958 Kanuni za Mungu za Kutenda Hazibadiliki

Mungu ni Mwangalifu na Anawajibika katika kushughulikia Kwake, njia Zake, usimamizi, uongozi, na utawala wa kila chombo, mtu, na kiumbe hai miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba, na Hajawahi kuwa mzembe katika hili.

1 Yeye ni mwenye neema na mkarimu kwa wale walio wazuri; Kwa wale waovu, Anawapa adhabu bila huruma; na kwa viumbe hai mbalimbali, Anafanya mipango ifaayo kwa wakati na kwa njia ya kawaida kulingana na mahitaji mbalimbali ya ulimwengu wa wanadamu katika nyakati mbalimbali, kiasi kwamba hawa viumbe hai mbalimbali wanapata miili kulingana na nafasi wanayochukua kwa njia ya utaratibu, na kuhama kati ya ulimwengu yakinifu na ulimwengu wa kiroho kwa njia ya utaratibu. Iwe ni katika ulimwengu wa kiroho au ulimwengu yakinifu, kanuni ambazo Mungu hutekeleza matendo hazibadiliki. Bila kujali kama unaweza kuona matendo ya Mungu au la, kanuni zao hazibadiliki. Daima, Mungu amekuwa na kanuni sawa kwa jinsi Anavyotekeleza matendo kwa vitu vyote na kuvishughulikia vitu vyote. Hili halibadiliki.

2 Mungu atakuwa mkarimu kwa wale walio miongoni mwa wasioamini ambao angalau wanaishi ipasavyo, na kuwapa nafasi wale walio katika kila dini ambao wana tabia nzuri na hawatendi maovu, kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao katika vitu vyote vinavyosimamiwa na Mungu, na kufanya kile ambacho wanafaa kufanya. Vivyo hivyo, kati ya wale wanaomfuata Mungu, kati ya wateule Wake, Mungu habagui mtu yeyote kulingana na kanuni Zake hizi. Ni mwema kwa kila mtu anayeweza kumfuata kwa dhati, na kupenda kila mtu anayemfuata kwa dhati. Ni kwamba tu kwa aina hizi mbalimbali za watu—wasioamini, aina tofauti za watu wenye imani, na wateule wa Mungu—anachowazawadia wao ni tofauti.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 957 Mungu Atumai Mwanadamu Atubu kwa Kweli

Inayofuata: 959 Matokeo ya Kukera Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp