900 Mungu Amwokoa Mwanadamu kwa Kiwango cha Juu Zaidi

1 Mungu hakuja wakati huu ili kuwaangusha watu, lakini badala yake kuwaokoa watu kwa kiwango kikubwa kiwezekanacho. Je, ni nani asiyefanya makosa kabisa? Je, kila mtu akiangushwa, basi unawezaje kuitwa wokovu? Makosa mengine hufanywa kimakusudi na makosa mengine kufanywa bila kupenda. Kwa mambo ya bila kupenda, unaweza kubadilika baada ya kuyatambua, hivyo Mungu angekugonga kabla hujabadilika? Je, hivi ndivyo Mungu huwaokoa watu? Bila kujali iwapo unakosea bila kupenda ama kutokana na asili ya uasi, lazima ukumbuke: Harakisha na uuzindukie uhalisi. Endelea kwa bidii; bila kujali ni hali gani inayotokea, lazima uendelee kwa bidii.

2 Mungu anafanya kazi ili kuwaokoa watu na Hatawagonga watu Anaotaka kuwaokoa bila taratibu. Bila kujali kiasi chako cha mgeuzo, hata kama Mungu angekuangusha mwishowe, basi Mungu angefanya hivyo kwa uhaki; wakati huo utakapofika, Atakufanya uelewe. Sasa hivi jukumu lako la pekee ni kuendelea kwa bidii, kutafuta kubadilishwa na kutafuta kumridhisha Mungu; unapaswa kujali tu kuhusu kuutimiza wajibu wako kulingana na mapenzi ya Mungu. Hapana kosa katika hili! Mwishowe, bila kujali jinsi Mungu anavyokushughulikia, hilo daima hufanywa katika uhaki; hupaswi kushuku hili au kuwa na wasiwasi nalo; hata kama huwezi kuelewa uhaki wa Mungu hivi sasa, kutakuwa na siku ambayo utaridhishwa.

Umetoholewa kutoka katika “Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 899 Nia Ya Mungu ya Kumwokoa Mwanadamu Haitabadilika

Inayofuata: 901 Mradi tu Usimwache Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp