763 Upendo wa Mungu Lazima Uonjwe Katika Maisha Halisi

1 Ukitaka kuona upendo wa Mungu, ukitaka kwa kweli kupitia katika upendo wa Mungu, hivyo ni lazima uzame katika uhalisi, ni lazima uzame katika maisha halisi, na kuona kwamba kila kitu afanyacho Mungu ni upendo, na wokovu, na kwamba watu waweze kuacha kile ambacho si safi, na kwa ajili ya kusafisha mambo ndani yao ambayo hayana uwezo wa kuridhisha mapenzi ya Mungu.

2 Mungu hutumia maneno kumkimu mwanadamu na wakati huo huo kutengeneza mazingira katika maisha halisi ambayo huwaruhusu watu kupitia. Ikiwa, kwa kutumia nuru na uelekezaji wa maneno ya Mungu, unaomba mara kwa mara, na kuchunguza, na kutafuta, ambayo kwayo unagundua kile unachofaa kuweka katika vitendo, kutafuta fursa ya Kazi ya Roho Mtakatifu, unashirikiana na Mungu kwa kweli, na huvurugiki na kuchanganyikiwa, basi utakuwa na njia katika maisha halisi, na kumridhisha Mungu kwa kweli.

3 Ukimridhisha Mungu, ndani yako kutakuwa na uelekezaji wa Mungu, na hasa kubarikiwa na Mungu, ambako kutakupa hisia za furaha: utahisi hasa umeheshimika kwa kuwa umemridhisha Mungu, na utahisi umeng'aa kwa ndani, na katika moyo wako utakuwa wazi na mwenye amani, dhamiri yako itafarijiwa na haitakuwa na shutuma, utahisi furaha ndani yako uwaonapo ndugu na dada zako. Hii ndio maana ya kufurahia upendo wa Mungu, na kwa kweli huku ndiko kumfurahia Mungu. Furaha ya watu kutokana na upendo wa Mungu inapatikana kwa kupitia matukio: kwa kupitia matatizo, na kupitia uwekaji ukweli katika vitendo, wanapata baraka za Mungu. Kama utaweka ukweli katika vitendo kwa njia hii, basi hatua kwa hatua utakuza ufahamu wazi zaidi wa kazi ya Mungu, na wakati huo utakuwa unahisi kuwa maneno ya Mungu mbele yako yatakuwa wazi kabisa.

Umetoholewa kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 762 Humpendi Mungu Kwa Dhati

Inayofuata: 764 Kumpenda Mungu, Lazima Upitie Uzuri Wake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp