Kupata Mwili Ni Nini?
Sote tunajua kwamba miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alikuja mwilini katika ulimwengu wa mwanadamu kama Bwana Yesu ili kuwakomboa wanadamu, na Akahubiri, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17). Pia Alionyesha ukweli kiasi kikubwa, na ili kukamilisha kazi ya ukombozi, Alisulubishwa msalabani kama sadaka ya dhambi ya wanadamu, na hivyo kuhitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema. Hii ilikuwa kazi iliyofanywa ili kuwakomboa wanadamu mara ya kwanza Mungu alipokuja katika mwili. Ingawa dini ya Kiyahudi ilijaribu sana kumhukumu Bwana Yesu na kuungana na serikali ya Kirumi kumsulubisha, miaka elfu mbili baadaye, injili ya Bwana Yesu imeenea kote duniani. Hii inathibitisha kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, Mungu mmoja wa kweli na Muumba ambaye Alionekana ili kufanya kazi katika mwili. Lakini watu wengi hawatambui kwamba Bwana Yesu ni Mungu mwenye mwili. Badala yake, wao humchukulia Bwana Yesu kama mtu wa kawaida. Hata wachungaji wengi katika dini hawatambui kwamba Bwana Yesu ni Mungu, na wanafikiri tu kuwa Yeye ni Mwana mpendwa wa Mungu. Leo, ingawa kuna waumini wengi sana wa Bwana, ni watu wachache wanaojua kwa kweli kwamba Bwana Yesu ni Mungu, na hakuna anayejua maana na thamani ya ukweli wote ulioonyeshwa na Bwana Yesu. Kwa hivyo, katika suala la kumkaribisha Bwana, wengi wameanguka katika maafa kwa sababu hawawezi kuisikia sauti ya Mungu. Kwa wale wasioweza kusikia sauti ya Mungu, ingawa kwa nje wanaonekana kuamini kwa shauku, iwapo wangeiona sura ya Mwana wa Adamu katika Bwana Yesu, je, kweli wangeweza kuendelea kumwamini Bwana na kumfuata? Je, wangeweza kumhukumu Bwana Yesu kama mtu wa kawaida na kukana kwamba Yeye ni Mungu? Iwapo wangemsikia Bwana Yesu akionyesha ukweli kiasi kikubwa sana hivi leo, je, bado wangeweza kumhukumu Bwana Yesu kwa kusema maneno ya kumkufuru na kumpigilia misumari msalabani tena? Kulingana na ukweli wa jinsi Mafarisayo walivyomlaani Bwana Yesu, tunaweza kusema kwa hakika kwamba kama wale wote wanaomwamini Bwana leo kweli wangemwona katika mfano Wake wa asili kama Mwana wa Adamu, pana uwezekano mkubwa kwamba watu wengi wangekimbia, na wengi zaidi wangemhukumu na kumlaani Bwana Yesu, kama tu Mafarisayo, na wangemsulubisha msalabani tena. Wengine wanaweza kupinga ninaposema kwa namna hii, lakini kila ninachosema ni ukweli. Hakuna mtu ambaye angeweza kutambua kwamba Mwana wa Adamu mwenye mwili ndiye kuonekana kwa Mungu kwa sababu hasa wanadamu wamepotoka sana, na wao hutegemea tu macho katika kumwamini Mungu. Hii inatuonyesha kwamba kupata mwili ni fumbo kuu. Kwa maelfu ya miaka, hakuna mtu ambaye ameweza kuelewa kipengele hiki cha ukweli. Ingawa waumini wanajua kwamba Bwana Yesu ndiye Mungu mwenye mwili, hakuna ambaye ameweza kueleza kwa uwazi kupata mwili ni nini na jinsi tunavyopaswa kumwelewa Mungu mwenye mwili.
Kwa hivyo, kwa nini Mungu aliamua kupata mwili ili kuonekana na kufanya kazi? Tukizungumza kwa usahihi, upotovu wa wanadamu ulihitaji Mungu kuja katika mwili kufanya kazi ya wokovu. Kwa maneno mengine, kuja katika mwili pekee ndiko kungeweza kutimiza wokovu kamili wa wanadamu. Mungu alipata mwili mara mbili ili kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu. Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, na Alikuja kufanya kazi ya ukombozi. Wengine wanaweza kuuliza, Kwa nini Mungu hakumtumia mtu kufanya kazi ya ukombozi? Kwa nini Mungu alipata mwili? Kwa sababu wanadamu wote waliopotoka hubeba dhambi, sisi sote ni wenye dhambi, kumaanisha kwamba hapakuwa na sadaka za dhambi zilizostahili. Ni Mwana wa Adamu pekee ambaye hakuwa na dhambi, kwa hivyo Mungu alipata mwili kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya ukombozi Mwenyewe. Ni hili pekee lililoonyesha haki na utakatifu wa Mungu kwa kweli, lilimfedhehesha Shetani kabisa na kumuacha bila sababu za kumshtaki Mungu. Hili pia liliruhusu wanadamu kujua upendo wa kweli wa Mungu na huruma Yake kwao. Bwana Yesu alipomaliza kazi ya ukombozi, Alitabiri kwamba Atakuja tena. Leo, Bwana Yesu amerudi, na ndiye Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli kiasi kikubwa na Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho ili kutakasa kabisa upotovu wa wanadamu, kuwaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi na nguvu za Shetani, na kuwaleta wanadamu kwenye hatima nzuri. Lakini kisichotarajiwa ni kwamba, ingawa Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli kiasi kikubwa sana, bado Anapingwa na kulaaniwa vikali na nguvu za wapinga Kristo katika ulimwengu wa kidini, ambao hata wameshirikiana na Chama tawala cha Kikomunisti cha China ili kujaribu kuzuia, kuharibu, na kupiga marufuku kuonekana kwa Mungu na kazi Yake katika siku za mwisho. Wao hufanya kila wawezalo kukana kwamba Mwenyezi Mungu ni kuonekana kwa Mungu mwenye mwili, na pia humshutumu na kumkufuru Mwenyezi Mungu kama mtu wa kawaida, jambo ambalo linafichua wazi kabisa sura mbaya ya nguvu za wapinga Kristo katika ulimwengu wa kidini kama wale wanaochukia ukweli na kumpinga Mungu. Tukitazama nyuma miaka elfu mbili, tunaona kwamba makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo wa dini ya Kiyahudi waliona heri kufa kufa kuliko kumkubali Bwana Yesu kama Masihi. Walimwainisha Bwana Yesu kama mtu wa kawaida ambaye Alizungumza maneno ya kumkufuru Mungu, walifanya yote waliyoweza ili kumpinga, kumhukumu, na kumkufuru Bwana Yesu, na hatimaye wakampigilia misumari msalabani, na kufanya uhalifu mbaya sana uliofanya walaaniwe na kuadhibiwa na Mungu. Leo, Mwenyezi Mungu anaonekana na kufanya kazi kwa mfano wa Mwana wa Adamu. Watu wengi wameona kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, wamesikia sauti ya Mungu, na wote wamekubali kwa furaha kazi ya Mungu katika siku za mwisho na kumkaribisha Bwana. Hata hivyo, kuna watu wengi ambao hawamjui Mungu mwenye mwili, ambao bado wanamchukulia Mwenyezi Mungu kama mtu wa kawaida, na ambao pia wanahukumu na kulaani wale wote wanaomkubali Mwenyezi Mungu, wakisema kwamba wanamwamini mtu wa kawaida. Watu hawa wanafikiri kuwa wanaelewa Biblia, kwa hivyo wanakataa kuchunguza njia ya kweli na kulaani na kumpinga Mwenyezi Mungu kwa hasira, na kutenda dhambi ya kumsulubisha Mungu tena. Kwa nini kupata mwili kwa Mungu mara mbili kumelaaniwa na kukataliwa na mwanadamu? Ni kwa sababu watu hawamjui Mungu, hawaelewi ukweli ni nini, na wanaelewa machache sana kuhusu fumbo kuu la kupata mwili. Pia ni kwa sababu wanadamu wamepotoshwa sana na wana asili ya kishetani. Mbali na kudharau na kuchukia ukweli, pia wana uhasama mkuu na Mungu na hawana hofu hata kidogo. Kwa kweli, kuna waumini wacha Mungu mno ambao wamedanganywa na CCP, mfalme wa pepo, na vikosi vya wapinga Kristo vya kidini kutokana na ujinga wao na wamechukua njia ya kumpinga Mungu. Sababu ya kushindwa kwao ni ukosefu wa maarifa kuhusu kupata mwili na ukweli, kwa hivyo hawawezi kusikia sauti ya Mungu, na kwa hivyo wanamchukulia Mungu mwenye mwili kama mtu wa kawaida na vilevile kumhukumu na kumkufuru Yeye. Ni wazi kuona kwamba kuelewa ukweli wa kupata mwili ni muhimu kwetu ili kumkaribisha Bwana na kuinuliwa katika ufalme wa mbinguni. Ni suala muhimu sana linalohusiana na hatima yetu ya mwisho.
Watu wengi watauliza, kwa kuwa Bwana Yesu ni Mungu mwenye mwili na Amefanya kazi ya ukombozi, na wanadamu tayari wameokolewa na kumgeukia Mungu, kwa nini Mungu bado anahitaji kuja katika mwili katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu ili kuwaokoa wanadamu? Kuna maana kubwa sana katika hili. Kwa ufupi, Mungu kuja katika mwili mara mbili ili kuwakomboa wanadamu, na kisha kutusafisha kabisa na kutuokoa kuliamuliwa kabla na Mungu muda mrefu kabla ya ulimwengu kuumbwa. Kuna unabii katika Biblia unaosema kwamba Mungu atakuja katika mwili mara mbili kama Mwana wa Adamu. Mara ya kwanza, kupitia kusulubishwa kama sadaka ya dhambi, Alikamilisha kazi ya ukombozi, ili dhambi za watu zisamehewe, lakini watu hawakukwepa dhambi wala kupata utakatifu. Mara ya pili, kupitia kuonyesha ukweli na kazi ya hukumu, Atawatakasa wanadamu kikamilifu, Atawaokoa kabisa wanadamu kutoka kwa dhambi na ushawishi wa Shetani, Atatamatisha enzi, na kuleta wanadamu kwenye hatima nzuri. Kwa hivyo, kupata mwili mara mbili kumekusudiwa kuwakomboa wanadamu, na kisha kuwaokoa kabisa wanadamu. Mungu anakuja katika mwili mara mbili ili kukamilisha mpango Wake wa usimamizi wa kuwaokoa wanadamu. Leo, kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho imeshinda na kukamilisha kundi la watu wakawa washindi, Mungu amemshinda Shetani na kupata utukufu, na kunaweza kusemekana kwamba Mungu Amekamilisha kazi Yake kuu. Haya ni mambo ambayo tayari Mungu amefanya. Sasa tunaweza kuona umuhimu wa ajabu wa kupata mwili kwa Mungu katika siku za mwisho. Kwa upande mmoja, kulitamatisha enzi ya zamani, Enzi ya Neema, na kuanzisha enzi mpya, Enzi ya Ufalme. Kwa upande mwingine, kunawatakasa kabisa na kuwaokoa wanadamu, na kuwaleta wanadamu kwenye hatima nzuri. Kazi ya ukombozi na kazi ya hukumu zinakamilishwa na Mungu mwenye mwili, kwa hivyo kupata mwili kwa Mungu mara mbili kwa hakika kuna umuhimu mkubwa. Leo, Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli kiasi kikubwa sana na kufanya mambo makuu katika ulimwengu wetu, hivyo kwa nini bado kuna watu wengi sana ambao hawaijui kazi ya Mungu? Watu wengi bado wanakataa kukiri kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mwenye mwili, wanashikilia fikira za kidini, wanaamini kwamba Bwana Yesu pekee ndiye Mungu, na kusisitiza kwamba ni kwa kufuata Biblia pekee ndiyo tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ni upumbavu na ujinga ulioje kufanya hivyo! Watu wapumbavu kama hao wanawezaje kusikia sauti ya Mungu? Na wanawezaje kugundua ukweli wote ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu? Hatimaye, hii ni kwa sababu watu hawana maarifa kuhusu Mungu mwenye mwili na hawawezi kutambua sauti ya Mungu, hivyo hawawezi kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Watu hawa wajinga, hawa wanawali wapumbavu, kamwe hawatapata kibali cha Mungu hata waamini kwa miaka mingapi. Ni dhahiri kwamba, ukitaka kumkaribisha Bwana, maarifa kuhusu Mungu mwenye mwili na kuelewa ukweli wa kupata mwili ni muhimu! Kwa hivyo, kupata mwili ni nini hasa? Na tunapaswa kuelewa vipi kupata mwili? Tunawezaje kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na wa uwongo? Tutaelewa baada ya kusoma neno la Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu). “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni). “Mungu aliyepata mwili anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kilichozidi kuliko hiki, kwa kuwa Anacho kiini cha Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambavyo haviwezi kufikiwa na mwanadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa uliochukuliwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kuonyesha tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu vizuri, na kumpa binadamu uzima” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Neno la Mungu linasema wazi kwamba kupata mwili ni Roho wa Mungu kufanyika mwili, yaani, Roho wa Mungu anavaa mwili ili kuwa mtu wa kawaida, na kisha kuonekana na kufanya kazi katika ulimwengu wa mwanadamu. Kwa ufupi, inamaanisha kwamba Roho wa Mungu anavaa mwili na kuwa Mwana wa Adamu. Kwa nje, Mungu mwenye mwili ni mtu wa kawaida, Asiye wa tabaka la juu wala wa ajabu, Yeye hula, Hujivisha, na Hujisafirisha kama tu watu wa kawaida na Huishi maisha ya kawaida. Anahitaji kula Anapohisi njaa na kulala Anapochoka, Yeye hupata mihemko ya kawaida ya binadamu, kwa kweli Yeye huishi miongoni mwa wanadamu, na hakuna anayeweza kuona kwamba Yeye ni Mungu wa vitendo mwenye mwili. Lakini licha ya kuwa mtu wa kawaida tu, kuna tofauti kubwa kati Yake na wanadamu walioumbwa. Yeye ni kupata mwili kwa Mungu, na Roho wa Mungu yu ndani Yake. Ana ubinadamu wa kawaida, lakini pia Ana uungu mkamilifu, unaoonekana wazi na kudhihirika. Hilo linadhihirika hasa kwa kuwa Anaweza kuonyesha ukweli na kufichua mafumbo wakati wowote au mahali popote. Anaweza kuonyesha na kushuhudia tabia ya Mungu, yote Mungu anayo na aliyo, akili na mawazo ya Mungu, upendo wa Mungu, na kudura na hekima ya Mungu, ili watu wote waweze kumjua na kumwelewa Mungu. Anaweza pia kufunua mafumbo yote katika Biblia, ambayo ina maana kwamba Anaweza kufungua kitabu kilichotabiriwa katika Ufunuo. Hii inathibitisha kwamba Ana uungu mkamilifu. Kwa nje, Kristo ni mtu wa kawaida, lakini Ana uwezo wa kuonyesha ukweli kiasi kikubwa sana, kuwaamsha watu, na kuwaokoa wanadamu waliopotoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ni nani awezaye kufanya mambo haya pasipo Roho wa Mungu ndani yake? Kwa hakika hakuna mtu maarufu au mashuhuri awezaye kufanya mambo kama hayo, kwa sababu hakuna mtu maarufu au mashuhuri anayeweza kuonyesha ukweli. Hana ukweli hata kidogo. Hawezi hata kujiokoa, kwa hivyo anawezaje kuwaokoa wanadamu wote? Mungu mwenye mwili anaweza kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, na hakuna mwanadamu aliye na uwezo huo. Kitabu kiitwacho Neno Laonekana katika Mwili ni matamshi ya Mungu katika siku za mwisho, na ni ushuhuda wa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa kuwa watu wateule wa Mungu wamepitia kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho na kukubali kunyunyiziwa na kuchungwa na Mwenyezi Mungu Mwenyewe, wote wamehisi jinsi kazi ya Mungu mwenye mwili ni ya utendaji sana. Mungu kwa kweli anaishi miongoni mwa watu, na Huonyesha ukweli kulingana na hali yetu halisi ili kutusaidia na kuturuzuku, na pia kufichua upotovu wa imani zetu katika Mungu, ufuatiliaji na mitazamo iliyo na makosa, na kila aina ya tabia za kishetani ndani yetu, ili tuweze kupata maarifa na mabadiliko. Pia Mungu hutuambia shauku na matakwa Yake kwa watu, Akitupa malengo ya vitendo na sahihi zaidi ya kufuatilia na kanuni za utendaji, ili tuweze kuingia katika hali halisi ya ukweli, kupokea wokovu wa Mungu, na kukwepa kabisa nguvu za giza za Shetani. Yeyote anayemfuata Mwenyezi Mungu hupata kujua kwa kina kwamba bila Mungu mwenye mwili kuja kuonyesha ukweli ili kuhukumu na kuadibu watu, hawezi kamwe kutambua asili zake za dhambi, wala kuweza kuepuka utumwa na vikwazo vya dhambi. Pia anatambua kwamba tabia zake potovu zinaweza kusafishwa tu kwa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, anaweza kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa kuwa tu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu yenye haki, na ni kwa kuishi kwa kufuata neno la Mungu pekee ndipo anaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu, kustahili kupokea ahadi na baraka za Mungu, na kuletwa katika ufalme wa mbinguni. Fikiria hili: Bila Mungu mwenye mwili kuja na kuonyesha ukweli sana katika siku za mwisho, je, tungepata fursa hii ya kipekee ya kuokolewa? Je, tungeweza kupokea hukumu na kuadibu kwa Mungu na kufurahia baraka tele za Mungu? Bila kupata mwili kwa Mungu katika siku za mwisho, wanadamu wote wangeandikiwa maangamizo, na hakuna ambaye angepokea wokovu. Ni kama neno la Mwenyezi Mungu linavyosema, “Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na pia Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hamumkubali kwa urahisi?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).
Sasa, watu wengine wanaweza kuuliza, “Sura ya Mungu mwenye mwili ni ya kawaida, na uungu Wake umefichwa ndani ya mwili Wake, hivyo iwapo Mungu amekuja, tunawezaje kumtambua kuwa Mungu mwenye mwili?” Maneno ya Mwenyezi Mungu yanatuonyesha njia. Mwenyezi Mungu anasema, “Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Kutoka katika neno la Mungu, tunaweza kuona kwamba kumtambua Mungu mwenye mwili hakutegemei sura Yake, wala kutegemea familia Alikozaliwa, kama Ana cheo au uwezo, au iwapo Ana hadhi kubwa katika ulimwengu wa kidini. Hakutegemei mambo haya. Badala yake, kunategemea iwapo Ana kiini cha Mungu, kama Anaweza kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Hiki ndicho kipengele muhimu zaidi. Ikiwa Anaweza kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu, basi hata kama Alizaliwa katika familia ya kawaida na Hana mamlaka na cheo katika jamii, Yeye ni Mungu. Kama tu katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi, Alizaliwa katika familia ya kawaida, Akaja ulimwenguni katika hori, Hakuwa mrefu au mwenye miraba minne, na Hakuwa na hadhi au mamlaka, lakini Aliweza kuonyesha ukweli, Akawapa watu njia ya toba, na kuweza kusamehe dhambi za watu. Wale waliopenda ukweli, kama wanafunzi Wake Petro na Yohana, waliona katika kazi ya Bwana Yesu na ukweli Aliouonyesha kwamba Alikuwa na nguvu na mamlaka ya Mungu na walimtambua Bwana Yesu kuwa Masihi, hivyo walimfuata na kupata wokovu wa Bwana. Leo, Mungu Amekuja tena Akiwa mwili katika ulimwengu wa mwanadamu, na ingawa kwa nje Anaonekana kuwa mtu wa kawaida, Mwenyezi Mungu anaweza kuonyesha ukweli kiasi kikubwa na kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Wengi katika nchi na maeneo yote wameona ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu, wameitambua sauti ya Mungu, wamemkubali Mwenyezi Mungu, na kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Wameanza kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuelewa ukweli kiasi. Wote wana uzoefu na ushuhuda mzuri sana, na wanajitolea kwa hali na mali kuhubiri injili na kumshuhudia Mungu. Ukweli unathibitisha kwamba ni mtu anayeweza kuonyesha ukweli, kuhukumu na kuwatakasa watu, na kuwaokoa wanadamu kikamilifu pekee ndiye Kristo na Mungu mwenye mwili. Hii ni dhahiri. Ikiwa mtu hawezi kuonyesha ukweli, na anaweza tu kuwadanganya wengine kwa kuonyesha miujiza, hii ni kazi ya roho mwovu. Iwapo anajiita Mungu, yeye ni Kristo wa uongo anayejifanya kuwa Mungu. Ili kumjua Mungu mwenye mwili, tunahitaji kuwa na uhakika na ukweli huu: Ni Mungu mwenye mwili pekee anayeweza kuonyesha ukweli, kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na kuwaokoa wanadamu kabisa kutoka kwa nguvu za Shetani.
Mwenyezi Mungu Ameonyesha ukweli kiasi kikubwa sana na kufanya kazi nzuri sana katika siku za mwisho, lakini kuna watu wengi wanaompuuza, na wanamngoja tu Bwana Yesu aje waziwazi juu ya wingu. Watu kama hao watalia na kusaga meno watakapokuwa wakiangamia katika maafa. Hili linatimiza unabii katika Ufunuo: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye” (Ufunuo 1:7). Mwenyezi Mungu pia anasema, " “Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia.” Hatimaye, hebu tusome kifungu cha neno la Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?