4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana.… Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu” (Yohana 5:22-27).

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Leo, ni kwa sababu ya uchafu wako ndiyo Ninakuhukumu, na ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako ndiyo Ninakuadibu. Mimi sijivunii nguvu Zangu kwenu au kuwadhulumu kwa makusudi; Ninafanya mambo haya kwa sababu ninyi, ambao mmezaliwa katika nchi hii ya uchafu, mmenajisiwa vikali kwa uchafu. Mmepoteza uadilifu na ubinadamu wenu kabisa na mmekuwa kama nguruwe waliozaliwa katika pembe chafu zaidi za ulimwengu, na kwa hiyo ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mnahukumiwa na ndiyo Ninawaachia huru hasira Yangu. Ni kwa sababu hasa ya hukumu hii ndiyo mmeweza kuona kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba Mungu ndiye Mungu mtakatifu; ni kwa sababu hasa ya utakatifu Wake na haki Yake ndiyo Anawahukumu na kuachia huru hasira Yake juu yenu. Kwa sababu Anaweza kufichua tabia Yake yenye haki Aonapo uasi wa mwanadamu, na kwa sababu Anaweza kufichua utakatifu Wake anapoona uchafu wa mwanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na wa asili, na bado Anaishi katika nchi ya uchafu. Mungu angelikuwa mtu na kufuata mfano wa mwanadamu na kugaagaa na wanadamu katika matope machafu, basi kusingelikuwa na chochote kitakatifu kumhusu, na Asingelikuwa na tabia yenye haki, na kwa hiyo Asingelikuwa na haki ya kuhukumu uovu wa mwanadamu, wala Asingelikuwa na haki ya kutekeleza hukumu ya mwanadamu. Mtu angelimhukumu mtu mwingine, haingekuwa kana kwamba anajipiga kofi usoni? Watu ambao wote ni wachafu kwa kiwango sawa wanastahili vipi kuwahukumu wale ambao ni sawa na wao? Ni Mungu mtakatifu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu. Mwanadamu angewezaje kuhukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na mwanadamu angewezaje kuwa na sifa za kulaani dhambi hizi? Mungu Asingelikuwa na sifa ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki Mwenyewe? Tabia potovu za watu zinapofichuliwa, Mungu hunena ili Awahukumu watu, na ni hapo tu ndipo watu wanapoona kuwa Yeye ni mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa

Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali tabia yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua tabia yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni kwa kubadilisha vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza na Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu, na kuwafanya watu kuvielewa ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikisha matokeo haya sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, sembuse mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Dhana za mwanadamu zinakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Dhana asili za mwanadamu zinaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, dhana za mwanadamu zisingefichuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefichuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu zaidi kwa utendaji, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii. Kama mwanadamu anaamini tu kuwa Mungu alikuja kuonekana naye na kumfurahisha, basi imani kama hizo hazina thamani, na hazina umuhimu. Maarifa ya mwanadamu ni ya kijuujuu mno! Ni kwa Mungu kutekeleza kazi Yeye mwenyewe ndivyo Mungu anaweza kufanya kazi yake vizuri na kikamilifu. Mwanadamu hana uwezo wa kuifanya kwa niaba ya Mungu. Kwa kuwa yeye hana utambulisho wa Mungu ama kiini Chake, hana uwezo wa kufanya kazi hii, na hata kama mwanadamu angekuwa na uwezo, haingekuwa na matokeo yoyote. Wakati wa kwanza Mungu kuwa mwili kwa ajili ya ukombozi, ilikuwa ni ili kuwakomboa wanadamu wote kutoka kwa dhambi, ili kufanya mwanadamu aweze kutakaswa na kusamehewa dhambi zake. Kazi ya ushindi pia inafanywa na Mungu binafsi miongoni mwa wanadamu. Kama, katika awamu hii, Mungu angekuwa wa kusema tu ya unabii, basi nabii au mtu ambaye ana kipawa angepatikana wa kuchukua nafasi Yake; kama unabii pekee ungesemwa, mwanadamu angechukua nafasi ya Mungu. Lakini ikiwa mwanadamu binafsi angefanya kazi ya Mungu Mwenyewe na angefanya kazi kwa maisha ya mwanadamu, haingewezekana kwake kufanya kazi hii. Ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi: Ni lazima Mungu binafsi awe mwili ili kufanya kazi hii. Katika Enzi ya Neno, kama unabii pekee ungesemwa, basi Isaya au nabii Eliya wangepatikana wakifanya kazi hii, na hakungekuwepo na haja ya Mungu Mwenyewe kuifanya kazi hii binafsi. Kwa sababu kazi ambayo inafanywa katika awamu hii si tu ya kuongea kuhusu unabii, na kwa sababu ni ya umuhimu mkubwa zaidi kuwa kazi ya maneno inatumiwa kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, kazi hii haiwezi fanywa na mwanadamu, na ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi. Katika Enzi ya Sheria Yehova alifanya sehemu ya kazi ya Mungu, ambapo baadaye alinena baadhi ya maneno na kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa manabii. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu angemwakilisha Yehova katika kazi yake, na waonaji wangeweza kutabiri mambo na kutafsiri baadhi ya ndoto kwa niaba Yake. Kazi iliyofanyika hapo mwanzo haikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu moja kwa moja, na ilikuwa bila uhusiano na dhambi ya mwanadamu, na mwanadamu alitakiwa tu atii sheria. Kwa hivyo, Yehova hakuwa wa kuwa na mwili na kujifichua Mwenyewe kwa mwanadamu; badala yake Yeye aliongea moja kwa moja na Musa na wengine, akawafanya wao kusema na kufanya kazi kwa niaba yake, na kusababisha wao wafanye kazi moja kwa moja miongoni mwa wanadamu. Awamu ya kwanza ya kazi ya Mungu ilikuwa uongozi wa mwanadamu. Ilikuwa ndio mwanzo wa vita dhidi ya Shetani, lakini vita hivi vilikuwa bado kuanza rasmi. Vita rasmi dhidi ya Shetani vilianza na kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya kwanza, na vimeendelea hadi leo. Tukio la kwanza la vita hivi ni wakati Mungu aliyepata mwili alisulubishwa msalabani. Kusulubiwa kwa Mungu aliyekuwa mwili kulimshinda Shetani, na ilikuwa mafanikio ya awamu ya kwanza katika vita. Wakati Mungu mwenye mwili alianza kufanya kazi kwa mwanadamu moja kwa moja, huu ulikuwa mwanzo rasmi wa kazi ya kumrejesha mwanadamu, na kwa sababu hii ilikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ilikuwa kazi ya kufanya vita na Shetani. Awamu ya kazi iliyofanywa na Yehova hapo mwanzo ilikuwa tu ya uongozi wa maisha ya mwanadamu duniani. Ilikuwa ndio mwanzo wa kazi ya Mungu, na hata ingawa ilikuwa bado haijashirikisha vita vyovyote, au kazi kuu yeyote, ilikuwa imeweka msingi kwa ajili ya kazi ya vita vijavyo. Baadaye, awamu ya pili ya kazi wakati wa Enzi ya Neema ilihusisha kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ambayo ina maana kuwa Mungu Mwenyewe alitengeneza kwa ustadi kazi ya mwanadamu. Hii ilikuwa ni lazima ifanywe na Mungu: ilihitaji kuwa Mungu binafsi awe mwili, na kama hangekuwa mwili, hakuna mwingine angeweza kuchukua nafasi yake katika awamu hii ya kazi, kwa kuwa iliwakilisha kazi ya kupambana dhidi ya Shetani moja kwa moja. Kama mtu angekuwa amefanya kazi hii kwa niaba ya Mungu, wakati mwanadamu alisimama mbele ya Shetani, Shetani hangeweza kutii na haingewezekana kumshinda yeye. Ilibidi iwe Mungu aliyepata mwili aliyekuja kumshinda, kwa kuwa kiini cha Mungu mwenye mwili bado ni Mungu, Yeye bado ni maisha ya mwanadamu, na bado Yeye ni Muumba; chochote kitakachotokea, utambulisho Wake na kiini havitabadilika. Na kwa hivyo, Yeye alivaa mwili na alifanya kazi ili kusababisha kujisalimisha kwa Shetani. Katika awamu ya kazi ya siku za mwisho, kama mwanadamu angefanya kazi hii na angefanywa kusema maneno moja kwa moja, basi hangeweza kusema maneno hayo, na kama unabii ungesemwa, basi haungekuwa na uwezo wa kumshinda mwanadamu. Kwa kuchukua mwili, Mungu huja kumshinda Shetani na kusababisha kujisalimisha kwake kamili. Wakati Yeye atamshinda Shetani kabisa, kumshinda mwanadamu kikamilifu, na kumpata mwanadamu kabisa, awamu hii ya kazi itakamilika na mafanikio kutimizwa. Katika usimamizi wa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa naibu wa Mungu na kuwa Mungu wakati hayupo. Hasa, kazi ya kuongoza enzi na kuzindua kazi mpya ina haja kubwa zaidi kufanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kumpa mwanadamu ufunuo na kwa kumpa yeye unabii kunaweza kufanywa na mwanadamu, lakini kama ni kazi ambayo ni lazima ifanywe na Mungu binafsi, kazi ya vita kati ya Mungu Mwenyewe na Shetani, basi kazi hii haiwezi kufanywa na mwanadamu. Katika awamu ya kwanza, wakati hakukuwepo na vita dhidi ya Shetani, Yehova binafsi aliongoza wana wa Israeli kutumia unabii uliosemwa na manabii. Baadaye, awamu ya pili ya kazi ilikuwa vita na Shetani, na Mungu Mwenyewe binafsi akawa mwili, kuja katika mwili, ili kufanya kazi hii. Chochote ambacho kinahusisha vita na Shetani pia kinahusisha kupata mwili kwa Mungu, ambayo ina maana kuwa vita hivi haviwezi kufanywa na mwanadamu. Kama mwanadamu angekuwa wa kufanya vita, hangeweza kumshinda Shetani. Jinsi gani yeye angekuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya Shetani wakati bado yumo chini ya utawala wake? Mwanadamu yumo katikati: Kama wewe utaegemea kuelekea kwa Shetani wewe ni wa Shetani, lakini wewe ukimridhisha Mungu wewe ni wa Mungu. Kama mwanadamu angeweza kuwa mbadala wake Mungu katika kazi ya vita hivi, je, yeye angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo? Kama angekuwa na uwezo, je, hangeangamia kitambo sana? Je, yeye si angekuwa ameingia katika ulimwengu wa jahanamu muda mrefu uliopita? Na hivyo, mwanadamu hana uwezo wa kuchukua nafasi ya Mungu katika kazi yake, ambayo ni kusema kwamba mwanadamu hana kiini cha Mungu, na kama ungepambana na Shetani hungeweza kumshinda Shetani. Mwanadamu anaweza tu kufanya baadhi ya kazi; anaweza kushinda baadhi ya watu, lakini hawezi kuwa mbadala wa Mungu katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Je, ni jinsi gani mwanadamu atafanya vita na Shetani? Shetani ataweza kukushika mateka kabla hata hujaanza. Ni wakati Mungu Mwenyewe hufanya vita dhidi ya Shetani na mwanadamu kufuata na kutii Mungu katika msingi huu tu ndipo mwanadamu anaweza kupatwa na Mungu na kutoroka kutokana na vifungo vya Shetani. Kile mwanadamu anaweza kufikia kwa hekima yake na uwezo wake mwenyewe ni kidogo sana; hana uwezo wa kufanya mwanadamu akamilike, kumwongoza mwanadamu, na, zaidi ya hayo, kumshinda Shetani. Akili na hekima ya mwanadamu haviwezi kuharibu miradi ya Shetani, hivyo je, ni jinsi gani mwanadamu awezavyo kufanya vita na Shetani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Iliyotangulia: 3. Tofauti ni ipi kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na kazi ya Roho?

Inayofuata: 5. Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp