1015 Baraka Kuu Zaidi Ambayo Mungu Anaweka Juu Ya Mwanadamu

1 Kwa kuwa maneno Yangu yametimilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu.

2 Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida. Leo hii, nyote mko hai mbele Yangu; kesho nyote mtakua hai ndani ya ufalme Wangu. Je, si hii ndiyo baraka kubwa zaidi ambayo Nimempa mwanadamu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 20” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1014 Uzuri wa Ufalme

Inayofuata: 1016 Ufalme Unapokuja Kikamilifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp