773 Uko Tayari Kumpa Mungu Upendo Ulio Moyoni Mwako

1 Ikiwa mtu anaamini katika Mungu lakini hana kusudi la kufuatilia, basi maisha yake huwa kazi bure, na wakati ufikapo wa yeye kufa, wao wana anga la samawati na ardhi ya vumbi tu ya kutazama. Je, hayo ni maisha ya maana? Ikiwa unaweza kutimiza masharti ya Mungu ukiwa bado hai, hili si jambo zuri? Mbona kila mara unatafuta tatizo, na mwenye huzuni? Katika ahadi Niliyofanya na Mungu, Mimi nampa tu moyo Wangu na Simpumbazi kwa maneno Yangu. Singefanya kitu kama hicho—Mimi niko radhi tu kumfariji Mungu Nimpendaye kwa moyo Wangu, ili Roho Wake aliye mbinguni afarijiwe. Moyo unaweza kuwa na thamani lakini upendo una thamani kuu zaidi. Niko radhi kumtolea Mungu upendo wa thamani kubwa zaidi moyoni Mwangu ili kile Anachofurahia kiwe ni kitu kizuri zaidi Nilichonacho, ili Akamilishwe na upendo Ninaomtolea Yeye.

2 Je, uko radhi kumpa Mungu upendo wako ili Afurahie? Je, uko radhi kuifanya hii kuwa raslimali yako wewe ya kuendelea kuishi? Ninachoona kutokana na uzoefu Wangu ni kwamba kadri Ninavyompa Mungu upendo mwingi, ndivyo Ninavyohisi kwamba Ninaishi kwa furaha, na Nina nguvu zisizo na mipaka, Niko radhi kutoa mwili na mawazo Yangu yote kama dhabihu, na kuhisi kila mara kwamba Siwezi kabisa kumpenda Mungu vya kutosha. Ikiwa kweli unataka kumpenda Mungu, utakuwa kila mara na upendo zaidi wa kumrudishia Yeye. Ikiwa hali ni hiyo, ni mtu gani na ni kitu gani kina uwezo wa kuzuia upendo wako kwa Mungu? Mungu huona upendo wa wanadamu wote kuwa wa thamani; Yeye hulimbikiza baraka Zake nyingi zaidi juu ya wote wanaompenda Yeye. Hii ni kwa sababu upendo wa mwanadamu ni mgumu sana kupatikana, kunao kidogo sana, na nusura usiweze kupatikana.

Umetoholewa kutoka katika “Njia … (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 772 Kadri Unavyozidi kumridhisha Mungu, Ndivyo Unavyozidi Kubarikiwa

Inayofuata: 774 Maonyesho ya Petro ya Upendo kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp