931 Matendo ya Ajabu ya Mungu Katika Kusimamia Vitu Vyote
1 Kwa karne nyingi kijito kidogo kilichururika taratibu kuzunguka chini ya mlima. Kwa kufuata njia ambayo mlima uliifanya, kijito kidogo kilifanikiwa kufika nyumbani; kilijiunga na mto, na kutiririka kwenda baharini. Chini ya uangalizi wa mlima, kijito kidogo hakikuweza kupotea. Kijito na mlima ilihimiliana na kutegemeana; ilitiana nguvu, kutenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.
2 Kwa karne nyingi, upepo mkali haukuacha tabia yake ya kuvuma kwenye mlima. Upepo mkali ulivumisha kimbunga “ulipoutembelea” mlima kama ulivyofanya kabla. Uliutisha mlima, lakini haukuwahi kupenya katikati ya mlima. Upepo na mlima vilihimiliana na vilitegemeana; vilitiana nguvu, vilitenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.
3 Kwa karne nyingi, wimbi kubwa wala halikupumzika, na kamwe halikuacha kupanuka. Lingenguruma na kuvurumiza tena na tena kwenda kwenye mlima, lakini mlima haukuwahi kusogea hata inchi moja. Mlima uliilinda bahari, na kwa namna hii viumbe ndani ya bahari viliongezeka na kustawi. Wimbi na mlima mkubwa vilihimiliana na vilitegemeana; vilitiana nguvu, vilitenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” katika Neno Laonekana katika Mwili