Swali la 1: Unashuhudia kwamba Mungu amepata mwili na kuwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, lakini wachungaji na wazee wengi wa dini wameamua kwamba wakati ambapo Bwana atarudi Atashuka juu ya wingu. Hili kimsingi ni kulingana na maandiko haya: “Huyu Yesu, ambaye amechukuliwa kutoka kwa ninyi kwenda mbinguni, atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni” (Matendo 1:11). “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye(Ufunuo 1:7). Aidha, wachungaji na wazee wa dini pia wametufundisha kwamba Bwana Yesu yeyote ambaye hashuki juu ya wingu ni wa uongo na anapaswa kukataliwa. Hatujui kama dhana hii inalingana na Biblia au la. Je, kweli huu ni ufahamu sahihi?

Jibu:

Tukiisoma Biblia kwa makini, haitakuwa vigumu kupata ushahidi wa hili. Katika vifungu mbalimbali kadhaa kutoka kwa Biblia, inatabiriwa waziwazi kwamba kuja kwa Mungu mara ya pili ni kupata mwili. Kwa mfano: “Kuweni tayari pia: kwani Mwana wa Adamu atakuja wakati ambapo hamfikiri” (Luka 12:40). “Kwa kuwa kama vile umeme, umulikavyo toka upande mmoja chini ya mbingu, na kumulika upande mwingine chini ya mbingu; ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. Lakini kwanza, ni lazima apate mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki” (Luka 17:24-25). Unabii wote huu unazungumza kuhusu “Mwana wa Adamu” au “Mwana wa Adamu atakuja.” Msemo huu “Mwana wa Adamu” unahusu Yule ambaye amezaliwa kwa mwanadamu na ana ubinadamu wa kawaida. Kwa hiyo Roho hawezi kuitwa Mwana wa Adamu. Kwa mfano, kwa kuwa Yehova Mungu ni Roho, Hawezi kuitwa “Mwana wa Adamu.” Watu wengine wameona malaika, malaika pia ni viumbe wa kiroho, kwa hiyo hawawezi kuitwa Mwana wa Adamu. Wale wote walio na sura ya mwanadamu lakini wana miili ya kiroho hawawezi kuitwa “Mwana wa Adamu.” Bwana Yesu aliyepata mwili Aliitwa “Mwana wa Adamu” na “Kristo” kwa sababu alikuwa mwili wa Roho wa Mungu na kwa hiyo Akawa mwanadamu wa kawaida, Akiishi miongoni mwa wanadamu wengine. kwa hiyo wakati Bwana Yesu alisema “Mwana wa Adamu” na “Mwana wa Adamu atakuja,” Alikuwa akirejelea kuja kwa Mungu kwa njia ya kupata mwili katika siku za mwisho.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Bwana Yesu kwa kurudiarudia Alitabiri kwamba Angekuja tena kama Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu linaashiria Mungu mwenye mwili, kama vile Bwana Yesu katika mwili ambaye anaonekana kama mtu wa kawaida, asiye wa ajabu kwa nje, anayekula, kunywa, kulala na kutembea kama mwanadamu wa kawaida. Lakini mwili wa kiroho wa Bwana Yesu baada ya kufufuka ulikuwa tofauti, ambao ungeweza kupenyeza kuta, kuonekana na kupotea. Ulikuwa hasa wa kimiujiza. Hivyo Hangeitwa Mwana wa Adamu. Alipokuwa akitabiri kuhusu kurudi kwa Mwana wa Adamu, Bwana Yesu alisema, “Lakini kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24). Bwana atarudi kama mwili wa kiroho ukishuka juu ya wingu na kuonekana hadharani kwa utukufu mkuu, wakati watu wote lazima wainame na kuabudu, ni nani angethubutu kumpinga au kumshutumu? Bwana Yesu alisema, “Lakini kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24). Maneno haya yatatimizwaje? Ni pale ambapo tu Mungu mwenye mwili anaonekana kufanya kazi kama Mwana wa Adamu, wakati watu hawatambui kwamba Yeye ni Kristo mwenye mwili, ndio watathubutu kumshutumu na kumkataa Kristo kulingana na mawazo na dhana zao wenyewe. Je, hamwoni kuwa hii ndiyo hali? Aidha, Bwana Yesu pia alitabiri, “Lakini kuhusu siku hiyo na saa hiyo hakuna mwanadamu aijuaye, hakuna, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, bali Baba” (Mathayo 13:32). “Iwapo basi hutakesha, nitakujia kama mwizi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako” (Ufunuo 3:3). Kama Bwana Yesu angeshuka juu ya wingu katika mwili wa kiroho, basi kila mtu angejua kulihusu na angeweza kuliona. Lakini Bwana Yesu alitabiri Atakaporudi, ni “hakuna mwanadamu aijuaye,” “wala Mwana” na “kama mwizi.” Maneno haya yatatimizwaje? Kama Bwana Yesu angeonekana katika mwili wa kiroho, Angekosaje kujua kulihusu Mwenyewe? Ni wakati tu ambapo Mungu anakuwa mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho, kuwa mtu wa kawaida, ndiyo maneno kwamba Mwana hatajua kulihusu yatatimia. Kama tu Bwana Yesu asemavyo, kabla ya kufanya huduma Yake, hata Yeye hakujua kuhusu utambulisho Wake kama Kristo aliyekuja kutimiza kazi ya ukombozi. Hivyo, Bwana Yesu mara nyingi aliomba kwa Mungu Baba. Mpaka pale ambapo Bwana Yesu alianza kutimiza huduma Yake, ni hapo tu ndipo alitambua utambulisho Wake.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Bwana Yesu alitabiri kuwa Atarudi na Akasema maneno mengi kuihusu, lakini nyinyi mnashikilia tu unabii kuwa Bwana atashuka na mawingu na hamtafuti na kuchunguza nabii zingine muhimu zilizoongelewa na Bwana. Hii inafanya kutembea katika njia mbaya kuwa rahisi na kuachwa na Bwana! Kweli sio tu unabii wa “kushuka na mawingu” ndiyo upo katika Biblia. Kuna unabii mwingi kama huo kuwa Bwana atakuja kama mwizi na kushuka kwa siri. Kwa mfano, Ufunuo 16:15, “Tazama, mimi nakuja kama mwizi.” Mathayo 25:6, “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha.” Na Ufunuo 3:20, “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi.” Unabii huu wote unarejelea Mungu kuwa mwili kama Mwana wa Adamu na kushuka kwa siri. “Kama mwizi” kunamaanisha kuja kwa upole, kwa siri. Watu hawatajua kuwa Yeye ni Mungu hata kama watamwona au kumsikia, kama tu ilivyokuwa awali wakati Bwana Yesu alitokea na kufanya kazi Yake wakati wa kupata mwili Kwake kama Mwana wa Adamu. Kutoka nje, Bwana Yesu alikuwa tu Mwana wa Adamu wa kawaida na hakuna yeyote alijua Yeye ni Mungu, ndiyo sababu Bwana Yesu alitumia “kama mwizi” kama analojia ya kutokea na kazi ya Mwana wa Adamu. Hii ni inastahili sana! Wale ambao hawapendi ukweli, bila kujali jinsi Mungu katika mwili anavyoongea au kufanya kazi, au ukweli ngapi Anaoonyesha, hawakubali. Badala yake, wanamchukulia Mungu mwenye mwili kama mtu wa kawaida na kumshutumu na kumwacha Yeye. Hiyo ndiyo sababu Bwana Yesu alitabiri kuwa Atarudi: “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24-25). Kulingana na unabii wa Bwana, kurudi Kwake kutakuwa “kuja kwake Mwana wa Adamu.” “Mwana wa Adamu” inarejelea Mungu katika mwili, sio mwili wa kiroho uliofufuka wa Bwana Yesu ukishuka na mawingu kuonekana wazi mbele ya watu wote. Mbona hali ni hii? Ikiwa ungekuwa mwili wa kiroho uliofufuka wa Bwana Yesu ambao ungekuwa unashuka kwa watu wote na mawingu, ingekuwa nguvu ya ajabu na ya kushtua ulimwengu. Kila mtu angeanguka chini na hakuna yeyote atathubutu kukataa. Kwa hali hiyo, je, Bwana Yesu aliyerudi bado Atastahimili mateso mengi na kukataliwa na kizazi hiki? Bila shaka hapana! Hiyo ndiyo sababu Bwana Yesu alitabiri kuwa kurudi Kwake kutakuwa “kuja kwake Mwana wa Adamu” na “kama mwizi.” Kwa kweli, inarejelea Mungu mwenye mwili kama Mwana wa Adamu kufika kwa siri.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Sasa, injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu imekuwa ikienezwa Bara Uchina kote kwa zaidi ya miaka 20. Imeenea kwa kina hadi madhehebu na vikundi mbalimabali. Katika wakati huu, kwa sababu ya ukandamizaji wa hasira na kuchukuliwa hatua za kinidhamu na serikali ya CCP, pamoja na kampeni ya propaganda ya vyombo vya habari ya CCP, Mwenyezi Mungu tayari ni jina ya kaya ambao kila mtu anaijua. Baadaye, ukweli wote ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu na video na filamu mbalimbali za Kanisa la Mwenyezi Mungu zimekuwa zikitolewa hatua kwa hatua mtandaoni, ikienezwa kote ulimwenguni. Watu katika ulimwengu wa kidini wote wamesikia kuihusu utaratibu wa ushuhuda mbalimbali za Kanisa la Mwenyezi Mungu. Watu wengi sana wametoa ushuhuda kuwa Mungu Amerejea. Hii kwa kikamilifu inatimiza unabii wa Bwana Yesu: “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6). Basi kwa nini wachungaji na wazee wa kanisa wa kidini bado kwa hasira wanashutumu na kukataa kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho? Kuna unabii mwingi sana kuhusu kurudi kwa Bwana katika Biblia, hivyo kwa nini wamekazia macho unabii kuhusu Bwana kushuka na mawingu? Kwa nini hawatafuti kabisa wanaposikia kuna ushuhuda ingine kuhusu kuja kwa Bwana? Kwa nini, wakati wanajua kuwa Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi na wameona halisi ya kazi ya Mungu, je, bado kwa ukaidi wameshikilia dhana na fikira zao za kukataa na kushutumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Je, watu hawa wanapenda ukweli na kwa kweli kutarajia kurudi kwa Bwana au la? Je, hao ni bikira wenye busara au bikira wapumbavu? Ikiwa hao ni bikira wenye busara na kwa kweli wanatarajia kurudi kwa Bwana, basi mbona, wanaposikia sauti ya Mungu na kuona injili ya ufalme ikisitawi, bado kwa ukaidi wanashutumu na kukataa? Je, huu unaweza kuwa uaminifu wao wa kutamani na kutarajia Bwana aonekane? Je, hii inaweza kuwa ishara yao halisi ya kufurahia kurudi kwa Bwana? Hatimaye, kwa kweli, imani yao katika Bwana na kutarajia kurudi kwa Bwana Yesu ni buni, lakini kutarajia kwao kubarikiwa na kuingia katika ufalme wa mbinguni ni kweli! Wanaamini kwa Bwana sio kwa ajili ya kutafuta ukweli na kupata uzima, sio kwa ajili ya kupata ukweli na kwenda mbali ya dhambi. Ni nini wanachojali zaidi kuhusu? Ni wakati Bwana Atashuka kuwachukua moja kwa moja juu katika ufalme wa mbinguni na kuwafanya waepuke mateso ya mwili na kufurahia baraka za ufalme wa mbinguni. Hili ni kusudi lao halisi la kumwamini Mungu! Mbali na sababu hii, ni sababu gani waliyo nayo ya kukana Mwenyezi Mungu, Anayeonyesha ukweli kuokoa binadamu? Kila mtu anaweza kufikiria kuihusu. Ikiwa mtu anapenda ukweli na kwa kweli anatamani Mungu Aonekane, watafanyaje wakati wanaposikia kuwa Bwana Amekuja? Hawatasikiliza, hawataangalia, hawatawasiliana nayo? Je, watakana kwa upofu, kushutumu na kukataa? Bila shaka hapana! Kwa sababu mtu ambaye kwa dhati anatamani kuonekana kwa Mungu na anakaribisha kufika kwa Mungu anatarajia mwanga wa kweli kuonekana, ukweli na haki zikitawala moyoni mwake. Anatarajia kuja kwa Mungu kuwaokoa binadamu na kuwasaidia watu kuepuka dhambi kabisa ili kutakaswa na kupatwa na Mungu. Lakini wale ambao wanangoja tu Bwana kushuka na mawingu bado wanakataa na kumkana Mwenyezi Mungu, hasa wale viongozi wa kidini ambao kwa hasira wanashutumu na kumkataa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhifadhi hali na maisha yao—hao ni watu wote ambao wanadharau ukweli na kuchukia ukweli. Wote ni wasioamini na wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu wa siku za mwisho. Baada ya Mungu katika mwili kumaliza kazi Yake ya wokovu, hawa watu wataanguka ndani ya maafa hayo ya mmoja kati ya miaka milioni, wakilia na kusaga meno yao. Basi unabii wa Bwana kushuka na mawingu kuonekana wazi utakuwa umetimizwa kikamilifu: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye” (Ufunuo 1:7).

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: 8. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Inayofuata: Swali la 2: Ingawa wale wanaomwamini Bwana wanajua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, watu wachache sana wanaelewa ukweli wa kupata mwili. Wakati ambapo Bwana atarudi, Akionekana tu kama Bwana Yesu alivyofanya, akiwa Mwana wa Adamu na kufanya kazi, watu kweli hawatakuwa na njia ya kumtambua Bwana Yesu na kukaribisha kurudi Kwake. Kwa hiyo kupata mwili kweli ni nini? Ni nini kiini cha kupata mwili?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp