A. Mahitaji ya Mungu kwa Mwanadamu

605. Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza rasmi kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinavyotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kuna maana ya kuanza maisha ya watu wa Mungu—uko radhi kuyakubali mafunzo hayo? Uko radhi kuhisi hali ya uharaka? Uko radhi kuishi chini ya nidhamu ya Mungu? Uko radhi kuishi chini ya kuadibu kwa Mungu? Wakati ambapo maneno ya Mungu yatakujia na kukujaribu, utafanyaje? Na utafanya nini wakati ambapo utakabiliwa na kila aina ya ukweli? Zamani, umakini wako haukuwa kwenye maisha; leo, lazima uingie katika uhalisi wa maisha, na kufuatilia mabadiliko katika tabia yako ya maisha. Hili ndilo lazima litimizwe na watu wa ufalme. Wale wote ambao ni watu wa Mungu lazima wawe na uzima, lazima wakubali mafunzo ya ufalme, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Hili ndilo Mungu anahitaji kwa watu wa ufalme.

Masharti ya Mungu kwa watu wa ufalme ni kama yafuatayo:

1) Lazima wakubali maagizo ya Mungu, ambalo ni kusema, lazima wakubali maneno yote yaliyonenwa katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

2) Lazima waingie katika mafunzo ya ufalme.

3) Lazima wafuatilie kufanya mioyo yao iguswe na Mungu. Wakati ambapo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na una maisha ya kiroho ya kawaida, utaishi katika eneo la uhuru, ambalo lina maana kuwa utaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo wa Mungu. Ukiishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu tu ndipo utakuwa wa Mungu.

4) Lazima wapatwe na Mungu.

5) Lazima wawe dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani.

Haya mambo matano ni maagizo Yangu kwenu. Maneno Yangu yananenwa kwa watu wa Mungu, na kama hutaki kuyakubali maagizo haya, Sitakulazimisha—lakini ukiyakubali kwa kweli, basi utaweza kuyafanya mapenzi ya Mungu. Leo, anzeni kuyakubali maagizo ya Mungu, na kufuatilia kuwa watu wa ufalme na kufikia viwango vinavyohitajika kuwa watu wa ufalme. Hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia. Kama ungependa kufanya mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu, basi lazima uyakubali maagizo haya matano, na kama unaweza kuyatimiza, utaupendeza moyo wa Mungu na kwa hakika utatumiwa sana na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

606. Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo wa kudumu na usiopungua kwa Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la mwisho la kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili. Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu haipo bila sababu, na kutokana na hili inaonekana ni kwa nini Mungu kila mara hufanya kazi ya hali ya juu na yenye mahitaji makali. Ndiyo maana unafaa kujawa na imani katika Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu hufanywa kwa ajili yako, ili kwamba uweze kupokea urithi Wake. Hii sio kwa ajili ya utukufu wa Mungu bali ni kwa ajili ya wokovu wako na kufanya kundi hili la watu walioteswa na nchi najisi kuwa wakamilifu. Sharti uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo Nawahimiza wale wote wasiojua, wasio na hisia na ufahamu: Usimjaribu Mungu wala kumpinga tena. Mungu Ameshavumilia mateso yote ambayo mwanadamu hajaweza kupitia, na hapo awali Ameteseka na kudhihakiwa kwa niaba ya mwanadamu. Je, nini kingine ambacho huwezi kukiachilia? Je, ni nini muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu? Ni nini kinachoweza kuwa juu ya upendo wa Mungu? Tayari ni kazi ngumu maradufu kwa Mungu kutekeleza kazi Yake katika nchi hii chafu. Ikiwa mwanadamu anatenda dhambi kwa kujua na kwa makusudi, kazi ya Mungu itabidi kurefushwa. Katika tukio lolote, hili silo pendeleo la yeyote wala si la maana kwa yeyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?

607. Maneno Ninayozungumza ni ukweli unaoelekezwa kwa wanadamu wote, na wala hayajaelekezwa kwa mtu mahususi au aina fulani ya mtu. Kwa hiyo, mnapaswa kuzingatia kuyaelewa maneno Yangu kutoka katika mtazamo wa ukweli, na vile vile mdumishe mtazamo wa uangalifu na uaminifu kamili. Msipuuze hata neno moja au ukweli Ninaozungumza, na wala usiyachukulie maneno Yangu kwa dharau. Katika maisha yenu, Naona mengi ambayo mnafanya ambayo hayana uhusiano na ukweli, kwa hivyo Nawaambia kwa uwazi kwamba muwe watumishi wa ukweli, ili msiwe watumwa wa uovu na ubaya, na kwamba msiukanyage ukweli na kuchafua sehemu yoyote ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo onyo Langu kwenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

608. Natumai tu kwamba hamtapoteza juhudi Zangu zenye maumivu na zaidi ya hayo, kwamba mnaweza kuelewa utunzaji wote na fikira ambazo Nimetumia, mkiyachukulia maneno Yangu kama msingi wa jinsi mnavyotenda kama binadamu. Iwe ni maneno ambayo mko tayari kuyasikiliza au la, iwe ni maneno ambayo mnafurahia kuyakubali au mnayakubali bila raha, lazima muyachukulie kwa uzito. Vinginevyo, tabia na mienendo yenu ya kawaida na isiyojali itanifadhaisha sana na, hata zaidi, itanichukiza Mimi. Natumai sana kwamba nyote mnaweza kuyasoma maneno Yangu tena na tena—mara elfu kadhaa—na hata kuyakariri. Ni kwa njia hiyo tu ndiyo hamtayaacha matarajio Yangu kwenu. Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishi namna hiyo sasa. Badala yake, nyote mmezama katika maisha ya anasa ya kula na kunywa hadi kushiba, na hakuna yeyote kati yenu anayeyatumia maneno Yangu kuusitawisha moyo na nafsi yake. Kwa sababu hii Nimefikia hitimisho kuhusu uso wa kweli wa mwanadamu: Mwanadamu anaweza kunisaliti wakati wowote, na hakuna yeyote anayeweza kuwa mwaminifu kabisa kwa maneno Yangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)

609. Mungu anataka upendo mmoja wa mtu, naye humhitaji mtu amilikiwe na maneno Yake na upendo wa mtu Kwake. Kuishi ndani ya maneno ya Mungu, kugundua kile ambacho mtu anapaswa kutafuta kutoka ndani ya maneno Yake, kumpenda Mungu kama matokeo ya maneno Yake, kukimbia huku na huku kwa ajili ya maneno ya Mungu, kuishi kwa ajili ya maneno ya Mungu—haya yote ni mambo ambayo mtu anapaswa kufikia. Kila kitu lazima kijengwe kulingana na maneno ya Mungu, na hapo tu ndipo mtu ataweza kukidhi matakwa ya Mungu. Kama mwanadamu hajatayarishwa na maneno ya Mungu, basi yeye ni funza tu ambaye amemilikiwa na Shetani. Yapime moyoni mwako mwenyewe—ni maneno mangapi ya Mungu ambayo umekita mizizi yake ndani yako? Ni katika mambo gani unaishi kulingana na maneno Yake? Ni katika mambo gani ndiyo hujakuwa ukiishi kulingana nayo? Kama maneno ya Mungu hayajakumiliki kikamilifu, basi ni nini hasa kilicho moyoni mwako? Katika maisha yako ya kila siku, je, unadhibitiwa na Shetani, au unamilikiwa na maneno ya Mungu? Je, maombi yako yameanzishwa kutoka kwa maneno Yake? Je, umeondoka katika hali yako mbaya kupitia nuru ya maneno ya Mungu? Kuchukua maneno ya Mungu kama msingi wa kuwepo kwako, hili ndio jambo kila mtu anapaswa kuingia ndani. Kama maneno ya Mungu hayapo katika maisha yako, basi unaishi chini ya ushawishi wa giza, wewe ni muasi dhidi ya Mungu, unampinga Mungu, na huheshimu jina Lake—imani ya watu kama hao katika Mungu ni uharibifu na usumbufu kabisa. Je, ni kiasi gani cha maisha yako kimeishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Ni kiasi gani cha maisha yako hakijaishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Je, ni kiasi gani cha kile ambacho maneno ya Mungu yamehitaji kwako kimetimizwa ndani yako? Ni mangapi yamepotea ndani yako? Je, umechunguza mambo kama hayo kwa karibu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

610. Je, mnayo nia ya kustarehe katika baraka Zangu duniani, baraka zilizo sawa na zile za mbinguni? Je, mko tayari kushughulikia ufahamu wa Mimi, na kufurahia maneno Yangu na ufahamu wako kunihusu, kama vitu vya thamani zaidi na vya maana katika maisha yenu? Je, kweli mnaweza kuwa watiifu Kwangu kikamilifu, bila fikira kwa matarajio yenu wenyewe? Je, kweli mna uwezo wa kujiruhusu kuuwawa na Mimi, na kuongozwa na Mimi, kama kondoo? Je, kunao kati yenu walio na uwezo wa kutimiza vitu kama hivi? Inawezekana kuwa wote wanaokubaliwa na Mimi na kupokea ahadi Zangu ndio wanaopokea baraka Zangu? Je, mmeelewa chochote kutoka katika maneno haya? Nikiwajaribu, je, mnaweza kweli kujiweka wenyewe katika huruma Yangu, na, katikati ya majaribu haya, mtafute nia Yangu na muelewe moyo Wangu? Mimi sitamani wewe uweze kuongea maneno mengi matamu, au utoe hadithi nyingi za kufurahisha; badala yake Ninauliza kuwa uweze kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu, na kwamba unaweza kuingia kikamilifu na kwa kina katika hali halisi. Kama Singezungumza moja kwa moja, je, ungeacha kila kitu kilicho karibu na wewe na ukubali kutumiwa na Mimi? Je, hii siyo hali halisi Ninayohitaji? Je, ni nani aliye na uwezo wa kuelewa maana iliyo katika maneno Yangu? Lakini bado Ninaomba kwamba msilemewe tena na mashaka, kwamba muwe waangalifu katika kuingia kwenu na kufahamu kiini cha maneno Yangu. Hii itazuia hali ya nyinyi kutoelewa maneno Yangu, na hali ya kutokuwa na uwazi kuhusu maana Yangu, na hivyo kukiuka amri Zangu za utawala. Natumaini kuwa mtaelewa Nia Yangu kwenu katika maneno Yangu. Msifikiri juu ya matarajio yenu tena, na mtende vile ambavyo mmeamua mbele Yangu kutii mipango ya Mungu katika kila kitu. Wale wote wanaosimama miongoni mwa kaya Yangu wanapaswa kufanya mengi kiasi wanachoweza; unafaa utoe hali yako bora zaidi kwa sehemu ya mwisho ya kazi Yangu duniani. Je, unayo nia ya kuviweka vitu vya aina hii katika matendo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 4

611. Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani, walinde lango la nyumba Yangu kwa ajili Yangu, waweze kusaidiana na kupeana mahitaji, kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati itakuwa ni kuchelewa sana kwa majuto. Kwa nini Ninawafunza kwa uharaka huo? Kwa nini Ninawaambia ukweli wa ulimwengu wa kiroho? Kwa nini Ninawakumbusha na kuwaonya mara kwa mara? Je, mmewahi kufikiri juu ya hili? Je, mmewahi kulielewa? Hivyo, hamhitaji tu kuweza kuwa wazoefu kwa kutegemeza juu ya msingi wa zamani, bali, zaidi, kuondoa uchafu ndani yenu chini ya uongozi wa maneno ya leo, mkiruhusu kila maneno Yangu kukita mzizi na kustawi ndani ya roho zenu, na muhimu zaidi, kuzaa matunda zaidi. Hiyo ni kwa sababu kile Ninachokiomba si maua angavu yaliyostawi sana, bali matunda mengi—matunda, zaidi ya hayo, ambayo hayaharibiki. Je, mnaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu? Ijapokuwa maua katika chumba cha kuhifadhia mimea hayahesabiki kama nyota, na huwavutia watalii wote, mara tu yanaponyauka, yanachanika kama njama za udanganyifu za Shetani, na hakuna anayeonyesha kupendezwa nayo. Lakini kwa wale ambao wamerushwa na upepo na kuchomwa na jua na kuwa na ushuhuda Kwangu, ingawa maua haya si mazuri, mara yanaponyauka, hapo panatokea tunda, maana haya ndiyo matakwa Yangu. Ninapozungumza maneno haya, mnaelewa kiwango kipi? Mara maua yanaponyauka na kuzaa matunda, na mara matunda haya yote yanaweza kutolewa kwa ajili ya furaha Yangu, Nitakamilisha kazi Yangu yote duniani, na Nitaanza kufurahia udhihirisho wa hekima Yangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 3

612. Watu ambao wamemwamini Mungu kwa muda mrefu sasa wametumainia hatima iliyo nzuri, watu wote ambao wanamwamini Mungu wanatumai kwamba bahati nzuri itawajia kwa ghafla, na wote wanatumai kwamba bila kujua, watajikuta wameketi kwa amani sehemu moja au nyingine kule mbinguni. Lakini Ninasema kwamba watu hawa, pamoja na mawazo yao mazuri hawajawahi kujua kama wana sifa ya kupokea bahati nzuri kama hiyo inayoanguka kutoka mbinguni, au kukaa juu ya kiti huko mbinguni. Kwa sasa ninyi mna maarifa mazuri kujihusu, lakini bado mnatarajia kwamba mnaweza kuepuka maafa ya siku za mwisho na mkono wa Mwenyezi anapowaadhibu wale waovu. Inaonekana kana kwamba kuwa na ndoto tamu na kutaka vitu kama tu wanavyopenda ni sifa ya kawaida ya watu wote ambao Shetani amewapotosha, na sio fikra ya mtu fulani binafsi. Hata hivyo, bado Nataka kukomesha tamaa zenu badhirifu na hamu zenu za kupata baraka. Kwa kuwa dhambi zenu ni nyingi na ukweli wa kutotii kwenu ni mwingi na unaongezeka kila wakati, haya yanawezaje kupatana na mipango yenu mizuri ya baadaye? Kama unataka kuendelea unavyopenda kuwa mwenye makosa, bila chochote kinachokuzuia, lakini bado unataka ndoto zitimie, basi Nakusihi uendelee katika usingizi wako na usiamke kamwe, kwa sababu unaota ndoto isiyoweza kutimia, na haitatumika kukufanya upate upendeleo mbele za Mungu mwenye haki. Kama unataka tu ndoto zitimie, basi usiote kamwe, lakini kabiliana na ukweli milele, kabiliana na mambo ya hakika. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuokoa. Je, kwa maneno thabiti, hatua za mbinu hii ni zipi?

Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na uchunguze tabia na mawazo yako yote ambayo hayafuati ukweli.

Hiki ni kitu ambacho mnaweza kukifanya kwa urahisi, na Ninaamini kwamba watu wote wenye akili wanaweza kufanya hivi. Hata hivyo, wale watu ambao hawajui kamwe kile kinachomaanishwa kuwa ni dhambi na ukweli ni tofauti, ni kwa sababu kwa kiwango cha chini, wao si watu wenye akili. Ninazungumza na watu ambao wameidhinishwa na Mungu, ambao ni waaminifu, hawajakiuka kwa uzito amri zozote za kiutawala, na wanaweza kutambua dhambi zao wenyewe kwa urahisi. Ingawa hiki ni kipengele kimoja ambacho Ninahitaji kutoka kwenu ambacho ni rahisi kwenu, sicho kipengele cha pekee Ninachohitaji kutoka kwenu. Haijalishi ni nini, Ninatumai kwamba hamtalicheka hitaji hili kwa siri, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kimzaha. Lichukulieni kwa umakini, na msilipuuze.

Pili, kwa kila moja ya dhambi na kutotii kwako unapaswa kutafuta ukweli unaolingana, na kisha uutumie ukweli huu kutatua masuala hayo. Baada ya hayo, badilisha matendo yako ya dhambi na mawazo yako na vitendo vya kutotii kwa kutenda ukweli.

Tatu, unapaswa kuwa mtu mwaminifu, si mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, na usiwe mtu mdanganyifu daima. (Hapa Ninakusihi tena uwe mtu mwaminifu.)

Kama unaweza kutimiza vipengele hivi vyote vitatu basi una bahati, wewe ni mtu ambaye ndoto zako zinatimia na ambaye umepata bahati nzuri. Labda mtayachukulia mahitaji haya matatu yasiyovutia kwa umakini, au labda mtayachukulia kwa uzembe. Kwa vyovyote vile, nia Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka mawazo yenu katika matendo, si kuwafanyia mzaha au kuwadanganya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

613. Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu. Kama kila mojawapo ya mazungumzo ambayo Nimekuwa nayo pamoja nanyi hayajatosha kuvuta umakini wenu, basi huenda Sitasema mengine. Hata hivyo, nyinyi mnaelewa matokeo ya hayo. Sipumziki kamwe, kwa hiyo Nisiponena, Nitafanya kitu ili watu wakitazame. Ninaweza kuufanya ulimi wa mtu uoze, au mtu afe na viungo vyake vitolewe, au kumpa mtu kasoro za neva na kumfanya atende kama mwendawazimu. Au, hata tena, Ninaweza kuwafanya baadhi ya watu wavumilie maumivu makali Ninayowasababishia. Kwa njia hii Ningejihisi mwenye furaha, mwenye furaha sana na kuridhika sana. Imesemwa daima kwamba “Mema hulipizwa kwa mema, na maovu kwa maovu,” mbona isiwe hivyo sasa? Kama unataka kunipinga Mimi na unataka kutoa hukumu fulani kunihusu, basi Nitauozesha mdomo wako, na hilo litanipendeza Mimi sana. Hii ni kwa sababu mwishowe hujafanya lolote linalohusiana na ukweli, sembuse na maisha, ilhali kila kitu Ninachofanya ni ukweli, kila kitu kinahusiana na kanuni za kazi Yangu na amri za utawala Nilizoweka rasmi. Kwa hiyo, Namsihi sana kila mmoja wenu ajikusanyie matendo mema kiasi, acheni kufanya maovu mengi sana, na mtii matakwa Yangu katika wakati wenu wa bure. Kisha Nitajihisi furaha. Kama mngetoa (au kuchangia) katika ukweli mara elfu mojaya juhudi mnazoweka katika mwili, basi Nasema hungekuwa na dhambi za mara kwa mara na midomo mibovu. Je, hili si dhahiri?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

614. Kama mmoja wa wanadamu walioumbwa, lazima ushikilie nafasi yako inayofaa, na ujiendeshe kwa adabu. Shikilia kwa uwajibikaji kile ulichokabidhiwa na Muumba. Usivuke mipaka, au kufanya mambo yaliyo nje ya upeo wa uwezo wako au ambayo yanamchukiza Mungu. Usifuatilie kuwa mtu mkuu, mtu mwenye uwezo upitao wa kibinadamu, au mtu adhimu sana, na usifuatilie kuwa Mungu. Yote haya ni matamanio ambayo watu hawapaswi kuwa nayo. Kufuatilia kuwa mtu mkuu au mtu mwenye uwezo upitao wa kibinadamu ni upuuzi. Kufuatilia kuwa Mungu ni jambo la aibu zaidi; ni jambo la kuchukiza, na la kudharauliwa. Kilicho cha thamani kweli, na kile ambacho viumbe walioumbwa wanapaswa kushikilia kuliko kitu kingine chochote, ni kuwa kiumbe aliyeumbwa wa kweli; hili ndilo lengo pekee ambalo watu wote wanapaswa kufuatilia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

615. Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na yenye uaminifu, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, siku itakapowadia, Mungu hatakosa kumjali mtu yeyote ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni kwa njia hii tu Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa walengwa wa chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, mkitoa juhudi zote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutoa juhudi za maisha yote kwa ajili ya kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

616. Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayofaa na inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo? Je, wewe unayepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho unaweza kueleza tabia ya Mungu yenye haki kwa utondoti? Je, unaweza kuishuhudia tabia ya Mungu kwa uwazi na usahihi? Je, utasimulia vipi yale uliyoyaona na kuyapitia kwa wale waumini wa kidini wenye kusikitisha, waliopungukiwa, na wenye uchaji wa dhati ambao wana njaa na kiu ya haki na wanakungoja wewe uwachunge? Ni watu wa aina gani ndio wanaokungoja wewe uwachunge? Unaweza kuwaza kweli? Je, unafahamu mzigo ulio mabegani mwako, agizo lako, na jukumu lako? Hisia yako ya misheni ya kihistoria iko wapi? Utatumikiaje ipasavyo kama bwana wa enzi ijayo? Je, una hisia thabiti ya kuwa bwana? Bwana wa vitu vyote anapaswa kuelezwaje? Je, kwa kweli ni bwana wa viumbe hai wote na vitu vyote vya kimwili ulimwenguni? Una mipango gani ya maendeleo ya awamu inayofuata ya kazi? Ni watu wangapi wanaokungoja wewe uwachunge? Je, kazi yako ni nzito? Wao ni waliopungukiwa, wa kusikitisha, vipofu, na waliochanganyikiwa, wakilomboleza gizani—njia iko wapi? Jinsi wanavyotamani nuru, kama kimondo, ishuke ghafla na kutawanya nguvu za giza ambazo zimemkandamiza mwanadamu kwa miaka mingi. Wanatumaini kwa hamu, na kutamani, mchana na usiku—ni nani anayeweza kujua hili kikamilifu? Hata siku ambayo nuru inapita kwa kasi, watu hawa wanaoteseka sana hubaki wamefungwa katika gereza la giza bila tumaini la kuachiliwa; kulia kwao kutakoma lini? Ni bahati mbaya iliyoje ya roho hizi dhaifu ambazo hazijawahi kupata pumziko, na kwa muda mrefu zimefungwa katika hali hii kwa minyororo isiyo na huruma na historia iliyoganda. Na ni nani amesikia sauti ya kilio chao? Ni nani aliyeona hali yao ya kuhuzunisha? Je, umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyo na huzuni na wasiwasi? Anaweza kuvumiliaje kuwaona wanadamu wasio na hatia, ambao Yeye aliwaumba kwa mikono Yake Mwenyewe, wakiteseka mateso kama hayo? Wanadamu, baada ya yote, ndio wahasiriwa ambao wametiwa sumu. Na ingawa mwanadamu ameendelea kuishi hadi leo, ni nani angejua kwamba wanadamu kwa muda mrefu wametiwa sumu na yule mwovu? Je, umesahau kwamba wewe ni mmoja wa wahasiriwa? Je, huna nia ya kujitahidi, kwa sababu ya upendo wako kwa Mungu, kuwaokoa wasaliaji hawa wote? Je, huna nia ya kutoa nguvu zako zote ili kumlipa Mungu, anayewapenda wanadamu kama mwili Wake Mwenyewe? Unaelewaje hasa kuhusu kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, kweli una azimio na imani ya kuishi maisha ya maana ya mtu mwenye kujitoa, anayemtumikia Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

617. Wewe ni kiumbe aliyeumbwa—unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu lakini unaishi ndani ya mwili wako mchafu, basi wewe si mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kwa kuwa wewe ni binadamu, unapaswa kujitumia kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso! Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu na Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kutoka kwa ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya uelekezi wa Shetani, na kukanyagiwa kabisa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au kupata njia ya kweli, basi kuna umuhimu gani katika kuishi kwa namna hii? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale mnaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (2)

618. Mnapaswa kutafuta kufanya vyote muwezavyo kumpenda Mungu katika mazingira haya yenye amani. Katika siku za baadaye hamtakuwa na nafasi zaidi za kumpenda Mungu, kwani watu huwa tu na nafasi ya kumpenda Mungu katika mwili; wanapoishi katika ulimwengu mwingine, hakuna atakayenena kuhusu kumpenda Mungu. Je, hili si jukumu la kiumbe aliyeumbwa? Kwa hiyo unapaswa kumpenda Mungu vipi katika siku zako za uhai? Umeshawahi kufikiri juu ya hili? Je, unangoja mpaka ufe ili umpende Mungu? Je, haya si maneno matupu? Leo, kwa nini hufuatilii kumpenda Mungu? Je, kumpenda Mungu huku ukiwa na shughuli nyingi kunaweza kuwa upendo halisi kwa Mungu? Madhumuni ya kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu itafika mwisho hivi punde ni kwa sababu Mungu tayari ana ushuhuda mbele ya Shetani; hivyo, hakuna haja ya mwanadamu kufanya chochote, mwanadamu anatakiwa tu kufuatilia kumpenda Mungu katika miaka ambayo yuko hai—hili ndilo jambo muhimu. Kwa sababu masharti ya Mungu si mengi, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa kuna hamu kuu ndani ya moyo Wake, Amefichua muhtasari wa hatua inayofuata ya kazi kabla ya hatua hii ya kazi kumalizika, ambalo linaonyesha kwa dhahiri kuna kiasi gani cha muda: kama Mungu hangekuwa na hamu ndani ya moyo Wake, je, Angeyanena maneno haya mapema hivyo? Ni kwa sababu muda ni mfupi ndio maana Mungu anafanya kazi kwa njia hii. Inatarajiwa kwamba mnaweza kumpenda Mungu kwa mioyo yenu yote, kwa akili zenu zote, na kwa nguvu zenu zote, jinsi tu mnavyotunza maisha yenu wenyewe. Je, haya siyo maisha yenye maana kuu zaidi? Ni wapi pengine ambapo mngeweza kupata maana ya maisha? Je, ninyi si vipofu kabisa? Je, uko tayari kumpenda Mungu? Je, Mungu anastahili kupendwa na mwanadamu? Je, watu wanastahili kuabudiwa na mwanadamu? Kwa hiyo, unapaswa kufanya nini? Mpende Mungu kwa ujasiri, bila kusita, na uone kile ambacho Mungu atakufanyia. Uone kama atakufisha. Kwa muhtasari, kazi ya kumpenda Mungu ni muhimu zaidi kuliko kunukuu na kuandika mambo kwa ajili ya Mungu. Unapaswa kukipa kipaumbele kilicho muhimu zaidi, ili maisha yako yaweze kuwa ya thamani zaidi na yajae furaha, na kisha unapaswa kusubiri “hukumu” ya Mungu kwako. Nashangaa iwapo mpango wako utahusisha kumpenda—Ningependa kwamba mipango ya watu wote iwe ile inayokamilishwa na Mungu, na iwe ya uhalisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 42

619. Mwanadamu lazima azingatie kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na hapaswi kuridhika na hali yake ya sasa. Kuishi kama mfano wa Petro, lazima awe na maarifa na uzoefu wa Petro. Mtu lazima ashikilie mambo ambayo ni ya juu na zaidi ya yaliyo makuu. Ni lazima yeye afuatilie kwa ndani zaidi, usafi zaidi wa upendo wa Mungu, na maisha ambayo yana thamani na umuhimu. Haya tu ndiyo maisha; hivi tu ndivyo mwanadamu atakuwa sawa na Petro. Lazima kuzingatia kuwa makini kwa kuingia kwako kwa upande chanya, na lazima uhakikishe kwamba haurudi nyuma kwa ajili ya urahisi wa kitambo na kupuuza mambo mengine makubwa, zaidi maalum, na zaidi kwa ukweli wa vitendo. Upendo wako lazima uwe wa vitendo, na lazima utafute njia ya kujitoa katika upotovu huu, maisha yasiyo na kujali ambayo hayana tofauti na ya mnyama. Lazima uishi maisha ya maana, maisha ya thamani, na usijipumbaze, au kufanya maisha yako kama kitu cha kuchezea. Kwa kila mtu ambaye anatumai kumpenda Mungu, hakuna ukweli usioweza kupatikana, na hakuna haki wasioweza kusimama imara nayo. Unafaa kuishije maisha Yako? Unapaswa kumpenda Mungu vipi na kutumia upendo huu ili kukidhi hamu Yake? Hakuna jambo kubwa zaidi katika maisha Yako. Zaidi ya yote, lazima uwe na matarajio hayo na uvumilivu, na hupaswi kuwa kama wanyonge wasio na nia. Lazima ujifunze jinsi ya kupitia maisha ya maana, na kuuona ukweli wa maana, na hupaswi kujichukua kipurukushani katika njia hiyo. Bila wewe kujua, maisha Yako yatakupita tu; na baada ya hapo, je utakuwa una fursa nyingine ya kumpenda Mungu? Je, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu baada ya kufa? Lazima uwe na matarajio na dhamiri sawa na ya Petro; maisha Yako ni lazima yawe na maana, na usifanye mchezo na nafsi yako. Kama mwanadamu, na kama mtu ambaye anamfuata Mungu, ni lazima uweze kufikiria na kuyachukulia maisha yako kwa makini—ukizingatia jinsi unavyopaswa kujitoa mwenyewe kwa Mungu, jinsi unapaswa kuwa na imani yenye maana zaidi katika Mungu, na jinsi, kwa kuwa wewe unampenda Mungu, unapaswa kumpenda Yeye kwa njia ambayo ni safi zaidi, nzuri zaidi, na bora zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

620. Mahitaji sahihi ya Mungu kwa wanadamu na wale ambao wanamfuata ni kama ifuatavyo. Mungu anahitaji mambo matano kutoka kwa wale wanaomfuata; imani ya kweli, ufuasi wenye uaminifu, utiifu kamili, ufahamu wa kweli na heshima za kutoka moyoni.

Katika mambo haya matano, Mungu anahitaji kuwa watu wasimshuku tena, wala kumfuata wakitumia fikira zao au mitazamo isiyoeleweka na iliyo dhahania; Ni lazima wamfuate Mungu bila fikira au dhana zozote. Mungu anahitaji kuwa wote wanaomfuata wafanye hivyo kwa uaminifu, sio kwa shingo upande au bila kujizatiti. Mungu anapokupa mahitaji yoyote, au kukujaribu, kukuhukumu, kukushughulikia na kukupogoa, au kukuadhibu na kukuangamiza, unapaswa kuwa mtiifu kabisa Kwake. Hufai kuuliza kilichosababisha, au kuweka masharti, au hata uongee kuhusu sababu. Utiifu wako lazima uwe usio na shaka. Maarifa ya Mungu ni kipengele ambacho watu wengi wanakosea. Mara kwa mara wanamlazimishia Mungu misemo, matamshi, na maneno ambayo hayahusiani na Yeye, wakiamini kuwa haya maneno ndiyo ya kweli kuhusu kumfahamu Mungu. Kumbe hawajui kuwa hii misemo, ambayo inatoka kwa fikira za watu, ung’amuzi wao, na busara zao, havina uhusiano wowote na kiini cha Mungu. Na kwa hiyo, Ninataka kukwambia kuwa, katika ufahamu wa watu unaotamaniwa na Mungu, Mungu haulizi tu kwamba umtambue Mungu na maneno Yake, lakini kuwa ufahamu wako juu ya Mungu ni sahihi. Hata kama unaweza kusema sentensi moja tu, au una ufahamu mdogo tu, huu ufahamu mdogo ni sahihi na wa kweli, na unalingana na kiini cha Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hapendi sifa na wao kumtukuza Yeye kwa hali isiyo halisi na yenye nia mbaya. Zaidi ya hayo, Anachukia watu wanapomchukulia kama hewa. Anachukia ambapo, wakati wa majadiliano juu ya mada kuhusu Mungu, watu wanazungumza kimzaha, wakiongea kwa hiari bila ya kujali, wakiongea wapendavyo; zaidi ya hayo, anawachukia wale wanaojifanya wanamjua Mungu, na wanaringa kuhusu ufahamu wa Mungu, wakijadili mada kuhusu Mungu bila mipaka au kipimo. La mwisho Kati ya yale mahitaji matano lilikuwa ni kumheshimu Mungu kutoka moyoni. Hili ndilo hitaji kuu la Mungu kwa wale wote wanaomfuata. Wakati mtu ana ufahamu wa kweli na sahihi kumhusu Mungu, anaweza kumheshimu Mungu na kuepuka maovu. Heshima hii hutoka ndani ya moyo wake, ni ya hiari, na sio kwa sababu Mungu amemshurutisha. Mungu hataki utoe zawadi ya mwelekeo wowote wa kupendeza, au tabia, au mienendo ya nje Kwake; badala yake, anataka kwamba umheshimu na umwogope kutoka ndani ya moyo wako. Heshima hii inaafikiwa kutokana na mabadiliko katika tabia ya maisha yako, kwa sababu una ufahamu juu ya Mungu, kwa sababu unaelewa matendo ya Mungu, kwa sababu ya uelewa wako wa kiini cha Mungu, na kwa sababu umetambua ukweli kuwa wewe ni mmoja wa viumbe wa Mungu. Na kwa hiyo, nia yangu ya kutumia neno “kutoka moyoni” kwa kurejelea heshima hapa ni kwamba wanadamu waelewe kuwa heshima ya watu kwa Mungu inapaswa kutoka ndani ya mioyo yao.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

621. Nyote mnapaswa sasa kujichunguza haraka iwezekanavyo, ili muone ni kiasi gani cha usaliti wenu Kwangu umebaki ndani yenu. Ninangojea kwa shauku jibu lenu. Msiwe wazembe katika kushughulika na Mimi. Kamwe Mimi huwa sichezi michezo na watu. Nikisema Nitafanya jambo basi kwa hakika Nitalifanya. Natumai kila mmoja wenu ataweza kuwa mtu ambaye anayachukulia maneno Yangu kwa uzito, na asifikirie ni kana kwamba maneno hayo ni ubunifu wa kisayansi. Kile Ninachotaka ni matendo ya wazi kutoka kwenu, siyo mawazo yenu. Kisha, ni lazima myajibu maswali Yangu, ambayo ni kama yafuatavyo:

1) Ikiwa kwa kweli wewe ni mtendaji huduma, je, unaweza kutoa huduma Kwangu kwa uaminifu, bila dalili yoyote ya uzembe au mtazamo hasi?

2) Je, ukigundua kuwa Sijawahi kukuthamini, bado utaweza kusalia na kunitolea huduma kwa maisha yako?

3) Ikiwa bado Sifanyi chochote kwako licha ya wewe kutumia bidii nyingi, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika hali ya mashaka?

4) Ikiwa, baada ya wewe kujitumia kwa ajili Yangu, Siyaridhishi mahitaji yako madogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi, au hata ukasirike na kunitukana kwa sauti kubwa?

5) Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana, ukinipenda sana, lakini bado unateseka na ugonjwa, umaskini, na kutengwa na marafiki na jamaa zako, au ikiwa unavumilia taabu nyingine zozote maishani, je, bado uaminifu na upendo wako Kwangu utaendelea?

6) Ikiwa hakuna lolote kati ya yale ambayo umefikiria moyoni mwako linalingana na kile ambacho Nimefanya, je, utaitembea vipinjia yako ya baadaye?

7) Ikiwa hupokei chochote kati ya mambo ambayo ulitarajia kupokea, je, unaweza kuendelea kuwa mfuasi Wangu?

8) Ikiwa hujawahi kuelewa dhumuni na umuhimu wa kazi Yangu, je, unaweza kuwa mtu mtiifu ambaye hatoi hukumu kiholela na kufanya maamuzi?

9) Je, unaweza kuthamini maneno yote ambayo Nimeyanena na kazi yote ambayo Nimeifanya wakati Nimekuwa pamoja na wanadamu?

10) Je, unaweza kuwa mfuasi Wangu mwaminifu, aliye tayari kuvumilia mateso ya maisha kwa ajili Yangu, ingawa hupokei chochote?

11) Kwa ajili Yangu, je, unaweza kuacha kufikiria, kupanga, au kutayarisha njia yako ya baadaye ya kuishi?

Maswali haya yanawakilisha mahitaji Yangu ya mwisho Ninayotaka kutoka kwenu, nami Natumai kuwa ninyi nyote mnaweza kunipa majibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

622. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwingine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili katika wakati ujao na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, lazima bado Nikuambie: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

Iliyotangulia: XIII. Maneno Juu ya Mahitaji, Ushawishi, Maliwazo na Maonyo ya Mungu

Inayofuata: B. Kushawishi kwa Mungu wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp