Swali la 2: Ingawa wale wanaomwamini Bwana wanajua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, watu wachache sana wanaelewa ukweli wa kupata mwili. Wakati ambapo Bwana atarudi, Akionekana tu kama Bwana Yesu alivyofanya, akiwa Mwana wa Adamu na kufanya kazi, watu kweli hawatakuwa na njia ya kumtambua Bwana Yesu na kukaribisha kurudi Kwake. Kwa hiyo kupata mwili kweli ni nini? Ni nini kiini cha kupata mwili?

Jibu:

Kuhusu swali la ni nini kupata mwili, na ni nini kiini cha Mungu mwenye mwili, mngesema, hii ni siri ya ukweli ambao hakuna muumini anayeelewa. Ingawa waumini kwa maelfu ya miaka wamejua kwamba Bwana Yesu ni kupata mwili kwa Mungu, hakuna anayeelewa kupata mwili na kiini halisi cha kupata mwili. Ni sasa tu ambapo Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho amekuja, ndipo kipengele hiki cha siri ya ukweli kimefichuliwa kwa mwanadamu.

…………

Kupata mwili ni Roho wa Mungu aliyevaa mwili, yaani , Roho wa Mungu anatokea katika mwili akiwa na ubinadamu wa kawaida na fikira za mwanadamu za kawaida, na hivyo anakuwa mtu wa kawaida Akifanya kazi na kuzungumza miongoni mwa wanadamu. Mwili huu una ubinadamu wa kawaida, lakini pia una uungu kamili. Ingawa kwa sura ya nje mwili Wake unaonekana ni wa kawaida, Anaweza kuifanya kazi ya Mungu, Anaweza kuonyesha sauti ya Mungu, kuwaongoza na kuwaokoa wanadamu. Hili ni kwa sababu ana uungu kamili. Uungu kamili unamaanisha kwamba chote ambacho Roho wa Mungu anamiliki—tabia ya asili ya Mungu, Kiini cha Mungu takatifu na cha haki, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu za Mungu—haya yote yametokea katika mwili. Mwili huu ni Kristo, ni Mungu wa vitendo ambaye Yuko hapa duniani kufanya kazi na kuwaokoa wanadamu. Kutokana na sura Yake ya nje, Kristo ni Mwana wa Adamu wa kawaida, lakini Yeye ni tofauti na mwanadamu yeyote aliyeumbwa kwa kweli. Mwanadamu aliyeumbwa ana ubinadamu pekee, hana hata dalili yoyote ya kiini cha uungu. Kristo, hata hivyo, hana ubinadamu wa kawaida pekee; la muhimu zaidi, Ana uungu kamili. Kwa hiyo, Ana kiini cha Mungu, Anaweza kumwakilisha Mungu kabisa, kuonyesha ukweli wote kama Mungu Mwenyewe, kuonyesha tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho, na kumjalia mwanadamu na ukweli, njia, na uzima. Hakuna mwanadamu aliyeumbwa anaweza kufanya matendo magumu kama hayo. Kristo anafanya kazi na kunena, Anaonyesha tabia ya Mungu, na chote ambacho Mungu anacho na Alicho katika mwili Wake. Haijalishi vile Anavyoonyesha neno la Mungu na kufanya kazi ya Mungu, Yeye hufanya hivyo daima katika ubinadamu wa kawaida. Ana mwili wa kawaida, hakuna chochote cha ajabu kumhusu. Hili linathibitisha kwamba Mungu amekuja katika mwili, Amekuwa mwanadamu wa kawaida tayari. Mwili huu wa kawaida umetimiza ukweli wa “Neno Laonekana katika Mwili.” Yeye ni Mungu mwenye mwili wa vitendo. Kwa kuwa Kristo ana uungu kamili, Anaweza kumwakilisha Mungu, kuonyesha ukweli, na kuwaokoa wanadamu. Kwa kuwa Kristo ana uungu kamili, Anaweza kuonyesha neno la Mungu moja kwa moja, sio tu kupeleka au kupitisha neno la Mungu. Anaweza kuonyesha ukweli wakati wowote na mahali popote, Akiruzuku, Akinyunyizia, na kumchunga mwanadamu, Akiwaongoza wanadamu wote. Ni kwa sababu tu Kristo ana uungu kamili, na Anamiliki utambulisho na kiini cha Mungu, ndio tunaweza kusema kwamba Yeye ni kupata mwili kwa Mungu, Mungu Mwenyewe wa vitendo.

Siri kubwa zaidi ya kupata mwili haina uhusiano na kama mwili wa Mungu ni mkubwa kwa kimo au kama ule wa mwanadamu wa kawaida. Badala yake inahusu ukweli kwamba uungu kamili umejificha ndani ya mwili huu wa kawaida. Hakuna mwanadamu anayeweza kugundua au kuuona uungu huu. Kama tu wakati ambapo Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, kama mtu yeyote hangekuwa amesikia sauti Yake na kupitia neno na kazi Yake, basi hakuna ambaye angetambua kwamba Bwana Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu. Kwa hiyo kupata mwili kwa Mungu ndiyo njia bora zaidi ya Yeye kushuka kisirisiri miongoni mwa wanadamu. Wakati Bwana Yesu alikuja, hakuna mtu angeweza kujua kutokana na sura Yake ya nje kwamba Alikuwa Kristo, Mungu mwenye mwili, na hakuna mtu angeweza kuona uungu uliofichwa ndani ya ubinadamu Wake. Ni baada tu ya Bwana Yesu kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya ukombozi wa wanadamu, ndipo mwanadamu aligundua kwamba neno Lake lina mamlaka na nguvu, na wakati huo tu ndipo wanadamu walianza kumfuata. Ni wakati ambao Bwana Yesu alionekana kwa watu baada ya kufufuka tu, ndipo walitambua kwamba Yeye ni Kristo mwenye mwili, kuonekana kwa Mungu. Kama hangekuwa ameonyesha ukweli na kufanya kazi Yake, hakuna mtu angemfuata. Kama hangeshuhudia ukweli kwamba Yeye ni Kristo, kuonekana kwa Mungu, hakuna mtu angemtambua. Kwa kuwa mwanadamu anaamini kwamba kama Yeye ni Mungu mwenye mwili kweli, mwili Wake unapaswa kuwa na sifa za miujiza, Anapaswa kupita uwezo wa binadamu, Awe mwenye kimo kipana, cha nguvu, na umbo refu, Hapaswi kuzungumza na mamlaka na nguvu tu, bali Anapaswa pia kufanya ishara na miujiza popote Aendapo—hivi ndivyo Mungu aliyepata mwili Anapaswa kufanana. Kama Yeye ni wa kawaida katika sura ya nje, kama mwanadamu mwingine yeyote wa kawaida, na ana ubinadamu wa kawaida, basi Yeye bila shaka si kupata mwili kwa Mungu. Hebu tukumbuke tena, wakati Bwana Yesu alipata mwili kunena na kufanya kazi, haijalishi vile Alivyoonyesha ukweli na sauti ya Mungu, hakuna aliyemtambua. Makuhani wakuu, waandishi, Mafarisayo wa Kiyahudi sana hawakumtambua. Wakati walimsikia mtu fulani akitoa ushuhuda kwa Bwana Yesu hata walisema: Huyu si mwana wa Yusufu? Je, huyu si Mnazareti? Kwa nini makuhani wakuu, waandishi, Mafarisayo wazungumze hivi kumhusu? Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa na ubinadamu wa kawaida katika sura ya nje. Alikuwa mtu wastani, wa kawaida, na Hakuwa na umbo refu, kwa hiyo hakuna aliyemkubali. Kwa kweli, hata ingawa Yeye ni Aliyepata mwili, Anapaswa kuwa na ubinadamu wa kawaida kwa hakika, Anapaswa kuwaonyesha watu kwamba mwili ambao Mungu anajivika ni mwili wa kawaida, Anaonekana kama mwanadamu wa kawaida. Kama Mungu angejivika mwili wa anayepita uwezo wa binadamu, usio wa mtu aliye na ubinadamu wa kawaida, basi maana yote ya kupata mwili ingepotea. Kwa hiyo, lazima Kristo awe na ubinadamu wa kawaida. Ni kwa njia hii pekee ndio inaweza kuthibitishwa kwamba Yeye ni Neno aliyepata mwili.

…………

Tunaona waziwazi kwamba Mungu mwenye mwili lazima awe na ubinadamu wa kawaida, la sivyo, Hangekuwa kupata mwili kwa Mungu. Katika umbo la nje, Anafanana na mtu wa kawaida, na hakuna chochote cha miujiza kuhusu ubinadamu Wake. Kwa hiyo, tukimpima Kristo tukitumia dhana na mawazo yetu, hatutawahi kumkiri au kumkubali Kristo. Kwa kiwango kikubwa zaidi tutakiri tu kwamba Yeye ni nabii Aliyetumwa na Mungu, au yule ambaye Mungu hutumia. Ikiwa tunataka kumjua Kristo kweli, lazima tuchunguze maneno yake na kazi kuona kama kile ambacho Anaonyesha ni sauti ya Mungu Mwenyewe, ikiwa maneno Anayoonyesha ni madhihirisho ya tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho, na kuona kama kazi Yake na ukweli Anaoonyesha unaweza kuwaokoa wanadamu. Wakati huo tu ndipo tunaweza kumjua, kumkubali na kumtii Kristo. Ikiwa hatutafuti ukweli, hatuchunguzi kazi ya Mungu, hata tukiyasikia maneno ya Mungu na kuiona kazi ya Kristo, bado hatutamjua Kristo. Hata kama tuko na Kristo tangu asubuhi mpaka usiku, bado tutamchukulia kama mwanadamu wa kawaida na hivyo tutampinga na kumshutumu Kristo. Kwa kweli, ili kumkiri na kumkubali Kristo, yote tunayohitaji kufanya ni kuitambua sauti ya Mungu na kukiri kwamba Anafanya kazi ya Mungu. Lakini kujua kiini cha uungu wa Kristo na hivyo kutimiza utiifu wa kweli kwa Kristo na kumpenda Mungu wa vitendo, lazima tugundue ukweli ndani ya maneno na kazi ya Kristo, tuone tabia ya Mungu na chote ambacho Mungu anacho na Alicho, tuone kiini kitakatifu, uweza, na hekima ya Mungu, tuone kwamba Mungu ni mwenye upendo na tukubali makusudi Yake yenye ari. Ni kwa namna hii tu ndio mtu anaweza kumtii Kristo kweli na kumwabudu Mungu wa vitendo katika moyo wake.

Sisi waumini sote tunajua kwamba namna ambayo Bwana Yesu alihubiri, neno Aliloonyesha, siri za ufalme wa mbinguni ambazo Alifichua, na matakwa Aliyotoa kwa mwanadamu yote yalikuwa ukweli, yote yalikuwa sauti ya Mungu Mwenyewe, na yote yalikuwa madhihirisho ya tabia ya maisha ya Mungu na chote ambacho Anacho na Alicho. Miujiza aliyofanya—kuwaponya wagonjwa, kutoa pepo, kutuliza upepo na bahari, kuwalisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili, na kuwafufua wafu—yote yalikuwa madhihirisho ya mamlaka na nguvu za Mungu Mwenyewe, ambavyo hakuna mwanadamu aliyeumbwa aliye navyo au anayeweza kuwa navyo. Wale walioutafuta ukweli wakati huo, kama vile Petro, Yohana, Mathayo, na Nathanieli, walitambua kutoka kwa neno na kazi ya Bwana Yesu kwamba Yeye ni Masihi aliyeahidiwa, na hivyo wakamfuata na wakapokea wokovu Wake. Ilhali Mafarisayo wa Kiyahudi, licha ya kusikia mahubiri ya Bwana Yesu na kumwona Akifanya miujiza, bado walimwona kama mtu wa kawaida tu, Asiye na nguvu au kimo, Kwa hiyo walithubutu kumpinga na kumshutumu vikali bila woga hata kidogo. Mwishowe walitenda dhambi kubwa zaidi kwa kumpigilia misumari Bwana Yesu juu ya msalaba. Somo la Mafarisayo linahitaji tafakari ya kina! Hili linafichua waziwazi asili yao ya mpinga Kristo ya kuchukia ukweli na kumchukia Mungu, na inafichua upumbavu na ujinga wa wanadamu wapotovu. Wakati huu, Mwenyezi Mungu aliyepata mwili, kama tu Bwana Yesu, Anafanya kazi ya Mungu Mwenyewe ndani ya ubinadamu wa kawaida. Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote ambao wanadamu wapotovu wanahitaji ili kuokolewa, na Anatekeleza kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Yeye hahukumu na kufichua tu asili ya kishetani ya wanadamu wapotovu na ukweli wa upotovu wao, Amefichua pia siri zote za mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita wa kuwaokoa wanadamu, Amefafanua njia ambayo wanadamu wanaweza kuwekwa huru kutoka kwa dhambi, watakaswe na kuokolewa na Mungu, Amefichua tabia yenye haki ya asili ya Mungu, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, na nguvu na mamlaka ya Mungu ya pekee…. neno na kazi ya Mwenyezi Mungu ni dhihirisho kamili la utambulisho na kiini cha Mungu Mwenyewe. Siku hizi, wale wote wanaomfuata Mwenyezi Mungu wamesikia sauti ya Mungu katika neno na kazi ya Mwenyezi Mungu, wameona dhihirisho la neno la Mungu katika mwili na wamekuja mbele za kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, wakipokea utakaso na kukamilishwa kwa Mungu. Wale wa ulimwengu wa kidini ambao bado wanakana, wanapinga, na kushutumu Mwenyezi Mungu wamefanya kosa lile lile kama la Mafarisayo wa Kiyahudi, wakimtendea Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, kama mtu mwingine yeyote wa kawaida, bila kujali kutumia jitihada hata kidogo kutafuta na kuchunguza ukweli wote ambao Mwenyezi Mungu ameonyesha, hivyo wanampigilia Mungu misumari msalabani tena na kukasirisha tabia ya Mungu. Kama awezavyo kuona mtu, ikiwa mwanadamu anashikilia dhana na fikira zake, na hatafuti na kuchunguza ukweli ambao Kristo anaonyesha, hataweza kutambua sauti ya Mungu inayoonyeshwa na Kristo, hataweza kukubali na kutii kazi ya Kristo, na hatawahi kupokea wokovu wa Mungu katika siku za mwisho. Ikiwa mwanadamu haelewi ukweli wa kupata mwili, hataweza kukubali na kutii kazi ya Mungu, Atamshutumu Kristo na kumpinga Mungu, na kuna uwezekano pia wa yeye kupokea adhabu na laana za Mungu. Kwa hiyo, katika imani yetu, ili kuokolewa na Mungu, ni muhimu kabisa tutafute ukweli na kuelewa siri ya kupata mwili!

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: Swali la 1: Unashuhudia kwamba Mungu amepata mwili na kuwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, lakini wachungaji na wazee wengi wa dini wameamua kwamba wakati ambapo Bwana atarudi Atashuka juu ya wingu. Hili kimsingi ni kulingana na maandiko haya: “Huyu Yesu, ambaye amechukuliwa kutoka kwa ninyi kwenda mbinguni, atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni” (Matendo 1:11). “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye(Ufunuo 1:7). Aidha, wachungaji na wazee wa dini pia wametufundisha kwamba Bwana Yesu yeyote ambaye hashuki juu ya wingu ni wa uongo na anapaswa kukataliwa. Hatujui kama dhana hii inalingana na Biblia au la. Je, kweli huu ni ufahamu sahihi?

Inayofuata: Swali la 3: Mbona Mungu amepata mwili katika siku za mwisho, akiwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu? Ni nini tofauti ya kweli kati ya mwili wa roho wa Bwana Yesu kufufuliwa kutoka kwa kifo na Mwana wa Adamu mwenye mwili? Hili ni suala ambalo hatulielewi—tafadhali shiriki ushirika kuhusu hili.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp