1014 Uzuri wa Ufalme

1 “Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee kamwe, na hakuna mtu ambaye yuko kama alivyokuwa. Ninapumzika katika kiti cha enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima….” Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu ya sasa. Wateule wote wa Mungu wanarudi kwa umbo lao la asili, kwa sababu hiyo malaika, ambao wameteseka kwa miaka mingi sana, wanaachiliwa, kama tu asemavyo Mungu, “kila mmoja akiwa na uso kama wa mtakatifu ndani ya moyo wa binadamu.” Kwa sababu malaika hufanya kazi duniani na kumhudumia Mungu duniani, na utukufu wa Mungu husambaa kila mahali ulimwenguni, mbingu inaletwa duniani, na dunia inainuliwa kwenda mbinguni. Kwa hivyo, mwanadamu ni kiungo kinachounganisha mbingu na dunia; mbingu na dunia haziko mbali tena, hazijatengana tena, lakini zimeunganishwa kama kitu kimoja.

2 Kotekote ulimwenguni, Mungu na mwanadamu ndio pekee wanaoishi. Hakuna vumbi wala uchafu, na vitu vyote vinafanywa upya, kama mwanakondoo mdogo anayelala katika ukanda wa mbuga wa kijani kibichi chini ya anga, akifurahia neema yote ya Mungu. Na ni kwa sababu ya ujio wa kijani kibichi ndiposa pumzi ya uhai inaangaza, kwani Mungu anakuja duniani kuishi pamoja na mwanadamu milele yote, kama ilivyosemwa kutoka kinywani mwa Mungu kwamba “Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena.” Hii ni ishara ya kushindwa kwa shetani, ni siku ya pumziko la Mungu, na siku hii itatukuzwa na kutangazwa na watu wote, na itafanyiwa kumbukumbu na watu wote. Wakati ambapo Mungu ametulia juu ya kiti cha enzi pia ndio wakati ambapo Mungu anahitimisha kazi Yake duniani, na ndio wakati ule ambao siri zote za Mungu zinaonyeshwa kwa mwanadamu; Mungu na mwanadamu watakuwa katika upatanifu daima, hawatakuwa mbali tena—haya ni mandhari mazuri ya ufalme!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 16” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1013 Mungu Hawaokoi Waovu

Inayofuata: 1015 Baraka Kuu Zaidi Ambayo Mungu Anaweka Juu Ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp