1017 Ahadi ya Mwisho ya Mungu kwa Binadamu

1 Wakati mtu anafanikiwa kupata maisha ya ukweli ya mwanadamu duniani na vikosi vizima vya Shetani vimefungwa, mwanadamu ataishi kwa urahisi katika ardhi. Mambo hayatakuwa magumu kama yalivyo sasa: Mahusiano ya binadamu, mahusiano ya kijamii, mahusiano changamani ya kifamilia…., haya ni ya kusumbua, machungu mno! Maisha ya mwanadamu hapa ni duni! Punde tu mwanadamu anaposhindwa, moyo wake na akili yake vitabadilika: atakuwa na moyo unaomcha Mungu na moyo ambao unampenda Mungu. Punde tu wote walio ulimwenguni ambao wanatafuta upendo wa Mungu wanaposhindwa, ambayo ni kusema, punde tu Shetani anaposhindwa, na punde tu Shetani—nguvu zote za giza—zimekwisha fungwa, basi maisha ya mwanadamu duniani yatakuwa yasiyotaabishwa, na ataweza kuishi huru duniani.

2 Kama maisha ya mwanadamu hayana mahusiano ya kimwili, na hayana changamani za mwili, basi itakuwa rahisi mno. Mahusiano ya kimwili ya mwanadamu ni changamani mno, na kwa mwanadamu kuwa na mambo kama hayo ni thibitisho kuwa yeye bado hajajikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa ndugu na dada, kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa wanafamilia wako, basi hungekuwa na wasiwasi, na hungekuwa na haja ya kuhofia kuhusu mtu yeyote. Hakuna kitakachoweza kuwa bora zaidi, na kwa njia hii mwanadamu atapunguziwa nusu ya mateso yake. Kuishi maisha ya kawaida ya binadamu duniani, mwanadamu atakuwa sawa na malaika; ingawa atakuwa bado na mwili, atakuwa sawa na malaika. Hii ni ahadi ya mwisho, ni ahadi ya mwisho ambayo mwanadamu amezawadiwa.

Umetoholewa kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1016 Ufalme Unapokuja Kikamilifu

Inayofuata: 1018 Ishara za Ushindi wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp