1021 Aandaacho Mungu kwa Binadamu Hakiwezi Kuwazika

1 Kile ambacho Nimewaandalia nyinyi, yaani, hazina nadra za thamani kutoka duniani kote, zote mtapewa nyinyi. Nyinyi hamuwezi kufahamu kuhusu wala hamuwezi kufikiri yote haya kwa sasa, na hakuna mwanadamu aliyefurahia hili hapo kabla. Wakati baraka hizi zitawajia, nyinyi mtajawa na furaha bila kikomo, lakini msisahau kwamba hizi zote ni nguvu Zangu, matendo Yangu, haki Yangu na hata zaidi, uadhama Wangu. (Nitawapa neema wale ambao Nitaamua kuwapa neema, na Nitawahurumia wale ambao Nitaamua kuwahurumia). Wakati huo, ninyi hamtakuwa na wazazi, wala hakutakuwa na mahusiano ya damu. Nyinyi nyote ni watu ambao Nawapenda, wana Wangu wapendwa. Hakuna mtu atakayethubutu kuwakandamiza nyinyi kutoka wakati huo na kuendelea. Utakuwa wakati wenu wa kukua na kuwa watu wazima, na wakati wenu wa kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma!

2 Ni nani anayethubutu kuwazuia Wana wangu wapendwa? Ni nani anayethubutu kuwashambulia wana Wangu wapendwa? Wote watawaheshimu wana Wangu wapendwa kwa sababu Baba ametukuzwa. Vitu vyote ambavyo hakuna mtu angeweza kufikiria daima vitaonekana mbele ya macho yenu. Vitakuwa havina kikomo, wasivyoisha, visivyo na mwisho. Kabla ya muda mrefu, nyinyi hakika hamtahitaji tena kuunguzwa na jua na kuvumilia joto linalotesa. Wala hamtalazimika kuteseka na baridi, wala mvua, theluji au upepo havitawafikia. Hii ni kwa sababu Nawapenda, na yote itakuwa ni dunia ya upendo Wangu. Nitawapa kila kitu mnachotaka, nami Nitawaandaa kwa ajili ya kila kitu ambacho mnahitaji. Nani anathubutu kusema kuwa Mimi si mwenye haki? Nitakuua mara moja, kwa sababu Nimewaambia kabla ya kuwa ghadhabu Yangu (dhidi ya waovu) itaendelea milele, nami Sitaachilia hata kidogo. Hata hivyo, upendo Wangu (kwa wana Wangu wapendwa) pia utaendelea milele.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 84” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1020 Watu Wote wa Mungu Hufungua Hisia Zao

Inayofuata: 1022 Binadamu Wapata Tena Utakatifu Waliokuwa Nao

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp