762 Humpendi Mungu Kwa Dhati

1 Mnafikiri kuwa mmeacha ya kutosha kwa ajili Yangu; mnafikiri kuwa upendo wenu Kwangu tayari umetosha. Ila ni kwa nini basi maneno yenu na matendo yenu huambatana na uasi na uongo daima? Mnanifuata, ilhali hamkubali neno Langu. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, kisha mnanitenga na kunitupa kando. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, na bado mko na shaka na Mimi. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, ilhali hamkubali kuwepo Kwangu. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali hamnitendei vile Ninavyopaswa kutendewa na mnafanya mambo yawe magumu Kwangu katika kila hatua. Je, hili linachukuliwa kama upendo?

2 Mnanifuata, na bado mnanichukua kama mjinga na kunidanganya Mimi katika kila jambo. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanihudumia, na bado hamnichi. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanipinga katika kila hali na kila jambo. Je, yote haya yanachukuliwa kama upendo? Mmejinyima mengi, huu ni ukweli, lakini bado hamjawahi kutenda Ninayowaagiza mfanye. Je, huu unaweza kuchukuliwa kama upendo? Uchunguzi wa makini unaashiria kuwa hamna upendo Kwangu ndani yenu. Baada ya miaka mingi sana ya kazi na maneno yote mengi Niliyosambaza, ni kiasi kipi mlichopokea kwa hakika? Je, hili halistahili kuangaliwa tena kwa makini?

Umetoholewa kutoka katika “Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 761 Una Upendo wa Kweli kwa Mungu?

Inayofuata: 763 Upendo wa Mungu Lazima Uonjwe Katika Maisha Halisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp