Kutoroka Hatari

12/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipia gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko makubwa, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao(Neno Laonekana katika Mwili). Niliposoma kifungu hiki hapo awali, nilikielewa tu kwa nadharia, lakini sikuwahi kukielewa au kukithamini kwa kweli. Baadaye, nilikamatwa, niliteswa na kuumizwa kikatili na CCP, na maneno ya Mungu ndiyo yaliyonielekeza kutoroka hatari mara mara kwa mara, Shetani alipokuwa akinidhuru. Niliona matendo ya Mungu ya ajabu na nikaona kwamba mamlaka ya maneno Yake yanashinda kila kitu. Nilipata ufahamu kiasi kumhusu Mungu na imani yangu iliongezeka.

Hii ilitukia mnamo 2006, wakati ambapo jukumu langu kanisani lilikuwa kuchapisha vitabu vya maneno ya Mungu. Nakumbuka wakati mmoja, wakati wa uwasilishaji, baadhi ya kina ndugu ambao walikuwa na jukumu la kuwasilisha vitabu na dereva mmoja wa kiwanda cha kuchapisha ambaye tulikuwa tuemkodi wote walikamatwa na polisi wa CCP. Nakala elfu kumi za Neno Laonekana katika Mwili zilizokuwa ndani ya gari hilo zote zilichukuliwa ngawira. Dereva huyo alitusaliti, kwa hivyo ndugu wengine karibu dazeni moja waliishia kukamatwa. Kesi hiyo ilizua vurugu katika mikoa miwili, halafu Kamati Kuu ikaanza kuisimamia. Serikali ya CCP baadaye iligundua kwamba nilikuwa kiongozi wa kanisa, na hata iliwatuma polisi wenye silaha wachunguze eneo langu la kazi. Wakati huo, walichukua ngawira magari hayo mawili na lori moja kutoka kwa kampuni ya kuchapisha ambayo tulikuwa tumefanya nayo kazi, na vilevile yuani 65,500 pesa taslimu kutoka kwao. Pia walichukua zaidi ya yuani 3,000 toka kwa ndugu waliokuwa wakisaidia katika kuwasilisha vitabu. Polisi walikuja kupekua nyumba yangu mara mbili baada ya hapo, wakivunja mlango kila wakati. Walivunja na kuponda chochote walichochukua, na kuiacha nyumba ikiwa imeharibika kabisa. CCP haikuishia kunikamata, lakini waliwazuilia majirani zangu na wengine niliohusiana nao, na wakajaribu kuwalazimisha waseme mahali nilipokuwa.

Sikuwa na lingine ila kukimbilia nyumbani kwa jamaa aliyeishi mbali sana ili kuepuka kukamatwa na kuteswa na CCP. Ajabu ni kwamba, jioni ya tatu nilipokuwa kule, polisi kutoka makazi yangu ya kudumu walishirikiana na polisi wa eneo lile wenye silaha na polisi wa jinai, na zaidi ya watu 100 walizingira nyumba ya jamaa yangu kiasi kwamba hakukuwa na chochote ambacho kingeingia ndani. Kisha polisi walijitoma ndani ya nyumba. Polisi dazeni moja au zaidi walinielekezea bunduki zao kichwani pangu, na mmoja wao akasema kwa sauti kuu, “Ukisogea kidogo tu, utakufa!” Waliangukiana huku wakikurupuka kunitia pingu, wakiupinda mkono wangu wa kulia nyuma ya bega langu na kuvuta juu mkono wangu wa kushoto kwa nguvu kutoka mgongoni. Hawakuweza kunitia pingu, kwa hivyo walitumia mguu kuvuta mkono wangu juu, kisha wakatia pingu vifundo vya mikono yangu kwa nguvu. Maumivu yale hayakuvumilika. Walichukua yuani 650 waliyopata kutoka kwangu na wakaniuliza mahali ambapo fedha za kanisa zilikuwa, na kuniambia kwamba niwakabidhi zote. Hili lilinikasirisha. Je, walikuwa “polisi wa umma” wa aina gani? Nilihudhuria mikutano,nilisoma maneno ya Mungu, na nilifanya wajibu wangu katika imani yangu, lakini walikusanya jeshi kubwa sana na kufanya hayo yote ili tu kunikamata, na sasa walitaka kupora na kubadhiri fedha za kanisa. Hiyo ilikuwa dhihaka iliyopita kiasi! Walipoona kwamba sikuzungumza, afisa mmoja alinijia na kunizaba kofi mara mbili vibaya sana, alinipiga mateke hadi nikaanguka chini. Kisha wakanipiga mateke kama mpira wa miguu. Nilizirai kutokana na maumivu. Nilipopata fahamu, nilikuwa kwenye gari la askari nikirudishwa katika makazi yangu ya kudumu. Mle garini, polisi walikuwa wamenitia silisili nzito, shingo yangu ikiwa imefungiwa mwishi mmoja wa silisili ile, na miguu yangu mwisho huo mwingine. Nilichoweza kufanya ni kukunjamana na kuwa mviringo, kisha kuegemea kifua na kichwa changu ili kujizuia kuanguka chini. Polisi walipoona nilivyotaabika, walinicheka tu na kusema kila aina ya mambo ya kuvunja heshima. Nilijua vizuri sana kwamba walikuwa wakinitendea kwa njia hiyo kwa sababu ya imani yangu katika Mwenyezi Mungu. Mstari huu ulionenwa na Mungu katika Enzi ya Neema ulinijia akilini: “Ikiwa dunia ikiwachukia, ninyi mnajua ya kwamba ilinichukia mimi kabla iwachukie ninyi(Yohana 15:18). Kadiri walivyozidi kunifedhehesha kwa njia hiyo, ndivyo nilivyozidi kuona waziwazi ubaya wao na asili zao za kishetani na zenye uovu za kumchukia Mungu. Niliwachukia hata zaidi. Nilimwita Mungu moyoni mwangu bila kukoma, nikimwomba Mungu aulinde moyo wangu, ili kwamba bila kujali nilikuwa karibu kukabili mateso aina gani, niweze kuwa shahidi na kumwaibisha Shetani. Baada ya kuomba, nilikumbuka maneno haya ya Mungu: “Uwe na utulivu ndani yangu, kwa maana Mimi ni Mungu wako, Mkombozi wenu wa pekee. Mnatakiwa kutuliza mioyo yenu nyakati zote, mkae ndani yangu; Mimi ni mwamba wako, msaidizi wenu(Neno Laonekana katika Mwili). Ni kweli. Kila kitu cha mwanadamu kiko ndani ya mikono na mipango ya Mungu, na ni Mungu anayeamua iwapo tunaishi au kufa. Kwa kuwa nilikuwa na Mwenyezi Mungu, kulikuwa na nini cha kuogopa? Wazo hili liliitia nguvu imani yangu, na nikawa tayari kumtegemea Mungu ili kukabiliana na mateso ya kikatili ambayo yalikuwa yakinisubiri.

Sijui nilizirai mara ngapi kutokana na maumivu wakati wa usafiri wa zaidi ya saa 18. Nakumbuka tu kwamba ilikuwa baada ya saa 8 usiku nilipofika kizuizini katika makazi yangu ya kudumu. Nilihisi kama kwamba damu yote mwilini mwangu ilikuwa imeganda. Mikono na miguu yangu ilikuwa imevimba sana, ilikuwa imekufa ganzi na haikuwa na hisia, na sikuweza kuisogeza hata kidogo. Nilisikia maafisa kadhaa wakiongea juu yangu, wakisema, “Mtu huyo amekufa?” Baadaye, walivuta pingu zangu kwa nguvu na kuniburuta. Nilihisi meno ya pingu zangu yaking’ata ndani kabisa ya nyama za mwili wangu, na kisha wakaniburuta kwa ukali nje ya gari na kunitupa chini kwa nguvu. Nilizirai kutokana na maumivu. Mara baada ya hapo, afisa mmoja aliniamsha kwa kunipiga teke kwa nguvu, kisha akaniburuta kwa ukali hadi kwenye seli ya wafungwa waliohukumiwa kifo. Siku iliyofuata, karibu polisi dazeni moja, wote wakiwa wamebeba bunduki, walinichukua kutoka kizuizini na kunipeleka mahali palipokuwa mbali nje ya viunga vya jiji. Palikuwa na uwanja mkubwa uliozungukwa na kuta ndefu. Palionekana kwamba palilindwa sana. Kulikuwa na polisi wenye silaha waliolinda, na maneno “Kituo cha Mafunzo ya Mbwa wa Polisi” yalikuwa yameandikwa kwenye ishara ya lango. Mara nilipofika chumbani, niliona kila aina ya vifaa vya kutesea vilivyokuwa vimetandazwa. Kuona hayo kulinijaza woga. Kwanza polisi walinisimamisha katikati ya uwanja na kuniamuru nisisogee. Walifungua tundu na kuwaachilia mbwa wanne wakali, kisha wakaniashiria na kuwaamrisha mbwa wale, ‘Nendeni, ueni!” Mbwa wale wanne wote walinirukia vikali na niliyafumba macho yangu haraka kwa sababu ya woga. Nilishtuka na kulikuwa na sauti iliyovuma katika kichwa changu. Nilikuwa na wazo moja tu: “Mungu! Niokoe! Niokoe!” Nilimwita Mungu moyoni mwangu tena na tena. Baada ya muda kidogo, niligundua ghafla kwamba mbwa wale walikuwa waking’ata tu nguo yangu, na hawakuwa wamenijeruhi hata kidogo. Kulikuwa pia na mbwa aliyeegemea mabegani pangu, akininusanusa na kuuramba uso wangu. Hakuwa pia akiniumiza. Nilimkumbuka ghafla nabii Danieli kutoka kwenye Biblia. Alitupwa katika tundu la simba kwa sababu alimwabudu Mungu, lakini Mungu alikuwa naye. Aliwatuma malaika wazibe midomo ya simba, kwa hivyo simba wale wenye njaa hawakumdhuru Danieli. Wazo hilo lilinipa imani kubwa zaidi. Nilihisi kwa kweli kuwa yote yamo mikononi mwa Mungu, na ilikuwa juu Yake iwapo ningeishi au kufa. Niliwaza, “Mungu akiniruhusu niuawe kwa ajili ya imani yangu leo, hiyo itakuwa heshima na sitalalamika.” Sikuzuiwa na wazo la kifo, na mara nilipokuwa tayari kutoa maisha yangu ili kuwa shahidi wa Mungu, niliona tendo lingine la ajabu la Mungu. Niliweza kusikia wale askari wakisema kwa sauti kuu, “Ua! Ua!” Lakini mbwa wale walikuja tu na kuuma mavazi yangu, walininusanusa na kuniramba, na kisha wakageuka na kukimbia. Polisi waliwasimamisha mbwa wale na kujaribu kuwafanya warudi kwangu na kunishambulia, lakini mbwa wale walitawanyika kwa hofu na wakakimbia, na bado hawakunuiuma. Polisi wale walishangaa na kusema, “Ni ajabu sana kwamba mbwa hawamuumi!” Kusikia hayo kulinifanya nikumbuke maneno ya Mungu: “Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote(Neno Laonekana katika Mwili). Kubakia salama salimini katikati ya kundi la mbwa wa polisi ni Mungu aliyekuwa Akinilinda sirini, na kunionyeshea uweza Wake na matendo Yake ya kushangaza. Imani yangu katika Mungu iliongezeka hata zaidi.

Polisi walipoona kwamba mambo hayakuwa yakienda kama walivyotarajia, walinipeleka kwenye chumba cha mateso na kunining’iniza ukutani kwa pingu. Kulikuwa na maumivu makali mara moja kwenye vifundo vya mikono yangu kana kwamba vilikuwa vimeng’atwa. Hata hivyo, bado hawakupumzika, bali walianza kunigonga na kunipiga mateke. Wakati polisi mmoja alipochoka, mwingine alichukua zamu. Nilipigwa kichapo cha mbwa na nilikuwa nimepoteza damu nyingi. Jioni iliwadia na bado hawakuniruhusu niende. Pindi nilipofumba macho yangu hata kidogo, walinitia umeme kwa kutumia kirungu chao cha umeme, na polisi mmoja alisema huku akinipiga, “Mtu akikugonga hadi uzirai, nitakuamsha kwa njia hiyo hiyo!” Nilipomsikia akisema hivyo. nilijua kwamba Shetani alikuwa akijaribu kila aina ya mateso katili kunishawishi ili nisalimu amri, ili kwamba nitakapoteswa hadi kuchanganyikiwa na nisiweze kufikiri vizuri, wapate habari juu ya kanisa kutoka kwangu. Kisha wangewakamata kina ndugu na kuchukua pesa za kanisa. Nilijikaza kisabuni, nikavumilia maumivu, na kujionya: “Hata nikinyongwa, sitakubali kamwe kushindwa na Shetani!” Waliendelea kunitesa hivyo hadi alfajiri ya siku iliyofuata. Nilihisi kama kwamba nilikuwa nimetolewa nguvu kabisa, kwamba kifo kingenipa nafuu, na sikuwa na nguvu ya kuvumilia tena. Nilikuwa nikimwita Mungu bila kukoma ndani ya moyo wangu: “Ee Mungu! Mwili wangu ni dhaifu, na siwezi kabisa kuvumilia tena. Wakati ambapo bado nina pumzi ya kupumua, wakati ambapo bado nina fahamu na niko macho, nakuomba Uichukue roho yangu. Sitakuwa Yuda na kukusaliti.” Nilikumbuka maneno haya ya Mungu baada ya maombi yangu: “Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika Mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, hata kuliko awali, Anakumbwa na hatari kubwa kwa kuja duniani wakati huu. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na kumbi za starehe; Anavyokabiliana navyo ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura za wauaji. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote(Neno Laonekana katika Mwili). Mungu ndiye Muumba. Yeye ni mkuu na mtukufu sana. Amekuwa mwili mara mbili, Akivumilia fedheha kuu ili kuonyesha ukweli na kuokoa binadamu, Akisakwa na kuteswa na Shetani kila wakati, Akilaaniwa na kukataliwa na ulimwengu wa dini, na kukataliwa na vizazi vyote viwili. Mateso ya Mungu yamekuwa makubwa sana. Kufikiri juu ya upendo wa Mungu kulinigusa sana, na niliamua, “Almradi nina pumzi moja iliyobaki ndani yangu, nitakuwa shahidi na kumwaibisha Shetani!” Polisi walipoona kwamba sikuwa nikisema chochote au kuomba msamaha kwa muda mrefu, waliogopa kwamba watanipiga hadi nife na hawataweza kuwasilisha ripoti zao. Waliacha kunipiga, lakini waliniacha nikinging’inia ukutani kwa siku mbili.

Hali ya hewa ilikuwa baridi sana wakati huo. Nilikuwa nimevalia nguo nyepesi na nilikuwa nimelowa maji kabisa, na aidha, sikuwa nimekula kwa siku kadhaa. Nilihisi kana kwamba sitaweza kuvumilia kwa muda mrefu zaidi. Ni wakati huo ndipo polisi walijaribu hila yao nyingine, wakimwita mwanasaikolojia ili ajaribu kushawishi mawazo yangu, kunitia kasumba. Mwanasaikolojia yule alisema, “Wewe bado ni mchanga, na una wazazi na watoto wako. Tangu ulipokamatwa, waumini wengine, pamoja na kiongozi wenu, hawajakuhangaikia hata kidogo. Je, si jambo la kipumbavu kwako kuteseka sana kwa niaba yao?” Niliposikia uwongo huu, niliwaza, “Je, ndugu zangu wakija kunitembelea, hawatakuwa wakiingia mtegoni? Unajaribu kunidanganya na kunishawishi kwa hila hizi, kutumia uhusiano wangu na kina ndugu ili nimwelewe Mungu visivyo, nimlaumu, na kumkataa. Sitakuacha ufanikiwe.” Kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, nilibaini hila ya Shetani na sikuzuzuliwa. Mwanasaikolojia yule aliposhindwa, alitikisa kichwa na kusema baadaye, “Huyu mtu hawezi kusaidiwa. Bila kujali tunachofanya, hatuwezi kabisa kupata chochote kutoka kwake. Hatabadili mawazo.” Alipokuwa akisema hayo, alitikisa kichwa chake na kwenda zake akiwa ameshindwa.

walioyesha tabia zao za kweli tena mara moja na kunining’iniza juu kwa siku nyingine. Kufikia jioni hiyo, nilikuwa baridi sana kiasi kwamba nilikuwa nikitetemeka kuanzia kichwani hadi kidoleni na nilihisi kana kwamba mikono yangu ilikuwa karibu kuanguka. Ilikuwa chungu sana. Nilichanganyikiwa, na nilihisi kama kwamba sikuweza kabisa kuendelea kuvumilia. Wakati huohuo, kundi la maafisa liliingia ghafla upesi, kila mmoja akishikilia fimbo yenye urefu wa karibu mita moja. Walianza kunipiga vibaya kwenye magoti na vifundo vya miguu, na maafisa wengine wakaanza kunifinya. Nilikuwa na maumivu makali sana kiasi kwamba nilitaka kufa. Wakati huo, nilichanganyikiwa kabisa. Mwishowe sikuweza kuvumilia tena, na nilianza kulia. Wazo la kumsaliti Mungu lilinijia akilini ghafla. Nilidhani kwamba labda ningezungumza juu ya imani yangu mwenyewe mradi nisiwahusishe ndugu zangu. Polisi waliponiona nikilia, walinishusha chini. Waliniacha nilale pale, wakanimwagia maji kidogo, na kuniruhusu nipumzike kidogo. Walichukua kalamu na karatasi waliyokuwa wameandaa mapema, tayari kuandika muhtasari. Nilipokuwa tu nikizidi kutumbukia katika majaribu ya Shetani na nilikuwa karibu kumsaliti Mungu, maneno ya Mungu yalinijia akilini waziwazi ghafla: “Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu…. Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili(Neno Laonekana katika Mwili). Hii ilinifanya nitambue kwamba tabia ya Mungu haivumilii kosa lolote, na yeyote amsalitiye Mungu hatapata rehema Yake kamwe. Nilizinguka ghafla na nikakumbuka Yuda akimsaliti Bwana Yesu kwa ajili ya vipande 30 vya fedha. Je, ningemsaliti Mungu kweli kwa ajili ya muda mfupi wa raha? Isingekuwa maneno ya Mungu yaliyonielekeza na kunitia nuru wakati ufaao, pengine ningemsaliti Mungu na kuhukumiwa milele! Nilikumbuka mstari kutoka katika wimbo wakati huo: “Kichwa changu kinaweza kupasuka na damu kutiririka, lakini ujasiri wa watu wa Mungu hauwezi kupotea. Ushawishi wa Mungu umo moyoni, ninaamua kumwaibisha Shetani Ibilisi” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliuimba moyoni mwangu na nilihisi imani yangu ikiongezeka. Maisha na kifo changu vilikuwa mikononi mwa Mungu, na nilijua kwamba nilipaswa kutii utaratibu Wake. Almradi nilikuwa na pumzi moja iliyobaki, nilipaswa kuwa shahidi na kamwe kutosalimu amri ya pepo wa CCP!

Walipoona kwamba nilikuwa nikilala tu sakafuni bila kusogea hata kidogo, waliendelea kunishawishi. Mmoja alisema, “Je, mateso haya yote yana maana? Tunakupa nafasi ya kufidia makosa yako, na kutuambia unachojua. Tayari tunajua kila kitu, ikiwa utazungumza au la. Tuna mashahidi wengi na ushahidi mwingi wa kukufanya ushtakiwe na kuhukumiwa.” Nilipowaona wakijaribu kila hila iliyopo kunishawishi ili nimsaliti Mungu na kuwasaliti waumini wengine, sikuweza kuzuia hasira yangu, na niliwafokea, “Kwa kuwa mnajua kila kitu, hakuna haja ya kuniuliza. Hata kama ningejua kila kitu, nisingewaambia kamwe!” Afisa mmoja alisema kwa ghadhabu, “Usipozungumza leo, utakufa. Usifikirie hata kwamba utatoka hapa ukiwa hai!” Nilimjibu kwa kusema, “Kwa kuwa nimeanguka mikononi mwenu, sikuwa nikitarajia kutoka hapa nikiwa hai, kwa vyovyote vile!” Afisa mmoja alinipiga teke kwenye utumbo kwa hasira, akiniacha nikihisi kana kwamba nilikuwa nimetumbuliwa. Wote waliniparamia tena na kuanza kunipiga mateke na ngumi, na nilizirai tena kutokana na maumivu. Nilipopata fahamu, nilikuwa nimefungwa kama awali, lakini juu zaidi wakati huu. Niliweza kuhisi mwili wangu wote ukianza kuvimba na sikuweza hata kuongea. Lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, sikuhisi maumivu yoyote hata kidogo. Jioni ilipofika, maafisa wanne wa polisi walikaa ili kunichunga na waliishia kulala wote. Ghafla, pingu zangu zilijifungua na nilianguka sakafuni polepole kana kwamba nilitengemezwa na kitu fulani chini yangu. Nisingepitia hayo mwenyewe, kamwe nisingeamini! Nilikumbuka Petro alipokuwa gerezani, na malaika kutoka kwa Bwana akamwokoa. Wakati huo, minyororo ya Petro ilianguka tu na mlango wa seli yake ukafunguka. Sikuthubutu kuamini kwamba nilikuwa nikipitia matendo ya Mungu ya ajabu kama Petro alivyofanya. Wakati huo nilihisi kweli kwamba nilikuwa nimeinuliwa na kubarikiwa na Mungu! Kwa kuwa niliguswa sana, nilipiga magoti upesi mbele za Mungu na kutoa sala ya shukrani. “Ee Mungu! Asante kwa rehema Yako na kwa kunijali. Niliteswa na Shetani hadi karibu nife mara nyingi, na Ulikuwa ukinilinda kimyakimya kila wakati, Ukiniruhusu nione uweza Wako na matendo Yako ya ajabu.” Maombi haya yalinigusa sana na nilikuwa na hisia ya ukunjufu ndani yangu. Nilitaka sana kusimama na kutoka nje, lakini sikuweza kusogeza mikono au miguu yangu, kwa hivyo sikuondoka. Kisha nililala sakafuni hadi siku iliyofuata, wakati ambapo polisi waliniamsha kwa kunipiga. Wale polisi waovu kisha walianza kunitesa kwa njia mpya. Walinipeleka kwenye chumba kingine na kuniamuru niketi kwenye kiti cha mateso ambacho kilikuwa kimeunganishwa na umeme. Walifunga shingo na kichwa changu kwa vibanio vya chuma na kufunga mikono yangu miwili kiasi kwamba sikuweza kusogea hata kidogo. Nilichoweza kufanya ni kumwomba Mungu kimyakimya. Wakati huo afisa alibonyeza swichi ya umeme na polisi wengine dazeni moja au zaidi walinikazia macho, ili kuona jinsi itakavyokuwa nitakaposhtushwa kwa umeme. Walishtuka walipoona kwamba sikuonyesha hisia zozote hata kidogo. Walikagua mfumo wote wa nyaya za umeme, na baada ya muda mrefu kidogo, wakati ambapo bado sikuonyesha hisia, mmoja wao alisema, “Je, kiti cha mateso kimeharibika? Kwa nini hakuna mkondo wa umeme?” Alinigonga kwa mkono wake bila kufikiria, na kwa mlio wa “zap!”, mshtuko wa umeme ulimrusha nyuma umbali wa mita moja ambapo alilala pale sakafuni akilia kwa maumivu. Maafisa wale wengine wote waliogopa sana kiasi kwamba walikimbia nje, na mmoja wao alijikwaa na kuanguka alipokuwa akiondoka kwa haraka. Muda mrefu ulipita kabla ya maafisa wawili kurudi ili kunifungua, wakitetemeka kwa hofu ya kushtushwa. Nilikuwa nimekaa kwenye kiti hicho cha mateso kwa saa nzima na nusu lakini sikuweza kuhisi umeme hata kidogo. Nilihisi kama kwamba nilikuwa nikiketi kwenye kiti cha kawaida. Hii ilikuwa kazi nyingine ya Mungu ya ajabu. Niliguswa sana. Wakati huo nilihisi kana kwamba nilikuwa tayari kupoteza chochote, hata maisha yangu. Almradi Mungu alikuwa nami, hiyo ingetosha.

Walinirudisha kizuizini baadaye. Nilikuwa nimejawa na majeraha na uchungu uliokuwa mikononi na miguuni pangu haukuvumilika. Mwili wangu wote ulikuwa mnyonge na dhaifu. Sikuweza kuketi au kusimama, au kumeza chakula. Nilichoweza kufanya ni kulala pale, kifudifudi. Mtu moja ambaye nilikuwa nikikaa naye katika seli hiyo ya wafungwa waliohukimiwa kifo alipogundua kwamba sikuwa nimemsaliti yeyote, alinistaajabia sana. Alisema, “Ninyi waumini ni mashujaa wa kweli!” Moyoni mwangu, nilimwomba Mungu huku nikimsifu. Baadaye polisi walijaribu kuwashawishi wafungwa wengine wanipige na kunitesa, lakini cha kushangaza ni kwamba, waliniunga mkono na kunitetea. Walisema, “Mtu huyu anamwamini Mungu, na hajafanya chochote kibaya. Mnataka kumtesa hadi afe.” Kwa sababu ya kuogopa kwamba mambo yangekosa kudhibitika, polisi hawakuthubutu kusema lolote, lakini waliondoka tu kimyakimya, wakiwa wameshindwa.

Polisi walipoona kwamba hawakuwa wakifaulu, walihamia mbinu nyingine, na wakaanza kushirikiana na walinzi wa gereza kule kizuizini ili wanipe kazi nyingi ya ziada ya kufanya. Kila siku walinilazimisha nitengeneze vifurushi viwili vya karatasi ya udi ya kuwachomea wafu, na kila kifurushi kilikuwa na bamba 1,600 ya jaribosi na karatasi iwakayo. Hii ilikuwa mara mbili ya kazi ambayo wafungwa wengine walipaswa kufanya. Mikono yangu iliumia vibaya sana na sikuweza kuinua chochote, sikuweza kabisa kumaliza kazi hiyo yote, hata nilipoifanya usiku kucha. Polisi walitumia udhuru huu kuniletea adhabu ya mwili, wakinilazimisha nioge kwa maji baridi yenye halijoto ya digrii 20 chini ya sifuri, au kunilazimisha nifanye kazi kila usiku mfululizo, au kulinda kwa muda mrefu. Nilikuwa nikilala kwa chini ya saa tatu kila usiku. Niliteseka hivi kwa mwaka mmoja na miezi minane kule kizuizini. Badaye, CCP ilinishtaki kwa “kutumia shirika la xie jiao kudhoofisha utekelezaji wa sheria” bila ushahidi wowote, na ikanihukumu miaka mitatu gerezani. Nilipotoka gerezani bado nilikuwa chini ya uangalizi wa makini wa kituo cha polisi cha eneo hilo. Sikuwa huru kwenda popote nilipotaka, na ilibidi niwe tayari kutokea pindi waliponiita. Sikuwa na uhuru wowote wa kibinafsi. Sikuweza kuhudhuria mikutano ya kanisa au kutekeleza wajibu wangu. Hali hii ilikuwa ngumu sana kwangu, na nilifikiri kwamba ikiwa nitaendelea kuchunguzwa na CCP kila wakati na nisiweze kufanya wajibu wangu kama kiumbe, je, hiyo haitakuwa hali mbaya sana kwangu? Kwa hivyo, baadaye niliondoka katika makazi yangu ya kudumu na kwenda mkoa mwingine ambapo mwishowe niliweza kufanya wajibu wangu.

Mateso makali ya CCP yameganda katika kumbukumbu yangu. Nimeuona uso wake mwovu, upinzani wake wa kishetani kwa Mungu na jinsi inavyowadhuru watu, na naichukia kabisa. Nilishuhudia pia matendo ya ajabu ya Mungu na uweza na ukuu Wake. Matendo ya Mungu ya ajabu ndiyo yaliyonilinda kiasi kwamba niliweza kutoroka mikononi mwa Shetani na hayo ndiyo yalininyakua kutoka hatarini. Kupitia mateso ya kikatili ya CCP, maneno ya Mungu ndiyo yaliyonielekeza, na nishati uhai Yake ndiyo ilinitegemeza kiasi kwamba niliweza kuendelea kuishi, na hii iliimarisha imani yangu ya kumfuata Mungu. Shukrani kwa Mungu! Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wakati wa mateso Ya Kikatili

Na Chen Hui, China Nililelewa katika familia ya kawaida nchini China. Baba yangu alikuwa katika jeshi na kwa sababu nilikuwa nimeongozwa na...

Upendo wa Mungu Hauna Mipaka

Na Zhou Qing, Mkoa wa ShandongNimepitia taabu ya maisha haya kikamilifu. Sikuwa nimeolewa kwa miaka mingi kabla ya mume wangu kufariki, na...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp