1027 Wanadamu Waingiapo Mapumzikoni

1 Mwanadamu aingiapo rahani, watenda maovu wataangamizwa, binadamu wote wataingia katika njia sahihi, na watu wa kila aina watakuwa na aina yao kulingana na kazi wanayopaswa kufanya. Hii tu ndiyo itakuwa siku ya binadamu kupumzika na mwenendo usioepukika wa maendeleo ya binadamu, na wakati tu binadamu wataingia rahani ndipo utimilifu mkubwa na wa mwisho wa Mungu utamalizika; hii itakuwa tamati ya kazi Yake. Hii kazi itamaliza maisha ya uharibifu ya kimwili ya binadamu, na itamaliza maisha ya binadamu potovu. Kutoka hapa binadamu wataingia katika ulimwengu mpya.

2 Ingawa mwanadamu anaishi kimwili, kuna tofauti kubwa kati ya kiini cha maisha yake na kiini cha maisha ya binadamu wapotovu. Maana ya kuwepo kwake na maana ya kuwepo kwa binadamu wapotovu pia ni tofauti. Ingawa haya si maisha ya mtu wa aina mpya, inaweza kusemwa kuwa maisha ya binadamu ambao wamepata wokovu na maisha yenye ubinadamu na busara kurejeshwa. Hawa ni watu ambao hawakumtii Mungu wakati mmoja, na ambao walishindwa na Mungu wakati mmoja na baadaye kuokolewa na Yeye; hawa ni watu waliomwaibisha Mungu na baadaye wakamshuhudia. Uwepo wao, baada ya kupitia na kuendelea kuishi baada ya jaribio Lake, ni uwepo wa maana kubwa zaidi; ni watu waliomshuhudia Mungu mbele ya Shetani; ni watu wanaofaa kuishi.

3 Baada ya kushindwa kabisa, Shetani hatawasumbua binadamu tena, na mwanadamu hatakuwa tena na tabia potovu ya kishetani. Wale watu wasiotii watakuwa wameangamizwa tayari, na wale watu wanaotii pekee ndio wataishi. Na basi familia chache sana zitasalimika bila kuharibika; mahusiano ya kimwili yatawezaje kuweko? Maisha ya kimwili ya zamani ya mwanadamu yatapigwa marufuku kabisa, Bila tabia potovu ya kishetani, maisha ya watu hayatakuwa tena maisha ya zamani ya siku zilizopita, lakini badala yake maisha mapya. Watu sasa wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao. Wakati wote watakuwa wameingia rahani hakutakuwa na mahusiano ya kimwili tena. Binadamu kama hawa tu ndio watakuwa wa haki na watakatifu, binadamu kama hawa tu ndio watamwabudu Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1026 Mungu Afanya Mipango ya Kufaa kwa Mwanadamu wa Kila Aina

Inayofuata: 1028 Maisha Mapumzikoni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp