1005 Mahitaji ya Mwisho ya Mungu kwa Mwanadamu

1 Ikiwa kwa kweli wewe ni mtendaji huduma, je, unaweza kutoa huduma Kwangu kwa uaminifu, bila dalili yoyote ya uzembe au mtazamo hasi? Je, ukigundua kuwa Sijawahi kukuthamini, bado utaweza kusalia na kunitolea huduma ya maisha yote? Ikiwa bado Ninakudharau sana licha ya wewe kutumia bidii nyingi, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika mashaka? Ikiwa, baada ya wewe kufanya matumizi kwa ajili Yangu, Siyaridhishi mahitaji yako madogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi, au hata ukasirike na kunitukana kwa sauti kubwa?

2 Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana, ukinipenda sana, ilhali unateseka na ugonjwa, umaskini, na kutengwa na marafiki na jamaa zako, au ikiwa unavumilia taabu nyingine zozote maishani, bado uaminifu na upendo wako Kwangu utaendelea? Ikiwa hakuna lolote kati ya yale ambayo umefikiria moyoni mwako linalingana na kile ambacho Nimefanya, je, utaitembea njia yako ya baadaye kwa namna gani? Ikiwa hupokei lolote kati ya mambo ambayo ulitarajia kupokea, je, unaweza kuendelea kuwa mfuasi Wangu?

3 Ikiwa hujawahi kuelewa kusudi na umuhimu wa kazi Yangu, je, unaweza kuwa mtu mtiifu ambaye hatoi hukumu kiholela na kufanya maamuzi? Je, unaweza kuthamini maneno yote ambayo Nimeyanena na kazi yote ambayo Nimeifanya wakati Nimekuwa pamoja na wanadamu? Je, unaweza kuwa mfuasi Wangu mwaminifu, aliye tayari kuvumilia mateso ya maisha kwa ajili Yangu, ingawa hupokei chochote? Je, unaweza kuachilia kuzingatia, kupanga, au kuandaa njia yako ya kuendelea kuishi ya siku za baadaye kwa ajili Yangu?

Umetoholewa kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1004 Matakwa ya Mungu kwa Wafuasi Wake

Inayofuata: 1006 Masharti Manne ya Mungu Kumkamilisha Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp