado yeye ana maarifa ya Mungu lakini kidogo sana. Taabu zote za mwanadamu ziliumbwa na Shetani, ni Shetani ndiye alileta mateso katika maisha ya mwanadamu, na ni baada tu ya Shetani kufungwa ndipo mwanadamu ataweza kutoroka kikamilifu kutoka katika bahari ya mateso. Na bado utumwa wa Shetani unahitimika kupitia kushindwa na kupatwa kwa moyo wa mwanadamu, kwa kumfanya mwanadamu mabaki ya vita dhidi ya Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 591)

Leo, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa mkamilifu ni vitu ambavyo vinafuatwa kabla yeye hajakuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani, na ndiyo malengo ambayo mwanadamu hutafuta kabla ya utumwa wa Shetani. Kwa kiini, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili, au kufanywa wa kutumika vilivyo, ni kutoroka kutoka katika ushawishi wa Shetani. Harakati ya mwanadamu ni kuwa mshindi, lakini matokeo ya mwisho yatakuwa ni kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ni kwa kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani tu ndipo mwanadamu ataweza kuishi maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ya kumwabudu Mungu. Leo, harakati ya mtu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamilifu ndiyo mambo ambayo yanafuatwa kabla ya kuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani. Haya yanafuatwa kimsingi kwa ajili ya kutakaswa na kuweka ukweli katika vitendo, na ili kufanikisha ibada ya Muumba. Kama mwanadamu anamiliki maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ambayo hayana taabu na matatizo, basi mwanadamu hawezi kushiriki katika harakati za kuwa mshindi. “Kuwa mshindi” na “kufanywa kamili” ni malengo ambayo Mungu humpa mwanadamu kufuatilia, na katika ufukuziaji wa malengo haya, Yeye husababisha mwanadamu kuweka ukweli katika vitendo na kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye umuhimu. Lengo ni kumkamilisha mtu na kumpata yeye, na harakati ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili ni njia tu. Kama, hapo mbeleni, mwanadamu ataingia kwenye hatima ya ajabu, hakutakuwepo na kurejelea kuwa mshindi na kukamilika, kutakuwepo tu na kila kiumbe kikitekeleza wajibu wake. Leo, mwanadamu anafanywa kufuata mambo haya tu ili kufafanua upeo wa mwanadamu, ili harakati ya mwanadamu ilengwe zaidi na iwe ya utendaji zaidi. La sivyo, mwanadamu angeishi katikati ya dhahania isiyo dhahiri, na kufuatilia kuingia katika uzima wa milele, na kama ingekuwa hivyo, je, si mwanadamu hata angelikuwa hafifu hata zaidi? Kufuata njia hii, bila malengo au kanuni—je, hii sio kujidanganya? Hatimaye, harakati hii ingekuwa kama kawaida bila mazao; na mwishowe, mwanadamu bado angemilikiwa na Shetani na hangeweza kujinasua mwenyewe kutokana nayo. Mbona ajikabili mwenyewe kwenye harakati kama hii isiyo na sababu? Wakati mwanadamu ataingia kwenye hatima ya milele, mwanadamu atamwabudu Muumba, na kwa sababu mwanadamu amepata wokovu na kuingia ahera, mwanadamu hawezi kimbiza malengo yoyote, wala, zaidi ya hayo, yeye hatakuwa na haja ya kuhangaika kuwa atazingirwa na Shetani. Kwa wakati huu, mwanadamu atajua nafasi yake, na atatekeleza wajibu wake, na hata kama hataadibiwa au kuhukumiwa, kila mtu atatekeleza jukumu lake. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa kiumbe katika sura na hadhi pia. Hakutakuwepo tena na tofauti ya juu na chini; kila mtu atatekeleza tu kazi tofauti. Bado mwanadamu ataishi katika hatima ya wanadamu yenye utaratibu na ifaayo, mwanadamu atatekeleza wajibu wake kwa ajili ya kumwabudu Muumba, na wanadamu kama hawa ni wanadamu wa milele. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa amepata maisha yaliyoangaziwa na Mungu, maisha chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, na maisha pamoja na Mungu. Wanadamu wataishi maisha ya kawaida duniani, na wanadamu wote wataingia katika njia sahihi. Mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 utakuwa umemshinda Shetani kabisa, ambayo ina maana kuwa Mungu atakuwa amerejesha sura ya awali ya mwanadamu kufuatia kuumbwa kwake, na kwa hivyo, nia ya awali ya Mungu itakuwa imetimizwa. Hapo mwanzo, kabla mwanadamu hajapotoshwa na Shetani, mwanadamu aliishi maisha ya kawaida duniani. Baadaye, alipopotoshwa na Shetani, mwanadamu alipoteza maisha haya ya kawaida, na kwa hivyo kazi ya Mungu ya usimamizi ikaanza, na vita dhidi ya Shetani ikaanza ili kurejesha maisha ya kawaida ya mwanadamu. Ni wakati tu ambapo usimamizi wa kazi ya Mungu wa miaka 6,000 utafikia kikomo ndipo maisha ya mwanadamu yatakapoanza rasmi hapa duniani, ni wakati huo tu ndipo mwanadamu atakapokuwa na maisha mazuri, na Mungu atarejesha lengo la kumuumba mwanadamu hapo mwanzoni, na pia kufanana kwake kwa asili na mwanadamu. Na kwa hivyo, punde tu atakuwa na maisha ya kawaida ya mwanadamu duniani, mwanadamu hatafuatilia kuwa mshindi ama kuwa kamili, kwa kuwa mwanadamu atakuwa mtakatifu. “Washindi” na “kukamilishwa” ambako watu huzungumzia ni malengo yaliyopewa mwanadamu ili kufuata wakati wa vita kati ya Mungu na Shetani, na yapo tu kwa sababu mwanadamu amepotoshwa. Ni kwa kukupa lengo na kukufanya wewe kufuata lengo hili, ndipo Shetani atashindwa. Kukuambia uwe mshindi au ufanywe kamili ama utumike kunahitaji ya kwamba uwe na ushuhuda ili umwaibishe Shetani. Mwishowe, mwanadamu ataishi maisha ya mwanadamu wa kawaida duniani, na mwanadamu atakuwa mtakatifu, na wakati hii itatendeka, je, watatafuta kuwa washindi? Je, wote si viumbe wa uumbaji? Kuzungumza kuhusu kuwa mshindi na kuwa yule aliyekamilika, maneno haya yanaelekezwa kwa Shetani, na uchafu wa mwanadamu. Je, hii “mshindi” si kuhusu ushindi dhidi ya Shetani na majeshi ya uhasama? Unaposema kuwa wewe umefanywa mkamilifu, nini hicho ndani yako ambacho kimekamilishwa? Je, si kuwa umevua mwenyewe tabia potovu ya kishetani, ili uweze kufaulu kupata upendo mkuu wa Mungu? Mambo kama haya yanasemekana kuhusu mambo machafu ndani ya mtu, na kuhusu Shetani; na hayasemwi kuhusu Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 592)

Wakati mtu anafanikiwa kupata maisha ya ukweli ya mwanadamu duniani na vikosi vizima vya Shetani vimefungwa, mwanadamu ataishi kwa urahisi katika ardhi. Mambo hayatakuwa magumu kama yalivyo sasa: Mahusiano ya binadamu, mahusiano ya kijamii, mahusiano changamani ya kifamilia…., haya ni ya kusumbua, machungu mno! Maisha ya mwanadamu hapa ni duni! Punde tu mwanadamu anaposhindwa, moyo wake na akili yake vitabadilika: atakuwa na moyo unaomcha Mungu na moyo ambao unampenda Mungu. Punde tu wote walio ulimwenguni ambao wanatafuta upendo wa Mungu wanaposhindwa, ambayo ni kusema, punde tu Shetani anaposhindwa, na punde tu Shetani—nguvu zote za giza—zimekwisha fungwa, basi maisha ya mwanadamu duniani yatakuwa yasiyotaabishwa, na ataweza kuishi huru duniani. Kama maisha ya mwanadamu hayana mahusiano ya kimwili, na hayana changamani za mwili, basi itakuwa rahisi mno. Mahusiano ya kimwili ya mwanadamu ni changamani mno, na kwa mwanadamu kuwa na mambo kama hayo ni thibitisho kuwa yeye bado hajajikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa ndugu na dada, kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa wanafamilia wako, basi hungekuwa na wasiwasi, na hungekuwa na haja ya kuhofia kuhusu mtu yeyote. Hakuna kitakachoweza kuwa bora zaidi, na kwa njia hii mwanadamu atapunguziwa nusu ya mateso yake. Kuishi maisha ya kawaida ya binadamu duniani, mwanadamu atakuwa sawa na malaika; ingawa atakuwa bado na mwili, atakuwa sawa na malaika. Hii ni ahadi ya mwisho, ni ahadi ya mwisho ambayo mwanadamu amezawadiwa. Leo mwanadamu anapitia kuadibu na hukumu; Je, unafikiri matukio kama haya ya mwanadamu hayana maana? Je, kazi ya kuadibu na kuhukumu inaweza kufanywa bila sababu. Hapo awali ilisemekana kuwa kuadibu na kuhukumu mwanadamu ni kumweka katika shimo lisilo na mwisho, ambayo ina maana ya kuchukua majaliwa na matarajio. Hii ni kwa ajili ya jambo moja: utakasaji wa mwanadamu. Mwanadamu hawekwi kwenye shimo lisilo na mwisho kimakusudi, ambapo baadaye Mungu hukata tamaa juu yake. Badala yake, ni ili kushughulika na uasi ndani ya mwanadamu, ili hatimaye mambo ndani ya mwanadamu yaweze kutakasika, ili aweze kuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu, na awe kama mtu mtakatifu. Iwapo hii itafanywa, basi yote yatakuwa yametimia. Kwa kweli, wakati mambo hayo ndani ya mwanadamu ambayo yanapaswa kushughulikiwa yameshughulikiwa, na mwanadamu anakuwa na ushuhuda wa mwangwi, Shetani pia atashindwa, na hata ingawa kunaweza kuwa na mambo machache ambayo awali ndani ya mwanadamu hayakuwa yametakasika kabisa, punde tu Shetani ameshindwa, Shetani hawezi tena kusababisha taabu, na wakati huo mwanadamu atakuwa ametakaswa kabisa. Mwanadamu hajawahi kupitia maisha kama haya, lakini wakati Shetani anashindwa, yote yatakuwa yametulizwa na mambo hayo pumbavu ndani ya mwanadamu yatatatuliwa yote; matatizo mengine yote yataisha punde tu tatizo kuu litakapokuwa limetatuliwa. Wakati wa kupata kwa mwili kwa Mungu duniani, wakati Yeye binafsi anafanya kazi miongoni mwa watu, kazi yote ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na Yeye atamshinda Shetani kupitia kumshinda mwanadamu na kuwafanya kamili. Wakati nyinyi mtakuwa na ushuhuda wa ajabu, hii, pia, itaonyesha kushindwa kwa Shetani. Kwanza mwanadamu anashindwa na hatimaye anafanywa kamili kabisa ili kumshinda Shetani. Kwa kiini, hata hivyo, pamoja na kushindwa kwa Shetani hii pia vilevile ni wokovu wa wanadamu wote kutoka kwa shimo la bahari hii ya mateso. Bila kujali kama kazi hii inatendeka katika ulimwengu mzima au katika nchi ya China, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani na kuleta wokovu kwa wanadamu wote ili mwanadamu aweze kuingia pahali pa kupumzika. Mungu mwenye mwili, mwili huu wa kawaida, ni kwa usahihi kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni kuleta wokovu kwa wale wote walioko chini ya mbingu wanaompenda Mungu, ni kwa ajili ya kushinda wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, kwa ajili ya kumshinda Shetani. Msingi wa kazi yote ya Mungu ya usimamizi haitengani na kushindwa kwa Shetani ili kuleta wokovu kwa watu wote. Kwa nini, katika mengi ya kazi hii, daima inasemekana kwenu kuwa na ushuhuda? Na ushuhuda huu unaelekezewa nani? Je, si unaelekezwa kwa Shetani? Ushuhuda huu unafanyiwa Mungu, na unafanywa ili kushuhudia kuwa kazi ya Mungu imetimiza matokeo yake. Kuwa na ushuhuda inahusiana na kazi ya kumshinda Shetani; kama hakungekuwa na vita dhidi ya Shetani, basi mwanadamu hangetakiwa kuwa na ushuhuda. Ni kwa sababu kwamba Shetani lazima ashindwe, kwa wakati huo huo kama kuokoa mwanadamu, Mungu anataka kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wake mbele ya Shetani, ambao Yeye hutumia kufanya vita na Shetani. Kwa hivyo, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu na chombo cha kumshinda Shetani, na kwa hivyo mwanadamu yumo katika msingi wa usimamizi mzima wa Mungu, na Shetani ni mlengwa wa uharibifu, adui. Unaweza kuhisi kuwa haujafanya kitu chochote, lakini kwa sababu ya mabadiliko katika tabia yako, umekuwa na ushuhuda, na ushuhuda huu unaelekezwa kwa Shetani na haufanywi kwa mwanadamu. Mwanadamu hajafaa ili afurahie ushuhuda kama huu. Je, jinsi gani yeye ataweza kuelewa kazi inayofanywa na Mungu? Mlengwa wa vita vya Mungu ni Shetani; mwanadamu, wakati huo huo, ni mlengwa wa wokovu. Mwanadamu ana tabia potovu ya kishetani, na hana uwezo wa kuelewa kazi hii. Hii ni kwa sababu ya kupotoshwa na Shetani and asili kwa mwanadamu, bali inaelekezwa na Shetani. Leo, kazi kuu ya Mungu ni kumshinda Shetani, yaani, kumshinda mwanadamu kabisa, ili kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wa mwisho wa Mungu mbele ya Shetani. Kwa njia hii, mambo yote yatatimika. Kwa matukio mengi, kwa macho yako pekee inaonekana kwamba hakuna chochote ambacho kimefanyika, lakini kwa kweli, kazi tayari imekamilika. Mwanadamu anahitaji kwamba kazi yote iliyokamilika iwe ya kuonekana, bali bila kuifanya inayoonekana wazi kwako, Nimemaliza kazi yangu, kwa kuwa Shetani ametii, ambayo ina maana kuwa yeye ameshindwa kabisa, ya kuwa busara yote ya Mungu, nguvu na mamlaka yamemshinda Shetani. Huu ndiyo ushuhuda mahsusi ambao ni lazima mtu awe nao, na ingawa haijidhihirishi kwa uwazi katika mwanadamu, ingawa haionekani kwa macho pekee, Shetani tayari ameshindwa. Ujumla wa kazi hii lazima uelekezwe dhidi ya Shetani, na inafanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Shetani. Kwa hivyo, kuna mambo mengi ambayo mwanadamu haoni kuwa ni mafanikio, lakini ambayo, machoni pa Mungu, yalikuwa na mafanikio kwa muda mrefu uliopita. Hii ni moja ya ukweli wa ndani wa kazi yote ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 593)

Wale wote ambao wamo tayari kufanywa kamili wana nafasi ya kukamilishwa, kwa hivyo kila mtu ni sharti apumzike: katika siku zijazo ninyi wote mtaingia kwenye hatima. Lakini kama huko tayari kufanywa kamili, na huko tayari kuingia katika ufalme wa kustaajabisha, basi hilo ni tatizo lako mwenyewe. Wale wote ambao wako tayari kufanywa kamili na ni waaminifu kwa Mungu, wale wote ambao hutii, na wale wote ambao hufanya kazi yao kwa uaminifu watu wote kama hawa wanaweza kufanywa kamili. Leo, wale wote ambao hawatekelezi majukumu yao kwa uaminifu, wale wote ambao si waaminifu kwa Mungu, wale wote ambao hawajiwasilishi kwa Mungu, hasa wale ambao wamepokea kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu lakini hawaweki mafundisho hayo kwenye vitendo—watu wote kama hawa hawawezi kufanywa kamili. Wote wale ambao wako tayari kuwa waaminifu na kumtii Mungu wanaweza kufanywa kamili, hata kama ni wapumbavu kwa kiasi kidogo, wote hao ambao wako tayari kufuatilia wanaweza kufanywa kamili. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hili. Ili mradi umo tayari kufuata mwelekeo huu, unaweza kufanywa kamili. Mimi sina nia ya kuwacha au kuondoa chochote kati ya hizo miongoni mwenu, lakini ikiwa mwanadamu hajitahidi kufanya vyema, basi utakuwa unajiangamiza mwenyewe; siyo Mimi ndiye ninakuondoa, lakini ni wewe mwenyewe. Kama wewe mwenyewe hutajitahidi kufanya vyema—ikiwa wewe ni mvivu, au hutekelezi jukumu lako, au si mwaminifu, au hufuati ukweli na daima unafanya unavyotaka, ukitenda bila kujali, ukipigania umaarufu wako na bahati yako mwenyewe na huna maadili katika kushirikiana na jinsia tofauti, basi utabeba mzigo wa dhambi zako mwenyewe; hustahili huruma ya yeyote. Lengo langu ni kwa ajili ya nyinyi nyote mfanywe kamilifu, na kuwa angalao muweze kushindwa, ili awamu hii ya kazi iweze kumalizika kwa mafanikio. Mapenzi ya Mungu ni kuwa kila mtu aweze kufanywa kamili, na kupatwa naye hatimaye, na kutakaswa naye kabisa, na kuwa mmoja anayependwa na Yeye. Haijalishi kama Ninasema nyinyi ni wa fikra za kurudi nyuma au wa kimo cha umaskini—hii yote ni ukweli. Huku kusema kwangu hakuthibitishi kuwa Mimi nina nia kukuacha wewe, kwamba Mimi Nimepoteza matumaini kwenu, au kwa kiasi kidogo kwamba sina nia ya kuwaokoa. Leo Nimekuja kufanya kazi ya ukombozi wenu, ambayo ni kusema kuwa kazi ambayo Mimi hufanya ni mwendelezo wa kazi ya ukombozi. Kila mtu ana nafasi ya kufanywa kamili: Ili mradi uko tayari, ili mradi ufuate, na mwishowe wewe utaweza kutimiza matokeo haya, na hakuna hata mmoja wenu ambaye ataachwa. Kama wewe ni mtu wa kimo cha umasikini, mahitaji Yangu kwenu yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha umaskini; kama wewe ni wa kimo cha juu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha juu; kama wewe ni mjinga na hujui kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa ujinga wako; kama wewe unajua kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa ukweli kwamba wewe unajua kusoma na kuandika; kama wewe ni mkongwe, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa umri wako; kama wewe una uwezo wa kutoa ukarimu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa hilo; kama wewe unasema huwezi kutoa ukarimu, na unaweza tu kufanya kazi fulani, iwe ni kueneza injili, au kuchunga huduma ya kanisa, au kuhudhuria mambo mengine kwa ujumla, Ukamilifu Wangu kwako utakuwa kwa mujibu wa kazi ambayo wewe hufanya. Kuwa mwaminifu, kutii hadi mwisho kabisa, na kutafuta upendo mkuu wa Mungu—mambo haya ni lazima uyakamilishe, na hakuna vitendo vizuri zaidi kuliko mambo haya matatu. Hatimaye, mtu anatakiwa kuyafikia mambo haya matatu, na kama anaweza kuyafikia hayo atafanywa kamili. Lakini, zaidi ya yote, ni lazima ujitahidi na kuendelea kwa bidii, na usiwe wa kukaa tu kuelekea hapo. Nimesema kwamba kila mtu ana nafasi ya kufanywa mkamilifu, na ana uwezo wa kukamilishwa, na hili ni kweli, lakini hujaribu kuwa bora zaidi katika ufuatiliaji wako. Kama huwezi kuvifikia vigezo hivyo vitatu, mwishowe lazima uondolewe. Nataka kila mtu afaulu kufikia wengine, nataka kila mtu awe na kazi na kupata nuru wa Roho Mtakatifu, na kuwa na uwezo wa kutii hadi mwisho kabisa, kwa sababu huu ni wajibu wa kila mmoja wenu ambao mnapaswa kufanya. Wakati nyinyi wote mmetimiza wajibu wenu, mtakuwa wote mmefanywa kamili, mtakuwa pia na ushuhuda wa kustaajabisha. Wale wote walio na ushuhuda ni wale ambao wamekuwa na ushindi juu ya Shetani na wanapewa ahadi ya Mungu, na wao ndio watakaobaki kuishi katika hatima ya ajabu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 594)

Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake. Iwapo Mungu hatamshinda Shetani na kuokoa binadamu, ambao wamepotoshwa, Mungu hatawahi tena kuweza kuingia rahani. Mungu anakosa pumziko akosavyo mwanadamu. Wakati Mungu ataingia rahani tena, mwanadamu pia ataingia rahani. Maisha ya pumziko ni yale bila vita, bila uchafu, bila udhalimu unaoendelea. Hii ni kusema kwamba hayana unyanyasaji wa Shetani (hapa “Shetani” inamaanisha nguvu za uhasama), upotovu wa Shetani, na pia uvamizi wa nguvu yoyote inayompinga Mungu. Kila kitu kinafuata aina yake na kuabudu Bwana wa uumbaji. Mbingu na dunia ni shwari kabisa. Haya ni maisha matulivu ya binadamu. Mungu aingiapo rahani, hakuna udhalimu wowote utakaoendelea duniani, na hakutakuwa na uvamizi wowote wa nguvu za uhasama. Binadamu pia wataingia ulimwengu mpya; hawatakuwa tena binadamu waliopotoshwa na Shetani, lakini badala yake binadamu ambao wameokolewa baada ya kupotoshwa na Shetani. Siku ya pumziko ya binadamu pia ni siku ya pumziko ya Mungu. Mungu alipoteza pumziko Lake kwa sababu wanadamu hawakuweza kuingia rahani; haikuwa kwamba Hakuweza awali kupumzika. Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi ndani ya mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo. Mungu atarudia nafasi yake ya awali, na kila mtu atarudia nafasi yake husika. Hizi ndizo hatima ambazo Mungu na mwanadamu wataishi ndani kwa utaratibu huu baada ya mwisho wa usimamizi wote wa Mungu. Mungu ana hatima ya Mungu na mwanadamu ana hatima ya mwanadamu. Apumzikapo, Mungu ataendelea kuwaongoza binadamu wote kwa maisha yao duniani. Akiwa kwa mwangaza wa Mungu, mwanadamu atamwabudu Mungu wa kweli aliye mbinguni. Mungu hataishi tena miongoni mwa binadamu, na mwanadamu pia hataweza kuishi na Mungu katika hitimisho la Mungu. Mungu na mwanadamu hawawezi kuishi ndani ya ulimwengu sawa; badala yake, wote wawili wana njia zao binafsi za kuishi. Mungu ndiye anayeongoza binadamu wote, wakati binadamu wote ni matokeo ya kazi ya Mungu ya usimamizi. Ni binadamu wanaoongozwa; kuhusu kiini, binadamu si sawa na Mungu. Kuingia rahani kunamaanisha kurudi pahali pa awali pa mtu. Kwa hivyo, Mungu aingiapo rahani, kunamaanisha kwamba Mungu amerudi pahali Pake pa awali. Mungu hataishi tena duniani ama kushiriki kwa furaha na mateso ya binadamu wakati yupo miongoni mwa binadamu. Binadamu wanapoingia rahani, kunamaanisha kwamba mwanadamu amekuwa kiumbe halisi; binadamu watamwabudu Mungu wakiwa duniani na kuwa na maisha ya kawaida ya wanadamu. Watu hawatakuwa tena wasiomtii Mungu ama kumpinga Mungu; watarudia maisha asili ya Adamu na Hawa. Haya ndiyo maisha na hatima binafsi ya Mungu na binadamu baada ya kuingia rahani. Kushindwa kwa Shetani ni mwelekeo usioepukika katika vita kati ya Mungu na Shetani. Kwa njia hii, kuingia kwa Mungu rahani baada ya kukamilika kwa kazi Yake ya usimamizi na wokovu kamili wa mwanadamu na kuingia rahani pia kunakuwa mielekeo isiyoepukika. Pahali pa pumziko pa mwanadamu ni duniani, na pahali pa Mungu pa pumziko ni mbinguni. Wakati binadamu wanamwabudu Mungu katika pumziko, wataishi duniani, na wakati Mungu anaongoza sehemu iliyobaki ya binadamu katika pumziko, Atawaongoza kutoka mbinguni, sio kutoka duniani. Mungu bado atakuwa Roho, wakati mwanadamu bado atakuwa mwili. Mungu na mwanadamu wote wawili wana njia zao tofauti za kupumzika. Mungu anapopumzika, Atakuja na kujitokeza miongoni mwa mwanadamu, mwanadamu anapopumzika, ataongozwa na Mungu kutembea mbinguni na pia kufurahia maisha mbinguni. Baada ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, Shetani hatakuweko tena, na kama Shetani, wale watu waovu pia hawatakuweko tena. Kabla ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, wale watu waovu waliomtesa Mungu wakati mmoja duniani na adui waliokuwa hawamtii duniani watakuwa tayari wameangamizwa; watakuwa wameangamizwa na majanga makubwa ya siku za mwisho. Baada ya hao watu waovu kuangamizwa kabisa, dunia haitajua tena unyanyasaji wa Shetani. Binadamu watapata wokovu kamili, na hapo tu ndipo kazi ya Mungu itaisha kabisa. Haya ndiyo masharti ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 595)

Kukaribia kwa mwisho wa kila kitu kunaonyesha mwisho wa kazi ya Mungu na kunaonyesha mwisho wa maendeleo ya binadamu. Hii inamaanisha kwamba binadamu kama walivyopotoshwa na Shetani wamefika mwisho wao wa maendeleo, na kwamba vizazi vya Adamu na Hawa vitakuwa vimekamilisha uenezi wake. Na pia inamaanisha ya kwamba itawezekana kwa binadamu kama hawa, baada ya kupotoshwa na Shetani, kuendelea kustawi. Adamu na Hawa wa mwanzoni hawakuwa wamepotoshwa, lakini Adamu na Hawa waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni walivurugwa na Shetani. Wakati Mungu na mwanadamu wanaingia rahani pamoja, Adamu na Hawa—waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni—na vizazi vyao hatimaye watafika mwisho; binadamu wa baadaye bado watakuwa na vizazi vya Adamu na Hawa, lakini hawatakuwa watu wanaomilikiwa na Shetani. Badala yake, watakuwa watu waliookolewa na kutakaswa. Hawa watakuwa binadamu ambao wamehukumiwa na kuadibiwa, na walio watakatifu. Hawa watu hawatakuwa sawa na jamii ya binadamu kama ilivyokuwa awali; mtu anaweza kusema kwamba hao ni watu wa aina tofauti kabisa na Adamu na Hawa wa awali. Hawa watu watakuwa wamechaguliwa kutoka miongoni mwa wote waliopotoshwa na Shetani, na watakuwa ndio watu ambao hatimaye wamesimama imara wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, watakuwa kundi la mwisho la watu miongoni mwa wanadamu potovu. Kundi hili la watu ndilo tu litaweza kuingia katika raha ya mwisho pamoja na Mungu. Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. Walikuwa wamekombolewa wakati mmoja, na pia walikuwa wamehukumiwa na kuadibiwa; walikuwa pia wamemhudumia Mungu wakati mmoja, lakini siku ya mwisho itakapofika, bado wataondolewa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wao na kwa sababu ya kutotii na kutokombolewa kwao. Hawatakuwa tena katika ulimwengu wa baadaye, na hawatakuweko tena miongoni mwa jamii ya binadamu ya baadaye. Watenda maovu wote na yeyote na wote ambao hawajaokolewa wataangamizwa wakati watakatifu miongoni mwa binadamu wataingia rahani, bila kujali kama wao ni roho za wafu ama wale wanaoishi bado katika mwili. Bila kujali enzi ya hizi roho zitendazo maovu na watu watenda maovu, ama roho za watu wenye haki na watu wanaofanya haki wako, mtenda maovu yeyote ataangamizwa, na yeyote mwenye haki ataishi. Iwapo mtu ama roho inapokea wokovu haiamuliwi kabisa kulingana na kazi ya enzi ya mwisho, lakini inaamuliwa kulingana na iwapo wamempinga ama kutomtii Mungu. Kama watu wa enzi ya awali walifanya maovu na hawangeweza kuokolewa, bila shaka wangekuwa walengwa wa adhabu. Kama watu wa enzi hii wanafanya maovu na hawawezi kuokolewa, hakika wao pia ni walengwa wa adhabu. Watu wanatengwa kwa msingi wa mema na mabaya, sio kwa msingi wa enzi. Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya Yeye kumaliza kutekeleza kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga binadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa binadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi binadamu wote bado hawangeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta binadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, binadamu wote watakuwa watakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 596)

Watu leo hawawezi kutengana na mambo ya mwili; hawawezi kuacha starehe za mwili, wala hawawezi kuiacha dunia, pesa, ama tabia yao potovu. Watu wengi wanaendelea na shughuli zao kwa hali ya uzembe. Kwa kweli, hawa watu hawana Mungu mioyoni mwao hata kidogo; zaidi ya hayo, hawamchi Mungu. Hawana Mungu mioyoni mwao, na hivyo hawawezi kutambua yote anayofanya Mungu, na hawawezi kabisa kuamini maneno Azungumzayo kwa mdomo Wake. Watu hawa ni wa mwili sana, wamepotoshwa sana na hawana ukweli wowote, zaidi ya hayo, hawaamini kwamba Mungu anaweza kuwa mwili. Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili—yaani, yeyote asiyeamini kazi na hotuba ya Mungu anayeonekana na haamini Mungu anayeonekana lakini badala yake anaabudu Mungu asiyeonekana mbinguni—hana Mungu katika moyo wake. Ni watu wasiomtii na wanaompinga Mungu. Watu hawa hawana ubinadamu na fahamu, kusema chochote kuhusu ukweli. Kwa watu hawa Mungu anayeonekana na kushikika hawezi kuaminika zaidi, lakini Mungu asiyeonekana wala kushikika ni Mungu wa kuaminika na pia Anayefurahisha nyoyo zao. Wanachotafuta si ukweli wa uhalisi, wala si kiini cha kweli cha uhai, wala nia za Mungu; badala yake, wanatafuta msisimko. Mambo yoyote yanayoweza kuwaruhusu kufikia tamaa zao ni, bila shaka, imani na shughuli zao. Wamwamini Mungu tu ili kuridhisha tamaa zao, si kutafuta ukweli. Hawa watu si watenda maovu? Wanajiamini sana, na hawaamini kwamba Mungu aliye mbinguni atawaangamiza, hawa “watu wazuri.” Badala yake, wanaamini kwamba Mungu atawaruhusu kubaki na, zaidi ya hayo, Atawatuza vizuri sana, kwani wamemfanyia Mungu mambo mengi na kuonyesha kiwango kikubwa cha “uaminifu” Kwake. Kama wangemtafuta Mungu anayeonekana, wangelipiza kisasi mara moja dhidi ya Mungu na kukasirika wakati hawatapata tamaa zao. Hawa ni watu waovu wanaotaka kuridhisha tamaa zao; si watu wa uadilifu wanaosaka ukweli. Watu kama hao ni wale wanaojulikana kama waovu wanaomfuata Kristo. Wale watu wasioutafuta ukweli hawawezi kuamini ukweli. Hawawezi kabisa kutambua matokeo ya baadaye ya binadamu, kwani hawaamini kazi ama hotuba yoyote ya Mungu anayeonekana, na hawawezi kuamini hitimisho la baadaye la binadamu. Hivyo, hata wakimfuata Mungu anayeonekana, bado wanatenda maovu na hawatafuti ukweli, wala hawatendi ukweli Ninaohitaji. Wale watu wasioamini kwamba wataangamizwa kinyume ni kwamba ni wale watu watakaoangamizwa. Wote wanajiamini kuwa wajanja sana, na wanaamini kwamba wao wenyewe ndio wanaotenda ukweli. Wanafikiria mwenendo wao mbovu kuwa ukweli na hivyo wanauthamini. Hawa watu waovu wanajiamini sana; wanachukua ukweli kuwa mafundisho ya dini, na kuchukua vitendo vyao vibovu kuwa ukweli, na mwishowe watavuna tu walichopanda. Watu wanapojiamini zaidi na wanapokuwa na kiburi zaidi, ndipo hawawezi zaidi kupata ukweli; watu wanapomwamini Mungu wa mbinguni zaidi, ndipo wanampinga Mungu zaidi. Hawa ndio watu watakaoadhibiwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 597)

Kabla ya binadamu kuingia rahani, iwapo kila aina ya mtu ataadhibiwa ama kutuzwa kutaamuliwa kulingana na iwapo wanatafuta ukweli, iwapo wanamjua Mungu, iwapo wanaweza kumtii Mungu anayeonekana. Waliomhudumia Mungu anayeonekana lakini bado hawamjui wala kumtii hawana ukweli. Watu hawa ni watenda maovu, na watenda maovu bila shaka wataadhibiwa; zaidi ya hapo, wataadhibiwa kulingana na mienendo yao mibovu. Mungu ni wa mwanadamu kumwamini, na pia Anastahili utii wa mwanadamu. Wale wanaomwamini tu Mungu asiye yakini na asiyeonekana ni wale wasiomwamini Mungu; zaidi ya hapo, hawawezi kumtii Mungu. Kama hawa watu bado hawawezi kumwamini Mungu anayeonekana wakati kazi Yake ya ushindi inakamilika, na pia wanaendelea kutomtii na kumpinga Mungu anayeonekana katika mwili, hawa wanaoamini isiyo yakini bila shaka, wataangamizwa. Ni kama ilivyo na wale miongoni mwenu—yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa. Iwapo una ukweli na iwapo unampinga Mungu hayo yanaamuliwa kulingana na asili yako, si kulingana na sura yako ama hotuba na mwenendo wako wa mara kwa mara. Asili ya kila mtu inaamua iwapo ataangamizwa; hii inaamuliwa kulingana na asili iliyofichuliwa na mienendo yao na kutafuta kwao ukweli. Miongoni mwa watu wanaofanya kazi sawa na pia kufanya kiasi sawa cha kazi, wale ambao asili yao ni nzuri na wanaomiliki ukweli ni watu wanaoweza kubaki, lakini wale ambao asili yao ya ubinadamu ni mbovu na wasiomtii Mungu anayeonekana ni wale watakaoangamizwa. Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya binadamu yanahusiana na binadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakuna kosa lolote litakalotokea, na hakutakuwa na kosa hata moja litakalofanywa. Ni pale tu ambapo watu wanafanya kazi ndipo hisia za binadamu ama maana itaingilia. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote. Sasa kuna watu wengi wasioweza kutambua hatima ya baadaye ya binadamu na ambao pia hawaamini maneno Nisemayo; wote wasioamini, pamoja na wasiotenda ukweli, ni mapepo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 598)

Wanaotafuta na wasiotafuta sasa ni aina mbili tofauti ya watu, na wao ni aina mbili ya watu na hatima mbili tofauti. Wanaotafuta maarifa ya ukweli na kutenda ukweli ni watu ambao Mungu ataokoa. Wale wasiojua njia ya ukweli ni mapepo na adui; ni vizazi vya malaika mkuu na wataangamizwa. Hata wacha Mungu wanaomwamini Mungu asiye yakini—je, si mapepo pia? Watu wanaomiliki dhamiri nzuri lakini hawakubali njia ya ukweli ni mapepo; asili yao ni ile inayompinga Mungu. Wale wasiokubali njia ya ukweli ni wale wanaompinga Mungu, na hata kama watu hawa wanavumilia taabu nyingi, bado wataangamizwa. Wasio tayari kuiwacha dunia, wasioweza kuvumilia kutengana na wazazi wao, wasioweza kuvumilia kujiondolea raha zao za mwili, wote hawamtii Mungu na wote wataangamizwa. Yeyote asiyemwamini Mungu aliyepata mwili ni pepo; zaidi ya hayo, wataangamizwa. Wanaoamini lakini hawatendi ukweli, wasiomwamini Mungu aliyepata mwili, na wale ambao hawaamini kabisa kuwepo kwa Mungu wataangamizwa. Yeyote anayeweza kubaki ni mtu ambaye amepitia uchungu wa usafishaji na kusimama imara; huyu ni mtu ambaye kweli amepitia majaribio. Yeyote asiyemtambua Mungu ni adui; yaani, yeyote aliye ndani ama nje ya mkondo huu ambaye hamtambui Mungu aliyepata mwili ni adui wa Kristo! Shetani ni nani, mapepo ni nani, na nani ni maadui wa Mungu kama si wapinzani wasiomwamini Mungu? Wao si watu wasiomtii Mungu? Wao si watu wanaodai kwa maneno kuamini lakini hawana ukweli? Wao si wale watu wanaofuata tu kupata kwa baraka lakini hawawezi kumshuhudia Mungu? Bado unachanganyika na wale mapepo leo na kuwa na dhamiri na mapenzi kwao, lakini kwa hali hii huenezi nia nzuri kuelekea kwa Shetani? Je, huchukuliwi kuwa unashiriki na mapepo? Kama watu siku hizi bado hawawezi kutofautisha kati ya mema na maovu, na wanaendelea kuwa wenye kupenda na kuhurumia bila kufikiri na bila nia yoyote ya kutafuta mapenzi ya Mungu au kuweza kwa njia yoyote kushikilia nia za Mungu kama zao wenyewe, basi miisho wao utakuwa dhalili zaidi. Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili ni adui wa Mungu. Kama unaweza kushikilia dhamiri na mapenzi kuelekea kwa adui, je, hujakosa hisia ya haki? Kama unalingana na wale Ninaowachukia na wale Nisiokubaliana nao, na bado unashikilia mapenzi na hisia za binafsi kwao, basi wewe si asiyetii? Humpingi Mungu kimakusudi? Je, mtu kama huyu anamiliki ukweli? Ikiwa watu wako na dhamiri kwa maadui, wana upendo kwa mapepo na wana huruma kwa Shetani, basi hawaikatizi kazi ya Mungu kimakusudi? Wale watu wanaomwamini Yesu tu na hawamwamini Mungu aliyepata mwili wakati wa siku za mwisho na wale wanaodai kwa maneno kumwamini Mungu aliyepata mwili lakini wanafanya maovu wote ni adui wa Kristo, sembuse wale watu wasiomwamini Mungu. Hawa watu wote wataangamizwa. Kiwango ambacho mwanadamu anamhukumu mwanadamu kinatokana na tabia zake; aliye na mwenendo mzuri ni mtu mwenye haki, na aliye na mwenendo wa kuchukiza ni mwovu. Kiwango ambacho Mungu anamhukumu mwanadamu kinatokana na iwapo asili ya mtu inamtii Yeye; anayemtii Mungu ni mtu mwenye haki, na asiyemtii Mungu ni adui na mtu mwovu, bila kujali iwapo tabia ya mtu huyu ni nzuri ama mbaya, na bila kujali iwapo hotuba ya mtu huyu ni sahihi ama si sahihi. Watu wengine wanatamani kutumia matendo mazuri kupata hatima nzuri ya baadaye, na watu wengine wanataka kutumia hotuba nzuri kununua hatima nzuri. Watu wanaamini kimakosa kwamba Mungu anaamua matokeo ya mwanadamu kulingana na tabia ama hotuba yake, na kwa hivyo watu wengi watataka kutumia haya kupata fadhila ya muda mfupi kupitia udanganyifu. Watu ambao baadaye watasalimika kupitia pumziko wote watakuwa wamevumilia siku ya dhiki na pia kumshuhudia Mungu; wote watakuwa watu ambao wamefanya jukumu lao na wana nia ya kumtii Mungu. Wanaotaka tu kutumia fursa kufanya huduma ili kuepuka kutenda ukweli hawataweza kubaki. Mungu ana viwango sahihi vya mipangilio ya matokeo ya kila mtu; Hafanyi tu maamuzi haya kulingana na maneno na mwenendo wa mtu, wala Hayafanyi kulingana na tabia zao wakati wa kipindi kimoja cha muda. Hakika Hatakuwa na huruma na mwenendo wowote mbaya wa mtu kwa sababu ya huduma ya mtu ya zamani kwa Mungu, wala Hatamnusuru mtu kutokana na kifo kwa sababu ya gharama kwa Mungu ya mara moja. Hakuna anayeweza kuepuka adhabu ya uovu wake, na hakuna anayeweza kuficha tabia zake mbovu na hivyo kuepuka adhabu ya maangamizi. Kama mtu anaweza kweli kufanya jukumu lake, basi inamaanisha kwamba ni mwaminifu milele kwa Mungu na hatafuti tuzo, bila kujali iwapo anapokea baraka ama bahati mbaya. Kama watu wana uaminifu kwa Mungu waonapo baraka lakini wanapoteza uaminifu wao wasipoweza kuona baraka na mwishowe bado wasiweze kumshuhudia Mungu na bado wasiweze kufanya jukumu lao kama wapasavyo, hawa watu waliomhudumia Mungu wakati mmoja kwa uaminifu bado wataangamizwa. Kwa ufupi, watu waovu hawawezi kuishi milele, wala hawawezi kuingia rahani; watu wenye haki tu ndio mabwana wa pumziko. Baada ya binadamu kuingia katika njia sawa, watu watakuwa na maisha ya kawaida ya binadamu. Wote watafanya jukumu lao husika na kuwa waaminifu kabisa kwa Mungu. Watatoa kabisa kutotii kwao na tabia yao iliyopotoshwa, na wataishi kwa ajili ya Mungu na kwa sababu ya Mungu. Watakosa uasi na upinzani. Wataweza kabisa kumtii Mungu. Haya ndiyo maisha ya Mungu na mwanadamu na maisha ya ufalme, na ni maisha ya pumziko.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 599)

Wanaopeleka watoto na jamaa zao wasioamini kabisa kanisani ni wachoyo sana na wanaonyesha ukarimu wao. Watu hawa wanalenga tu kuwa wenye upendo, bila kujali iwapo wanaamini au la na iwapo ni mapenzi ya Mungu. Wengine wanaleta wake zao mbele ya Mungu, ama kuleta wazazi wao mbele ya Mungu, na bila kujali iwapo Roho Mtakatifu anakubali ama anafanya kazi Yake, kwa upofu “wanawachukua watu wenye vipaji” kwa ajili ya Mungu. Kuna faida gani inayoweza kupatikana kutokana na kueneza ukarimu huu kwa watu hawa wasioamini? Hata kama hawa wasioamini wasio na uwepo wa Roho Mtakatifu wanapambana kumfuata Mungu, bado hawawezi kuokolewa kama mtu anavyodhani wanaweza. Wanaopokea wokovu kwa kweli si rahisi hivyo kuwapata. Wale ambao hawajapitia kazi ya Roho Mtakatifu na majaribio na hawajakamilishwa na Mungu aliyepata mwili hawawezi kukamilika kabisa. Kwa hivyo, watu hawa hawana uwepo wa Roho Mtakatifu kutoka wakati wanaanza kumfuata Mungu kwa jina. Kulingana na hali yao halisi, hawawezi tu kufanywa kamili. Hivyo, Roho Mtakatifu Haamui kutumia nguvu nyingi kwao, wala Hawapatii nuru yoyote ama kuwaongoza kwa njia yoyote; Anawaruhusu tu kufuata na hatimaye kufichua matokeo yao—haya yametosha. Shauku na nia za mwanadamu zinatoka kwa Shetani, na hakuna vile zinaweza kukamilisha kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali mtu ni mtu wa aina gani, mtu lazima awe na kazi ya Roho Mtakatifu—je, mtu anaweza kumkamilisha mtu? Mbona mume anampenda mke wake? Na mbona mke anampenda mume wake? Mbona watoto ni watiifu kwa wazazi wao? Na mbona wazazi wanawapenda sana watoto wao? Watu kweli wana nia za aina gani? Je, si kuweza kukidhi mipango na tamaa zao za ubinafsi? Kweli ni ya mpango wa usimamizi wa Mungu? Ni ya kazi ya Mungu? Ni ya kutimiza wajibu wa kiumbe? Waliomwamini Mungu kwanza na hawangepata uwepo wa Roho Mtakatifu hawawezi kupata kazi ya Roho Mtakatifu; imeamuliwa kwamba watu hawa wataangamizwa. Bila kujali kiasi cha upendo ambao mtu anao kwao, hauwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Shauku na upendo wa mwanadamu unawakilisha nia za mwanadamu, lakini haviwezi kuwakilisha nia za Mungu na haviwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Hata mtu akieneza kiasi kikubwa zaidi cha upendo ama huruma kwa hao watu wanaomwamini Mungu kwa jina na kujifanya kumfuata Yeye lakini hawajui ni nini maana ya kumwamini Mungu, bado hawatapata huruma ya Mungu ama kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hata kama watu wanaomfuata Mungu kwa dhati ni wenye akili ndogo na hawawezi kuelewa kweli nyingi, bado wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu mara kwa mara, lakini wale walio wa akili nzuri kidogo, lakini hawaamini kwa dhati hawawezi kabisa kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Hakuna kabisa uwezekano wowote wa wokovu na watu hawa. Hata wakisoma maneno ya Mungu au wasikilize mahubiri mara kwa mara ama hata kumwimbia Mungu sifa, mwishowe hawataweza kubaki mpaka wakati wa pumziko. Iwapo mtu anatafuta kwa dhati hakuamuliwi na jinsi wengine wanamhukumu ama jinsi wengine karibu wanamwona, lakini kunaamuliwa na iwapo Roho Mtakatifu anamfanyia kazi na iwapo ana uwepo wa Roho Mtakatifu, na kunaamuliwa zaidi na iwapo tabia yake inabadilika na iwapo ana maarifa ya Mungu baada ya kupitia kazi ya Roho Mtakatifu kwa muda fulani; ikiwa Roho Mtakatifu anamfanyia mtu kazi, tabia ya mtu huyu itabadilika polepole, na mtazamo wake wa kumwamini Mungu utakua safi polepole. Bila kujali muda gani mtu anamfuata Mungu, kama wamebadilika, hii inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kwake. Kama hawajabadilika, inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwake. Hata kama hawa watu wanatoa huduma fulani, wanachochewa na nia zao za kupata bahati nzuri. Huduma ya mara kwa mara haiwezi kuchukua nafasi ya mabadiliko katika tabia yao. Hatimaye, bado wataangamizwa, kwani hakuna haja ya wale wanaotoa Huduma ndani ya ufalme, wala hakuna haja ya yeyote ambaye tabia yake haijabadilika kuwahudumia wale watu ambao wamekamilishwa na walio waaminifu kwa Mungu. Hayo maneno kutoka zamani, “Wakati mtu anamwamini Bwana, bahati inatabasamu kwa familia yake nzima,” yanafaa kwa Enzi ya Neema lakini hayana uhusiano na hatima ya mwanadamu. Yalifaa tu kwa hatua ya wakati wa Enzi ya Neema. Maana iliyokusudiwa ya maneno haya inaelekezwa kwa amani na baraka yakinifu ambazo watu wanafurahia; hayamaanishi kwamba familia nzima ya anayemwamini Bwana itaokolewa, wala hayamaanishi kwamba wakati mtu anapata bahati nzuri, familia yake nzima pia itaingia rahani. Iwapo mtu anapokea baraka ama kupata bahati mbaya inaamuliwa kulingana na kiini cha mtu, na haiamuliwi kulingana na asili ya kawaida ambayo mtu anashiriki na wengine. Ufalme hauna kabisa usemi kama huu ama kanuni kama hii. Kama mtu anaweza kusalimika hatimaye, ni kwa sababu amefikia mahitaji ya Mungu, na kama mtu hawezi hatimaye kubaki katika kipindi cha pumziko, ni kwa sababu mtu huyu hamtii Mungu na hajakidhi mahitaji ya Mungu. Kila mtu ana hatima inayofaa. Hatima hizi zinaamuliwa kulingana na asili ya kila mtu na hazihusiani kabisa. Mwenendo ovu wa mtoto hauwezi kuhamishwa kwa wazazi wake, na haki ya mtoto haiwezi kushirikishwa wazazi wake. Mwenendo ovu wa mzazi huwezi kuhamishwa kwa watoto wake, na haki ya mzazi haiwezi kushirikishwa watoto wake. Kila mtu anabeba dhambi zake husika, na kila mtu anafurahia bahati yake husika. Hakuna anayeweza kuchukua ya mwingine. Hii ni haki. Kwa mtazamo wa mwanadamu, iwapo wazazi wanapata bahati nzuri, watoto wao pia wanaweza, na watoto wakifanya maovu, wazazi wao lazima walipie dhambi zao. Huu ni mtazamo wa mwanadamu na njia ya mwanadamu ya kufanya vitu. Si mtazamo wa Mungu. Matokeo ya kila mtu yanaamuliwa kulingana na asili inayotoka kwa mwenendo wao, na daima yanaamuliwa inavyofaa. Hakuna awezaye kubeba dhambi za mwingine; hata zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kupokea adhabu badala ya mwingine. Hii ni thabiti. Malezi ya upendo ya mzazi kwa watoto wake hayamaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya watoto wake, wala upendo wenye utiifu wa mtoto kwa wazazi wake haumaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya wazazi wake. Hiyo ndiyo maana ya kweli ya maneno haya, “Basi kutakuwa na watu wawili shambani; mmoja wao atachukuliwa, na mwingine kuachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga katika kisiagi; mmoja atachukuliwa, na mwingine kuachwa.” Hakuna anayeweza kuwaingiza watoto wake watenda maovu rahani kwa msingi wa upendo wao wa kina kwa watoto wao, wala hakuna anayeweza kumwingiza mke wake (ama mume) rahani kwa sababu ya mwenendo wao wa haki. Hii ni kanuni ya utawala; hakuwezi kuwa na ubaguzi kwa mtu yeyote. Wanaotenda haki ni wanaotenda haki, na watenda maovu ni watenda maovu. Watenda haki watasalimika, na watenda maovu wataangamizwa. Watakatifu ni watakatifu; wao si wachafu. Wachafu ni wachafu, na hawana sehemu yoyote takatifu. Watu wote waovu wataangamizwa, na watu wote wa haki watasalimika, hata kama watoto wa watenda maovu wanafanya matendo ya haki, na hata kama wazazi wa mtu wa haki wanafanya matendo maovu. Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisizolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia. Wanaofanya wajibu wao na wasiofanya ni adui, wanaompenda Mungu na wanaomchukia Mungu ni wapinzani. Wanaoingia rahani na wale ambao wameangamizwa ni aina mbili ya viumbe wasiolingana. Viumbe wanaotimiza wajibu wao watasalimika, na viumbe wasiotimiza wajibu wao wataangamizwa; zaidi ya hayo, hii itadumu milele. Je, unampenda mume wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, unampenda mke wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, wewe ni mtiifu kwa wazazi wako wasioamini ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Mtazamo wa mwanadamu wa kumwamini Mungu ni sahihi ama la? Mbona unamwamini Mungu? Unataka kupata nini? Unampenda Mungu jinsi gani? Wasioweza kutimiza wajibu wao kama viumbe na hawawezi kufanya juhudi nzima wataangamizwa. Watu leo wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao, na pia ushirikiano wa damu, lakini baadaye hii yote itavunjwa. Waumini na wasioamini hawalingani ila wanapingana. Walio rahani wanaamini kwamba kuna Mungu na wanamtii Mungu. Wasiomtii Mungu wote watakuwa wameangamizwa. Familia hazitakuwa tena duniani; kunawezaje kuwa na wazazi na watoto ama mahusiano kati ya waume na wake? Kutoambatana kati ya imani na kutoamini kutakuwa kumevunja haya mahusiano ya kimwili!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 600)

Awali hakukuwa na familia miongoni mwa binadamu; mwanamume na mwanamke tu walikuwepo—aina mbili tofauti za wanadamu. Hakukuwa na nchi, sembuse familia, lakini kwa sababu ya upotovu wa mwanadamu, watu wa aina yote walijipanga katika koo binafsi, baadaye kukua kwa nchi na mataifa. Nchi na mataifa haya yalikuwa na familia ndogo binafsi, na kwa namna hii watu wa aina yote walisambazwa miongoni mwa jamii mbalimbali kulingana na tofauti ya lugha na mipaka igawayo. Kwa kweli, bila kujali idadi ya jamii zilizo duniani, binadamu wana babu mmoja pekee. Mwanzoni, kulikuwa na watu wa aina mbili tu, na aina hizi mbili zilikuwa mwanamume na mwanamke. Hata hivyo, kwa sababu ya maendeleo ya kazi ya Mungu, kupita kwa historia na mabadiliko ya kijiografia, kwa viwango mbalimbali aina hizi mbili za watu ziliendelezwa kuwa watu wa aina nyingine zaidi. Mwishowe, bila kujali idadi ya jamii zilizo katika binadamu, binadamu wote bado ni viumbe wa Mungu. Bila kujali jamii ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; wote ni vizazi vya Adamu na Hawa. Hata kama hawajatengenezwa na mikono ya Mungu, ni vizazi vya Adamu na Hawa, ambao Mungu Mwenyewe aliumba. Bila kujali aina ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; kwa sababu ni wa binadamu, ambao uliumbwa na Mungu, hatima yao ni hiyo ambayo binadamu wanapaswa kuwa nayo, na wamegawanywa kulingana na kanuni zinazopanga binadamu. Hiyo ni kusema kwamba, watenda maovu na wenye haki, hata hivyo, ni viumbe. Viumbe wafanyao maovu wataangamizwa hatimaye, na viumbe wafanyao matendo ya haki watasalimika. Huu ni mpangilio unaofaa sana wa viumbe wa aina hizi mbili. Watenda maovu hawawezi, kwa sababu ya kutotii kwao, kukataa kwamba ni viumbe wa Mungu lakini wameporwa na Shetani na hivyo hawawezi kuokolewa. Viumbe wa mwenendo wa haki hawawezi kutegemea ukweli kwamba watasalimika kukataa kwamba wameumbwa na Mungu na bado wamepokea wokovu baada ya kupotoshwa na Shetani. Watenda maovu ni viumbe wasiomtii Mungu; ni viumbe ambao hawawezi kuokolewa na tayari wameporwa na Shetani. Watu wanaotenda maovu ni watu pia; ni watu waliopotoshwa mno na watu wasioweza kuokolewa. Jinsi walivyo viumbe pia, watu wa mwenendo wa haki pia wamepotoshwa, lakini ni watu walio tayari kuacha tabia yao potovu na wanaweza kumtii Mungu. Watu wa mwenendo wa haki hawajajaa haki; badala yake, wamepokea wokovu na kuacha tabia yao potovu kumtii Mungu; watashikilia msimamo huo mwishowe, lakini hii si kusema kwamba hawajapotoshwa na Shetani. Baada ya kazi ya Mungu kuisha, miongoni mwa viumbe Wake wote, kutakuwa na wale watakaoangamizwa na wale watakaosalimika. Huu ni mwelekeo usioepukika wa kazi Yake ya usimamizi. Hakuna anayeweza kuyakataa haya. Watenda maovu hawawezi kusalimika; wanaomtii na kumfuata Mungu hadi mwishowe hakika watasalimika. Kwa sababu kazi hii ni ya usimamizi wa binadamu, kutakuwa na wale watakaobaki na wale watakaoondolewa. Haya ni matokeo tofauti ya watu wa aina tofauti, na hii ndiyo mipango inayofaa zaidi ya viumbe Wake. Mpango wa mwisho wa Mungu kwa mwanadamu ni kugawa kwa kuzivunja familia, kuyavunja mataifa na kuivunja mipaka ya kitaifa. Ni moja isiyo na familia na mipaka ya kitaifa, kwani mwanadamu, hata hivyo, ni wa babu mmoja na ni kiumbe wa Mungu. Kwa ufupi, viumbe wafanyao maovu wataangamizwa, na viumbe wanaomtii Mungu watasalimika. Kwa njia hii, hakutakuwa na familia, hakutakuwa na nchi na hasa hakutakuwa na mataifa katika pumziko la baadaye; binadamu wa aina hii ni aina takatifu kabisa ya binadamu. Adamu na Hawa waliumbwa awali ili mwanadamu aweze kutunza mambo yote duniani; mwanadamu awali alikuwa bwana wa vitu vyote. Nia ya Yehova ya kumuumba mwanadamu ilikuwa kumruhusu mwanadamu kuwa duniani na pia kutunza vitu vyote duniani, kwani mwanadamu awali hakuwa amepotoshwa na pia hakuweza kutenda maovu. Hata hivyo, baada ya mwanadamu kupotoshwa, hakuwa mtunzaji wa vitu vyote tena, na madhumuni ya wokovu wa Mungu ni kurejesha kazi hii ya mwanadamu, kurejesha ufahamu wa awali wa mwanadamu na utii wake wa awali; binadamu rahani watakuwa picha halisi ya matokeo ambayo kazi ya Mungu ya wokovu inatarajia kufikia. Ingawa hayatakuwa tena maisha kama yale ya bustani ya Edeni, kiini chake kitakuwa sawa; binadamu hawatakuwa tu nafsi yake ya awali isiyo potovu, lakini badala yake binadamu waliopotoshwa na kisha kupata wokovu. Watu hawa waliopata wokovu hatimaye (yaani, baada ya kazi Yake kuisha) wataingia rahani. Vivyo hivyo, matokeo ya wale walioadhibiwa pia yote yatafichuliwa mwishowe, na wataangamizwa tu baada ya kazi Yake kuisha. Hii ni kusema kwamba baada ya kazi Yake kuisha, watendao maovu na wale waliookolewa wote watafichuliwa, kwani kazi ya kufichua watu wa aina zote (bila kujali iwapo ni watenda maovu ama waliookolewa) itatekelezwa kwa watu wote wakati huo huo. Watenda maovu wataondolewa, na wale wanaoweza kubaki watafichuliwa wakati huo huo. Kwa hivyo, matokeo ya watu wa aina zote yatafichuliwa wakati huo huo. Hataliruhusu kwanza kundi la watu waliookolewa kuingia rahani kabla ya kuweka kando watenda maovu na kuwahukumu au kuwaadhibu kidogo kidogo; ukweli kwa kweli si hivyo. Wakati watenda maovu wanaangamizwa na waliosalimika wanaingia rahani, kazi Yake katika ulimwengu mzima itakuwa imemalizika. Hakutakuwa na utaratibu wa kipaumbele miongoni mwa wale wanaopata baraka na wale wanaopata taabu; wanaopokea baraka wataishi milele, na wanaopata taabu wataangamia milele. Hizi hatua mbili za kazi zitakamilika wakati huo huo. Ni hasa kwa sababu kuna watu wasiotii ndiyo maana haki ya watu wanaotii itafichuliwa, na ni hasa kwa sababu kuna wale waliopokea baraka ndiyo maana taabu ya wale wanaotenda maovu kwa sababu ya mwenendo wao mbovu itafichuliwa. Kama Mungu hakufichua watenda maovu, hao watu wanaomtii Mungu kwa dhati hawangeona jua; kama Mungu hangewapelekea wanaomtii katika hatima inayofaa, wasiomtii Mungu hawangeweza kupata adhabu wanayostahili. Huu ndio mwendo wa kazi Yake. Kama hangefanya kazi hii ya kuadhibu maovu na kutuza mazuri, viumbe Wake hawangeweza kuingia hatima zao husika. Mwanadamu aingiapo rahani, watenda maovu wataangamizwa, binadamu wote wataingia katika njia sahihi, na watu wa kila aina watakuwa na aina yao kulingana na kazi wanayopaswa kufanya. Hii tu ndiyo itakuwa siku ya binadamu kupumzika na mwenendo usioepukika wa maendeleo ya binadamu, na wakati tu binadamu wataingia rahani ndipo utimilifu mkubwa na wa mwisho wa Mungu utamalizika; hii itakuwa tamati ya kazi Yake. Hii kazi itamaliza maisha ya uharibifu ya kimwili ya binadamu, na itamaliza maisha ya binadamu potovu. Kutoka hapa binadamu wataingia katika ulimwengu mpya. Ingawa mwanadamu anaishi kimwili, kuna tofauti kubwa kati ya kiini cha maisha yake na kiini cha maisha ya binadamu wapotovu. Maana ya kuwepo kwake na maana ya kuwepo kwa binadamu wapotovu pia ni tofauti. Ingawa haya si maisha ya mtu wa aina mpya, inaweza kusemwa kuwa maisha ya binadamu ambao wamepata wokovu na maisha yenye ubinadamu na busara kurejeshwa. Hawa ni watu ambao hawakumtii Mungu wakati mmoja, na ambao walishindwa na Mungu wakati mmoja na baadaye kuokolewa na Yeye; hawa ni watu waliomwaibisha Mungu na baadaye wakamshuhudia. Uwepo wao, baada ya kupitia na kuendelea kuishi baada ya jaribio Lake, ni uwepo wa maana kubwa zaidi; ni watu waliomshuhudia Mungu mbele ya Shetani; ni watu wanaofaa kuishi. Watakaoangamizwa ni watu wasioweza kumshuhudia Mungu na hawafai kuishi. Maangamizo yao yatakuwa kwa sababu ya mwenendo wao mwovu, na maangamizo ni hatima yao bora zaidi. Mwanadamu aingiapo baadaye katika ulimwengu mzuri, hakutakuwa na mahusiano kati ya mume na mke, kati ya baba na binti ama kati ya mama na mwana wa kiume ambayo mwanadamu anafikiria atapata. Wakati huo, mwanadamu atafuata aina yake, na familia itakuwa tayari imevunjwa. Baada ya kushindwa kabisa, Shetani hatawasumbua binadamu tena, na mwanadamu hatakuwa tena na tabia potovu ya kishetani. Wale watu wasiotii watakuwa wameangamizwa tayari, na wale watu wanaotii pekee ndio wataishi. Na basi familia chache sana zitasalimika bila kuharibika; mahusiano ya kimwili yatawezaje kuweko? Maisha ya kimwili ya zamani ya mwanadamu yatapigwa marufuku kabisa; mahusiano ya kimwili yatawezaje kuweko kati ya watu? Bila tabia potovu ya kishetani, maisha ya watu hayatakuwa tena maisha ya zamani ya siku zilizopita, lakini badala yake maisha mapya. Wazazi watapoteza watoto, na watoto watapoteza wazazi. Waume watapoteza wake, na wake watapoteza waume. Watu sasa wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao. Wakati wote watakuwa wameingia rahani hakutakuwa na mahusiano ya kimwili tena. Binadamu kama hawa tu ndio watakuwa wa haki na watakatifu, binadamu kama hawa tu ndio watamwabudu Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 601)

Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote. Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Maangamizo ya mwisho ya wale wana wa uasi pia yatafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 602)

Mwanadamu atakamilishwa kabisa katika Enzi ya Ufalme. Baada ya kazi ya ushindi, mwanadamu atapitishwa kwenye mambo magumu ya kusafishwa na taabu. Wale ambao wanaweza kushinda na kushuhudia katika taabu hii ndio hatimaye watakaofanywa wakamilifu; wao ndio washindi. Katika taabu hii, mwanadamu anahitajika kukubali kusafishwa huku, na kusafishwa huku ndio tukio la mwisho la kazi ya Mungu. Itakuwa mara ya mwisho ambapo mwanadamu atasafishwa kabla ya hitimisho la kazi zote za usimamizi wa Mungu, na wale wote wanaomfuata Mungu lazima wakubali jaribio hili la mwisho, lazima wakubali kusafishwa huku kwa mwisho. Wale ambao wamekabiliwa na taabu ni wale wasiokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu na uelekezi wa Mungu, lakini wale ambao wameshindwa kwa kweli na wanatafuta mapenzi ya Mungu kwa kweli hatimaye watasimama imara; ndio wale ambao wana ubinadamu, na wanaompenda Mungu kwa kweli. Bila kujali Mungu hufanya nini, hawa washindi hawatapungukiwa na maono, na bado watauweka ukweli katika matendo bila kufeli katika ushuhuda wao. Wao ndio watakaosimama mwishowe kutoka kwenye taabu kubwa. Hata ingawa wale wanaovua samaki katika maji yenye mawimbi mengi bado wanaweza kusaidiwa leo, hakuna yeyote atakayeepuka taabu, na hakuna atakayeepuka jaribio la mwisho. Kwa wale wanaoshinda, taabu ya aina hii ni usafisho mkubwa; lakini wale wanaovua katika maji yenye mawimbi, ni kazi ya kuondolewa kamili. Bila kujali jinsi wanavyojaribiwa, utii wa wale wenye Mungu ndani ya mioyo yao hubaki vile vile; lakini kwa wale wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao, wakati kazi ya Mungu hainufaishi miili yao, wanabadilisha mtazamo wao kwa Mungu, na hata kumkimbia Mungu. Hawa ndio wale hawatasimama imara mwishoni, wanaotafuta baraka za Mungu na hawana tamaa ya kujitolea wenyewe kwa Mungu na kujikabidhi wenyewe Kwake. Watu duni wa aina hii watafukuzwa wakati kazi ya Mungu itakapofikia kikomo, na wao hawafai kuonewa huruma yoyote. Wale wasiokuwa na ubinadamu, hawawezi kumpenda Mungu kwa kweli. Wakati mazingira ni mema na salama, au kama kuna faida inayoweza kupatwa, wao ni watiifu kabisa kwa Mungu, lakini wakati walilokuwa wanataka limepatikana au hatimaye kukataliwa, wanageuka mara moja. Hata kama ni kwa muda wa usiku mmoja tu, wao watatoka katika hali ya tabasamu, watu wenye “mioyo mikunjufu” hadi wenye sura mbovu na wauaji wakatili, ghafla wakiwatendea wafadhili wao wa jana kana kwamba ni adui wa milele, bila chanzo wala sababu. Ikiwa mapepo haya hayatarushwa nje, mapepo haya ambayo yanaweza kuua bila kusita, je, hayatakuwa hatari iliyofichika? Kazi ya kumwokoa mwanadamu haitimizwi kufuatia kazi ya kukamilisha ushindi. Ingawa kazi ya ushindi imefika kikomo, kazi ya kumtakasa mwanadamu haijafika kikomo; kazi hiyo itamalizika tu wakati mwanadamu amesafishwa kikamilifu, wakati wale ambao wamejikabidhi kwa Mungu kikweli wamekamilishwa, na wakati wale wadanganyifu wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao wamesafishwa. Wale ambao hawamridhishi Mungu katika hatua ya mwisho ya kazi Yake wataondolewa kabisa, na wale watakaoondolewa kabisa ni wa yule mwovu. Kwa kuwa hawawezi kumtosheleza Mungu, wao ni waasi dhidi ya Mungu, na hata kama watu hawa wanamfuata Mungu leo, hili si thibitisho kwamba wao ndio watakaosalia mwisho. Kwa maneno mengine “wale ambao humfuata Mungu hadi mwisho watapokea wokovu,” maana ya “kufuata” ni kusimama imara katikati ya taabu. Leo, wengi wanaamini kwamba kumfuata Mungu ni rahisi, lakini wakati kazi ya Mungu inakaribia kuisha, utajua maana halisi ya “kufuata.” Kwa sababu tu kwamba unaweza kumfuata Mungu leo baada ya kushindwa, si thibitisho kwamba umo miongoni mwa wale watakaokamilishwa. Wale wasioweza kustahimili majaribu, wale wasioweza kuwa washindi wakiwa kwenye taabu, hatimaye, watashindwa kusimama imara, na basi kushindwa kumfuata Mungu hadi mwisho kabisa. Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya yanaweza kumshawishi binadamu kikamilifuHafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba “ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano” ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli. Kwa misingi ya kazi zao na shuhuda zao tofauti, washindi katika ufalme watatumika kama makuhani au wafuasi, na wale wote watakaoshinda taabu watakuwa mwili wa makuhani katika ufalme. Baraza la makuhani litaundwa wakati kazi ya injili ulimwenguni kote itafikia kikomo. Wakati huo ukitimia, yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu yatakuwa jukumu lake ndani ya ufalme wa Mungu, na kuishi kwake pamoja na Mungu katika ufalme. Katika baraza la makuhani, patakuwepo makuhani wakuu na makuhani, na watakaosalia watakuwa wana na watu wa Mungu. Haya yote huamuliwa na ushuhuda wao kwa Mungu wakati wa majaribu; sio nyadhifa zinazopeanwa kwa wazo la ghafla. Wakati hadhi ya mwanadamu itakuwa imeianzishwa, kazi ya Mungu itamalizika, kwa kuwa kila mojawapo imewekwa kulingana na aina yake na kurejeshwa katika hali yake halisia, na hii ndiyo alama ya ukamilisho wa kazi ya Mungu, na haya ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu na matendo ya mwanadamu, na ndiko kubainika kwa yale maono ya kazi ya Mungu na ushirikiano wa mwanadamu. Mwishowe, mwanadamu atapata pumziko katika ufalme wa Mungu, na, Mungu pia, atarejea kwenye makazi Yake kupumzika. Haya ndiyo yatakayokuwa matokeo ya miaka 6,000 ya ushirikiano wa mwisho kati ya Mungu na mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 603)

Wale miongoni mwa ndugu ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani, na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi sio tu kwamba hawatashindwa kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomwasi Mungu. Wakati ambapo mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini. Ikiwa usemi na mwenendo wa muumini daima havina mpango na bila kizuizi kama asiyeamini, basi huyu muumini ni mwovu zaidi kumpiku asiyeamini; yeye ni ibilisi halisi. Wale walio kanisani ambao wanaeneza matamshi yao yenye sumu, wale miongoni mwa ndugu ambao wanasambaza uvumi, kuchochea utengano na kufanya magenge wanapaswa kufukuzwa kutoka kanisani. Lakini watu hawa wamezuiwa kwa kuwa sasa ni enzi tofauti ya kazi ya Mungu, kwa sababu wamehukumiwa kuwa vyombo vya kuondolewa. Wale waliopotoshwa na Shetani wote wana tabia iliyopotoka. Hata hivyo, baadhi ya watu wana tabia potovu tu, huku kuna wengine walio tofauti: Si tu kwamba wana tabia potovu za kishetani, lakini asili zao pia ni mbovu kupita kiasi. Si tu kwamba maneno yao na vitendo vyao vinafichua tabia zao potovu za kishetani; watu hawa, aidha ndio Shetani wa kweli. Tabia yao inakatiza na kuvuruga kazi ya Mungu, inaharibu uingiaji wa kina ndugu katika uzima, na kuharibu maisha ya kawaida ya kanisa. Mbwa mwitu hawa waliovalia ngozi ya kondoo lazima waondolewe nje siku moja, na mtu lazima awe na mtazamo usiojizuia kwa vibaraka hawa wa Shetani; mtu lazima awe na mtazamo wa kuachwa kwao. Ni katika kufanya hili pekee ndipo mtu ataweza kusimama upande wa Mungu na wale wasioweza kufanya hili wako katika ushirika na Shetani. Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakienda kwa mikogo na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti zao na mataifa yana sheria zao; je, hali sio hivi hata zaidi katika nyumba ya Mungu? Je, matarajio sio makali hata zaidi? Je, hakuna amri nyingi hata zaidi za utawala? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea; Yeye ni Mungu anayewaua watu. Je, watu kweli hawajui hili tayari?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 604)

Kila moja ya kanisa lina watu wanaolivuruga kanisa, watu wanaokatiza kazi ya Mungu. Watu hawa wote ni Shetani wanaojifanya katika familia ya Mungu. Watu kama hawa ni waigizaji wazuri: wanakuja mbele Yangu na uchaji mkubwa, wakiinama na kuchakura, wakiishi kama mbwa koko, wakijitolea “yote” waliyo nayo ili kufanikisha malengo yao wenyewe—lakini mbele ya kina ndugu, anaonyesha sura yake mbaya. Anapomwona mtu akiutenda ukweli anamshambulia na kumtenga; anapomwona mtu wa kutisha kumpiku yeye mwenyewe, anamsifu mno na kujipendekeza kwake, wakitenda kama viongozi wa kiimla kanisani. Inaweza kusemwa kuwa mengi ya makanisa yana aina hii ya “nyoka mwovu wa ndani,” aina hii ya “mbwa wa kupakata” kati yao. Wanatembea kwa siri kwa pamoja, wakikonyezana na kuashiriana, na hakuna hata mmoja wao anayetenda ukweli. Yeyote aliye na sumu zaidi ndiye “ibilisi mkuu,” na yeyote aliye na hadhi ya juu zaidi huwaongoza, akipeperusha bendera yao juu zaidi. Watu hawa wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani, wakieneza ubaya wao, wakiachilia kifo, wakifanya watakavyo, wakisema wanachopenda, bila anayethubutu kuwakomesha, wakijawa na tabia za kishetani. Punde tu wanapoanza kusababisha usumbufu, hewa ya kifo inaingia ndani ya kanisa. Wale wanaotenda ukweli katika kanisa wanaachwa na wanashindwa kufikia uwezo wao, ilhali wale wanaovuruga kanisa na kusambaza kifo wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani. Cha ziada ni, watu wengi huwafuata. Aina hii ya kanisa iko chini ya udhibiti wa Shetani na ibilisi ni mfalme wao. Iwapo watu wa kanisa hawataamka na kuwafukuza hao ibilisi wakuu, basi pia watakuja kuangamia siku moja. Kuanzia leo na kuendelea hatua lazima zichukuliwe dhidi ya kanisa la aina hii. Ikiwa wale wanaoweza kutenda ukweli kidogo hawatafuti kufanya hivyo, basi kanisa hilo litaondolewa. Ikiwa hakuna mtu yeyote kanisani aliye radhi kuutenda ukweli, hakuna yeyote anayeweza kuwa shahidi kwa Mungu, basi kanisa hilo linapasa kutengwa kabisa, miunganisho yao na makanisa mengine kukatizwa. Hili linaitwa “kuzika kifo”; hii ndiyo maana ya kumfukuza Shetani. Iwapo kanisa lina waonevu kadhaa wa hapo, na wanafuatwa na “nzi wadogo” wasio na ufahamu kabisa, na ikiwa washiriki wa kanisa, hata baada ya kuona ukweli, bado hawawezi kukataa vifungo na kuchezewa na hawa waonevu—basi hawa wajinga wataondolewa mwishoni. Ingawa nzi hawa wadogo wanaweza kuwa hawajafanya lolote baya, wao ni wenye hila hata zaidi, wadanganyifu hata zaidi na wenye kukwepa hata zaidi na kila mtu aliye namna hii ataondolewa. Hakuna yeyote atakayeachwa! Wale walio wa Shetani watarudishwa kwa Shetani, ilhali wale walio wa Mungu hakika watakwenda kutafuta ukweli; hili linaamuliwa na asili zao. Acheni wale wote wanaomfuata Shetani waangamie! Hakuna huruma watakayoonyeshwa watu hawa. Acheni wale wanaofuata ukweli wapate utoaji na muwakubalie kufurahia neno la Mungu hadi mioyo yao itosheke. Mungu ni mwenye haki; Yeye hawatendei watu kwa udhalimu. Ikiwa wewe ni ibilisi basi hutakuwa na uwezo wa kuutenda ukweli. Ikiwa wewe ni mtu anayetafuta ukweli basi ni wazi kuwa hutatekwa nyara na Shetani—hili halina tashwishi yoyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 605)

Wale wasiotafuta kuendelea daima wanataka wengine wawe wabaya na watepetevu kama wao wenyewe, wale wasiotenda ukweli wanawaonea gere wale wanaotenda ukweli. Wale wasiotenda ukweli daima wanataka kuwadanganya wale wapumbavu na wasio na ufahamu. Mambo ambayo watu hawa wanaeneza yanaweza kukufanya usawijike, kuteleza kwenda chini, kuwa na hali isiyokuwa ya kawaida na kujawa na kiza ndani yako; yanaweza kukufanya usogezwe mbali na Mungu, na yanakufanya uuthamini mwili na kujihusisha na tamaa. Wale ambao hawapendi ukweli, ambao daima humshughulikia Mungu kwa uzembe hawana maarifa ya binafsi, na tabia zao huwashawishi watu kufanya dhambi na kuasi Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo wala kuwaruhusu wengine kutenda ukweli. Wanathamini dhambi na hawana chuki kwao wenyewe. Hawajifahamu wenyewe na huwakomesha wengine kujifahamu wenyewe, na huwakomesha wengine kuwa na matamanio ya kujua ukweli. Wale wanaowadanganya hawawezi kuona mwangaza na huanguka gizani, hawajijui wenyewe, na ukweli kwao si wazi na wanakuwa mbali zaidi na zaidi na Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo na huwakomesha wengine kutenda ukweli, wakiwaleta watu hao wajinga mbele yao. Badala ya kusema kuwa wanamwamini Mungu ingekuwa vyema kusema kuwa wanawaamini mababu zao, kwamba kile wanachoamini ni sanamu zilizo mioyoni mwao. Ingekuwa vyema kwa wale watu wanaosema kuwa wanamfuata Mungu kufungua macho yao watazame vizuri waone ni nani wanayemwamini hasa: Je, ni Mungu unayemwamini hakika, ama Shetani? Ikiwa unajua kuwa unayemwamini si Mungu ila sanamu zako mwenyewe, basi ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Ikiwa hakika hujui unayemwamini ni nani, basi, pia, ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Kusema hivi kutakuwa kukufuru! Hakuna anayekushurutisha umwamini Mungu. Msiseme kuwa mnaniamini Mimi, kwa kuwa Niliyasikia maneno hayo hapo kale wala Sitamani kuyasikia tena, kwa kuwa mnachoamini ni sanamu zilizo katika mioyo yenu na nyoka waovu wa ndani walio miongoni mwenu. Wale wanaotikisa vichwa vyao wanaposikia ukweli, wanaotabasamu sana wanaposikia mazungumzo ya kifo ni watoto wa Shetani, na wote ni vyombo vya kuondolewa. Kuna watu wengi kanisani ambao hawana ufahamu, na jambo la uongo linapotendeka wanasimama tu upande wa Shetani. Wanapoitwa vibaraka wa Shetani wanahisi kuwa wamekosewa sana. Wanasemekana kuwa hawana ufahamu, lakini daima wanasimama upande usiokuwa na ukweli. Hakujakuwa na wakati muhimu ambapo wamesimama upande wa ukweli, hakuna wakati mmoja ambapo hawasimami na kutetea mjadala juu ya ukweli. Je, kweli hawana ufahamu? Kwa nini daima wao husimama upande wa Shetani isipotarajiwa? Kwa nini hawasemi neno lolote la haki ama lenye mantiki kwa ukweli? Je, hali hii kweli imetokana na kuchanganyikiwa kwao kwa ghafla? Kadri mtu anapokuwa na ufahamu mdogo, ndivyo anavyozidi kushindwa kusimama upande wa ukweli. Je, hili linaonyesha nini? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu wanapenda uovu? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu ni watoto waaminifu wa Shetani? Je, ni kwa nini daima wanaweza kusimama upande wa Shetani na kuzungumza lugha moja naye? Kila neno na tendo lao, na maonyesho yao yanathibitisha vya kutosha kuwa wao sio wapenzi wa ukweli kwa namna yoyote, lakini badala yake wao ni watu wanaochukia ukweli. Kwamba wanaweza kusimama upande wa Shetani kunadhihirisha kuwa hakika Shetani anawapenda ibilisi hawa wadogo wanaopigana kwa ajili ya Shetani katika maisha yao yote. Je, taarifa hizi za kweli si wazi sana? Ikiwa hakika wewe ni mtu unayependa ukweli, basi kwa nini huwaheshimu wale wanaotenda ukweli, na mbona unawafuata mara moja wale wasiotenda ukweli punde kwa kuwaangalia tu? Je, hili ni tatizo la aina gani? Sijali iwapo una ufahamu au la, sijali kwamba umelipa gharama kuu kiasi gani, sijali kuwa nguvu zako ni kuu kiasi gani na sijali ikiwa wewe ni nyoka mwovu wa ndani ama kiongozi anayepeperusha bendera. Ikiwa nguvu zako ni kuu basi ni kwa ajili tu ya usaidizi wa nguvu za Shetani; ikiwa hadhi yako iko juu, basi ni kwa sababu kuna wengi waliokuzunguka wasiotenda ukweli; ikiwa hujafukuzwa basi ni kwa kuwa sasa sio wakati wa kazi ya kufukuza, bali ni wakati wa kazi ya kuondoa. Hakuna haraka ya kukufukuza sasa. Ninasubiri tu siku ambayo Nitakuadhibu baada ya wewe kuondolewa. Yeyote asiyetenda ukweli ataondolewa!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 606)

Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walio tayari kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walio radhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walio radhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni waakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa. Wale wasiotenda ukweli hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa makusudi. Lakini sasa Sifanyi kazi ya kufukuza. Watafichuliwa tu na kuondolewa mwishoni. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasiotenda ukweli hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Kabla ya mwisho wa kila mtu kufichuliwa, wale wanaovuruga kanisa na kukatiza kazi kwanza wataachwa upande moja. Pindi kazi itakapokamilika, watu hawa watafunuliwa mmoja baada ya mwingine kabla ya kuondolewa. Wakati wa kutoa ukweli, Siwatilii maanani kwa sasa. Ukweli wote unapofichuliwa kwa mwanadamu watu hao wanapasa kuondolewa, kwa kuwa huo pia utakuwa wakati ambapo watu wataainishwa kulingana na aina yao. Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasiotenda ukweli lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaotenda ukweli mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasiotenda ukweli mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaotenda ukweli na wale wasioutenda. Ninawashauri wale ambao hawana mpango wa kutenda ukweli watoke kanisani haraka iwezekanavyo ili kuepuka kutenda dhambi nyingi zaidi. Wakati utakapofika, hata majuto yatakuwa yamechelewa, na hasa wale wanaofanya magenge na kufanya migawanyiko, na wale nyoka waovu wa ndani katika kanisa lazima watoke haraka sana. Watu hawa ambao ni wenye asili ya mbwa mwitu mwovu hawana uwezo wa mabadiliko, ni heri watoke kanisani kwa nafasi inayopatikana mwanzo, wasiweze kuyavuruga maisha mazuri ya ndugu tena, na hivyo kuepuka adhabu ya Mungu. Nyinyi ambao mlienda pamoja nao mtafanya vema kutumia nafasi hii kutafakari juu yenu wenyewe. Je, mtawafuata waovu nje ya kanisa, ama kusalia na kufuata kwa unyenyekevu? Lazima uzingatie jambo hili kwa makini. Ninawapa nafasi moja zaidi ya kuchagua. Ninalisubiri jibu lenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 607)

Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. Kabla Sijaendelea, mnafaa kwanza kuelewa yafuatayo: Maneno Ninayoongea ni ukweli unaoelekezwa kwa wanadamu wote, na wala hayajaelekezwa kwa mtu mahususi au aina fulani ya mtu. Kwa hiyo, mnapaswa kumakinikia kupokea maneno Yangu kutoka katika mtazamo wa ukweli, na vile vile mdumishe mtazamo wa uzingativu na uaminifu kamili. Msipuuze hata neno moja au ukweli Ninaoongea, na wala usichukulie maneno Yangu kwa dharau. Katika maisha yenu, Naona mengi ambayo mnafanya ambayo hayana uhusiano na ukweli, kwa hivyo Nawaambia moja kwa moja muwe watumishi wa ukweli na wala si kutawaliwa na maovu na ubaya. Msikanyage ukweli na kuchafua sehemu yoyote ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo onyo Langu kwenu. Sasa Nitaanza kuzungumza kuhusu mada ya sasa:

Kwanza, kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnastahili kumletea Mungu utulivu wa akili katika mambo yote na kumtosheleza katika kila jambo. Kwa maneno mengine, lazima muwe wenye maadili katika matendo yenu na kutii ukweli katika mambo kama hayo. Kama hali hii inazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na kila mwanadamu. Punde utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hii ndiyo maana ya kutoidhinishwa na Mungu.

Pili, mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. Kile Ninachoongea ni rahisi sana lakini ni kigumu maradufu kwenu. Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina matendo mengine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkuu mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Nyinyi wote ni werevu sana na stadi katika kupima uungwana wa mtu kwa kipimio chenu wenyewe; kwa hiyo kazi Yangu inakuwa rahisi zaidi. Na kwa sababu nyinyi mnaficha siri katika mioyo yenu, basi, Nitawatumeni, mmoja baada ya mwingine, katika janga kupitia ili “mfundishwe” kupitia moto, ili baadaye mtajitolea kabisa katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitapokonya maneno “Mungu ni Mungu wa uaminifu,” kutoka kwa vinywa vyenu na kisha ndipo mtakapojigamba na kujitanua kifua na kulalama, “Ujanja ndio moyo wa binadamu!” Hali za akili zenu zitakuwa zipi wakati huu? Ninafikiri hamtajisahau sana na majivuno kama mlivyo sasa. Na sembuse hamtakuwa “wa maana sana kiasi cha kutoeleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme. Unafaa kujua kama kunayo imani ya kweli na uaminifu wa kweli ndani yako, kama una rekodi ya kuteseka kwa ajili ya Mungu, na kama umemtii Mungu kikamilifu. Kama unakosa hivi Nilivyotaja, basi ndani yako kunabaki kutotii, udanganyifu, ulafi, na kutotosheka. Kwa vile moyo wako si mwaminifu, hujawahi kupokea utambuzi mzuri kutoka kwa Mungu na hujawahi kuishi katika mwangaza. Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ni mtu asiye mwaminifu sana, mtu mwenye moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa, jinsi ilivyoandikwa katika rekodi ya majaliwa yako. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, na bado kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la ukweli, basi bado unatarajia Mungu kukutuza? Bado unatumai Mungu akuchukue kama kipenzi Chake? Je, kufikiria huku si kwa upuzi? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, hivyo nyumba ya Bwana inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe, ambaye mikono yake si safi?

Jambo la tatu Ninalotaka kuwaambia ni hili: Kila mwanadamu, katika kuishi maisha yake ya imani katika Mungu, amemkataa na kumdanganya Mungu wakati fulani. Baadhi ya matendo mabaya hayahitaji kurekodiwa kama kosa, lakini mengine hayasameheki; kwani mengi ni yale yanayokiuka amri za utawala, yaani, yanaikosea tabia ya Mungu. Wengi ambao wanajali majaliwa yao binafsi wanaweza kuuliza matendo haya ni yapi. Lazima mjue kwamba nyinyi mna kiburi na wenye majivuno kiasili, na hamko radhi kutii ukweli. Kwa sababu hii, Nitawaambia kidogo kidogo baada ya nyinyi kutafakari kujihusu. Ninawashawishi kuwa na ufahamu bora zaidi wa yaliyomo katika amri za utawala na kujua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana kuendelea kufunga vinywa vyenu na kufyata ndimi zenu dhidi ya kuropokwa bila kizuizi kwa mazungumzo ya mbwembwe, na bila kujua mtaikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza. Kwa sababu nyinyi hamna maadili katika matendo yenu, kufanya na kutenda kile ambacho hufai kufanya hivyo, basi utapokea adhabu inayokufaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ni mwenye maadili sana katika hali hizi zote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, wewe hutenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi huna budi ila kuwa mtoto wa kuzimu. Kwa binadamu inaweza kuonekana kwamba umetenda matendo machache tu yasiyolingana na ukweli na si chochote zaidi. Je, una habari, hata hivyo, kwamba katika macho ya Mungu, tayari wewe ni mmoja ambaye kwake hakuna tena sadaka ya dhambi? Kwani umevunja amri za utawala za Mungu zaidi ya mara moja na hujaonyesha ishara yoyote ya kutubu, kwa hivyo huna chaguo lolote ila kutumbukia kuzimu pale ambapo Mungu anamwadhibu mwanadamu. Katika wakati wao wa kufuata Mungu, idadi ndogo ya watu ilitenda matendo yaliyoenda kinyume na kanuni, lakini baada ya kushughulikiwa na kuongozwa, waligundua polepole upotovu wao, na kisha wakachukua njia iliyo sawa ya uhalisi, na leo wanabaki wenye msingi imara katika njia ya Bwana. Binadamu kama hawa ndio watakaobakia mwisho. Ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; kama wewe ni mtu mwaminifu na unayetenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako huikosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na unao moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako ni ya kiwango kilichowekwa. Yeyote asiyemcha Mungu na asiye na moyo unaotetema kwa woga atakiuka amri za utawala za Mungu kwa urahisi. Wengi humhudumia Mungu kwa misingi ya hisia kali, na hawajui katu amri za utawala za Mungu, sembuse kuelewa athari za neno Lake. Na kwa hivyo, na nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya vitu vinavyokatiza usimamizi wa Mungu. Kwa hali za uzito sana, wanatupwa nje na kunyang’anywa fursa yoyote zaidi ya kumfuata, na wanatupwa kuzimu bila ya kuwa na uhusiano wowote mwingine na nyumba ya Mungu unakoma. Watu hawa hufanya kazi katika nyumba ya Mungu wakiwa na nia nzuri zisizojua na wanaishia kuikasirisha tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wakuu na mabwana katika nyumba ya Mungu na kujaribu kufanya yatumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa bila jitihada. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wanaojihusisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo unapoweza kujua siku zote kumhusu Mungu. Maarifa haya si mafungu wala mafundisho, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya karibu na Mungu, na ithibati kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisi wa maarifa na hujajiandaa ukweli, basi huduma yako ya shauku itakuletea tu hali ya chuki ya kupindukia na kuchukizwa sana kwa Mungu. Sasa unafaa kuelewa kwamba imani katika Mungu si masomo tu ya teolojia.

Ingawa maneno Ninayotumia kuwaonya ni mafupi, vyote Nilivyovifafanua hapa ndivyo vinavyokosekana zaidi ndani yenu. Lazima mjue kwamba kile Ninachozungumzia sasa ni kwa minajili ya kazi Yangu ya mwisho miongoni mwa binadamu, kwa ajili ya kuamua hatima ya binadamu. Sipendelei kufanya kazi nyingi zaidi isiyo na maana, na wala Sipendelei kuendelea kuwaongoza wale binadamu wasio na matumaini kama mti uliooza, sembuse wale walio na nia mbaya kisiri. Pengine siku moja mtaelewa nia za dhati zinazoyasukuma maneno Yangu na michango ambayo Nimemfanyia mwanadamu. Pengine siku moja mtafahamu kanuni inayowawezesha kuamua hatima yenu binafsi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 608)

Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata kwa miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii na uasi wenu mwingi dhidi Yangu kwa hii miaka mingi, kwa sababu hakuna mtakatifu hata mmoja kati yenu, nyinyi pia ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba daima Mimi hujirudia mbele yenu. Sitaki kuishi kuishi pamoja na nyinyi kwa namna hii—lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine. Natumai mtaniendekeza, nami Natumai hata zaidi kwamba mtaweza kuamini kila neno Ninalosema, na bado zaidi, kwamba mtaweza kufahamu kwa kina maana ya maneno Yangu. Msiwe na shaka juu ya yale Ninayosema, au hata kuchukua maneno Yangu mnavyotaka na kuyatupilia mbali kwa hiari, jambo ambalo mimi Ninaona halistahimiliki. Msiyahukumu maneno Yangu, wala kutoyachukulia kwa uzito, au kusema kwamba daima Nawajaribu, au mbaya zaidi, kusema kwamba kile ambacho Nimewaambia kinakosa usahihi. Ninaona kuwa mambo haya hayavumiliki. Kwa sababu mnanichukulia Mimi na kuyachukulia Ninayoyasema kwa shaka kuu na kamwe hamyazingatii, Ninamwambia kila mmoja wenu kwa uzito kabisa: Msiunganishe kile Ninachosema kwa falsafa, msikiweke pamoja na uongo wa matapeli, na hata zaidi, msiyajibu maneno Yangu kwa dharau. Labda katika siku zijazo hakuna mtu yeyote atakuwa na uwezo wa kuwaambia yale Ninayowaambia nyinyi, au kuzungumza na nyinyi kwa huruma sana, sembuse kuwaeleza mambo haya kwa uvumilivu hivi. Siku zijazo zitatumika katika kukumbuka nyakati zile nzuri, au kwa kulia kwa sauti kubwa, au kugumia kwa maumivu, au mtakuwa mkiishi katika usiku wa giza bila hata chembe ya ukweli au kupewa maisha, au kusubiri tu bila matumaini, au katika majuto machungu mengi kiasi kwamba hamwezi kufikiri…. Huu uwezekano mbadala hauwezi kuepukika kabisa kwa mtu yeyote kati yenu. Kwa sababu hakuna hata mmoja wenu ambaye anamiliki kiti ambacho kwacho kwa kweli mnamwabudu Mungu; mnajitumbukiza katika dunia ya uasherati na maovu, kuchanganya ndani ya imani yenu, ndani ya roho zenu, nafsi, na miili, mambo mengi yasiyohusiana na maisha na ukweli na kwa kweli yanapingana nayo. Hivyo kile Ninachotumai kwenu ni kuwa muweze kuletwa kwa njia ya mwanga. Tumaini Langu la pekee ni kwamba muweze kujitunza, muweze kujiangalia, si kuweka mkazo mwingi sana juu ya hatima yenu kiasi kwamba muitazame mienendo na dhambi zenu kwa kutojali.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 609)

Watu ambao wanamwamini Mungu kwa muda mrefu sasa wametumainia hatima iliyo nzuri, watu wote ambao wanamwamini Mungu wanatumai kwamba bahati nzuri itawajia ghafla, na wote wanatumai kwamba bila kujua, watajikuta wameketi kwa amani pahali pamoja au pengine mbinguni. Lakini Ninasema watu hawa kwa mawazo yao mazuri hawajawahi kujua kama wana sifa ya kupokea bahati nzuri kama hiyo inayoanguka kutoka mbinguni, au kukaa juu ya kiti huko mbinguni. Kwa sasa nyinyi mna maarifa mazuri kujihusu, lakini bado mnatarajia kwamba mnaweza kuepuka maafa ya siku za mwisho na mkono wa mwenye Uweza ukiwaadhibu wale waovu. Inaonekana kana kwamba kuwa na ndoto tamu na kutaka vitu kama tu wanavyopenda ni jambo la kawaida la watu wote ambao Shetani amewapotosha, si kipaji cha ajabu cha mtu fulani binafsi. Hata hivyo, bado Nataka kukomesha tamaa zenu badhirifu na hamu zenu za kupata baraka. Kwa kuwa dhambi zenu ni nyingi na ukweli wa kutotii kwenu ni mwingi na unaongezeka kila wakati, haya yanawezaje kupatana na ramani zenu nzuri za baadaye? Kama unataka kuendelea unavyopenda kuwa mwenye makosa, bila chochote kinachokuzuia, lakini bado unataka ndoto zitimie, basi Nakusihi uendelee katika usingizi wako na usiamke kamwe, kwa sababu unaota ndoto isiyoweza kutimia, na haitatumika kukufanya uwe mtu usiye wa kawaida mbele ya Mungu mwenye haki. Kama unataka tu ndoto zitimie, basi usiote kamwe, lakini kabiliana na ukweli milele, kabiliana na mambo ya hakika. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuokoa. Je, kwa maneno thabiti, hatua za taratibu hizi ni zipi?

Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na kuchunguza mwenendo na mawazo yako yote ambayo hayafuati ukweli.

Hiki ni kipengee ambacho mnaweza kukifanya kwa urahisi, na Ninaamini kwamba watu wanaofikiri wanaweza kufanya hivi. Hata hivyo, wale watu ambao hawajui kamwe ni nini maana ya dhambi na ukweli ni tofauti, kwa sababu kimsingi wao si watu wa kufikiri. Mimi nazungumza na watu ambao wamethibitishwa na Mungu, ni waaminifu, hawajazikosea vibaya amri za utawala, na wanaweza kupata dhambi zao wenyewe kwa urahisi. Ingawa hiki ni kipengee ambacho Ninahitaji kwenu ambacho ni rahisi kwenu, sicho kipengee cha pekee Ninachohitaji kwenu. Lolote litokealo, Ninatumai kwamba hamtalicheka hitaji hili kwa siri, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kimzaha. Lichukulieni kwa umakini, na msilipuuze.

Pili, kwa kila moja ya dhambi na kutotii kwako tafuta ukweli unaoambatana na utumie ukweli huu kuzitatua, kisha badilisha vitendo vyako vya dhambi na mawazo yako na vitendo vya kutotii na kutenda ukweli.

Tatu, kuwa mtu mwaminifu, si mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, mwenye hila daima. (Hapa Ninakusihi tena uwe mtu mwaminifu.)

Kama unaweza kutimiza vipengee hivi vyote vitatu basi una bahati, wewe ni mtu ambaye ndoto zake zinatimia na ambaye hupata bahati nzuri. Labda mtayachukulia maombi haya matatu yasiyovutia kwa umakini, au labda mtayachukulia bila kuwajibika. Kwa vyovyote vile, azma Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka mawazo yenu katika matendo, si kuwadhihaki au kuwadanganya.

Madai Yangu yanaweza kuwa rahisi, lakini kile Ninachowaambia si rahisi hivyo kama kujumlisha moja na moja upate mbili. Kama mnazungumzia tu mambo haya bila kufikiria, mkiongea sana kwa kuparaganya kwa maneno matupu ya majivuno yanayopita kiasi, basi ramani zenu na matakwa yenu yatakuwa ukurasa mtupu milele. Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale kati yenu ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Kinyume cha hayo, Mimi Huwatendea wale ambao hawajatosheleza madai Yangu kwa adhabu, siyo zawadi, sembuse huruma yoyote. Labda mnawaza kwamba kwa kuwa wafuasi kwa miaka mingi mnaweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote hadi sasa mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na kutokuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa bora zaidi Niigeuze miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa utupu, kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 610)

Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu. Kama kila mojawapo ya mazungumzo ambayo Nimekuwa nayo na nyinyi hayajatosha kuvuta nadhari yenu, basi huenda Sitasema mengine. Hata hivyo, nyinyi mnaelewa matokeo ya hayo. Sipumziki kamwe, kwa hiyo Nisiponena, Nitafanya kitu ili watu wakitazame. Ningeweza kuufanya ulimi wa mtu uoze, au mtu afe na viungo vyake kutolewa, au kumpa mtu kasoro za neva na kumfanya atende kama mwendawazimu. Au, basi tena, Ningeweza kufanya baadhi ya watu wavumilie maumivu makali Ninayowasababishia. Kwa njia hii Ningejihisi mwenye furaha, mwenye furaha sana na kufurahishwa sana. Imesemwa daima kwamba “Mema hulipizwa kwa mema, na maovu kwa maovu,” mbona isiwe hivyo sasa? Kama unataka kunipinga Mimi na unataka kutoa hukumu fulani kunihusu, basi Nitauozesha mdomo wako, na hilo litanipendeza Mimi sana. Hii ni kwa sababu mwishowe hujafanya lolote linalohusiana na ukweli, sembuse na maisha, ilhali kila kitu Ninachofanya ni ukweli, kila kitu kinahusiana na kanuni za kazi Yangu na amri za utawala Ninazoeleza rasmi. Kwa hiyo, Namsihi sana kila mmoja wenu kujilimbikiza wema kiasi, acha kufanya maovu mengi sana, na usikize madai Yangu katika wasaa wako. Kisha mimi Nitahisi furaha. Kama mngetoa (au kusaidia) kwa ukweli moja kwa elfu ya juhudi mnazoweka katika mwili, basi Nasema hungekuwa na dhambi mara kwa mara na midomo mbovu. Je, hili si dhahiri?

Kadri dhambi zako zilivyo nyingi, ndivyo nafasi zako za kupata hatima iliyo nzuri zilivyo chache. Kinyume chake, kadri dhambi zako zilivyo chache, ndivyo nafasi zako za kusifiwa na Mungu zilivyo nyingi. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi kiwango ambapo haiwezekani Mimi kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa jasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile kitakachokupata. Kama wewe ni mtu mwenye ari anayetenda ukweli basi kwa hakika una fursa ya kusamehewa dhambi zako, na kiwango cha kutotii kwako kitakuwa kidogo zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu asiye radhi kutenda ukweli basi hakika dhambi zako mbele ya Mungu zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitakua zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeangamia kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kufurahisha ya kupokea baraka itaharibiwa. Usizichukulie dhambi zako kama makosa ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu ubora wako wa tabia ulio duni ulifanya isiwezekane kuutenda, na hata zaidi, usizichukulie tu dhambi ulizofanya kama matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri zaidi. Kama unajua vizuri kujisamehe na unajua vizuri kujitendea kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hataupata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukusumbua, lakini zitakuzuia kuwahi kutosheleza madai ya ukweli na kukufanya milele kuwa mwenzi mwaminifu wa Shetani. Ushauri Wangu kwako bado ni: Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa makini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kuhusu hatima yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 611)

Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kupona kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba “siku za mwisho” ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza ulimwengu na anga. Iko hivyo ili Niweze kupata utukufu mkuu, ili viumbe vyote duniani viweze kupitisha utukufu Wangu kwa mataifa yote, milele katika vizazi vyote, na viumbe vyote mbinguni na duniani viweze kuuona utukufu wote ambao Nimepata duniani. Kazi inayofanyika katika siku za mwisho ni kazi ya ushindi. Sio uongozi wa maisha ya watu wote duniani, lakini hitimisho la maisha ya milenia ya mwanadamu yasiyoangamia, ya mateso katika dunia. Matokeo yake ni kwamba kazi ya siku za mwisho haiwezi kuwa kama miaka elfu kadhaa ya kazi katika Israeli, wala haiwezi kuwa kama ile miaka kadhaa tu ya kazi katika Yuda ambayo iliendelea kwa milenia mbili mpaka kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu katika mwili. Watu wa siku za mwisho hukutana tu na kuonekana tena kwa Mkombozi katika mwili, na kupokea kazi binafsi na maneno ya Mungu. Haitakuwa miaka elfu mbili kabla ya siku za mwisho hazijafika ukingoni; zi fupi, kama wakati ambao Yesu alifanya kazi ya Enzi ya Neema katika Yuda. Hii ni kwa sababu siku za mwisho ni hitimisho la nyakati nzima. Ni ukamilisho na tamatisho la mpango wa miaka elfu sita wa usimamizi wa Mungu, na kuhitimisha safari ya maisha ya mateso ya mwanadamu. Hazichukui binadamu wote hadi katika enzi mpya au kuruhusu maisha ya mwanadamu kuendelea. Hiyo haitakuwa na umuhimu wowote kwa ajili ya mpango Wangu wa usimamizi au kuwepo kwa mwanadamu. Kama mwanadamu angeendelea kwa namna hii, basi hivi karibuni wao wangeangamizwa kabisa na ibilisi, na zile nafsi za wale walio Wangu hatimaye zingeangamizwa na mikono yake. Kazi Yangu inadumu kwa miaka elfu sita tu, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala Sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kudhibiti yote Hatafanya kazi tena duniani. Lakini Nitafanya jambo moja duniani: Nitamfanya tena mwanadamu, mwanadamu aliye mtakatifu, na aliye mji Wangu mwaminifu duniani. Lakini ujue kwamba Sitaiangamiza dunia nzima, wala kuangamiza ubinadamu mzima. Nitahifadhi theluthi moja iliyobaki—theluthi moja inayonipenda na imeshindwa kabisa na Mimi, na Nitaifanya theluthi hii iwe yenye kuzaa matunda na kuongezeka duniani kama Israeli walivyofanya chini ya sheria, kuwalisha kwa kondoo wengi mno na mifugo, na utajiri wote wa dunia. Mwanadamu huyu atabaki na Mimi milele, hata hivyo si mwanadamu mchafu wa kusikitisha wa leo, lakini mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa wale wote ambao wamepatwa na Mimi. Mwanadamu wa aina hii hataharibiwa, kusumbuliwa, au kuzungukwa na Shetani, na atakuwa mwanadamu wa pekee anayepatikana duniani baada ya ushindi Wangu juu ya Shetani. Ni wanadamu ambao leo wameshindwa na Mimi na wamepata ahadi Yangu. Na hivyo, wanadamu ambao wameshindwa katika siku za mwisho pia ndio watakaosamehewa na kupata baraka Zangu za milele. Huu utakuwa ushahidi wa pekee wa ushindi Wangu dhidi ya Shetani, na nyara za pekee za vita Vyangu na Shetani. Hizi nyara za vita zimeokolewa nami kutoka utawala wa Shetani, na ni thibitisho la pekee na matunda ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita. Wao huja kutoka kila taifa na dhehebu, na kila mahali na nchi ulimwenguni mwote. Ni wa jamii tofauti, na wana lugha mbalimbali, mila na rangi ya ngozi, na huenea katika kila taifa na dhehebu la duniani, na hata kila pembe ya dunia. Hatimaye, watakuja pamoja na kuunda ubinadamu kamili, mkusanyiko wa binadamu usiofikiwa na majeshi ya Shetani. Wale miongoni mwa wanadamu ambao hawajaokolewa na kushindwa na Mimi watazama kwa kimya mpaka chini ya bahari, na watachomwa kwa moto wa kuteketeza milele. Nitamwangamiza mwanadamu huyu mzee aliye mchafu sana, kama tu vile Nilivyoangamiza wazaliwa wa kwanza na ng’ombe wa Misri, na kuacha tu Waisraeli, waliokula nyama ya mwanakondoo, kunywa damu ya mwanakondoo, na kutia alama vizingitini mwa milango yao kwa damu ya mwanakondoo. Si watu ambao wameshindwa na Mimi na ni wa jamii Yangu ndio wale pia wanaokula nyama Yangu, Mwanakondoo na kunywa damu Yangu, Mwanakondoo, na wamekombolewa na Mimi na kuniabudu Mimi? Si watu wa namna hiyo kila mara huandamwa na utukufu Wangu? Si hao wasio na nyama Yangu, Mwanakondoo tayari wamezama kimya kwa kina cha bahari? Leo mnanipinga, na leo maneno Yangu ni kama tu yale yaliyosemwa na Yehova kwa wana na wajukuu wa Israeli. Lakini ugumu katika kina cha nyoyo zenu unafanya ghadhabu Yangu kukusanya, na kuleta mateso zaidi juu ya miili yenu, hukumu zaidi juu ya dhambi zenu, na ghadhabu zaidi juu ya udhalimu wenu. Ni nani atakayeweza kusamehewa katika siku Yangu ya ghadhabu, mnaponitendea kwa namna hii leo? Udhalimu wa nani utaweza kuepuka macho Yangu ya kuadibu? Dhambi za nani zinaweza kuepuka mikono Yangu, Mwenyezi? Uasi wa nani unaweza kuhepa hukumu Yangu, Mwenyezi? Mimi, Yehova, Nasema hivyo kwenu, kizazi cha jamii ya Mataifa, na maneno Ninayosema nanyi yanashinda matamko yoyote yale ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, ilhali bado nyinyi ni wagumu kuliko watu wote wa Misri. Je, si mnahifadhi ghadhabu Yangu Ninapofanya kazi kwa utulivu? Jinsi gani mnaweza kuepuka salama bila ya madhara kutoka siku Yangu, Mwenyezi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 612)

Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Iliyotangulia: Kuingia Katika Uzima (VI)

Inayofuata: Kumjua Mungu (I)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp