674 Yote Afanyayo Mungu ni Kumkamilisha na Kumpenda Mwanadamu

1 Tangu wakati wa watendaji huduma mpaka leo, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ni ya ajabu, haiwezi kueleweka kwa mwanadamu, na akitumia akili yake hawezi kufikiria jinsi Mungu hufanya kazi, na pia huona vile kimo chake ni kidogo na kwamba kiasi kikubwa chake ni cha kutotii. Mungu alipomlaani mwanadamu, ilikuwa ili Atimize athari, na Hakumuua mwanadamu. Ingawa Alimlaani mwanadamu, Alifanya hivyo kupitia maneno, na laana Zake hazikumwangukia mwanadamu kwa kweli, kwani kile ambacho Mungu alilaani kilikuwa kutotii kwa mwanadamu, na kwa hiyo maneno ya laana Zake pia yalikuwa kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Kama Mungu atamhukumu mwanadamu au kumlaani, yote mawili humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu: Yote mawili yanafanywa ili kukifanya kamili kile ambacho ni kichafu ndani ya mwanadamu.

2 Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu, na inafaa kwa uhalisi. Kotekote katika enzi zote Mungu hajawahi kufanya kazi kama hii; leo, Yeye hufanya kazi ndani yenu ili muweze kufahamu hekima Yake. Ingawa mmepitia maumivu fulani ndani yenu, mioyo yenu inajisikia thabiti na kwa amani; ni baraka yenu kuweza kufurahia hatua hii ya kazi ya Mungu. Haijalishi kile mnachoweza kupata katika siku za baadaye, yote mnayoona kuhusu kazi ya Mungu ndani yenu leo ni upendo.

3 Mungu kukushughulikia wewe ni ili kukuokoa, na ingawa unaweza kuhisi maumivu kidogo wakati huo, siku itafika ambapo kutatokea mabadiliko katika tabia yako. Wakati huo, utakumbuka ya nyuma na kuona vile kazi ya Mungu ni ya hekima, na huo utakuwa wakati ambao utaweza kufahamu kwa kweli mapenzi ya Mungu. Labda huwezi kuliona kwa dhahiri sasa, lakini siku itafika ambapo utaona kwamba siku ya kutukuzwa kwa Mungu imefika, na uone jinsi ni ya maana kumpenda Mungu, ili utakuja kuyajua maisha ya binadamu, na mwili wako utaishi katika ulimwengu wa kumpenda Mungu, kwamba roho yako itawekwa huru, maisha yako yatajaa furaha, na kwamba daima utakuwa karibu na Mungu, na utamtegemea Mungu daima. Wakati huo, utajua kweli jinsi kazi ya Mungu ni ya thamani leo.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 673 Maana ya Majaribio na Usafishaji wa Mungu wa Mwanadamu

Inayofuata: 675 Kusudi la Kazi ya Mungu ya Usafishaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp