A. Kuhusu Ufunuo wa Mungu wa Kazi Yake katika Enzi ya Sheria

21. Wakati huu, umuhimu, kusudi na awamu za kazi ya Yehova huko Israeli zilikuwa kuanzisha kazi Yake katika dunia nzima, ambayo, ikichukua Israeli kama kituo chake, ilienea polepole hadi kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hii ni kanuni ambayo kwayo Anafanya kazi katika ulimwengu mzima—kuunda mfano na kisha kuupanua hadi watu wote ulimwenguni watakuwa wamepokea injili Yake. Waisraeli wa kwanza walikuwa wa ukoo wa Nuhu. Watu hawa walikuwa wamejawa tu na pumzi ya Yehova, na walielewa kiasi cha kutosha ili kushughulikia mambo muhimu ya msingi ya maisha, lakini hawakujua Yehova alikuwa Mungu wa aina gani, au mapenzi Yake kwa mwanadamu, sembuse jinsi wanavyopaswa kumcha Bwana wa viumbe vyote. Kuhusu iwapo kulikuwa na sheria na kanuni za kutiiwa,[a] au iwapo kulikuwa na wajibu ambayo viumbe walioumbwa wanapaswa kumfanyia Muumba, wa ukoo wa Adamu hawakujua hata kidogo kuhusu mambo haya. Yote waliyojua ilikuwa kwamba mume anapaswa kutokwa jasho na kufanya kazi ili kukimu familia yake, na kwamba mke anapaswa kumtii mume wake na kuendeleza jamii ya binadamu ambao Yehova alikuwa ameumba. Kwa maneno mengine, watu wa aina hii, ambao walikuwa na pumzi ya Yehova na uzima Wake pekee, hawakujua kabisa kuhusu jinsi ya kufuata sheria za Mungu au jinsi ya kumridhisha Bwana wa viumbe vyote. Walielewa kidogo sana. Kwa hivyo ingawa hakukuwa na kitu kisicho kipotovu au cha udanganyifu mioyoni mwao na wivu na ugomvi viliibuka miongoni mwao mara chache, hata hivyo hawakuwa na maarifa au ufahamu wa Yehova, Bwana wa viumbe vyote. Mababu hawa wa mwanadamu walijua tu kula vitu vya Yehova, na kufurahia vitu vya Yehova, lakini hawakujua kumcha Yehova: hawakujua kwamba Yehova ndiye Yule wanayepaswa kumwabudu kwa kupiga magoti. Kwa hiyo wangeweza kuitwa viumbe Wake vipi? Kama hali ingekuwa hivi, je maneno, “Yehova ndiye Bwana wa viumbe vyote” na “Alimuumba mwanadamu ili mwanadamu aweze kumdhihirisha Yeye, kumtukuza Yeye, na kumwakilisha Yeye”—hayangekuwa yamesemwa bure? Watu ambao hawamchi Yehova wangewezaje kuwa ushuhuda kwa utukufu Wake? Wangewezaje kuwa dhihirisho la utukufu Wake? Je, maneno ya Yehova “Nilimuumba mwanadamu kwa mfano Wangu” si yangekuwa silaha mikononi mwa Shetani basi—yule mwovu? Maneno haya basi hayangekuwa alama ya fedheha kwa Yehova kumuumba mwanadamu? Ili kukamilisha hatua hiyo ya kazi, baada ya kuwaumba wanadamu, Yehova hakuwaagiza au kuwaongoza kutoka wakati wa Adamu hadi ule wa Nuhu. Badala yake, baada ya dunia kuharibiwa na gharika tu ndiyo wakati ambapo Alianza rasmi kuwaongoza Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa Adamu. Kazi na matamshi Yake huko Israeli yaliwapa watu wote wa Israeli mwongozo walipokuwa wakiishi maisha yao katika nchi yote ya Israeli, na kwa njia hii yakaonyesha binadamu kwamba Yehova hakuweza tu kupuliza pumzi ndani ya mwanadamu, ili aweze kuwa na uhai kutoka Kwake na kuinuka kutoka mavumbini kuwa mwanadamu aliyeumbwa, lakini kwamba pia Angeweza kuwachoma wanadamu, na kuwalaani wanadamu, na kutumia fimbo Yake kuwatawala wanadamu. Kwa hivyo, pia waliona kwamba Yehova angeweza kuyaongoza maisha ya mwanadamu duniani, na kuzungumza na kufanya kazi miongoni mwa binadamu kulingana na saa za mchana na za usiku. Alifanya kazi hiyo ili tu viumbe Wake waweze kujua kwamba mwanadamu alitoka kwa mavumbi yaliyochaguliwa na Yeye, na aidha kwamba mwanadamu alikuwa ameumbwa na Yeye. Siyo haya tu, lakini kazi Aliyoanza huko Israeli ilikusudiwa ili kwamba watu na mataifa (ambao kwa kweli hawakuwa wametengwa na Israeli, lakini badala yake walikuwa wameenea kutoka kwa Waisraeli, ilhali bado walikuwa wa ukoo wa Adamu na Hawa) waweze kupokea injili ya Yehova kutoka Israeli, ili viumbe wote walioumbwa ulimwenguni waweze kuwa na uwezo wa kumcha Yehova na kumchukulia kuwa mkuu. Yehova asingeanza kazi Yake huko Israeli, lakini badala yake, baada ya kuwaumba wanadamu, awaache waishi maisha machangamfu duniani, basi katika hali hiyo, kwa sababu ya asili ya maumbile ya mwanadamu (asili inamaanisha kwamba mwanadamu hawezi kamwe kujua vitu ambavyo hawezi kuviona, yaani kwamba hangejua kwamba ilikuwa ni Yehova ambaye aliwaumba wanadamu, sembuse sababu yake kufanya hivyo), hangejua kamwe kwamba ilikuwa Yehova aliyewaumba wanadamu au kwamba Yeye ni Bwana wa viumbe vyote. Kama Yehova angemuumba mwanadamu na kumweka duniani, na kutoshughulika na yeye na kuondoka tu, badala ya kubaki miongoni mwa wanadamu ili kuwaongoza kwa kipindi cha muda, basi katika hali hiyo wanadamu wote wangekuwa wamerudi kuwa bure: hata mbingu na dunia na vitu vyote vingi Alivyoviumba, na wanadamu wote, vingerudi kuwa bure na aidha vingekanyagwa na Shetani. Kwa njia hii matakwa ya Yehova kwamba “Duniani, yaani, miongoni mwa viumbe Vyake, Anapaswa kuwa na mahali pa kusimama, mahali patakatifu” yangevunjwa. Na hivyo, baada ya kuwaumba wanadamu, kwamba Aliweza kubaki miongoni mwao kuwaongoza katika maisha yao, na kuzungumza nao kutoka miongoni mwao, yote haya yalikuwa ili kufanikisha hamu Yake, na kutimiza mpango Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

22. Katika Enzi ya Sheria, Yehova aliweka amri nyingi za Musa kupitisha kwa Waisraeli waliomfuata kutoka Misri. Amri hizi walipewa Waisraeli na Yehova, na hazikuwa na uhusiano kwa Wamisri: zilinuiwa kuwazuia Waisraeli. Yeye alizitumia amri kuwatolea madai. Iwapo waliishika Sabato, iwapo waliwaheshimu wazazi wao, iwapo waliziabudu sanamu, na kadhalika: hizi zilikuwa kanuni ambazo kwazo walihukumiwa kuwa wenye dhambi au wenye haki. Miongoni mwao, kuna baadhi walioangamizwa kwa moto wa Yehova, baadhi waliopigwa mawe hadi kufa, na baadhi waliopokea baraka za Yehova, na haya yaliamuliwa kulingana na iwapo walizitii amri hizi au la. Wale ambao hawakuishika Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakuishika Sabato wangeangamizwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuwaheshimu wazazi wao pia wangepigwa mawe hadi kufa. Yote haya yalikubaliwa na Yehova. Yehova alianzisha amri na sheria Zake ili, Alipokuwa akiwaongoza katika maisha yao, watu wangesikiliza na kuti neno Lake na kutoasi dhidi Yake. Alitumia sheria hizi kuidhibiti jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa karibuni, ili kuweka vizuri zaidi msingi wa kazi Yake ya baadaye. Na kwa hivyo, kwa msingi wa kazi ambayo Yehova alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya sheria.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

23. Wakati wa Enzi ya Sheria, kazi ya kumwelekeza mwanadamu ilifanyika katika Jina la Yehova, na awamu ya kwanza ya kazi ilifanyika duniani. Kazi ya awamu hii ilikuwa ni kujenga hekalu na madhabahu, na kutumia sheria kuwaongoza watu wa Israeli na kufanya kazi miongoni mwao. Kwa kuongoza watu wa Israeli, Alizindua kituo cha kazi Yake hapa duniani. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli. Nchi ya Israeli ilikuwa ya mahali takatifu pa kwanza pa kazi ya Yehova hapa duniani, na kazi ya Mungu ya hapo mwanzoni ilikuwa kote katika nchi ya Israeli. Hiyo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

24. Wkati Mungu alianza kazi Yake rasmi ya mpango Wake wa usimamizi, Aliweka wazi taratibu nyingi ambazo zilifaa kufuatwa na binadamu. Taratibu hizi zilikuwa ili kumruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida ya binadamu hapa duniani, maisha ya kawaida ya binadamu ambayo hayajatenganishwa na Mungu na uongozi Wake. Mungu alimwambia binadamu kwanza namna ya kuunda madhabahu, namna ya kuyaunda madhabahu. Baada ya hapo, Alimwambia binadamu namna ya kutoa sadaka, na kuamuru namna ambavyo binadamu alifaa kuishi—kile alichofaa kutilia maanani katika maisha, kile alichofaa kutii, kile anachofaa na hafai kufanya. Kile Mungu alichoweka wazi kwa binadamu kilikuwa kinakubalika chote, na pamoja na tamaduni, taratibu, na kanuni hizi Aliwastanisha tabia ya watu, kuongoza maisha yao, kuongoza uanzishaji wao wa sheria za Mungu, kuwaongoza kuja mbele ya madhabahu ya Mungu, kuwaongoza katika kuishi maisha miongoni mwa mambo mengine yote ambayo Mungu alikuwa amemuumbia binadamu na yaliyomilikiwa na mpangilio na marudio ya mara kwa mara na ya kiasi. Kwanza Mungu alitumia taratibu na kanuni hizi rahisi kuweka vipimo kwa binadamu, ili hapa duniani binadamu aweze kuwa na maisha ya kawaida ya kumwabudu Mungu, aweze kuwa na maisha ya kawaida; hivi ndivyo yalivyo maudhui mahususi ya mwanzo wa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. Taratibu na sheria zinajumuisha maudhui mapana mno, yote ni maelezo ya mwongozo wa Mungu wa mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria, lazima yangekubaliwa na kuheshimiwa na watu waliokuwa wamekuja kabla ya Enzi ya Sheria, ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika Enzi ya Sheria, na ni ithibati ya kweli ya uongozi na mwongozo wa Mungu kwa wanadamu wote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

25. Yehova aliwaumba wanadamu, ambayo ni kusema kwamba Yeye aliumba babu za wanadamu: Hawa na Adamu. Lakini hakuwapa akili zaidi au hekima. Ingawa walikuwa tayari wanaishi duniani, hawakuelewa takriban chochote. Na kwa hiyo, kazi ya Yehova ya kuwaumba wanadamu ilikuwa imefanyika nusu tu, haikuwa imekaribia kukamilika. Alikuwa ameumba tu mfano wa mwanadamu kutoka kwa udongo na kumpa pumzi Yake, lakini Hakuwa amempa mwanadamu radhi ya kutosha kumcha Yeye. Hapo mwanzo, mwanadamu hakuwa na akili ya kumcha Yeye, au kumwogopa Yeye. Mwanadamu alijua tu jinsi ya kuyasikiliza maneno Yake lakini hakujua ujuzi wa msingi wa maisha duniani na sheria za kawaida za maisha. Na kwa hiyo, ingawa Yehova aliumba mwanamume na mwanamke na kumaliza siku saba za shughuli, Hakukamilisha uumbaji wa mwanadamu hata kidogo, kwa maana mwanadamu alikuwa ganda tu, na hakuwa na uhalisi wa kuwa mwanadamu. Mwanadamu alijua tu kwamba ni Yehova aliyeumba wanadamu, lakini mwanadamu hakuwa na fununu ya jinsi ya kutii maneno na sheria za Yehova. Na kwa hiyo, baada ya kuumbwa kwa wanadamu, kazi ya Yehova ilikuwa mbali sana kumalizika. Pia alitakiwa kuwaongoza wanadamu kabisa mbele Yake ili wanadamu waweze kuishi pamoja duniani na kumcha Yeye, na ili wanadamu waweze kwa mwongozo Wake kuingia katika njia sahihi ya maisha ya kawaida ya binadamu duniani baada ya kuongozwa na Yeye. Kwa njia hii tu ndiyo kazi ambayo ilikuwa imeendeshwa kwa kiasi kikubwa kupitia jina la Yehova ilimalizika kabisa; yaani, kwa njia hii tu ndiyo kazi ya Yehova ya kuumba ulimwengu ilihitimishwa kabisa. Na kwa hiyo, kwa vile Alimuumba mwanadamu, Alipaswa kuongoza maisha ya wanadamu duniani kwa miaka elfu kadhaa, ili wanadamu waweze kutii amri na sheria Zake, na kushiriki katika shughuli zote za maisha ya kufaa ya binadamu duniani. Wakati huo tu ndio kazi ya Yehova ilikamilika kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

26. Kabla ya miaka elfu mbili ambapo Yehova alifanya kazi Yake, mwanadamu hakujua chochote, na karibu wanadamu wote walikuwa wamejipata katika upotovu, hadi, kabla ya uharibifu wa dunia na gharika, walikuwa wamefika kina cha uzinzi na upotovu ambapo mioyo yao haikuwa na Yehova, sembuse njia Yake. Hawakuelewa kamwe kazi ambayo Yehova angefanya; hawakuwa na mantiki, sembuse maarifa, na, kama mashine inayopumua, walikuwa hawamjui mwanadamu, Mungu, dunia, uhai na kadhalika kikamilifu. Duniani walishiriki katika ushawishi mwingi, kama yule nyoka, na walisema mambo mengi ambayo yalimkosea Yehova, lakini kwa sababu hawakujua Yehova hakuwaadibu au kuwafundisha nidhamu. Ni baada ya gharika tu, wakati Nuhu alikuwa na umri wa miaka 601, ndipo Yehova alijitokeza rasmi kwa Nuhu na kumwongoza yeye na familia yake, Akiongoza ndege na wanyama ambao walisalia baada ya gharika pamoja na Nuhu na ukoo wake, hadi mwisho wa Enzi ya Sheria, yote ikiwa ni miaka 2,500. Alikuwa akifanya kazi huko Israeli, yaani, alikuwa akifanya kazi kirasmi, kwa jumla ya miaka 2,000, na Alikuwa akifanya kazi huko Israeli sawia na nje ya Israeli kwa miaka 500, yote ikijumuisha miaka 2,500. Katika kipindi hiki, Aliwaagiza Waisraeli kwamba ili kumhudumia Yehova, iliwapasa kujenga hekalu, kuvaa majoho ya makuhani, na kutembea miguu mitupu kuingia hekaluni kunapopambazuka, viatu vyao visije vikachafua hilo hekalu na moto kushushwa chini kwao kutoka juu ya hekalu na kuwachoma hadi kufa. Walitekeleza wajibu wao na kutii mipango ya Yehova. Walimwomba Yehova hekaluni, na baada ya kupokea ufunuo wa Yehova, yaani, baada ya Yehova kuzungumza, waliuongoza umati na kuufunza kwamba wanapaswa kumcha Yehova—Mungu wao. Na Yehova aliwaambia kwamba ingewapasa kujenga hekalu na madhabahu, na katika wakati uliowekwa na Yehova, yaani, katika siku ya Pasaka, wangepaswa kuwatayarisha ndama na wanakondoo waliozaliwa karibuni kuwaweka juu ya madhabahu kama dhabihu kumhudumia Mungu, ili kuwazuia na kuweka uchaji kwa Yehova mioyoni mwao. Iwapo walitii sheria hii ikawa kipimo cha uaminifu wao kwa Yehova. Yehova pia aliwaagizia siku ya Sabato, siku ya saba ya uumbaji Wake. Akafanya siku baada ya Sabato kuwa siku ya kwanza, siku ya wao kumwabudu Yehova, kumtolea dhabihu, na kumtengenezea Muziki. Katika siku hii, Yehova aliwaita pamoja wakuhani wote ili kugawa dhabihu zilizokuwa juu ya madhabahu kwa ajili ya watu kula, ili wangeweza kufurahia dhabihu zilizokuwa juu ya madhabahu ya Yehova. Naye Yehova alisema kwamba walikuwa wamebarikiwa, kwamba walishiriki sehemu na Yeye, na kwamba walikuwa wateule Wake (ambalo lilikuwa agano la Yehova na Waisraeli). Hii ndiyo maana, hadi siku ya leo, watu wa Israeli bado wanasema kwamba Yehova ni Mungu wao pekee, na si Mungu wa watu wengine.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

27. Ingawa Yehova alisema matamshi mengi na kufanya kazi nyingi, Aliwaongoza watu kwa njia njema tu, akiwafunza watu hawa wasiojua jinsi ya kuwa binadamu, jinsi ya kuishi, jinsi ya kuelewa njia ya Yehova. Kwa kiwango kikubwa sana, kazi Aliyoifanya ilikuwa ili kuwasababisha watu kutii njia Yake na kufuata sheria Zake. Kazi hii ilifanywa kwa watu waliokuwa wamepotoshwa kwa kiasi kidogo; haikuenea kiasi cha kubadili tabia yao au maendeleo katika maisha. Alijishughulisha tu na kutumia sheria kuwazuia na kuwadhibiti watu. Kwa Waisraeli wa wakati huo, Yehova alikuwa Mungu katika hekalu tu, Mungu huko mbinguni. Alikuwa nguzo ya wingu, nguzo ya moto. Yote ambayo Yehova aliwataka wafanye ilikuwa ni kutii kile ambacho watu wa leo wanakijua kama sheria na amri Zake—mtu anaweza pia kusema kanuni—kwa sababu kile ambacho Yehova alifanya hakikunuiwa kuwabadilisha, ila kuwapa vitu zaidi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, kuwaagiza kutoka kinywani Mwake mwenyewe, kwa sababu baada ya kuumbwa, mwanadamu hakuwa na chochote alichopaswa kumiliki. Na kwa hivyo, Yehova aliwapa watu vitu ambavyo walipaswa kumiliki kwa ajili ya maisha yao duniani, Akiwafanya watu Aliokuwa ameongoza kuwashinda mababu zao, Adamu na Hawa, kwa sababu kile Yehova alichowapa kilishinda kile Alichokuwa amewapa Adamu na Hawa mwanzoni. Bila kujali, kazi ambayo Yehova alifanya huko Israeli ilikuwa tu kuwaongoza binadamu na kuwafanya binadamu wamtambue Muumba wao. Hakuwashinda wala kuwabadilisha, ila Aliwaongoza tu. Hii ndiyo kazi yote ya Yehova katika Enzi ya Sheria. Ndio usuli, masimulizi ya kweli, kiini cha kazi Yake katika nchi nzima ya Israeli, na mwanzo wa kazi Yake ya miaka elfu sita—kuendeleza udhibiti wa wanadamu kwa mkono wa Yehova. Kutokana na hili kulizaliwa kazi zaidi katika mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “kutiiwa”.

Iliyotangulia: I. Maneno Juu ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu ya Kuwaokoa Wanadamu

Inayofuata: B. Kuhusu Ufunuo wa Mungu wa Kazi Yake katika Enzi ya Neema

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp