732 Kwa Nini Mwanadamu Humdai Mungu Kila Mara?
1 Bila kujali kinachotokea kwao, au wanachoshughulikia, watu daima hulinda masilahi yao wenyewe na hulinda miili yao, na wao daima hutafuta sababu au kisingizio kinachowasaidia. Wao hawana ukweli hata kidogo, na kila kitu wanachofanya ni ili kutetea miili yao wenyewe na kwa kuzingatia matarajio yao wenyewe. Wote wanadai neema kutoka kwa Mungu, wakijaribu kupata manufaa yoyote wanayoweza kupata. Kwa nini wao hudai makubwa mno kwa Mungu? Hii inathibitisha kwamba watu kwa kawaida ni wenye tamaa. Hawana hisia yoyote mbele za Mungu, na katika kila kitu wanachofanya—iwe ni kuomba au kuwasiliana kwa karibu au kuhubiri—katika kile wanachofuatilia, na katika mawazo yao ya ndani na tamaa zao, wanamdai Mungu na kudai vitu kutoka Kwake, wakitumai kupata kitu kutoka Kwake. Hii inahusiana na asili ya binadamu.
2 Kwamba watu humdai Mungu madai mengi na wana tamaa nyingi mno za kupita kiasi za kuhusiana na Yeye inathibitisha kuwa ndani yao hakuna hisia yoyote inayopaswa kuwa na binadamu. Wao hudai haya kwa ajili yao wenyewe, au wanajaribu kuthibitisha uhalali na kutafuta udhuru kwa ajili yao wenyewe. Katika vitu vingi inaweza kuonekana kuwa kila kitu wanachokifanya hakina maana kabisa, jambo ambalo ni thibitisho kamili la mantiki ya Shetani ya “Kila mtu ajitetee mwenyewe au aangamie.” Ni tatizo lipi linathibitishwa na watu kumdai Mungu kupita kiasi? Inathibitisha kiwango cha kupotoshwa kwao na Shetani, ambayo inamaanisha kuwa, katika imani yao katika Mungu, watu hawamchukulii kama Mungu hata kidogo. Kwa nje, unamfuata Mungu, lakini katika mtazamo wako Kwake, na katika maswala mengi na maoni yako mengi, humchukulii kama Muumba hata kidogo.
Umetoholewa kutoka katika “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo