253 Mungu Amengoja Kwa Muda Mrefu Sana

Kiambata: Ni nani anayeweza kusema umesubiri kwa muda gani mwanadamu akurudie? Nani anayeweza kusema ni gharama gani ya bidii Umelipa kwa ajili ya mwanadamu? Nani anayeweza kusema jinsi rehema Yako ilivyo kuu? Na nani anayeweza kufahamu jinsi moyo Wako ulivyo mzuri na mzuri?

1 Nilikuamini kwa miaka mingi sana lakini sikufuatilia ukweli. Ingawa nilionekana kukufuata, moyo wangu haukuwa Wako. Daima nilikudanganya katika sala, nilikusifu kwa maneno tu. Nilifurahi sana kwa kufanya kazi kidogo, nilijichukulia utukufu wote. Nilisimama mbele Yako lakini kamwe sikukujua Wewe, na kamwe sikujua ukweli au maisha. Nilijali tu kujiandaa na mafundisho, na kamwe sikutenda au kupitia maneno Yako. Nikielewa ujuzi wa barua na mafundisho, nilifikiria nilikuwa mkuu sana.

2 Upendo Wako ulinijia kimya kimya, Ulinikemea, ukanifunza nidhamu, kanipogoa na kunishughulikia. Hukumu ya maneno Yako ilifunua barakoa ya unafiki wangu. Sikuteseka na kujitumia kulipa upendo Wako, lakini kwa ajili ya mwisho wangu tu, hatima yangu ya mwisho. Niliona jinsi nilivyokuwa mpotovu kabisa, mdanganyifu na mwovu sana. Nilipofunuliwa katika majaribu, nilikuelewa vibaya, na nililia na kukata tamaa kwa uchungu. Sikuwahi kuthamini nia Zako nzuri. Sikuwa na dhamiri na mantiki. Nikiwa mwasi sana, ningewezaje kustahili kuitwa binadamu?

3 Upendo Wako ulikuwa kama upepo wa joto uliouyeyusha moyo wangu mgumu. Ingawa majaribu na usafishaji vilikuwa vichungu, vilikusudiwa kuutakasa upotovu wangu. Sasa kwa kuwa naelewa mapenzi Yako, moyo wangu unageuka na ninalia kwa majuto. Najichukia kwa kuwa mwasi na mjinga, na kwa kutotii mapenzi Yako. Lakini daima Unaangalia na kusubiri, Ukifanya kila uwezalo kuniokoa. Moyo Wako unapendeza na mzuri sana, natamani kufuatilia ukweli na kuingia katika uhalisi. Nimeamua kutenda kama binadamu, na kufanya wajibu wangu kuufariji moyo Wako.

Kiambata: Nimeona jinsi ulivyo mwema na wa kupendeka. Ni Wewe tu unayestahili upendo wa mwanadamu. Sitakufanya Usubiri zaidi, nitakupa moyo wangu wa kweli. Naomba tu kwamba moyo wangu ukupende, ili nisijute tena. Naomba tu kwamba moyo wangu ukupende, na kwamba nilingane na Wewe.

Iliyotangulia: 252 Nimefurahia Upendo Mwingi wa Mungu

Inayofuata: 254 Tunakuabudu, Mwenyezi Mungu Mwenye Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki