250 Upendo wa Mungu Ni Halisi Kweli

1

Ee Mungu! Umekuwa mwili, mnyenyekevu na uliyejificha, ukionyesha ukweli kumwokoa wanadamu.

Lakini binadamu hawakujui, hata wanakupinga na kukuhukumu, wakiuumiza moyo Wako sana.

Ee Mungu! Unamlilia nani? Nani anayeweza kuuelewa moyo Wako?

Wewe peke Yako unabeba mapigo ya binadamu, lakini kamwe Husiti kutuokoa, duni na tusiojulikana.

Uasi wetu huuvunja moyo Wako, kutohisi kwetu hukuumiza.

Ah, mbona tunakuamini lakini tunakupinga, na kukutupa kando?

Ah, kwa nini tunakufuata lakini hatukupendi, tunajaribu tu kushika tu neema Yako?

Ni kupitia kwa hukumu tu ndipo tumegutuka, hakika tu vipofu na hatukujui Wewe.

Bahati yetu nzuri ya kufurahia hukumu Yako hakika ni wokovu Wako mkubwa.

2

Ee Mungu! Hukumu na kuadibu kwa maneno Yako yote ni ili kututakasa.

Lakini hatuelewi mapenzi Yako, tunakuelewa vibaya na kukulaumu.

Ee Mungu! Unamfanyia nani kazi? Unakosa usingizi na chakula kwa ajili ya nani?

Ee Mungu! Una wasiwasi kwa ajili ya nani? Unamzungumzia nani kwa uvumilivu?

Tumeumizwa na kukanyagwa na Shetani, Unaona hili kwa macho Yako na kusononeka.

Unatekeleza wokovu ndani yetu kwa maneno ya hukumu na kuadibu.

Ee, sisi ni chembe ya vumbi tu, tunastahilije kuthaminiwa na kujali Kwako?

Ee, sisi ni wachafu kama samadi, tunastahilije uinuaji na upendo kama huu kutoka Kwako?

Tunachukia upotovu wetu wa kina, hatuwezi kuona uzuri na ukarimu Wako.

Sasa tunaweza kupata utakaso na wokovu kutoka Kwako, tukutapenda na kuwa waaminifu Kwako daima.

Iliyotangulia: 249 Mungu Amenipa Upendo Mwingi Sana

Inayofuata: 251 Thamini Fursa ya Kumpenda Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp