850 Uhalisi na Uzuri wa Mungu
“Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha,” Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa.
1 Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake. Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye.
2 Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika. Badala ya kujiweka Yeye Mwenyewe katika cheo cha juu na cha utukufu, Mungu mwenyewe alitumia ngozi kutengeneza nguo za binadamu. Kitu hiki kinaweza kuwa rahisi ambacho baadhi huenda hata wasifikirie kwamba kinastahili kutajwa, lakini kinawaruhusu pia wale wote wanaomfuata Mungu lakini awali walikuwa na mawazo yasiyoeleweka kuhusu Yeye kuweza kupata maono kuhusu ukweli na uzuri Wake, na kuuona uaminifu Wake na asili Yake ya unyenyekevu.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili