161 Maneno Katika Mioyo ya Wakristo

1 Kwa nini ni vigumu sana kumwamini Mungu na kumshuhudia Mungu nchini China? Kwa nini CCP inamchukia Mungu na Wakristo sana? Wakati Katiba inapotaja uhuru wa imani ya kidini, kwa nini CCP inawatesa na kuwakamata Wakristo? Ndugu wengi wamefuatwa na kufuatiliwa na polisi, watu wengi sana wametupwa gerezani na kuteswa hadi kufa, wengi wamelazimika kukimbia makwao. Ni dhahiri kwamba imani katika Mungu ndiyo njia sahihi ya maisha ya mwanadamu, lakini inakashifiwa na kusingiziwa; ufalme wa mbinguni umefika, na Wakristo wanafanya toba, na bado wanakamatwa na kuteswa; watu wawili au watatu wakizungumza kuhusu imani katika Mungu, wanahukumiwa kama wanaofanya mkutano usio halali. Wanapokusanyika kusoma maneno ya Mungu, wanatuhumiwa kuvuruga utaratibu wa umma; kamera zinaenea katika kila mtaa na barabara, maafisa waliovalia kiraia na wapelelezi wako kila mahali, na wakiwa wazembe kidogo tu, wale wanaomwamini Mungu wanaweza kukamatwa na kufungwa. Ni lini tunaweza kukusanyika na kusoma maneno ya Mungu bila wasiwasi? Moyo wangu unalia. Ni sawa na sahihi kumwamini Mungu, kumfuata na kumshuhudia Kristo; mimi ni Mkristo, nami natamani ulimwengu wenye uhuru!

2 CCP imekuwa imekuwa na uhasama usio na huruma kwa Mungu nayo ikiyakomesha makanisa ya nyumbani, inawakashifu Wakristo kutumia vyombo vya habari vya mtandaoni, inahamasisha vikosi vya polisi kuwawinda Wakristo kwa ukali, ikitupa wavu wake mbali na kila mahali; inahimiza umma kuwaripoti Wakristo na kuwachunguza kwa karibu, haiachi chochote katika ufuatiliaje wake wa Kristo, na itafurahia tu Kristo atakapoondolewa; inayazingira makanisa, na kuwaacha Wakristo bila mahali pa kukaa. Hakuna kitu kisicho cha maana au kilicho haramu kuhusu sisi kumwamini Mungu na kumfuata Kristo; kwa nini CCP inawatesa Wakristo na kuwanyima haki yao ya maisha? Kwa nini inashutumu na kukandamiza maonyesho ya Kristo kuhusu ukweli wa kuokoa wanadamu? Kwa nini inawazuia watu kutafuta ukweli, kumfuata Kristo na kutembea katika njia sahihi ya maisha ya mwanadamu? Kwa nini inakataza kuhubiri na kushuhudia kuwasili kwa Mwokozi kati ya wanadamu? Mnaiita hii serikali ya kitaifa? Sheria ziko wapi, kanuni za mbinguni? Haki za binadamu ziko wapi, uhuru uko wapi? Uchina ni shimo la shetani! Ni sawa na sahihi kumwamini Mungu, kumfuata na kumshuhudia Kristo; mimi ni Mkristo, na ni haki yangu kuchagua njia ya uzima!

Iliyotangulia: 158 Ni Nani Anayeufikiria Moyo wa Mungu?

Inayofuata: 162 Kukimbia Kuelekea Njia ya Mwanga

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

64 Upendo wa Kweli

1Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao,nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini.Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki