716 Ni Wale tu walio na Ukweli Wanaweza Kuishi kwa Kudhihirisha Maisha Halisi
1 Ikiwa watu wana ufahamu wa kweli wa tabia ya Mungu, na wanaweza kutoa sifa ya kweli kwa utakatifu Wake na haki Yake, basi wanajua Mungu kwa kweli na kumiliki ukweli; ni hapo tu ndipo wanaishi nuruni. Ni wakati tu ambapo maoni ya watu kuhusu dunia na maisha yanabadilika ndipo wanabadilika kimsingi. Mtu anapokuwa na lengo la maisha na kujiheshimu kulingana na ukweli, mtu anapomtii Mungu kabisa na kuishi kulingana na neno la Mungu, mtu anapohisi kuwa na amani na kuchangamshwa ndani ya roho yake, moyo wa mtu unapokuwa huru bila giza, na mtu anapoishi kwa huru kabisa na bila kuzuiwa kwa uwepo wa Mungu—hapo tu ndipo atakapoishi maisha ya mwanadamu ya kweli na kuwa mtu anayemiliki ukweli.
2 Ukweli wote unaomiliki unatoka kwa neno la Mungu na kwa Mungu Mwenyewe. Mtawala wa ulimwengu mzima na kila kitu—Mungu Mkuu Zaidi—Anakupenda wewe, kama mtu halisi anayeishi maisha ya kweli ya mwanadamu. Je, nini linaweza kuwa la maana zaidi kuliko kibali cha Mungu? Mtu wa aina hii ni yule aliye na ukweli. Mungu tu ndiye ukweli. Mungu hudhibiti mbingu na dunia na vyote vilivyomo na ana mamlaka juu ya vyote. Kutoamini Mungu, kutomtii Mungu ni kutokuwa na uwezo wa kupata ukweli. Ukiishi kulingana na neno la Mungu, utahisi uwazi, udhabiti, na utamu usioweza kulinganishwa ndani kabisa ya moyo wako; utakuwa umepata uzima kwa kweli.
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo