1026 Mungu Afanya Mipango ya Kufaa kwa Mwanadamu wa Kila Aina

1 Binadamu wote bado ni viumbe wa Mungu. Bila kujali jamii ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; wote ni vizazi vya Adamu na Hawa. Bila kujali aina ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; kwa sababu ni wa binadamu, ambao uliumbwa na Mungu, hatima yao ni hiyo ambayo binadamu wanapaswa kuwa nayo, na wamegawanywa kulingana na kanuni zinazopanga binadamu. Viumbe wafanyao maovu wataangamizwa hatimaye, na viumbe wafanyao matendo ya haki watasalimika. Huu ni mpangilio unaofaa sana wa viumbe wa aina hizi mbili.

2 Baada ya kazi ya Mungu kuisha, miongoni mwa viumbe Wake wote, kutakuwa na wale watakaoangamizwa na wale watakaosalimika. Huu ni mwelekeo usioepukika wa kazi Yake ya usimamizi. Hakuna anayeweza kuyakataa haya. Watenda maovu hawawezi kusalimika; wanaomtii na kumfuata Mungu hadi mwishowe hakika watasalimika. Kwa sababu kazi hii ni ya usimamizi wa binadamu, kutakuwa na wale watakaobaki na wale watakaoondolewa. Haya ni matokeo tofauti ya watu wa aina tofauti, na hii ndiyo mipango inayofaa zaidi ya viumbe Wake.

3 Mpango wa mwisho wa Mungu kwa mwanadamu ni kugawa kwa kuzivunja familia, kuyavunja mataifa na kuivunja mipaka ya kitaifa. Ni moja isiyo na familia na mipaka ya kitaifa, kwani mwanadamu, hata hivyo, ni wa babu mmoja na ni kiumbe wa Mungu. Kwa ufupi, viumbe wafanyao maovu wataangamizwa, na viumbe wanaomtii Mungu watasalimika. Kwa njia hii, hakutakuwa na familia, hakutakuwa na nchi na hasa hakutakuwa na mataifa katika pumziko la baadaye; binadamu wa aina hii ni aina takatifu kabisa ya binadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1025 Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu Katika Siku za Mwisho

Inayofuata: 1027 Wanadamu Waingiapo Mapumzikoni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp